Ushauri wa bure: Madereva wa private cars tembeeni usiku kama unafanya Safari ndefu

nimenusurika kufa baada ya kupigwa sportlight kwa mstukizo na truck kubwa.
Nimepoteza marafiki wa moyoni wanne kwa mkupua wakiwa wanaaza kuinusa mwanza kwa sababu dreva alisinzia.

Kama sio mzoefu bora tupambane mchana tu.
Usiku haufai kama unajijua unatabia ya kusinzia! Lazma ujue sleeping pattern yako vyema. Mfano mie usingizi wangu ni saa 6-7 hapo lazma nilale nisipolala hapo jua silali mpaka kunakucha. Ila nikinywa energy drink kabla ya huo muda silali kabisa.

Cha muhimu pumzika vya kutosha mchana kisha hakikisha unapoanza safari uko well hydrated ili macho yaone vizuri pia unaweza kutumia energy drink ilio diluted na maji ili ku activate mwili pia caffeine huondosha usingizi!
 
Kweli kabisa, Usiku ni balaa. Huyu jamaa hii mada sijui anatafuta kuungwa mkono?
Kama upo willing kusumbuliwa njia nzima unatembea mchana tu! Zile kero za kupigwa mkono kila baada ya nusu saa hapana! Mara naomba leseni yako, unampa askari anaondoka nayo mnaanza kutongozana wee mambo ya kijinga sana hayo!

Mie siogopi kutembea usiku kama gari naiamini! Taa ziko poa na brakes ziko poa!
 
I bet kama hukupanda ally's star bus,, busi ni Dar blue
(sijasema wanatembea 127kms)
Kuhusu speed aisee Kwenye haya Mabus niliyopanda hamna nilikaa mbele karibu na Dereva nimeona jamaa anapiga Hadi speed 127 km/h.....kama ujuavyo bus likiwa speed hiyo ni balaa yaani Ngoma inatembea balaa Hadi Mwanza nyegezi tumeingia saa 4:48 usiku
 
Mi nasikitika speed za mabasi ni kubwa mno na hakuna hatua wanachukuliwa. Siku watu wakifa kwa makumi ndiyo watakurupuka na ukaguzi wa mabasi
 
Hiyo ni kweli . Juzi tarehe 27/4 ...Nilifuatana na gari moja linaitwa Malaika mimi naendesha Alphard niko speed 110 jamaa alinipita na moto wa hatari na hakupunguzi kwenye 50 yeye kinachomfanya apunguze mwendo ni hizo speed humps
Ukijaribu kumuiga unasimamishwa wewe mwenye private car yeye anachanja mbuga
Na imetokea hivyo mara nyingi
Labda Trafic na LATRA watueleze
Kuna siri gani?
 
Hao madereva wa Mabus ni Kama msafara wa raisi hawapigwi Cheti wala kusumbuliwa na traffic....
Sikuhizi ni mwendo mdundo Tu kama kawaida
 
Usiku inatakiwa uwe mzoefu sana na usiwe na papara! Nimeendesha usiku Mara nyingi, kuna changamoto kubwa sana sana!

Nimeshaendesha usiku mzima yaani zaidi ya 13hrs, kuna uchovu unaupata muda Fulani ambapo usipokua makini unapoteza.

My recent driving ilikua Sumbawanga to Morogoro, ilikua safari ndefu na nilipata changamoto za hapa na pale lakini nilisinzia Mara kadhaa na kujikuta nalazimika kusimama na kujinyoosha kidogo.

Kama huna macho mazuri, kuna Wapuuzi wanaendeshea full lights na kuna wengine wamefunga zile crystal lights ambazo ni hatari kwa kweli.

Pia kuna magari mabovu na ajali za hapa na pale, hii safari ya mwisho nilijikuta ghafla ni Lori limebeba container la 40ft limeanguka dakika hio saa kumi asubuhi maeneo ya Iyovi tena kwenye kona!
Lilifunga barabara kabisa na muda ule likawa linakuja tanker la mafuta likaligonga lile tanker.

Ni ajali mbaya ambayo ilitufanya tukae hapo kuanzia saa kumi asubuhi hadi saa nne asubuhi ndio tukaondoka.

Hivyo, kama una papara za kukimbia na kupenda ligi, usiku sio mahali salama! Kwa mtazamo wangu.
 
Saa zingine unatumia kauongo kidogo pale unapoombwa leseni. Unaweza kusema leseni umeisahau (sheria inakuruhusu kuipeleka kituo cha polisi ndani ya masaa 72), na wala hauendi mbali. Yaani safari yako ni ndani ya wilaya au mkoa husika uliposimamishwa na trafiki.

Ila kama kuna mfumo wa kupiga faini kwa kutumia namba ya gari, hapo inakuwa imekula kwako mazima.
 
Unafikiri ndio itaku save hio mbinu na wao wanajua ni uongo tu! Wanajuwa wazi unadanganya na hapo ndipo atapoanza kukusumbulia!
 
Wanadai wao wamenunua tochi! Sasa najiuliza kwa utaratibu huu kwanini tusijengewe high speed track pembezoni ili watu wawe wananunua speed tickets!

Badala ya kuanza kuchangishana shilingi 50 kwenye simu nilitegemea jambo kama hili liongelewe bungeni! Mie niko willing kulipa hata elfu 10 ilimradi tu nisikerwe na maaskari nikiwa safarini! Yani kwa hizi kero za rushwa na hongo kwa maaskari na kubambikiana overspeed notice ni bora kungekuwa na checkpoint maalum kuanzia Ubungo kwa Upande wa Morogoro road au Mwenge kwa upande wa bagamoyo road! Kutengwe bara bara maalum la highspeed way!
 
Kama nikiwa na hela za kuhonga matrafiki namwaga moto mchana tu! Wakikupiga cheti hewala tu
Nimeshawajulia.

Tafuta 5 za kutosha uwe nazo.

Hao wa highway hawana neno, 5 wanapokea, wengine wanakaza mpaka 10.

Mara ya mwisho nasafiri nilikuwa na 5 nyingi. Kwenye 50 najiachia wakinipiga mkono nawapa 5 wakikomaa nawapa 10.

Arusha ndo wanashupaza wakupige cheti.
 
Aisee inakuwaje mnasumbuliwa kiasi hicho?
 
Arusha lazma u graduate bila joho mzee baba😅😅😅
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…