Ushauri: Usiagize chochote nje ya nchi bila kujua gharama halisi za kodi na ushuru utakaolipia

Jun 1, 2021
99
125
Moja ya changamoto kubwa wanayokutana nayo wateja wetu ni kuagiza bidhaa kwa njia ya mtandao halafu kukutana na kodi/ushuru mkubwa wa kutoa mzigo pale Bandarini, Uwanja wa Ndege au mipakani.

Bei za viwandani (supplier) zinazowekwa mitandaoni huwa ni rahisi na zinavutia kuagiza. Mfano bei za magari, samani na teknolojia za kisasa zikiwemo simu, vishikwambi, kompyuta, washing machines na gadgets mbalimbali.

Tunashauri, kabla ya kuagiza bidhaa yoyote ile ni vyema kufahamu gharama halisi zitakazotozwa pindi mzigo utakapowasili nchini. Hii itasaidia kujua kama bajeti inaruhusu kuagiza mzigo husika kwa wakati huo au la. Ni busara kutumia ushauri au maelekezo kutoka kwa wakala wa forodha na wazoefu wa masuala haya (kama sisi) kwa msaada anuai.

Kwa takwimu zetu, tumeona wajasiriamali na wafanyabiashara wengi hasa wale ambao sio wazoefu wakipata hasara kutokana na kutomudu gharama za kuondosha mizigo yao bandarini au kulazimika kutumia pesa ambayo hawakuitarajia.

Swali fikirishi: Kwanini mizigo mingi hukwama bandarini? Kwanini baadhi ya watu au makampuni hutekeleza mizigo yao hadi kuishia kupigwa mnada?

worldlogisticsltd_162313443892349.jpg
 
Jun 1, 2021
99
125
Sasa mbona hata wewe hujatoa solution Nini kifanyike
Mkuu Ugumu.

Tumetoa ushauri kwa changamoto husika.

"Tunashauri, kabla ya kuagiza bidhaa yoyote ile ni vyema kufahamu gharama halisi zitakazotozwa pindi mzigo utakapowasili nchini. Hii itasaidia kujua kama bajeti inaruhusu kuagiza mzigo husika kwa wakati huo au la. Ni busara kutumia ushauri au maelekezo kutoka kwa wakala wa forodha na wazoefu wa masuala haya (kama sisi) kwa msaada anuai."

Je, ni solution ipi unayodhani tunapaswa kutoa zaidi? Karibu
 
Jun 1, 2021
99
125
Ameshatangaza biashara mwenzako

Hapana. Lengo letu ni kutoa ushauri kulingana na uzoefu wetu na hali halisi ilivyo. Tunaamini ushauri huu utasaidia kuwaepusha wanaoagiza bidhaa kutoka nje kuwa makini hasa wale wa mara ya kwanza. Hujawahi kusikia mizigo imetelekezwa hadi kupigwa mnada? Unadhani ni kwanini?
 
kijana13

JF-Expert Member
Sep 24, 2013
1,453
2,000
Kikuu naona ukinunua makadirio yako humohumo ndani...maana niliagiza mizigo ikafika bila matatizo ya Kodi nkapewa bila kutozwa chochote ...niliwatembelea silent ocen wakasema wao unalipa gharama ya kusafirishiwa mzigo ukifika unaenda chukua ..mwenye uzoefu na silient ocen atupe ...

Sent from my Infinix X657 using JamiiForums mobile app
 
Uko sahihi Kijana13, hata hivyo kuna tofauti kidogo hapo na tungependa kufafanua kama ifuatavyo:

1. Maduka ya Mtandaoni huambatanisha gharama za tozo na faida kwenye bidhaa utakazonunua kupitia kwao. Japo inapunguza mlolongo wa ufuatiliaji, lakini kuna ziada kubwa ya malipo mteja hufanya.

2. Kwanini ulipe pesa nyingi kwa kutumia mtu wa kati?

Njia sahihi ni kuwasiliana na wataalamu wakakushauri jinsi ya kununua bidhaa mwenyewe kutoka kwa supplier (sio intermediaries) kwani gharama zake huwa ni nafuu maradufu. Kwa mfano, sisi tunakushauri, kukuelekeza na kukusaidia kukokotoa gharama halisi za tozo za forodha kwa agency fee ndogo tofauti na ukitumia njia nyingine.

Aidha, kuepusha hofu ya kupoteza mzigo, kutapeliwa na kulipa gharama zaidi, tunawasaidia wateja kufuata mzigo moja kwa moja kutoka kwa supplier, kuclear na kuusafirisha hadi kwa mteja husika. Na hapa tunafanya kwa uwazi kupitia google excel spreadsheet ambayo inaonyesha movement ya mzigo tangu unatoka kwa supplier hadi unapokufikia.

3. Silent Ocean wanafanya kazi nzuri, lakini wamejikita zaidi China na Tanzania.
 
Ugumu wangu

JF-Expert Member
May 6, 2021
1,613
2,000
Mkuu Ugumu.

Tumetoa ushauri kwa changamoto husika.

"Tunashauri, kabla ya kuagiza bidhaa yoyote ile ni vyema kufahamu gharama halisi zitakazotozwa pindi mzigo utakapowasili nchini. Hii itasaidia kujua kama bajeti inaruhusu kuagiza mzigo husika kwa wakati huo au la. Ni busara kutumia ushauri au maelekezo kutoka kwa wakala wa forodha na wazoefu wa masuala haya (kama sisi) kwa msaada anuai."

Je, ni solution ipi unayodhani tunapaswa kutoa zaidi? Karibu
Ahsante Sana mkuu
 
Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom