TRA Tanzania
Member
- Jul 16, 2022
- 77
- 222
Kufuatia taarifa iliyoko katika mtandao wa Kijamii ikidai TRA imepandisha ushuru wa magari tunapenda kukanusha na kufafanua kama ifuatavyo;
1. Viwango vya kodi vinapitishwa na bunge na sio TRA.
2.Kodi hukokotolewa kwa kuzingatia thamani ya gari kwenye soko la dunia, gharama ya usafirishaji na bima. Ikiwa gari limenunuliwa kwa fedha za kigeni kiwango cha kubadilisha fedha cha siku husika kitatumika na sio ya wakati wa kuagiza gari hilo hivyo huenda ikatofuatiana na kiwango cha kikokotoo wakati wa kuagiza.
3. Umri wa gari unaweza kusababisha kodi ikaongezeka kutokana na uchakavu, kwa magari yaliyotengenezwa zaidi ya miaka 8 lakini haifiki miaka 10 kodi ya uchakavu ni 15% na gari lenye umri kuanzia miaka kumi na kuendelea tangu limetengenezwa kodi ya uchakavu ni 30%.
Kwa maelezo zaidi wasiliana nasi bure kwa simu namba 0800110016 au 0800 750075 au 0800 780078 siku ya Jumatatu mpaka Ijumaa kuanzia saa 2 kamili asubuhi mpaka saa 1 kamili jioni au tuma barua pepe kwenda huduma@tra.go.tz.
Pamoja tunajenga taifa letu
Imetolewa na: Idara ya Elimu kwa Mlipakodi na Mawasiliano