Mzalendo Uchwara
JF-Expert Member
- Jan 26, 2020
- 3,716
- 11,704
Facts
- Ni wazi kuwa wapinzani (wa kweli), wanaharakati, CCM Zanzibar, CCM wapenda mabadiliko bara na watanzania wengi kwa ujumla wao wanataka mabadiliko ya katiba ili kuondoa changamoto nyingi za kisheria na kiutawala zilizopo sasa.
- Ni wazi kuwa wazanzibari wengi (Mh. Rais akiwemo) wanatamani mabadiliko ya katiba ili kujaribu kutafuta ufumbuzi wa zinazoitwa kero za muungano.
- Ni wazi kabisa kuwa Rais Samia hawezi kuanzisha mchakato wa katiba mpya katika ungwe yake ya kwanza, itakuwa ni political suicide. Hivyo basi kuna uwezekano mkubwa zaidi wa kufufua mchakato akiwa katika ungwe yake ya mwisho (inshaallah).
- Ni wazi kuwa wapinzani wa kweli wamedhamiria kutoshiriki uchaguzi wowote nchini ambao utakua chini ya tume hii ya taifa ya uchaguzi (ya uchafuzi). Vilevile hawatoshiriki uchaguzi utakao simamiwa na ule mfumo kichekesho wa kusimamia uchaguzi wa serikali za mitaa kupitia waziri wa TAMISEMI. Jambo hili ni doa na hatari kwa ustawi wa nchi.
Ushauri
Lazima mchakato wa mabadiliko ya katiba uanzie mahali fulani, hivyo basi Mheshimiwa Rais nakuomba kwa unyenyekevu ukutane na wadau wote kwenye swala hili ikiwa ni pamoja na vyama vya siasa (hususani CDM), kisha mkubaliane kwa kuanza na marekebisho ya sheria ya uchaguzi ikiwa ni pamoja na kuirekebisha tume ya uchaguzi.
Hii itawezesha uchaguzi wa serikali za mitaa na uchaguzi mkuu 2025 kufanyika kwa uhalali machoni pa watanzania na jumuiya za kimataifa na vyama vyote vitaweza kushiriki. (Wewe Mheshimiwa sana utashinda ili uongoze kwa awamu ya pili).
Pia, CDM na wapinzani wengine watashinda viti vya kutosha bungeni na kwenye udiwani. Mheshimiwa Rais, utawahitaji sana watu hawa pindi utakapo fufua mchakato wa katiba mpya.
Hata wewe mwenyewe Mheshimiwa sana ukweli unaujua, upinzani wa mabadiliko ya katiba unaletwa na wana CCM wahafidhina kutoka Tanzania bara. Hivyo basi support ya vyama vya upinzani ni muhimu sana pamoja na ile ya wale CCM 'moderates' wa bara na CCM Zanzibar.
Kwenye hili lazima pande zote zikubali ku 'compromise' ili tupate pa kuanzia.