Ushauri: Nimpe zawadi gani mke wangu?

Ushauri: Nimpe zawadi gani mke wangu?

Mnunulie seti za dhahabu,
Hereni,
Cheni,
Pete,
Cha mkononi,
Cha kiunoni na miguuni (kama hua anavaa)
Ni vitu ambavyo atakua navyo siku zote na hata siku 'mkifulia' mtajua pa kuanzia (kidding)
 
Uzidishie UPENDO wa Dhati Tu

Mthamini Kama Mkeo Kipenzi Tena Mwaminifu Kwako

Ulimkuta Bikra?

Wewe ni mwanaume Wa Kwanza Kutoa Bikra Yake?

Bikra Ipi?

NAPITA Tu[emoji125] [emoji125] [emoji125]
Mkuu sina hakika 100% kama nimemkuta bikra. Ila nakumbuka cku ya kwanza kuingia kwake nilishawishika kwa kiasi kikubwa kwmb binti alkiwa bikra au kama kayumika ni zile za utoto utoto. [emoji4] LAKINI ubikra kwangu sio ishu kuubwa kivile. Mtu anaweza kuwa bikra na bado akaja kuwa shetani kwny ndoa.
 
Kwema lakini mkuu chifu77
 
Huu sasa ni ukorofi. mada za aina hii zinajadilika sehemu yoyote ile; iwe kijiweni, bar, hotelini, kwenye basi. Hata JF pia. Siku nyingine kabla hujaanza kukandya, toa kwanza ushauri mzuri ili tujue uwezo wako wa kufikiri uko juu au chini kiasi gani.
Kama ww mwenyewe umeshindwa kufikiri unadhani ni nani atakusaidia unaomba msaada hata zawadi ya kumununulia mkeo ina maana muda wote huo mlioishi hujajua mkeo anapenda kitu.
Kwa mtu muelewa zawadi ni zawadi tu hakuna zawadi ndogo hata kama utamununulia chupi atashukuru.
 
Hahaaa...kuna siku atakuja tena kuomba ushauri wa zawadi gani amnunulie mtoto wake maana amekuwa wa kwanza.....Huwa najiuliza kila siku ikiwa mambo ya kawaida sana kama haya (yaani ukae na mkeo 2-3 yrs usijue kitu anachokipenda??) mtu anakilimbilia JF watawezaje ku manage issues kubwa kubwa za kifamilia? Kila kitu kidogo break ya kwanza JF ina maana uwezo wa akili zetu umeshuka sanaa??
Ndo mana anamuona mkewe malaika mtakatifu....
 
Nimewahi kumnunulia. Ila nilipanga hii iwe bab kubwa. Tarehe 26 mwezi huu tunakamilisha miaka 8 ya ndoa yetu. Cku hiyo nitamtoa out na nitamshukuru kwa niaba yangu na ya watoto wetu 2 kwa UPENDO & JITIHADA zake.
Kumbe ulikuwa unajua cha kufanya
 
Zawadi inagusa pale inapogusa moyo wa mpokeaji kwa kujibu hitaji lake. Jibu la swali lako utalipata kwa mkeo ukimwendea kwa upelelezi mzuri. Maisha ya ndoa lazima uwe jasusi kiaina ili muda wote uweze kuikonga roho ya mwenzi wako.
Rejea story mbalimbali ya vitu anavyovitamani kuanzia nguo hadi gari. Ni mfuko wako tu. Zingatia rangi yake.
Unatakiwa ujue size.rangi.mshono au kama gari ndo usiseme.
Talk to her !!!
Wengine tunajua mpaka size za bra au hips au viatu rangi mpaka size ya kidole cha pete, hereni , mafuta na perfume.
Kwa kifupi mjue mkeo sisi hatumjui !!!
 
Mkuu nimetumia neno kutazama kwa maana ya kudadisi na kutathmini mienendo, upendo na bidii yake kwangu na kwa watoto. Pia nimeandika sina uhakika wa 100% wa wakati ujao. Ila kwa wakati uliopita na uliopo, anastahili kila kilicho chema kutoka kwangu.
Si kwa wakati ujao tu hata uliopita huwezi kuwa na uhakika wa 100% we sema unapenda tu
 
Zawadi inagusa pale inapogusa moyo wa mpokeaji kwa kujibu hitaji lake. Jibu la swali lako utalipata kwa mkeo ukimwendea kwa upelelezi mzuri. Maisha ya ndoa lazima uwe jasusi kiaina ili muda wote uweze kuikonga roho ya mwenzi wako.
Rejea story mbalimbali ya vitu anavyovitamani kuanzia nguo hadi gari. Ni mfuko wako tu. Zingatia rangi yake.
Unatakiwa ujue size.rangi.mshono au kama gari ndo usiseme.
Talk to her !!!
Wengine tunajua mpaka size za bra au hips au viatu rangi mpaka size ya kidole cha pete, hereni , mafuta na perfume.
Kwa kifupi mjue mkeo sisi hatumjui !!!
Nimekuelewa mkuu [emoji122] [emoji122]
 
Ni dalili zipi zinakufanya uamini hajachepuka

Si kwa wakati ujao tu hata uliopita huwezi kuwa na uhakika wa 100% we sema unapenda tu
Wakuu, nimemchunguza weee, nikampeleleza weee, nimefuatilia matendo na maongezi yake. Hana kona kona, hakuna hata kadalili ka usaliti. Na mbinu zangu za utafiti na udadisi naziamini. Sasa kwa nini niwe na wasiwasi. kwa miaka hii 8 huyu hajawahi kunisaliti.
 
Heshima kwenu wanajamvi. Mimi nimeoa na tumejaliwa kupata watoto 2. Mke wangu nimwaminifu, sijawahi kuona dalili zozote za kunisaliti; kwa kifupi hajawahi kuchepuka. Pia ana bidii sana katika kulea watoto wetu na ananitia moyo pale tunapopita ktk changamoto za kimapato au kijamii. huwa namshukuru kwa kuwa mke mwema na mama mzuri kwangu mimi na kwa watoto we2. TAKRIBAN mwezi sasa nafikiria nimpe zawadi gani? Ila bado sijapata jibu kwa sababu siwezi kumudu kitu kikubwa kama gari. NAOMBENI ushauri mwanamke wa aina hii anastahili zawadi gani?
inaonekana hujawajua vizuri hawa viumbe,waulize wenzio
 
Wakuu, nimemchunguza weee, nikampeleleza weee, nimefuatilia matendo na maongezi yake. Hana kona kona, hakuna hata kadalili ka usaliti. Na mbinu zangu za utafiti na udadisi naziamini. Sasa kwa nini niwe na wasiwasi. kwa miaka hii 8 huyu hajawahi kunisaliti.
Unafanya kazi gani
 
Back
Top Bottom