Ushauri: Nimpe zawadi gani mke wangu?

Ushauri: Nimpe zawadi gani mke wangu?

Hadi raha jamani!
Ni faraja kubwa pale mwenza anapoona mchango/bidii na loyalty iliyopo ndani yako na akatafuta namna ya kukuonesha kushukuru namna hii.
Hata kama utampa zawadi,nakushauri pia umlipe mkeo upendo na uaminifu kama vile yeye anavyokufanyia.
Sijui hata niseme nini cha zaidi,ila nimeipenda sana hii.
Kumbe kuna family zina upendo namna hii?Lucky you guys.
Yaa Raby nijaalie Mume kama huyu mimi pamoja na wanawake wenzangu....Aamin [emoji120] [emoji120] [emoji120]
 
Haya maneno ulioandika humu,mwambie usiache hata nukta.Hii ni zawadi tosha..
 
Inshaalah..
 
Haya maneno ulioandika humu,mwambie usiache hata nukta.Hii ni zawadi tosha..
Sawa mkuu. wadau wametoa michango iliyojaa busara na hekima, pamoja na kuungana na mimi kumpongeza my wife wangu. nadhani na yeye atajisikia vizuri kwa pongezi hizi.
 
Sawa, sina uhakika wa 100% wa Wakati ujao. Ila mpaka waleo hilo neno 'kumfuma' halipo. Kwa kutazama uaminifu wake tangu nimuoe, napata ujasiri wa kumuita mke mwema.
mkuu mtu yoyote ukimtazama kwa kumtazama huwezi kuona makosa yake...mtazame tena alafu tena alafu mchunguze ila jiandae na negative pia otherwise utajikuta ICU
 
mkuu mtu yoyote ukimtazama kwa kumtazama huwezi kuona makosa yake...mtazame tena alafu tena alafu mchunguze ila jiandae na negative pia otherwise utajikuta ICU
Mkuu nimetumia neno kutazama kwa maana ya kudadisi na kutathmini mienendo, upendo na bidii yake kwangu na kwa watoto. Pia nimeandika sina uhakika wa 100% wa wakati ujao. Ila kwa wakati uliopita na uliopo, anastahili kila kilicho chema kutoka kwangu.
 
Kapime DNA kwanza ujue km ni watoto wako halafu mpe zawadi ya mimba nyingine
 
Heshima kwenu wanajamvi. Mimi nimeoa na tumejaliwa kupata watoto 2. Mke wangu nimwaminifu, sijawahi kuona dalili zozote za kunisaliti; kwa kifupi hajawahi kuchepuka. Pia ana bidii sana katika kulea watoto wetu na ananitia moyo pale tunapopita ktk changamoto za kimapato au kijamii. huwa namshukuru kwa kuwa mke mwema na mama mzuri kwangu mimi na kwa watoto we2. TAKRIBAN mwezi sasa nafikiria nimpe zawadi gani? Ila bado sijapata jibu kwa sababu siwezi kumudu kitu kikubwa kama gari. NAOMBENI ushauri mwanamke wa aina hii anastahili zawadi gani?
Mnunulie vitu vinne tu lakini kila kitu hapa kitampa kumbukumbu kwenye maisha yake ya kila siku atakapokuwepo. Na kuwa muaminifu zaidi juu yako
1) Herini za Dhahabu
2) Kidani cha Dhahabu
3) Saa nzuri yenye samani
4) Pete mpya ya ndoa yenye samani kuliko ya mwanzo
Hivi vitu unaweza kuona vidogo lakini vina samani zaidi ya gari au smartphone. Samani yake kila akiviangalia hukukumbuka wewe kwani sio wanaume wengi wenye kufanya vitu hivyo pia anapokwenda huwa navyo humuondolea hata hamu ya kutaka kuchepuka na mtu mwengine kwenye maisha yake. Usisahau unapompa hivyo vitu mnunulie roses na chocolate ukimpa mpige na kiss na kumwambia maneno ya upendo.
 
Kapime DNA kwanza ujue km ni watoto wako halafu mpe zawadi ya mimba nyingine
Wala haihitajiki dna hapa. Watoto wamefanana na mimi utadhani nimeji-print mwenyewe. Kuanzia sura, kichwa, urefu mpaka masikio.
 
Mnunulie vitu vinne tu lakini kila kitu hapa kitampa kumbukumbu kwenye maisha yake ya kila siku atakapokuwepo. Na kuwa muaminifu zaidi juu yako
1) Herini za Dhahabu
2) Kidani cha Dhahabu
3) Saa nzuri yenye samani
4) Pete mpya ya ndoa yenye samani kuliko ya mwanzo
Hivi vitu unaweza kuona vidogo lakini vina samani zaidi ya gari au smartphone. Samani yake kila akiviangalia hukukumbuka wewe kwani sio wanaume wengi wenye kufanya vitu hivyo pia anapokwenda huwa navyo humuondolea hata hamu ya kutaka kuchepuka na mtu mwengine kwenye maisha yake. Usisahau unapompa hivyo vitu mnunulie roses na chocolate ukimpa mpige na kiss na kumwambia maneno ya upendo.
Nashukuru mkuu... sikuwa nafahamu kwamba vi2 hivi vitakuwa na impact kubwa ktk maisha yake. Walahi nitazifanyia kazi.
 
Kaa naye katika muda ulio tulia na mahali palipo tulia mweleze kile ulichonacho moyoni mwako na furaha iliyopo moyoni mwako juu yake kwa hisia za ndani kabisa ya moyo wako nayo itakuwa zawadi nzuri sana moyoni make huku ukisindikiza na neno, " nakupenda mke wangu, wewe ni wa thamani sana kwangu" . kwa haya utakuwa umeufurahisha sana moyo wake.
 
Maneno mazuri tu kwa mke wako yanatosha kuwa wewe mwenyewe ni zawadi kwake kutoka kwa MUNGU, furaha yake ikazidi kuliko sasa.
 
Back
Top Bottom