Heshima kwenu wanajamvi. Mimi nimeoa na tumejaliwa kupata watoto 2. Mke wangu nimwaminifu, sijawahi kuona dalili zozote za kunisaliti; kwa kifupi hajawahi kuchepuka. Pia ana bidii sana katika kulea watoto wetu na ananitia moyo pale tunapopita ktk changamoto za kimapato au kijamii. huwa namshukuru kwa kuwa mke mwema na mama mzuri kwangu mimi na kwa watoto we2. TAKRIBAN mwezi sasa nafikiria nimpe zawadi gani? Ila bado sijapata jibu kwa sababu siwezi kumudu kitu kikubwa kama gari. NAOMBENI ushauri mwanamke wa aina hii anastahili zawadi gani?