Ushauri: Nataka ninunue baiskeli kwa mazoezi na safari fupi fupi

Mad Max

JF-Expert Member
Oct 21, 2010
19,095
49,895
Wakuu kwema.

Mkazi wa Dar, nataka ninunue baiskeli kwaajili ya mazoezi na siku moja moja hali ya hewa ikiwa nzuri natumia kwenda nayo kazini (3KM kutoka nyumbani).

Naomba ushauri wenu, kwa budget ya mwisho Laki 1.5 naweza kupata aina gani ya baiskeli? Itatosha au niongeze?Je kuna brand ya kuzingatia? Kwa Dar es Salaam ni wapi nitapata kwa bei nzuri na imara? Nategemea kununua used, iwe kama hii kwenye picha (sio 100%) kama hii ila muundo huu, sio zile sewa.

images (9).jpeg
images (8).jpeg

Unavyonunua baiskeli naambiwa kuna size, je ni size ya matairi au? Mimi nina urefu wa cm 190 hivi je size hani itanifaa.

Nimeona nitafute basikeli kwasababu kazi yangu muda mwingi nakua nimekaa, hafu kila nikijaribu kwenda gym nashindwa kua na ratiba nzuri u akuta baada ya week naacha kwenda, na pia nataka hobby mpya.

Shukrani.
 
FEEDBACKS

WAKUU.
Asanteni nimeenda Tandika Nimenunua Baiskeli leo (jumamosi) bei 250k Size 26.

Nina mzuka sana ata sijaifunga sema mvua inazingua, kesho naenda kuzurura nayo Bagamoyo.

PXL_20240323_122204926.jpg
PXL_20240323_122227087.jpg


Tyre la mbele nimetoa ili itoshe kwenye buti. Inafungwa na spana no. 15 very simple.
 
FEEDBACKS

WAKUU.
Asanteni nimeenda Tandika Nimenunua Baiskeli leo (jumamosi) bei 250k Size 26.

Nina mzuka sana ata sijaifunga sema mvua inazingua, kesho naenda kuzurura nayo Bagamoyo.

View attachment 2942599View attachment 2942600

Tyre la mbele nimetoa ili itoshe kwenye buti. Inafungwa na spana no. 15 very simple.
Hongera sana! Mimi natumia baiskeli aina ya AMACO OASIS SE saizi 28.
 

IMG_20240220_193407_979.jpg
karibu kwenye chama chetu cha waendesha baiskeli... mnyamA huo hapo nilinunua 140,000/= ikiwa used.
shida ya hizi baiskeli za mtumba kifaa chake kikiharibika huwezi kupa exactly cha kufanana nacho.

baiskeli hiyo ilikuja na mipira myembamba sana, na spoket ya nyuma ilikuwa na gia 9. hii chombo ilikuwa inakimbia vibaya.

kizuri zaidi break zilizo kuja na hii bike zilikuwa za papo kwa hapo. popote una simama, hizo break zilipo isha siku wahi kupata break kama hizo.

matairi yalipo isha pia siku pata kama yale yalo kuja na baiskeli.

baiskeli hii nilikuwa naitumia kila siku kutoka Tabata, kisukuru kwenda mikocheni... kipindi kile cha korona. nilikuwa nainjoy sana...! nilikuwa natumia dakika 25 ha 35...! niliepuka hadha ya foleni na kugombania daladala...!

siku hizi nimekuwa mtu wa mapiki piki baiskeli nimeitupa...!
 
Back
Top Bottom