Dr Mathew Togolani Mndeme
JF-Expert Member
- Aug 2, 2010
- 201
- 808
Ushauri wa barakoa na mkanganyiko wake
Jana Marekani na Uingereza, ambazo ni nchi zenye nguvu kiuchumi na kuongoza katika ugunduzi na tafiti za kisayansi, zimetoa kauli zinazokinzana kuhusu uvaaji wa barakoa (masks) kama njia ya kujikinga na maambukizi ya ugonjwa wa Corona kwa mtu ambaye hajaambukizwa (mass masking).
Nina hofu kwamba maamuzi yao (hasa ya Marekani) yanakwenda kuongeza taharuki Afrika katika janga la Corona. Hii ni kwa sababu hadi sasa ushahidi unaonesha kwamba nchi nyingi Afrika zinaparamia mapendekezo au maamuzi yanayochukuliwa na nchi za Maghararibi bila kutazama mazingira ya utekelezaji wake katika nchi zetu.
Walichokisema kinaweza kabisa kuchukuliwa kama ushahidi wa kisayansi na nguvu zote zikahamishiwa kwenye uvaaji wa barakoa. Naomba nielezee mkanganyiko huu kwa kifupi, maana yake na tunavyoweza kuutumia.
Hadi juzi, taasisi ya udhibiti wa magonjwa ya Marekani (CDC) walikua na msimamo kwamba uvaaji wa barako hauna msaada kumkinga mtu kupata maambukizi. Ila jana walisema watapitia upya mapendekezo (recommendations) yao maana kuna dalili kwamba zinaweza kuwa na msaada. Leo wameibuka na mapendekezo mpya kwamba watu wanaweza kuvaa barakao zisizo za tiba kama njia ya kujikinga na maambukizi. Hata hivyo rais Trump yeye kasema hatava barakoa maana hayo ni mapendekezo tu.
Wakati huohuo, serikali ya Uingereza imeendelea na msimamo uliokua unajulikana katika viunga vya wanasayansi kwamba hakuna msaada kwenye kuvaa barakoa kwa mtu mzima. Katika kuweka msisitizo, wamesema wamewasiliana na watafiti wenzao kule Hong Kong (watu wanaposingizia barakoa zimesaidia) na wamewathibitishia kwamba hakuna ushahidi wa kisayansi kwamba zina msaada.
Nini msingi wa hoja za kisayansi kwa jambo hili?
Tangu maambukizi ya Corona yaliposhika kasi, kumekua na mjadala mkubwa wa matumizi ya barakoa kama moja ya vitu vinavyoweza kusaidia mtu kujikinga na maambukizi. Baadhi ya wanasayansi/watafiti wamekua wakijenga hoja kwamba barakoa zina msaada na hivyo watu washauriwe kuvaa. Hata hivyo nchi nyingi pamoja na Shirika la Afya Duniani (WHO) wamekua wakishauri kwamba uvaaji wa barakoa hauna msaada kumkinga mtu anayehudumia wenye maambukizi pekee (TAZAMA HAPA). Wanashauri parakoa kuvaliwa na mwenye maambukiki kupunguza uwezo wake wa kusambaza virusi anapokosa, kuongea au kupiga chafya.
Ukiachilia mbali hoja za kisayansi, wanananchi wa kawaida wamekua na mtizamo kwamba barakoa zinazuia kuambukizwa Corona. Fikra hii inahusishwa na ukweli kwamba tangu Corona ilipoanza kilichokua kinaonekana kule China ni watu waliozivaa kila mahali. Hii ikachukuliwa moja kwa moja kwamba ile ni kinga ya Corona. Ila ukweli uliopo ni kwamba uvaaji wa barako kwa China na hata Hong Kong ni utamaduni wa kila siku unaosababishwa na uchafuzi mkubwa wa hali ya hewa. Barakoa zinajulikana kitaalamu kwamba zina uwezo wa kusaidia kupunguza uvutaji wa hewa chafu. Hivyo kule China kutokuvaa barakao hasa kwenye miji mikubwa inachukuliwa kama uzembe (being irresponsible). Corona imewakuta wachina wakivaa barakoa na sio kwamba barakoa zimeanza kuvaliwa kama kinga ya Corona.
Lakini hata tukichukulia kwamba wachina walizivaa kujikinga na Corona, bado sio njia sahihi ya kuhitimisha kwamba ni kinga. Tukumbuke wao walipata ugonjwa huu wakiwa hawajui unatoka na nini na unaambukizwaje. Hivyo kwa taharuki waliyokua nayo walijaribu kila njia kutafuta kujikinga bila kujali njia hizo zina tija au la kwa sababu mwenye njaa hachagui chakula. Ila kwa sasa ulimwengu una uelewa mpana kwa kiasi fulani kuhusu ugonjwa wa Corona na unavyoenea hivyo sio sahihi kuendelea kuchukua hatua kwa taharuki au kubahatisha iwapo kuna nafasi ya kutumia akili na ushahidi wa kisayansi.
Kuna machapisho mengi ya kisayansi yanayojadili jambo hili ila katika ujumla wake, yanakubaliana kwamba hadi sasa hakuna ushahidi wowote wa kitafiti kuthibitisha kwamba barakoa zina uwezo wa kumkinga mtu mzima na maambukizi ya Corona. Kama zingekua kinga, ni wazi China wangeweza kuudhibiti ugonjwa mapema sana maana wao kuzivaa ni utamaduni. Pia nchi ambazo zinavaa kwa wingi kama Hong Kong na Korea zisingekua zinatoa taarifa ya wagonjwa wapya na vifo kila siku kama tunavyoona. Wanasayansi wanaotetea uvaaji wa barakoa, wanasema kutokuwepo kwa ushahidi wa kwamba zinasaidia, haimaanishi kuwa ni uthibitisho wa kutokua na msaada. Nikitafsiri hoja yao katika mazingira yetu nitasema: wewe ukisema hujawahi kuona paka anayepaa, haiwezi kutumika kama ushahidi kwamba hakuna paka anayepaa. Inawezekana kabisa tukiendelea kuchunguza paka wote tukakuta yuko anayepaa.
Nini ushahuri wangu?
Nina mambo makuu mnne ya kugusia kwenye jambo hili kama ushauri.

- Hakuna ushahidi kwamba barakao zinasaidia kujikinga na maambukizi. Haijalishi nani katoa mapendekezo, ila kisayansi na tiba, maamuzi hata kama yanaonekana ni mazuri kama hayana ushahidi wa kutosha wa kitafiti. Sio mapendekezo yote yanatumia ushahidi wa kisayansi. Mengine yanatolewa kulingana na mazingira hasa watu wanapokua kwenye taharuki au hawana njia mbadala ya kuitegemea. Tusichukulie mapendekezo ya CDC kama vile ndio amri ya 11 tukaanza kukimbizana na barakoa tukazua mengine na tija tusipate. Bado nafuatilia kujua CDC wamechukua ushahidi gani kufikia mapendekezo haya (bado natafuta desa walilotumia).
- Kuna baadhi ya tafiti za kisayansi zimeonesha kwamba uvaaji wa barakoa kwa wananchi (mass masking) unaweza kuwa na msaada wa kisaikolojia. Bila kujali kwamba zina kinga au vinginevyo, tafiti zimeonesha kuna watu hujisikia salama au wamekingwa kwa kiasi fulani wao wenyewe wanapokua wamevaa barakoa au/na watu wengine wanaowazunguka wamevaa pia. Hivyo, kwa kuwa jamii nzima ina taharuki na madhara ya kisaikolojia ya ugonjwa huu ni makubwa sana, tiba ya kisaikolojia inahitajika pia. Hivyo, kama mtu au watu wanajisikia salama zaidi wakivaa barakoa, wavae na watu wengine wasiwashangae wala kuwakosoa wakizivaa.
- Ninafahamu serikali inafanya kazi kubwa ya kutoa elimu hukusu mlipuko wa Corona. Ila ninawashauri wahusika waendelee kutoa elimu zaidi kwenye eneo hili kuhusu uhalisia wa msaada wa barakoa. Walizungumzie katika dhana ya kinga (based on existing scientific evidence) na katika dhana ya tiba ya kisaikolojia (mitigating psychological effects). Watu wajue kwamba sio lazima kuvaa lakini kama wanaona kuvaa kunawapa amani ya moyo zaidi, basi wavae. Elimu hii ni muhim sana kwani iwapo watu wengi watazivaa huku wakiwa hawana uelewa wa kitaalamu wa namna bora ya kuzivaa, kuzitumia, kuzitunza, na usafi wake, ni wazi zinaweza kuwa sababu ya maambukizo zaidi au kuleta madhara mengine ya kiafya.
- Kwa kuwa Marekani wamebadilisha mapendekezo yao, na tunajua nguvu yao kwenye taasisi ya kimataisa, kuna uwezekano mkubwa kabisa kwmaba WHO nao watabadilisha mapendekezo yao na kuhamasisha uvaaji wa Barakoa. Jana nimesikia afisa mmoja wa WHO akikaririwa kusema nao watapitia upya mapendekezo yao kuhusu barako baada ya Marekani kubadili. Tusishangae tukiona nao wanaaza kutushawishi kuvaa barakoa. Bado tukumbuke, sio kila mapendekezo tupewayo ni sahihi na yatatekelezeka.
Imeandikwa na MM Togolani (mmtogolani@gmail.com)
Mtafiti wa mifumo ya digitali katika ufuatiliaji na udhibiti wa magonjwa