Pole sana, kuna wanandoa Mume amelazimika kujitenga chumba ksb ya uchafu Wa mkewe. Mkewe ni mchafu nahis kupita huyo Wa kwako, Ila ksb anampenda sana hajamwacha alichofanya ni kujitenga chumba ili aondokane na baadhi ya uchafu Wa mkewe.
Chumba chake na usafi wake Wa chumba anamtegemea house 100%.
Wakitaka tendo LA ndoa, mume anamwambia mkewe lazima akaoge apige mswaki ,nguo atazokuja na chumbani ziwe zimefuliwa ndipo wanalala wote chumba cha mume, match ikiisha Mke anarudi jalalani (chumbani) kwake.
Mke ni mchafu zaidi ya wachafu, Ila ana uzuri Wa asili Wa mwonekano na umbo. Mume anasema amemwachia Mungu anasubiri muujiza tu, Ila hawezi kumwacha ukizingatia wana watoto, pia kikubwa anampenda.
Tafuta njia nzuri ya kuweza kumsaidia, Ila kama ni asili yake yake hawezi kubadilika, labda kwa muujiza.
Mume wake ni msafi sana, imebidi aingie gharama yakuajiri house gal 3 ili kuficha aibu ya mkewe ya mazingira ya nyumbani. Ila usafi wa mwili wamkewe ameshindwa ksb anaweza kaa siku hata 4 hajaoga tena hali ya hewa ya Dsm.
Ila mzuri sana kwa mwonekano wa nje, ila uchafu alionao nahisi anaweza shida kama atashindanishwa na wachafu wenzie. Pole sana