KIM KARDASH
JF-Expert Member
- Sep 21, 2011
- 5,139
- 1,139
- Thread starter
- #101
Mwalimu KK na wengine,
Mkaisome tena KATIBA ya sasa ya JMT muielewe. Rais wa JMT anaweza kuunda na kuendesha serikali bila ya chama chake kuwa na Wabunge wengi.
-Anao Wabunge 10 wa kuteua yeye mwenyewe kama Rais.
-Serikali inaendesha mambo yake mengi bila kutafuta ridhaa ya Bunge ikiwemo kusaini mikataba mbalimbali.
-Teuzi nyingi za Watendaji wakuu serikalini ni zake yeye mwenyewe na hazithibitishwi wala kuhojiwa na chombo kingine chochote mbali na uteuzi wa WAZIRI MKUU.
-Mchakato wa Bunge kumpigia Rais kura ya kutokuwa na IMANI naye ni mrefu na mgumu kwelikweli.
-Ni rahisi mno Rais kulivunja Bunge na serikali ikaendelea kuwepo.
CHADEMA, tafuteni kwanza URAIS wa JMT haya mengine mtayapata kwa ZIADA. KK haijui katiba yetu.
kuna kitu kimoja unakwepa sana kukizungumzia;upatikanaji wa mtendaji mkuu wa shughuli za serikali-waziri mkuu,hebu tueleze kwa mujibu wa katiba ambayo wewe mwenzetu umeisoma vizuri tunampataje pm na spika?