Ndio unaamka nini mzee?mbona nimeshajieleza sana ninachomaanisha.Ok ntakusaidia,kujikita kwenye ubunge ni kupigana kufa na kupona na kuwekeza nguvu nyingi kwenye harakati za ubunge ikiwa ni pamoja na kuhakikisha mnakua wa wagombea kila kona ya nchi hii,hapa intention yenu inakuwa ni kuwapata wabunge wengi kadiri mtakavyoweza kuvipita vyama vyote,na hili linawezekana kabisa mkijipanga sawasawa na kuachana na ndoto za urais kwanza,kila mwanachadema aimbe nyimbo ya ubunge na wabunge tu;mkifanikiwa kupata wabunge wengi maana nyie ndio mtakua na jeuri ya kuunda serikali kwa kuwa kwa mujibu wa katiba chama chenye wabunge wengi ndio kinachounda serikali sio chama chenye mgombea urais aliyepata kura nyingi,upo hapo kwanza???
Sasa basi mkishakua kwenye nafasi hiyo ya kuunda serikali ndio mnamchukua huyo mpendwa wenu bwana Slaa ambaye kwa kuwa nae atakua hakugombea urais kama mnavyopenda bali ubunge kama ninavyoshauri hapa mnampendekeza awe waziri mkuu kwa kuwa wakati huo atakua na sifa za kuwa waziri wetu mkuu,katiba yetu inasema waziri mkuu atapendekezwa na hatimaye kuidhinishwa na bunge kutoka miongoni mwa wabunge waliogombea na kuchaguliwa majimboni(wabunge wa kuteuliwa au viti maalum hapa hawatoki).N a kwakuwa bungeni sasa tuna uhakika kwamba tuko wengi ni wazi jina la slaa likienda bungeni litapita na ataapishwa kuwa waziri mkuu ambae atakaa na rais kuuunda baraza la mawaziri ambalo kutokana n wingi wa wabunge mliowapata mawaziri wengi kama sio wote watatoka chadema,kumbuka kwamba wakati huo huo wingi wa wabunge utawapatia pia spika na naibu spika ambao wanachaguliwa na wabunge!!je mpaka hapo rais amabe sio wenu atakua na kazi gani zaidi ya kuzindua kampeni za upandaji miti na mambo ya mazingira kwa kushirikiana na makamu wake.
Cha kwanza slaa akiingia madarakani kama waziri mkuu mtendaji anaichukua hazina na serikali za mitaa zinakua chini ya ofisi ya waziri mkuu!uchaguzi unaofuata urais ndio utakua unaitafuta chadema sio chadema kutafuta urais kutokana na kazi ambayo atapiga slaa kama waziri mku kila mtu atampenda na akisimama kwenye kugomea urais hamtakua na haja ya kukodi helkopta imzungushe kama mtalii,kazi itakua rahisi,ni strategy tu hakuna uchawi wala nini hapa lakini mwisho wa siku kupanga ni kuchagua kazi kwenu sisi wengine kazi yetu ni kuuza maneno tu utekelezaji ni kazi yenu makada wa chadema,japo nashangaa hapo juu wewe kada wa chadema unanituma mimi nikafanye kazi zako kuwashawishi wapiga kura wakichague chama wakati wewe umestarehe hapo kwenye computer yako ukiamini utaleta mabadiliko kwa ku type through keyboard,haiwezekani mzee ,anza sasa,jasho jingi wakati wa amani damu chache wakati wa vita,mkianza mapema kwa kuanzia Arumeru kumsindikiza mzee wangu slaa wakati wa uchaguzi mkuu kazi itakua nyepesi sana ndio maana yangu kuwataka mtoke jasho sasa ili wakati wa uchaguzi mkuu msipigike sana kuwanaadi wagombea ubunge wenu.