Ushauri: Adhabu gani inamfaa mtu huyu

Ushauri: Adhabu gani inamfaa mtu huyu

Status
Not open for further replies.
Pole kwa yaliyokukuta na nikuambie kitu Kimoja umekosea kusema wanaume wote ni MBWA wapo wenye utu wao Kama sie hapa sema unapopatwa na janga Kama hilo ni rahisi kuchukia jinsia husika!! Kuhusu swala lako Kama umeshindwa kbs kusamehe kuna njia moja nzuri Sana ya junk imeisha na yeye abakie na Siri inayoimuumiza Kama wewe!! Kisasi chochote ni gharama na inaweza kupelekea kifo chake au chako pia!! Ushauri Hakuna njia ya kulipa Kisasi Kama kumuonyesha kua tendo alilofanya linamaumivu!! Sawa ni aliwe TIGO na ajue ni wewe muhusika, tafuta pesa na tafuta watu wakifanya hio shughuli na apigwe picha huku unashuhudia!! Ukisema umuue hata wewe utakufa na roho yake itakulilia daima!!
 
Pole dada, kuua haitamaliza tatizo kuwa ulibakwa sanasana itakufanya usijisikie guilty. Jaribu kuwaona wanasaikolojia watakusaidia namna utakayoweza kuishi with the reality.
 
Dada, pole. Hapo hakuna kusamahe malipizi muhimu..
Ehe , naona kauli ya wanaume ni ma mbwa imewauma...huo ndo ukweli..yu mem your dooo....g!!!
Vp ile yakwenu ya wanawake wote wanajiuza??
Eee?? Mkuki kwa nguruwe....
Tena watu (wanaume) mliifurahia kwa nguvu zote...
Msj sent
 
Me nimsicha mwenye umri wa miaka 25-30. Kwetu ni kijijini ila kwa sababu ya shule ikanilazimu nije mjini nikawa naishi na ndugu zangu na sasa nina bachelor degree namshukuru Mungu. mimi si mwandishi mzuri samahani kama nitawakwaza.

Katika maisha yangu ya kuishi na ndugu nimepitia natatizo mengi sana ila kuna moja natamani kulipiza kisasi kwa namna inavyoniumiza . wanajamvi najitahidi sana kusahau lakini hii siku sitahisahau kuondolewa usichan wangu bila idhini yangu na mtu ambaye namwita baba mkubwa… wanaume ni ma. M.b.w.a

Nilihamia nyumbani kwa dada wa mama yangu ( ma mkubwa) nikiwa na umri wa 15 nilipoamia tu nyumbani kwake wakati huo nipo form two kwa ajili ya shule sitaki kutaja eneo ni kama miaka 8 sasa, mume wa mama yagu mkubwa akawa ananitaka kimapenzi wakati huo sijui hata mwanaume hapo kanifuatilia mdamrefu sana nIkataa. Kwa akili yangu ya kitoto nilimweleza mam yangu mkubwa mambo anyonifanyia baba nikaishiwa kutukanwa na kutengwa na ndugu pia wakiamini mimi natakakuvunja ndoa yao kama mzee alivowaeleza hapo ndipo mzee akapata nafasi nzuri.

Katika kupambana na hali hiyo siku moja nikiwa likizo naoga ili niende tution akaja akanivizia akanikuta naoga akanibaka . nilipata maumivu makali sana nilikaa kimya bila kumweleza mama yangu mkubwa ni siri yangu nawapa ninyi wnajamii mnisaidie kwa sasa siyo siri tena,

Nilishindwa kumweleza mtu huyo mzee alitengeneza mazingira ya me kukosa msaada hata kwa wazazi wangu kwa kisingizio me ni mvivu kusoma, ki ukweli sikua hivyo, basi ndugu jamaa na marafiki wakaniweka mbali nikiwa nipo mwenyewe sina msaada ndipo alipoweza timiza adhima yake.

Huyu ndiye mwanaume alinitoa bikra kwa ukatili huku nikipigwa na matusi juu mmh wanaume ninyi ni wanyama, tokea wakati huo nimeshakuwa na boyfriend zaidi ya 2 lakini nawaona makatili zaidi pale wanapoomba mzigo najikuta nachukia na nawachukia, pia nikiamua kuwapa basi tu kuondoa kero na sijawahi ona hiyo kitu furaha ya kufanya huo unyama zaidi ni matatizo na kero, tatizo kubwa nalo kutana nalo ni kupata mchubuko wakati wote nao fanya huo unyama. Wanaume nawachukia sana...............

Sasa ni hivi ni adhabu gani naweza mpa huyu mtu moyo wangu uridhike? Adhabu ninayoona inamfaa ni kumwondoa duniani nimeshajaribu mara nyingi nashindwa embu nisaidieni? Nataka nimuone anateseka kama mmimi nilivyoteseka na navyo teseka,….

natanguliza shukrani zangu,,,
kama sisi wanaume ni mbwa basi wewe ni mbwa jike
 
Pole. Kama unaweza kumwadhibu bila kupata madhara do it. Do it. Mtanisamehe kwa huu ushauri kwa kuwa hata mimi kuna mtu nimemweka kwenye mabano.
 
Bi mkubwa habari yako.

Hebu jaribu kutuliza akili yako na roho ya kulipiza kisasi na ile ya mauaji itulie.

Hivi jaribu kujiuliza jambo moja, unataka kumuua mwanadamu mwenzako je wewe ndiye uliyempa pumzi ya uhai?

Maisha na uhai ni zawadi mtu apewayo na Mungu wala hakuna mwanadamu awaye yoyote mwenye hati miliki ya pumzi ya mwanadamu mwenzake.

Kosa lililofanywa na Baba yako Mkubwa lisikufanye uingie kwenye laana ya kutoa uhai wa mwanadamu mwenzako. Je unakumbuka jinsi Kaini alivyopata maapizo toka kwa Mungu pale alipomuua nduguye?

Nikiachana na hilo sasa naelewa kwa nini katika ule uzi wa juzi wa yule dada aliyeeleza kuwa huwa hana hamu ya mapenzi, nawe ulichangia vile ulivyochangia.

Kumbe historia yako iliharibiwa mahali fulani na imepelekea mfumo wako mzima wa mahusiano kuharibika.

Ili uutibu moyo na akili yako inakubidi uamue kupadilisha namna unavyowachukulia wanaume.

1. Baba yako mkubwa hawakilishi wanaume wote duniani, wakati wewe unamuona ni mbaya lakini upande wa pili mkewe anamuona ndiye mwanaume bora kuliko wote duniani.

2. Waungwana husema kwamba, 'Kila shetani huwa na mbuyu wake'. Bi mkubwa inakupasa uanze kuamini kuwa kuna mwanaume mmoja ambaye aliumbwa kwa ajili yako naam kwa ajili ya moyo wako.
Mwanaume huyo kwa namna nyingine huwa hatokei kama nafsi, moyo na akili yako havijaanza kumuumba na kuamini katika njia ya chanya.

3. Jifunze kusamehe kama ambavyo wewe unavyosamehewa na wale waliokukosea.
Jaribu kujiuliza maishani mwako ni wangapi huwa unawakosea na makosa ambayo hao watu wanatamani walipize kisasi lakini watu hao wamekusamehe!!

Mwisho;
Usiache abadani kuomba, kusali na kuifuata njia ya Mungu katika maisha yako.
Kwa sisi Wakristo sina uhakika kama nawe ni miongoni mwetu, huwa tunaamini Mungu ndiye pekee anayelipiza kisasi kwa adui zetu.

asante watu8 kwa ushauri mzuri umenipa wakati mgumu kwa maneno hayo uliyoniambia nashukuru sana ni kweli kwa yote uliyosema nadhani sipo sahihi. but how can i forget this thing?
 
asante mamy! nimeshamwambia nitamfanya kitu na nitfanya tu,
mimi nilishawai kubakwa ila nilibakwa kwa hiari yangu so naelewa kidogo uchungu ulionao!
wewe cha kufanya sasa hivi msamehe tu huyo mbuzi maana ni too late na hao maboy wako huwafeel cause huwapendi na wao hawako lovely kivile..wamwage..ujue ukiwa na historia mbaya ya mapenzi halafu ukampata mtu kimeo unaweza kujichukia hata wewe mwenyewe wewe tulizana kwanza
 
Pole miss chagga
Tafadhali usimuue, hata umia wala jutia chochote.
Jitongozeshe huku umewaandaa wahuni uliowalipa. Akitia team basi wanaume wamfanyizie huku akirekodiwa na kupigwa picha.
Baada ya hapo uanze kum-black mail kuwa utazitundika picha kwenye mstimu wa umeme mtaani au kuwapa global publishers au kuziweka video rahatupu iwapo hata kupa mshiko utakao mtajia wakati huo.
Fanya ivo mpaka utakapojenga nyumba yako na kupata ka-vits au kabajaji ka kukuweka mjini.
 
Last edited by a moderator:
m bwa mwenyewe.
Nalog off

dada anahaki ya kusema hivyo kama kweli alitendewa hivyo ,mi mwenyewe nina demu ambaye alibakwa nilitaka kumuacha wanajf wakanishauri mpaka sasa nadumu nae ,hii nikama vita sio muda wakuoneana huruma dada fanya kweli ukimuacha atabaka mdogo wako ,u must b akiller 4 one people,
 
Hata yesu wanafunzi wake walimuliza tu tumie pangazetu akawa acha watumie badae akasema ya tosha,pia pale msalabani alisema baba wasamehe maana hawajui walitendalo lakini huyo babamkubwa alikua hajui alitendalo kweli au alikuwa amelewa au nimgonjwa wa akili kama sio basi msamaha miss chaga utoe kwa jicho la tatu ,
 
Pole sana ila wanaume wote siyo wabaya wapo wabaya na wazuri mimi ushauri wangu achana nae mungu atakulipia hapa dunian
 
Unyama haulipwi kwa unyama. Mshitakie Mungu wako na uishie hapo ila fuata ushauri wa Heaven on earth ili uondokane na kuona tendo la kufanya mapenzi ni unyama, vinginevyo hata ukipata bahati ya kuolewa hutafurahia tendo hilo maana kila utakapokuwa unalifanya utakumbuka siku uliyobakwa na hivyo kutolifurahia kabisa na kukosa raha (Utamu) inayohusiana na tendo hilo.
 
Last edited by a moderator:
Kwa nini anitese hivi .

Pole sana binti..

Huyo baba anakutesa kwa sababu hujataka kutafuta tiba....

Kwani ukipata ajali ukakatika mguu ndo unaamua kunywa sumu??

Basi chukulia hilo suala kama ajali na utafute tiba ili usonge mbele..

Kwa maelezo yako, ukishamuua Baba mkubwa utagundua kwamba kuna wanaume wengine wakatili nao utataka kuwaua...sasa utaua wangapi??

Hebu jiue mwenyewe, kwa kutafuta tiba na kulivua hilo gamba linalozidi kukukaba....

Babu DC!
 
Dada, pole. Hapo hakuna kusamahe malipizi muhimu..
Ehe , naona kauli ya wanaume ni ma mbwa imewauma...huo ndo ukweli..yu mem your dooo....g!!!
Vp ile yakwenu ya wanawake wote wanajiuza??
Eee?? Mkuki kwa nguruwe....
Tena watu (wanaume) mliifurahia kwa nguvu zote...
Msj sent

heh! Kumbe hii ni vita kati ya ke na me? Nilikuwa sijui!
 
Status
Not open for further replies.
Back
Top Bottom