The Monk
Platinum Member
- Oct 12, 2012
- 19,257
- 42,876
Nilishakata shauri mie na nyumba yangu ni kwa wa Malawi tu. Wale wa kulala hapo hapo.
Hiyo kidogo imetupunguzia msongo wa mawazo na mashinikizo ya damu ya reja reja, hawa wa kwetu unaamka asubuhi unakutana na barua dada amepotea. ( hapo haujaongelea usumbufu wa nauli uliyotuma ).
Mwingine anasema anaenda kusalimia kwao, mnamfungaishia vitu na pesa ya ziada anavyoenda kusalimia kwao, akirudi anakaa siku mbili anaondoka.
Mbaya zaidi wakishaondoka baada ya miezi miwili au mitatu, wanataka warudi tena. Hilo kosa sijawahi lifanya, bora tuhangaike ila sio kukurudisha.
Hawa wa Malawi kuna mtu anatutafutia ni mmalawi ila ameishi huku mda mrefu na kwa vile anatuelewa vizuri, hajawahi kutuangusha.
Tunashukuru hatujawahipata tukio la kupigwa na kitu kizito au cha ncha kali.