Ushahidi kuntu kuhusu utapeli uliojificha ndani ya biashara ya dada wa kazi (house girls)

The Monk

Platinum Member
Oct 12, 2012
17,246
2,000
Nilishakata shauri mie na nyumba yangu ni kwa wa Malawi tu. Wale wa kulala hapo hapo.

Hiyo kidogo imetupunguzia msongo wa mawazo na mashinikizo ya damu ya reja reja, hawa wa kwetu unaamka asubuhi unakutana na barua dada amepotea. ( hapo haujaongelea usumbufu wa nauli uliyotuma ).

Mwingine anasema anaenda kusalimia kwao, mnamfungaishia vitu na pesa ya ziada anavyoenda kusalimia kwao, akirudi anakaa siku mbili anaondoka.

Mbaya zaidi wakishaondoka baada ya miezi miwili au mitatu, wanataka warudi tena. Hilo kosa sijawahi lifanya, bora tuhangaike ila sio kukurudisha.

Hawa wa Malawi kuna mtu anatutafutia ni mmalawi ila ameishi huku mda mrefu na kwa vile anatuelewa vizuri, hajawahi kutuangusha.

Tunashukuru hatujawahipata tukio la kupigwa na kitu kizito au cha ncha kali.
 
R.K

JF-Expert Member
Feb 5, 2013
223
250

Subiri mashtaka ya kuhifadhi wahamihaji haramu
 
The Monk

Platinum Member
Oct 12, 2012
17,246
2,000
Subiri mashtaka ya kuhifadhi wahamihaji haramu

Yaje tu Boss wangu. Ntakua tayari kukabiliana nayo kuliko kero na usumbufu unaojitokeza pindi hawa wa kwetu wanapo lala mbele.

Hata hivyo hii biashara muda si mrefu itafikia tamati, dogo wa mwisho ana miaka mitano anaelekea sita.

Stress zitapungua.
 
tpaul

JF-Expert Member
Feb 3, 2008
17,039
2,000
Mzee baba mpaka umefikisha mabinti wote hao na changamoto zao hizo huachi kuwatumia madalali?. Huna ndugu zako au ndugu wa mkeo wakatafte mabinti huko makwao ?. Achana na madalali hao ni zaidi ya danger.
Mkuu kuna baadhi ya madalali ambao ni invisible, nakuja kugundua kuwa ni matapeli wakati tayari nimeishatapeliwa. Na wengine ni ndugu wa karibu lakini wanadririki kunifanyia uhuni. Dunia haina wema.
 
tpaul

JF-Expert Member
Feb 3, 2008
17,039
2,000
Sijamaliza kusoma maelezo yote ila nilipoelewa tu unachokizungumzia basi inatosha

Ushauri wangu chukueni kijijini kwenu wadada wa kazi... au ndo kizazi chenu chote kimezaliwa jijini hamna mjomba wala shangazi kule mkoani akawatafutia dada wa kazi
Asante kwa ushauri mkuu lakini hawohawo wajomba na ndugu ndio wakati mwingine hugeuka madalali uchwara na kuniingiza mujini bila shuruti. Inauma sana.
 
CONTROLA

JF-Expert Member
Sep 15, 2019
5,757
2,000
Jitahidi uwe na nyumba yako na uweke fensi ya maana, dada wa kazi ukitoka kwenda kazini unamuacha huko ndani ya geti Unafunga Geti unasepa na funguo zako.

Kama anaweza aruke ukuta atoroke aone kama ni rahisi, hii mbinu nilikua naiona ya kinyama enzi Aunt angu anaitumia kwake.

sikuwahi muelewa ukijumlisha aunt ndo mtu yenye pesa mingi mingi na roho yake ilikua ya Kama HAKIMU wa mahakama kuu.

Kumbe alikua na maana kubwa sana, sasa ndio naelewa kwann alikua akifanya vile...

Mkuu pambana tia Ukuta nyumba hiyo hizi dada za kazi zikiingia kwako ndio kafika huyo.

Kingine Muhimu kuajiri dada wa kazi mmoja ni tatizo, nyumba inatakiwa iwe na dada wa kazi wawili na sio chini ya wawili.

dada wa kazi akiwa mmoja basi hiyo nyumba isiwe na mtoto ila kama nyumba ina mtoto dada wa kazi hawatakiwi kuwa chini ya wawili.

Nilikua nikidhani ni ufahari kuona nyumba ina wasaidizi hadi wa 4 ila sasa naelewa kwann waboss wanaojielewa hawaajiri House girl mmoja.

Mkuu Anza leo Hakikisha unaajiri zaidi ya dada wakazi m1, kuna faida nyingi utazipata kuliko ukiajiri mmoja. Niko na vivid example hapa. Try n See.
 
Asante kwa ushauri mkuu. Kwa kweli wadada wa kazi wa siku hizi ni wasumbufu sana na ukijumlisha na utapeli wa mawakala tatizo linakuwa kubwa zaidi.
 
Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom