Ushabiki wa siasa katika taasisi za soka: Wakati umewadia sasa kwa FIFA kushusha rungu lake kwa vilabu vya Yanga na Simba

Huwezi kuona kasoro, ilihali hukwenda shule. Ndo mana mtaji wa CCM ni kuwafanya watanzania kubaki kwenye ujinga
Hahahaha nafikiri basi mtaji wa Chadema ni ku-manipulate watu waliochoka na maisha kama wewe ili Muda wote muwe mnafatilia vitu visivyo na tija kwenye maisha yenu/kuvitoa kasoro /kupinga kila kitu.
Hahahahaha, kwa nini!
Basi tu unajua vitu vingine havina maana zaidi ya kuuchosha moyo wa mtu
Kabisa
Ukiwa Ndani Jamiiforums.com
Utasema Nchi Haitawaliki Vile
yani unaweza kudhani muda wowote nchi inapinduliwa
 
Hahahaha nafikiri basi mtaji wa Chadema ni ku-manipulate watu waliochoka na maisha kama wewe ili Muda wote muwe mnafatilia vitu visivyo na tija kwenye maisha yenu/kuvitoa kasoro /kupinga kila kitu.Basi tu unajua vitu vingine havina maana zaidi ya kuuchosha moyo wa mtuyani unaweza kudhani muda wowote nchi inapinduliwa
Pole aisee!
 
Mo anayo pesa hachaguliwi cha kusema na mashabiki.

Tehteh...natania mkuu.
 
Bora wasiojulikana wamteke tena na kumvalisha ile kanga yake pendwa😒😒
 
Niseme tu binafsi jana nilikwazika sana tena mnoo, na wanasimba wengi sana na Watanzania tulikwazika.

Kitendo cha Mo Dewji kutumia platform ya michezo ambayo mashabiki wake tuna itikadi tofauti za kisiasa na kuanza kuwanadi wagombea wa CCM ni kitu cha hovyo sana.

Nimekitafsiri kama ubakaji wa ushabiki, maana kabla ya tukio hatukuambiwa kwamba kutakuwa kuna habari za kuwanadi wagombea wa CCM.

Wametusubiri tumeingia mule halafu wametupaka kinyesi na mambo yao ya CCM. Haikuwa sehemu yake ile, ni kutudharau wana Simba na watanzania, kutuchukulia kama wapumbavu.

Binafsi sio mtaalamu wa sheria, ila kama ikipendeza naomba wataalamu wa sheria, msilifumbie macho hili suala. Fanyeni hima hima, tulipeleke FIFA hili suala.

Please please wadau wote, hili suala lianzishiwe petition lifike FIFA. Inapaswa iwe mwisho wa upuuzi kama huu kwenye soka letu.

Hatuwezi kukubali, Mo Dewji lazima kuna consequences ya ulichokifanya jana. Haiwezi kupita kimya kimya.

Huu mwaka sasa basi, hakuna kitu kitapita bure bure.

Mmetuzoea vibaya wananchi. Sasa basi
Hamna hela nyinyi... Pigeni kimya.
 
Atuombe radhi wana simba, Jana katukwaza saana saana!!

Yaani ni sawa unaendelea kula pilau, jamaa anakuletea bamia dona ushushie..
 
Nyamaza wewe... Mwamedi kanunua timu, mashabiki na interest zao kwahiyo usimpangie wakati watu wenyewe mshalipiwa kila kitu ikiwa ni pamoja na kuwabusu wachezaji huku mkiwa mmejibinua
 
Wewe hujui unachokiongea maana hata shule hukwenda. Hujui mamlaka ya FIFA wewe..

Hii mbungi imekuzidi uwezo. Kuwa mpole
Usicheze na nguvu ya pesa wewe, sehemu pekee utakayosikia kelele Kama hizi ni Jamii Forums tu. Hakuna hata kima yoyote ya upinzani inaweza ongelea hili swala popote zaidi ya humu mlipojibatiza majina ya mitishamba. Mo ni zaidi ya ujuavyo.
 
Tuwekane sawa.

Shirikisho la soka duniani (FIFA) katika moja ya kanuni zake limetoa katazo la siasa kuingizwa katika masuala ya mpira wa miguu (soka).

Katika miaka ya hivi karibuni tumekuwa tukishuhudia hapa Tanzania vilabu vya Yanga na Simba vikijinasibisha na chama dola CCM. Na hili nimekuwa likifanyika kwa uwazi kabisa bila kificho kupitia watu wenye dhamana ndani ya vilabu hivi.

Mfano ni hapa juzi tu tumemsikia na kumuona mwekezaji katika klabu ya Simba akifanya siasa za wazi kabisa kumpendelea mmoja wa wagombea urais October 2020 mbele ya kadamnasi ya maelfu ya Watanzania wenye itikadi tofauti tofauti za kisiasa. Hii ni siasa ambayo FIFA imeikataza katika soka.

Kwa mnaokumbuka, mwaka 2015 kabla ya uchaguzi pale katika klabu ya Yanga kulikuwa na mabango yamewekwa yaliyosomeka "Chagua Magufuli". Hii ni siasa na katazo la FIFA linahusu.

Ipo mifano mingine mingi ya matukio ya kisiasa kuvihusu vilabu hivi. Sasa ifike mahali tuseme "HAPANA, IMETOSHA!".

Natoa rai kwa wafuasi wa vilabu hivi msiishie tu kulalamika kwenye mitandao kuhusu ubaradhuli huu bali chukueni hatua sasa. Hawa viongozi wanaojihusisha na siasa wawajibishwe wao binafsi, na hili linawezekana kwa kuwasilisha malalamiko yenu rasmi FIFA.

Vinginevyo mnatuachia sisi tusiokuwa wafuasi wa vilabu hivi vyenu kuviripoti FIFA vilabu vyenyewe, kitu ambacho kinaweza kupelekea vilabu kufungiwa kwa kujihusisha na masuala ya siasa na hivyo kuwanyima uhondo wafuasi wake.

TUMECHOKA!

The ball is in your court now. Move it, and FAST!
 
Back
Top Bottom