Ushabiki wa siasa katika taasisi za soka: Wakati umewadia sasa kwa FIFA kushusha rungu lake kwa vilabu vya Yanga na Simba

Mkongwe Mzoefu

JF-Expert Member
Aug 10, 2018
842
2,467
Wewe ni mwekezaji tuu, na unahisa sizizozidi 49% hivyo Simba haiwezi kuwa Mali yako completely na kufanya utakalo bila ridhaa ya wengine.

Nani kakutuma umpigie kampeni Magufuli katika shughuli rasmi za club bila ridhaa ya wanachama? Club yetu haina itikadi ya kisiasa wala kidini hivyo ukome na usirudie tena tabia hiyo.

Tuwekane sawa.

Shirikisho la soka duniani (FIFA) katika moja ya kanuni zake limetoa katazo la siasa kuingizwa katika masuala ya mpira wa miguu (soka).

Katika miaka ya hivi karibuni tumekuwa tukishuhudia hapa Tanzania vilabu vya Yanga na Simba vikijinasibisha na chama dola CCM. Na hili nimekuwa likifanyika kwa uwazi kabisa bila kificho kupitia watu wenye dhamana ndani ya vilabu hivi.

Mfano ni hapa juzi tu tumemsikia na kumuona mwekezaji katika klabu ya Simba akifanya siasa za wazi kabisa kumpendelea mmoja wa wagombea urais October 2020 mbele ya kadamnasi ya maelfu ya Watanzania wenye itikadi tofauti tofauti za kisiasa. Hii ni siasa ambayo FIFA imeikataza katika soka.

Kwa mnaokumbuka, mwaka 2015 kabla ya uchaguzi pale katika klabu ya Yanga kulikuwa na mabango yamewekwa yaliyosomeka "Chagua Magufuli". Hii ni siasa na katazo la FIFA linahusu.

Ipo mifano mingine mingi ya matukio ya kisiasa kuvihusu vilabu hivi. Sasa ifike mahali tuseme "HAPANA, IMETOSHA!".

Natoa rai kwa wafuasi wa vilabu hivi msiishie tu kulalamika kwenye mitandao kuhusu ubaradhuli huu bali chukueni hatua sasa. Hawa viongozi wanaojihusisha na siasa wawajibishwe wao binafsi, na hili linawezekana kwa kuwasilisha malalamiko yenu rasmi FIFA.

Vinginevyo mnatuachia sisi tusiokuwa wafuasi wa vilabu hivi vyenu kuviripoti FIFA vilabu vyenyewe, kitu ambacho kinaweza kupelekea vilabu kufungiwa kwa kujihusisha na masuala ya siasa na hivyo kuwanyima uhondo wafuasi wake.

TUMECHOKA!

The ball is in your court now. Move it, and FAST!

Niseme tu binafsi jana nilikwazika sana tena mnoo, na wanasimba wengi sana na Watanzania tulikwazika.

Kitendo cha Mo Dewji kutumia platform ya michezo ambayo mashabiki wake tuna itikadi tofauti za kisiasa na kuanza kuwanadi wagombea wa CCM ni kitu cha hovyo sana.

Nimekitafsiri kama ubakaji wa ushabiki, maana kabla ya tukio hatukuambiwa kwamba kutakuwa kuna habari za kuwanadi wagombea wa CCM.

Wametusubiri tumeingia mule halafu wametupaka kinyesi na mambo yao ya CCM. Haikuwa sehemu yake ile, ni kutudharau wana Simba na watanzania, kutuchukulia kama wapumbavu.

Binafsi sio mtaalamu wa sheria, ila kama ikipendeza naomba wataalamu wa sheria, msilifumbie macho hili suala. Fanyeni hima hima, tulipeleke FIFA hili suala.

Please please wadau wote, hili suala lianzishiwe petition lifike FIFA. Inapaswa iwe mwisho wa upuuzi kama huu kwenye soka letu.

Hatuwezi kukubali, Mo Dewji lazima kuna consequences ya ulichokifanya jana. Haiwezi kupita kimya kimya.

Huu mwaka sasa basi, hakuna kitu kitapita bure bure.

Mmetuzoea vibaya wananchi. Sasa basi
 
Akifanya utumbo huu? Atasbabisha tuache kuishabikia Simba. Muonyeni huyo mgabacholi.
Uliwahi kuona wapi Simba au yanga ikaongozwa na kiongozi toka upinzani?
Chadema mjikite kwenye Sera acheni kuhangaika na Mambo madogo,Kura Ni Siri yangu siwezi kuiacha Simba kisa Mo Ni ccm
Hata yanga akina mwakalebela na Mahindi msola wamezindua wiki ya wananchi huko Dodoma Ni siasa tu,lakini Mbowe mnazi wa Yanga hajajitoa yanga
 
Unajua maana ya mwenyekiti? Au unabwabwaja tu? Yeye ndiye alfa na omega. Leo akitoa mguu tu mtajikojolea mapajani. Aliwabeep tu kidogo kwamba anajihuzuru si mlimlamba miguu nyie nyie?
 
Kama alifanya hivyo atashangaa bidhaa zake na hiyo simba kkukosa mashabiki uwanjani. Chochote kitakachohusishwa na ccm ni kukisusia tu.

Simba itakuwa kama TBC muda si mrefu
 
Katumwa huyo kwa masilahi yake ya kibiashara.Alipotekwa; watu, hasa wapinzani,ndio walimtetea ila leo kasahau!

Anakwenda kinyume na sheria na taratibu za FIFA na anaweza hata kuadhibiwa.

Ujinga sana huu!!
Mlitetea! haha nyie watu nyie.
 
Uliwahi kuona wapi Simba au yanga ikaongozwa na kiongozi toka upinzani?
Chadema mjikite kwenye Sera acheni kuhangaika na Mambo madogo,Kura Ni Siri yangu siwezi kuiacha Simba kisa Mo Ni ccm
Hata yanga akina mwakalebela na Mahindi msola wamezindua wiki ya wananchi huko Dodoma Ni siasa tu,lakini Mbowe mnazi wa Yanga hajajitoa yanga
Kumbe ccm ni wazee wa mikakati. Wameshika kila mahala na pahala.
 
Katumwa huyo kwa masilahi yake ya kibiashara.Alipotekwa; watu, hasa wapinzani,ndio walimtetea ila leo kasahau!

Anakwenda kinyume na sheria na taratibu za FIFA na anaweza hata kuadhibiwa.

Ujinga sana huu!!
Huyu jamaa afukuzwe simba kama kuna mtu anajua sheria za FIFA au kanunu alizo vunja aziweka hapa ili zitumwe FIFA kuanzia leo sio shabiki wa simba
 
Unaachaje kula ugali wa Mo sembe?
Bavicha mlipiga kampeni kususia line za voda lakini michango yenu yote inapitia M pesa

Voda tumeisusia kabisa kwa mfano mimi mwenyewe muda wa maongezi kwa gharama ya serikali nilisajili laini ya voda 50,000 per month lakini sasa nimehamia mtandao mwingine. Kwanza voda gharama ni kubwa. Fuatilia utagundua ni mtandao ulioporomoka zaidi kwa muda mfupi. Hata madukani vocha zake hazitoki.
 
FIFA inatakiwa wapewe taarifa wale hawajui Cha MO wala nini ni adhabu kwenda mbele, Jamaa anaweza pigwa oini kujihusisha na mambo ya mpira maisha yote
Katumwa huyo kwa masilahi yake ya kibiashara.Alipotekwa; watu, hasa wapinzani,ndio walimtetea ila leo kasahau!

Anakwenda kinyume na sheria na taratibu za FIFA na anaweza hata kuadhibiwa.

Ujinga sana huu!!
 
Katumwa huyo kwa masilahi yake ya kibiashara.Alipotekwa; watu, hasa wapinzani,ndio walimtetea ila leo kasahau!

Anakwenda kinyume na sheria na taratibu za FIFA na anaweza hata kuadhibiwa.

Ujinga sana huu!!
Mlimtetea asifanyweje?

Mlishindwaje kutetea wengine?
 
Jana kanishangaza sana kufanya kampeni taifa hakika.

Aliposema CCM hoye watu kmy wakaitikia kama 500 kwenye uwanja unaobeba watu elf 60

Nilikuwa pia baa moja alivyosema Magufuli hoye watu wote wakaguna mle ndani ..

Ndio mjuwe uhalisia uliopo mtaani kwa sasa kuhusu CCM ...

Watu hawako tayari kutumiwa kwa namna yeyote..
 
Wewe ni mwekezaji tuu, na unahisa sizizozidi 49% hivyo Simba haiwezi kuwa Mali yako completely na kufanya utakalo bila ridhaa ya wengine.
Nani kakutuma umpigie kampeni Magufuli katika shughuli rasmi za club bila ridhaa ya wanachama?
Club yetu haina itikadi ya kisiasa wala kidini hivyo ukome na usirudie tena tabia hiyo.
Simba ni mali ya CCM na ushahidi upo.

Simba ni kama ilivyokuwa Channel ten na kuna siku itarejeshwa rasmi chamani.
 
Back
Top Bottom