Ushabiki wa siasa katika taasisi za soka: Wakati umewadia sasa kwa FIFA kushusha rungu lake kwa vilabu vya Yanga na Simba

Yanga ni mali ya CCM kwa 100%

Simba ni mali ya CCM kwa 51%

Huwezi kutenganisha vilabu hivi na CCM.

Maendeleo hayana vyama!
 
kuna mtangazaji alimtaja lissu wakati akitangaza mpira, ikaonekana ni mapenzi yake binafsi kwa kipenzi chake, wala hatukujipa muda kutafakari ana ushawishi kiasi gani katika kazi anayoifanya kwa wakati huo.


lakini sababu tumeamua kuwa wapuuzi, FIFA watatuacha na matatizo yetu.
 
Kwanini tusifanye petition ili habar iwafikie FIFA?

Nilitoa uzi jana kushauri hilo.. wanasheria mpo wapi?

Nafikiri ni wakati muafaka timu ya Simba na Mo washitakiwe FIFA na wapate adhabu stahiki ili iwe fundisho kwa team zingine, hebu wanasheria na wana Yanga kuweni kitu kimoja ktk hili ili watu hawa waadhibiwe hata kufungiwa maisha
 
NI kweli Simba tulikosea kuingiza siasa kwenye mpira, ila sasa mikia mbona kama ndio mnatamani sana tupigwe ban
 
ushasahau FIFA walishatufungiaga huko nyuma pivyu vilitubana?

ngoja tupeleke petition yetu halafu tuone kifuatacho.
baada ya kifuatacho nitakuita mezani tusemezane!
Hawakutugungia kwa sababu za kumpigia kampeni mmiliki wa timu!
 
Duh , aisee nyie jamaa kweli ni fungu la kukosa yaani mmebanwa kila mahali, sasa hata kwenye football pia nako hola, hamtakiwi, hamjishtukii tu kwamba kuna kitu hakiko sawa, wakati mwingine ni vizuri kujitathmini pia inawezekana kuna mahali hamko sawa, haiwezekani kila mahali Watanzania tuwakatae, ...
 
Duh , aisee nyie jamaa kweli ni fungu la kukosa yaani mmebanwa kila mahali, sasa hata kwenye football pia nako hola, hamtakiwi, hamjishtukii tu kwamba kuna kitu hakiko sawa, wakati mwingine ni vizuri kujitathmini pia inawezekana kuna mahali hamko sawa, haiwezekani kila mahali Watanzania tuwakatae, ...
hao wanaoshabikia chama dola ni kujipendekeza kwa ajili ya maslahi binafsi na si kukipenda chama.

Lissu atakaposhika dola October hii utaona msululu wa hawa hawa wakipanga foleni wakitamani kulamba masaburi yake!
 
Nafikiri ni wakati muafaka timu ya Simba na Mo washitakiwe FIFA na wapate adhabu stahiki ili iwe fundisho kwa team zingine, hebu wanasheria na wana Yanga kuweni kitu kimoja ktk hili ili watu hawa waadhibiwe hata kufungiwa maisha
sawasawa kabisa!
 
Tuwekane sawa.

Shirikisho la soka duniani (FIFA) katika moja ya kanuni zake limetoa katazo la siasa kuingizwa katika masuala ya mpira wa miguu (soka).

Katika miaka ya hivi karibuni tumekuwa tukishuhudia hapa Tanzania vilabu vya Yanga na Simba vikijinasibisha na chama dola CCM. Na hili nimekuwa likifanyika kwa uwazi kabisa bila kificho kupitia watu wenye dhamana ndani ya vilabu hivi.

Mfano ni hapa juzi tu tumemsikia na kumuona mwekezaji katika klabu ya Simba akifanya siasa za wazi kabisa kumpendelea mmoja wa wagombea urais October 2020 mbele ya kadamnasi ya maelfu ya Watanzania wenye itikadi tofauti tofauti za kisiasa. Hii ni siasa ambayo FIFA imeikataza katika soka.

Kwa mnaokumbuka, mwaka 2015 kabla ya uchaguzi pale katika klabu ya Yanga kulikuwa na mabango yamewekwa yaliyosomeka "Chagua Magufuli". Hii ni siasa na katazo la FIFA linahusu.

Ipo mifano mingine mingi ya matukio ya kisiasa kuvihusu vilabu hivi. Sasa ifike mahali tuseme "HAPANA, IMETOSHA!".

Natoa rai kwa wafuasi wa vilabu hivi msiishie tu kulalamika kwenye mitandao kuhusu ubaradhuli huu bali chukueni hatua sasa. Hawa viongozi wanaojihusisha na siasa wawajibishwe wao binafsi, na hili linawezekana kwa kuwasilisha malalamiko yenu rasmi FIFA.

Vinginevyo mnatuachia sisi tusiokuwa wafuasi wa vilabu hivi vyenu kuviripoti FIFA vilabu vyenyewe, kitu ambacho kinaweza kupelekea vilabu kufungiwa kwa kujihusisha na masuala ya siasa na hivyo kuwanyima uhondo wafuasi wake.

TUMECHOKA!

The ball is in your court now. Move it, and FAST!
Mkuu nakuunga Mkono kwa hili. Sisi wanachama wa SIMBA tumeumizwa saana na huu upuuzi wa huyu gabachori na amekuwa mbishi saana. Changamoto imekuwa wapi pa kuanzia ila nakuhakikishia tupo tayari kukuunga mkono wewe tuongoze. Tuwasiliane
 
Back
Top Bottom