Tujadili soka la tanzania kwa ajili ya kutoa kipaumbele kuibua vipaji

Kimalingano

JF-Expert Member
Mar 27, 2023
422
521
WATANZANIA TUWE CHAWA WA KUIBUA VIPAJI VYA SOKA

Soka letu,hususan ligi kuu,ni kama biashara ya machinga.

Namaanisha kuchuuza bidhaa usizozalisha.

Ligi kuu ambayo inatawaliwa na Simba na Yanga na kidogo Azam, wachezaji wa vilabu hivyo wanaoongoza ni raia wa kigeni.

Wachezaji kutoka Tanzania wanaouzwa nje ni wachache mno.Ilitakiwa angalau kila mwaka Tanzania iwe inauza nje angalau wachezaji watano.

Lakini ukweli ni kwamba unaweza kupita mwaka mzima bila hata mchezaji mmoja kuuzwa nje kwenye vilabu vya hadhi ya hivi vya kwetu.

Kunatakiwa kuwe na mkakati wa makusudi kuwa na programu ya kuibua na kuendeleza vijana wetu wakue kisoka.

Kwa kuwa sasa imeshabainika kuwa Watanzania wengi wana mapenzi ya dhati na soka kiasi cha kuachana na ushabiki wa siasa za vyama, Serikali na vyama vya siasa vihamasishe na kuhimiza TFF, Vilabu na Wadau mbalimbali kutilia mkazo uibuaji na uendelezaji vijana wa kiume na kike ili wabobee katika uchezaji wa soka.

Kuanzia sasa iwe ni ushujaa au fahari kuibua vipaji vya soka.
Tuwe machawa wa vipaji vya soka!!
 
Back
Top Bottom