Usaliti na Unafiki unavyoangamiza Taifa - Lema

Usaliti na Unafiki unavyoangamiza Taifa - Lema

Status
Not open for further replies.
Mkuu leo sisi wa Lumumba tuekaa viti vya VIP tukitazama mpambano na myukano ndani ya zizi la CHADEMA.
Mie naenda agiza popcorn na kuangalia episode hii inaendeleaje.
Tumeaonya kutofua nguo za ndani hadharani kwa afya hawasikii.
Sasa ndio inadhihirika hawa F4F wakikamata nchi, patakuwepo na idara maalum ya Majungu.

sawa kabisa endele a kukodelea ugali kwako huu ndio mpambano ha ha ha utangoja mpaka kyindi kya malesi
 
Chadema what is this? Mnataka kusema mmeshindwa kumaliza hili hadi hasira zinahamia huku?
Huu ni udhaifu kitaasisi!!

Wacha wasaliti wajulikane jamii ijue. huyu mnafiki amesababisha madiwani wetu wakafukuzwa. Ana unafiki mkubwa sana. nikikumbuka jinsi alivyokuwa mstari wa mbele kuwaambia madiwani wagome kuomba radhi.
Huyu mnafiki chama kinaendelea kumlea japo amesababisha madhara makubwa kwa chama. Chama kuwafukuzwa vijana akina Juliana Shonza, Mtela Mwampamba, Habib Mchange (Masalia) ni kwa sababu yake. Huyu kiongozi anatakiwa kushughulikiwa.

His days are numbered!
 
Ina maana unata kusema analo fanya lema lina jenga chama? umepotoka kabisa.

Kaka hakuna ubaya ni mada tu hiyo inategemea mtu anavyoitafsiri na hiyo inaruhusiwa kwa sababu hata kwenye somo la communication inaeleweka kila mtu anaperceive kitu kwa jinsi anavyokielewa acha mada ijadiliwe na itafikia tamati
 
Kama Mwigamba alisimamishwa uongozi kwa kutoa maoni na mtazamo wake kuhusu chadema tena kwa kutumia jina bandia, iweje huyu Lema ambaye mara zote anamwandama Zitto na sasa anataka afukuzwe kupitia JF naye asichukuliwe hatua za kinidhamu? au mkuki kwa Nguruwe? ina maana maoni ya Lema hayawezi kutolewa kwenye vikao halali vya chama?

masalia bwana kila jibu lazima umuweke zitto unamtetea au unamwangamiza,
 
lema ni jembe....huitaji kufafanua sana

mkuu Safety last lazima tusimame kwenye ukweli kuwa Lema kapotoka kabisa na katika hili ni busara kumwambia kapotoka na malalamiko yake ayapeleke kwenye vikao vya chama.

Huu utoto alio ufanya lema ni wa kukemea kabisa na hauendani na hadhi yake.

Ni vyema kumwambia kwenye hili hana tofauti na mwigamba.
 
Last edited by a moderator:
Niliwahi kukipenda sana hiki chama(CHADEMA) Kutoka moyoni kabisa nakumbuka hadi kadi ya uanachama nilichukua kwa moyo mkunjufu kabisa.....lakini nashangaa jinsi mapenzi yangu kwa chama changu yanavyoshuka kwa kasi....sijui hata kwa nini....
Dah...
 
Mkuu leo sisi wa Lumumba tuekaa viti vya VIP tukitazama mpambano na myukano ndani ya zizi la CHADEMA.
Mie naenda agiza popcorn na kuangalia episode hii inaendeleaje.
Tumeaonya kutofua nguo za ndani hadharani kwa afya hawasikii.
Sasa ndio inadhihirika hawa F4F wakikamata nchi, patakuwepo na idara maalum ya Majungu.

Hivi kuna chama cha majungu kama ccm?? Uchafu wa kila aina umo ccm! Ccm imefika hapo ilipo leo sababy ya majingu. CCM itachie madaraka, kwa namna yoyote ile kwa sababu ya hayohayo majungu, ili watanzania japo wapungue.
 
Busara imetangulizwa kabla hajatajwa. harufu ya kutajwa inanukia. obviously atajitaja mwenyewe kama kweli ni mzalendo. juzi kwenye gazeti alijitaja bila kutajwa.

mkuu naanza kupata picha vizuri, kweli kijamaa kinaboa sana na kinaamini kinajua kila kitu na jambo.
 
Umetajwa kuwa ni mmoja wa wasaliti na umepokea hongo kupitia simu yako. Vichupa usivisahau mambo yako jikoni.

Kwi kwi kwi teh teh teh.

kachupa ka sumu? Ben ana akili za kwenda chooni na kuvuka barabara tu......akili na usomi wote anauweka kando inapofika swala la chadema..............u can imagine unampa wizara ya madini.......na mbowe ndio raid, slaa waziri mkuu, ATAONGOZA NINI? ikiwa ni ''ndio slaa, dnio mbowe'' si riziki huyu atiii
 
Ndani ya CHADEMA hakuna usaliti wa unafiki bali kuna hofu ya mabadiliko ya uongozi, kuruhusu demokrasia iamue,kushindwa kukubali ulazima wa kutofautiana mitazamo na uhuru wa kutoa maoni.Ni nani amejiuliza ingekuwaje uzi huu ungeanzishwa na Zitto? Chama siyo mali ya Mhe.Zitto, Mbowe wala Dr.Slaa hivyo vijana wa CHADEMA hatutakiwi kuyumbishwa na viongozi wanaotutaka tunyosheane vidole badala ya kujenga chama na kuimarisha misingi. Frankly speaking, PR department is very crucial for political sustainability of our lovely party (CHADEMA).
 
Alichokitenda mwigamba na wewe unarudia kilekile, hapo unawachonganisha viongozi wa chama na wanachama, mh. LEMA yeyote yule anayejiona ni bora kuliko chama ni adui namba moja kwenye chama! Pia lema kubali kuheshimu mawazo ya wengine ndani ya chama, hakuna aliyekamilika, kila mtu ana mapungufu yake pengine hata wewe! Chadema kwa sasa ikiongozwa jazba na uzushi badala ya hoja,kanuni,katiba na sheria itajisambaratisha. Watanzania tunaopenda mabadiliko hatutaki ifike huko.
 
Kwani yeye anaporopoka nje ya vikao vya chama huwa hajui kama matatizo yoyote ndani ya chama yanaweza kujadiliwa kwa kufuata taratibu za vikao vya chama ili kuyapatia ufumbuzi matatizo hayo? Unakumbuka mwaka jana alikuja hapa na uzi wa kuomba samahani kwamba kuna makosa ametenda na akaomba samahani kwa wanachama wote wa chama na pia kuahidi kwamba mwaka 2013 atajitahidi kufuata ushauri mbali mbali ili awe karibu na viongozi wenzake katika kuboresha chama kuelekea 2015, lakini hakufanya hivyo. Naunga mkono hoja yako ya kutatua matatizo ya chama ndani ya chama, si ajabu imeshindikana kumdhibiti huyu ndani ya chama na hivyo hata kumjadili nje ya chama sioni tatizo. Alikuwa kimya kipindi kirefu sasa miaka miwili kabla ya uchaguzi mkuu wa 2015 ameanza kuleta mifarakano ambayo haistahili kuwemo chamani wakati muhimu kama huu wa kujenga mshikamano wa hali ya juu kuelekea katika uchaguzi muhimu sana kwa CHADEMA na Taifa letu..

Huyo msaliti ni nani? Vp umeshndwa kuongea hayo kwenye vikao vya chama unakuja hapa hadharani.
 
Tatizo la CHADEMA huyo wanayemwita msaliti ana nguvu na wakifuata njia za sheria na demokrasia anaweza kuwashinda kirahisi sana akawa yeye ndo mwenyekiti.

Sasa ndo maana wanazunguuka zunguuka kujaribu kutafuta loop hole ya kumuondoa.

Qanamuogopa huyo 'msaliti' kuliko wanavyoigopa CCM...

Hivi huyo so called msaliti ni nani?

Zitto?
 
Jamani jamani angalieni lisije likatimia lile andiko lililo nenwa na nabii Steven Wasira pale aliposema CDM haitafika 2015... ni angalizo tu msinipige mawe
 
kweli ww mlamba viatu wa slaa maana alikutoa kwenye uchaguzi kisa umefanya kampeni mapema na ukakubali matokeo na kuendelea kukipenda chama! je zitto angeweza kuvumilia?

zitto anafanya biashara gani ya kuweza kuwa na pesa kiasi alichonacho? ubunge tu? maana hajawahi kufanya kazi na hizo ndo kinamsumbua maana kwenye ofisi kuna levels of authority and responsibility! kunamtu aliwahi kulinganisha kati ya zitto na mnyika. nikamwambia bora ya mnyika hayupo sharp ila ni mtulivu na anareason ila huyu mwingine ni sharp intelligent but not sattled up stairs na nchi huwezi kumpa mtu wa aina hii!

Ndio kama chama kinajali, wangemuuliza na kuweka bayana kama ni utajiri kautoa wapi? kuna watu tunasumbua mjini kwa vitu vya kukodi tu.....poor people
 
Status
Not open for further replies.
Back
Top Bottom