Usaliti na Unafiki unavyoangamiza Taifa - Lema

Usaliti na Unafiki unavyoangamiza Taifa - Lema

Status
Not open for further replies.
Wole Soyinka aliwahi sema 'democracy is the voice of the people weather those people are
clever or stupids.......

sasa huyo 'msaliti' kama anakubalika na kupewa Uenyekiti akigombea

nyinyi kina Lema mtaweza kuheshimu maamuzi ya wanachama?
 
Mnalia kila siku hapa et ztto ni mnafiki,msaliti,mfukuzeni muone. Waoga wakubwa nyie! Zitto ndo turufu ya chadema na kna slaa wanamuogopa kuliko rama igondhu wa ulimboka. Mtalia sana na kulalamika wazalendo wa kweli tupo na zitto mwanzo mwisho
 
Mimi ni mwanacdm. Mkimfukuza zitto mtajuta jinsi chama kitakavyosambaratika. Mtafuata zitto kigoma kumpgia magoti arudi chamani.
Yericko na mungi si mmeleta ushahidi wa usaliti wa zitto? Mfukuzeni sasa mnalea usaliti? Nawaona hadi moyoni mnavyoogopa.
 
Umetajwa kuwa ni mmoja wa wasaliti na umepokea hongo kupitia simu yako. Vichupa usivisahau mambo yako jikoni.

Kwi kwi kwi teh teh teh.

Ben Saanane alitumiwa na mnafiki bila kujuwa alikuwa usalama wa chama (CISS)
 
Last edited by a moderator:
Mimi ni mwanacdm. Mkimfukuza zitto mtajuta jinsi chama kitakavyosambaratika. Mtafuata zitto kigoma kumpgia magoti arudi chamani.
Yericko na mungi si mmeleta ushahidi wa usaliti wa zitto? Mfukuzeni sasa mnalea usaliti? Nawaona hadi moyoni mnavyoogopa.

Jina la Zitto limekujaje hapa?
 
lema ni JEMBE arusha nawakubali sana kutuletea mbunge wa ukweli ........songa kamanda hawa vila wa jf sisi tunawagonga tu....."ni bora simba mia walioko nje kuliko nyoka mdogo aliyeko ndani" hahahaha.......
 
duuh!! ila inashangaza sana, hapa jamvini imekuwa ikilalamikiwa jinsi watu walio katika nafasi za kuingia kwenye vikao vya maamuzi wakishindwa kufanya maamuzi wanabaki wanalalamika, tu. Ndio maana tunasikitika kuona rais analalamika, PM analalamika, waziri analalamika.

Sasa the same huyu jamaa anatuletea, mtu ni mjumbe wa kamati kuu, baraza kuu na mkutano mkuu, pia ni waziri mmojawapo katika kambi ya Upinzani bungeni, badala ya yeye kuwa sehemu ya utatuzi, na yeye anakuwa sehemu ya migogoro, kwa nini asiyapeleke haya masuala vikaoni kwao? JF, ndio kikao cha CDM?

Very disappointing kwakweli, ila good thing huyo mnayemu attack jueni ana sikilizwa zaidi na society kuliko wewe crook!!

Tuseme hoja ya Posho za ubunge ndio imemfanya Lema leo kumtambua msaliti chamani? Hivi hatuwezi kuona any association baina ya bandiko la Lema na ghiliba zake zilizofeli za posho, so anajaribu kubadilisha upepo?
Anafikiri wote mna ubongo sawa na watoto wake.
 
Ndo nilikuwa nasubiri hii,naona chadema tumefikia pazuri
 
Teh teh teh Chadema mwendelezo ule ule wakuchafuana kwenye mitandao sijui Lema naye atachukuliwa hatua.
 
Lazima ifike muda watu watambue kuwa akili na busara zinahitajika sana ili kufanya nchi yetu isonge mbele. Chadema chini ya hawa akila Lema they dont seem kuelewa upinzani ni nini hasa na unatakiwa uwe vipi??

Lema, pole sana ukidhani umeandika kitu cha maana sana hapo juu kumbe pumba zile zile za akina slaa na mbowe na akina ben saa nane ( the puppet)

Kwanza, taja jina na weka wazi msaliti ni nani? maana inajulikana hauna ushirikiano na urafiki mzuri na zito zuberi kabwe, inajulikana

wewe , salaa, mbowe na wenzenu mmejitahidi kuwafanya wanachadema wengine waonekane mbumbumbu na hamnazo simply kwa sababu wamewaaamini mno, na kuwapenda, kwani CCM imewachosha, lakini mmekaa ki-NGO zaidi, kikanda, kikabila kila kukicha chuki na asilimia 90 ya mazungumzo yenu ni ugomvi wa chama chenu na si kuiondoa ccm inaleta nini?

1. ugomvi wa chama chenu unapoonekana kwa watu wa nje unawavunja moyo hasa wakichukulia historia za cuf na nccr mageuzi

2. ugomvi wa ndani unawarudisha nyuma na kuleta sintomfahamu nyingi kiasi cha kuwa vitani kila mmoja anarudi nyuma maana unaweka viulizo nani wa KUAMINIWA??

3. Unaendeleza ugonjwa wa yaleyale ya mwigamba ya kusemea mtandaoni hivyo basi inaonyesha kuwa

a/. hauna ubavu wa kuwa face hao unaowaita wasaliti ndani ya chama simply kwa sababu UNAOWAITA WASALITI SIO WASALITI ILA WANASIMAMIA HAKI NA UKWELI

b./ umekuja na hoja za wasaliti ukijua JF itaku support kwani JF wengi ni wanachadema, umesahau kuwa ni sehemu ya ukweli na uwazi, WEWE MBUNGE UKILIA HIVI, mwita maranya afanyaje????

c/. mnaowaita wasaliti hamuwezi kuwaondoa kwenye vikao vya chama maana watawashinda kwa hoja za katiba ya chama, kwa mfano HAIWEZEKANI KIJANA KAMA WEWE, SMART, NA AKIL ZAKO unakuwa wa KWANZA KUCHEKEA KUTOFANYA UCHAGUZI NA KATIBA YA CHAMA KUBAKWA kisa uonekane mzuri kwa mbowe na slaa?? mkipewa nchi mtafanyaje??

Hii dalili ya kusemea mitandaoni kwa mtu mkubwa kama wewe ni UDHAIFU na kwa akili zenu mnajua wengine hatuoni vile...na ndio maana mtaishia kutukuzwa na kupigiwa makofi na washabiki na sio umma......utasifiwa na vilaza na waliopofushwa na mahaba yaliyotokana na chuki kwa ccm na sio reality za kuwa nyie ni wakombozi

Lema, SOMA KWA NGUVU HAPA, HATA ZITTO MKIMTOA LEO NDANI YA CHADEMA, ATABAKAI KUWA ZITTO, zitto ni rais anayeishi mioyoni mwa watu, anapendwa, anaogopwa na mafisadi, anasimamia hoja zake, ana uthubutu NDIO YUKO HIVYO, nyakati zile unaendesha ujambazi arusha yeye alikuwa anasoma degree, anaendesha siasa chuo kiku...hajaanza leo....certainly ndani ya chadema watu wa caliber ya zitto hamna na wengine mmewaua au kuwafukuza

Zitto ni bright, tough na focused, hategemei siasa wala CDM yenu ambayo kila wakati mmepaka majina yote mabaya...Lema ,zitto angekuwa fisadi au msaliti hao CCM wangeisha muumbua.........hoja za uswis, hesabu za mashirika ya umma, buzwagi, kutaka kumtoa waziri mkuu, kutaja mishahara ya viongozi, na hoja zingine ndio zinazoifanya sio zito tu CHAMA KIZIMA CHA CDM KIONEKANE KINA WATU makini, lakini kuna uozo wa wewe, sugu na mtei ambao akili zenu mnazijua wenyewe

Yesu alisema, ikiwa ufalme utajifitini hautasimama...kamwe

we have plenty of problems IN THIS COUNTRY which need your attention and your solutions…. wewe UNAONGELEA WASALITI NDANI YA CHAMA??? Hao wasaliti umewajua lini?? wanaogopwa nini mpaka leo hii wasitolewe??

Hivi lema unajua chadema kinapendwa na hata wasio wanachadema?? fanyeni kitu kuwaaminisha watanzania mnaweza Zitto anafanya hivyo, Lissu anafanya hivyo, hata Slaa alivyokuwa mbunge alifanya hivyo...nyie wengine mnafanya nini??? HATUONI

Leo Lema ukifa utakumbukwa kwa lipi?? kuchukua jiwe na kumponda nalo mwigamba?? kufungwa jela?? kutukana matusi kuwa ile mimba ya Lowassa?? why u guys dont evaluate urself ila MNAOGOPA KIVULI CHA ZITTO?? where is nassari where is msigwa, wabunge woooooooote wa CDM ambaye ana international status, anayeweza kuongea kitu akaeleweka na kukubalika ni Zitto peke yake ndani ya CDM...................yet is your no. 1 enemy

utasema hooo sijataja hilo jina Lema, YOU ARE INFERIOR na ukiwa INFERIOR UTAJIONA UKO CHINI NA UTATAFUTA SUPPORT YA INFERIOR WENZAKO kumtafuta mchawi ni nini??

Kama aliyoyasema Mwigamba juzi ni usaliti, wenye akili tuna majibu………………kama post hii umeituma ukiwa na akili timamu, jiuzulu ubunge mkuu.

Lema, kila kitu kina mwisho wake, endeleeni na haya mnayoyafanya nakutakia maisha marefu ila UTAONA MWISHO WAKE, sio mzuri kwa chama.

Zitto kama hamumtaki amueni muondoeni kwenye NGO yenu, ATAISHI HE IS GRADUATE na anaweza kujisimamia. Lema ukiondolewa hapo kwenye siasa za chadema unazobebwa na wenye ufahamu mdogo na nguvu za akina mbowe, huna pa kwenda na hakuna atakayekuelewa.

Chadema, mliamua kwa pamoja hamtaki Posho ( sitting allowance) mmeanda bungeni Zitto katekeleza mliyoyaamua WENGINE, akiwem o wewe na Mbowe mmeshindwa……..Then ZITTO M’BAYA???????

Watchin u​
Nadhani Lema hakumtaja Zitto. Ila kwa sababu umemtaja, basi ngoja tumuongelee. Wewe ukimtizama unaona shujaa, right? Mimi naona msaliti, ndumila kuwili, mtu asiye na msimamo na ana uchu na madaraka. Pia nadhani ni mjinga. Rejea story zake humu humu JF utafikia conclusion kama yangu. Pengine unaweza kumwona amechanganyikiwa.

International status? Come on...JK anazo nyingi. Hata leo yupo nje. Kama hiyo ni sifa, liko wapi taifa la "international status?" Sijui wewe ila nikipewa nichague kati ya kina Nyerere, viongozi waliokaa nchini mwao na kulijua taifa na wale wanaosafiri kila siku kwa million 300 kila safari, ntachagua kina Nyerere.

Where is Msigwa?, where is Nassari?...wewe una akiri kama ya Zitto. Maana yeye uwasaliti wenzake kwa kujiona aishatembea dunia nzima. Ebu tuangalie akitembea anafanya nini. Niliudhulia mkutano wake miaka ya 2008 au 2004 huko Texas. Maongezi yake ni haya, "naachana na siasa hivyo kipindi kijacho sitagombea." Hivi hii ndo international status? Nakupa challenge, nenda mwamshe Nassari au Msigwa usingizini, muulize kama ataacha kupigania watanzania leo au kesho. Sijui atakujibu nini lakini kati ya hayo majibu, mojawapo litakuwa ni hapana.

Msigwa, Nassari, Lema, na wote ulowataja, they are our heroes. Hawa ni mashujaa. Wamepigwa mabomu karibu kila mkutano, Nassari kapigwa, juzi tu ametoka hospitali. Msigwa huyu jina lake lipo kwenye mswaki wa kamanda wa polisi Iringa. Hawa wakivua mashati yao, miili yao ina vidonda, mioyo yao ina majeraha walopata sababu ya kupigania watanzania, mimi na wewe wakati wewe na shujaa wako mkitafuta "international status" kwa kuwambia watu kwamba hamtawapigania tena. Hii si aibu?

Zitto anajua mabomu yanafananaje? Mwambie ajiunge na Chadema, then atajua ushujaa ni nini.
 
huyu atakuwa zitto natumai anaelekea kuwa kama mrema.siku si nyingi yangu macho!
 
Jiwe limerushwa gizani,sasa hivi ni vilio tu mara oh mtaje,mara oh vikao vya chama mara kanuni zimevunjwa.Leteni kanuni zilizovunjwa
 
Mkuu sindio nyie na LUmumba team kila siku mnapost habari za chadema uchaguzi,dr slaa,zito nk
Hizo mnazopost ni mambo ya kitaifa?
Mbona hamjadili mambo yaliyo serikalini inayohusu mafisadi wezi,majangili ndani ya chama cheni na serikali? Hilo sio jambo la kitaifa?
I hope uko CCM na nyie muwaondoe wasaliti ndani ya chama
Nadhani ujumbe wa Lema unafaa kuigwa na vyama vyote, fukuzeni wasaliti au nyoka ndani ya vyama vyenu.
sisi tusio na vyama tunawachunguza.

we are not interested in these cheap F4F , internal wranglings za CHADEMA.
Leteni mambo ya kitaifa hapa,
 
Yaliyosemwa sasa yameanza kujidhihirisha,sasa nimeamini yaliyosemwa juu ya chadema,yaani chama ni cha familia flani tu,akitokea mtu akawa maarufu kiasi cha kuungwa mkono na watanzania wengi huwa nongwa kwa chadema,
Alianza hayati chacha wangwe,akafuata Dr.kabour na sasa Zitto yupo kwenye rada.Hii kauli kaitoa Lema lkn kapewa baraka zote na katibu mkuu pamoja na mwenyekiti ili kuupima upepo,na kwa ndio maana huwezi sikia Lema akionywa wala kushambuliwa na viongozi wa juu,kauli ya lema ukioma imeungwa mkono na saanane jua Babu ndio kamwambia chakuandika.
Tunakushukuru Lema mpenda posho kwa kuonyesha kuwa wewe ni rangi gani.lkn nachopenda kushauri ni kuwa kama kweli unauhakika kuwa Zitto ndio mfadhili wa wasaliti basi iteni kikao mumfukuze,kama kiko si muhimu andikeni barua ya kumfukuza uanachama mumtumie kwenye e-mail yake,mumpigie simu kama mlivyofanya kwa Shonza.ili Mbaki watu wa Familia moja ktk chama mgawane posho vizuri bila kikwazo.
Lkn kuendelea kutiletea majungu na malalamiko kama binti aliyeachwa nabwana ni kuendelea kujodhalilisha.
Hoja kubwa iliyotumiwa na Lema na wenzake wakati wa kimuadhibu mwigamba ni kuwa hoja za mwigamba ni sahihi lakina hakutumia njia sahihi kuziwasilisha ,sasa vipi hoja hizi za lema ? tukubali kuwa ni sahihi.je kunatofauti ya njia iliyotumika na ile ya Mwigamba. tusubiri kusikia adhabu kwa Lema vinginevyo watanzania watazidi kuona unafiki,chuki, na usaliti mkubwa mbele ya macho ya watanzania.
 
Huyo msaliti ni nani? Vp umeshndwa kuongea hayo kwenye vikao vya chama unakuja hapa hadharani.

Nilitegemea ben saanane angemkemea lema,kwa kuleta mashitaka mitandaoni badala kupeleka kwenye vikao,hasa ikizingatiwa ye ni mjumbe wa kamati kuu.Lakini hivi ni vituko vya uchaguzi.
 
Tatizo letu hatutaka kukoselewa,lema ili kujenga chama imara migogoro haikwepek,chamsing kaeni vikao kuelezan ukweli,huwez kukosoa ccm juu ufisad wakat ndan chama ndio jogoo wa ufisad,udin na undugu.na lait lema ungekuwa mwkt chadema kingekufa zaman.kwan wew umwenyimwa hekima.na kutahadharish mukifukuza huyo jamaa mtajuta majuto ambayo hamtahau
 
Jina la Zitto limekujaje hapa?

zitto ndo anayetajwa na lema. pia wewe umeonesha namba ya zitto ndo ilikua inagawa hela. yericko alileta 'ushahidi mzito' kuwa zitto ndo msaliti. najua unajua kwa cdm zitto msaliti!
 
Status
Not open for further replies.
Back
Top Bottom