Usaliti na Unafiki unavyoangamiza Taifa - Lema

Usaliti na Unafiki unavyoangamiza Taifa - Lema

Status
Not open for further replies.
This is obviously personal attack from anonymous to the verified. We unaweza kuwa mwathirika wa the so called peeling back the mask!!

Mkuu Mungi hujamshtukia huyo coward tu?Nilimwambia aje na ile ID yake Really aone
 
Last edited by a moderator:
Ndani ya CHADEMA hakuna usaliti wa unafiki bali kuna hofu ya mabadiliko ya uongozi, kuruhusu demokrasia iamue,kushindwa kukubali ulazima wa kutofautiana mitazamo na uhuru wa kutoa maoni.Ni nani amejiuliza ingekuwaje uzi huu ungeanzishwa na Zitto? Chama siyo mali ya Mhe.Zitto, Mbowe wala Dr.Slaa hivyo vijana wa CHADEMA hatutakiwi kuyumbishwa na viongozi wanaotutaka tunyosheane vidole badala ya kujenga chama na kuimarisha misingi. Frankly speaking, PR department is very crucial for political sustainability of our lovely party (CHADEMA).

Huo ndio mchezo wa hapa mjini CDM. Wewe ukitaka ukubalike kirahisi kwenye viongozi wa Juu wa chama (mwenyekiti na katibu mkuu) onyesha tu upo against Zitto na tena ujifanye una siri nyingi kumhusu yeye, utakumbatiwa mara moja. Kuna kijana sasa hivi yupo hapa makao makuu na aliijariwa kwa kuleta taarifa maalumu kuhusu Zitto na ndio ticket iliyompa kazi. Taarifa zilizopo ni kwamba huyu kijana ni shushu, lakini atakumbatiwa kwa sababu tu anamwaga sumu kuhusu Zitto.

Hata huyu kibaraka Ben alikuwa hatakiwi hata kuonekana hapa makao makuu, lakini siku moja akaja akaomba sana aonane na Katibu Mkuu, akakubaliwa kwa shakashaka. Alipopata mwanya akammwagia katibu mkuu -----, lundo la uwongo kuhusu Zitto akimweleza jinsi walivyokuwa wanapanga mipango naye pamoja, lakini sasa yeye amegundua kosa na anaomba msamaha na akaahidi kusaidia kummaliza Zitto. Kuanzia siku hiyo akakumbatiwa akakabidhiwa na ofisi. Kumbe maskini wa Mungu Ben hata hajawahi kuonana na Zitto!!

Mkakati uliopo ni kuhakikisha Zitto anaondoka CHADEMA kabla 2014 haijagota. Wamegundua haondoki na hababaiki na chochote. Kibaya zaidi hawajaona akifanya kosa la kikanuni litakalohalalisha kufukuzwa. Alichofanya Lema hapa ni kum-provoke ili alipuke wapate pa kuanzia kwenye Kamati Kuu ijayo ambaye itaitishwa any time ndani ya mwezi huu wa 11. Washauri wa Zitto wamshauri awe mbali kabisa na ujinga huu, watalia.

Mimi binafsi nimepania nitajibu kila post ya hawa wajinga, ninawajua vizuri kuliko wanavyojijua wao. Makao Makuu kumebadilika sana, huyu Ben Sanane mnayemsifia hapa JF anaonekana choo kabisa na amejikunyata saa zote kama kuku. Ukweli utajulikana na tutajua nani mkweli.
 
We lema ni MKOSEFU WA UPEO SANA,HUNA FIKRA,HUNA MAONO,HUNA VISION NA HUFAI HATA KUWA MFANO WA KIONGOZ NDAN NA NJE YA CHAMA,KWA UFUPI WE NI KIHIYO NA KANJANJA...


Sasa skia tunajua lengo lako ni nin na nani uliemkusudia katika hili bandiko lako,kwa ufupi umemlenga Zitto kabwe,

Yakupasa ujiamin basi,kama una allegations ambazo unahis zipo kwa watu fulani kwa chama chako ulikuwa una haja gani ya kuzileta JF??una hofu kitu gani kukusanya ushahid wako wote na tuhuma zako ukazipeleka kwenye ngaz za chama chako mukamujabibisha zitto kabwe??kuja hapa kwa maneno ya mafumbo na kuchenga chenga ni ishara tosha ya kutojiamin na kumuhofia zitto kabwe,

Hivi lema wewe umefanya nin cha maana ndan ya chama hiki cha kujifananisha na zitto kabwe??na kama unahis kuna usalit anaufanya kipi kinakuzuia kuufanyia kazi na kuusema kwa umma wa watanzani wakaufaham??

Hii ni kututhibitishia sasa siasa za chadema zimejaa udini(zitto ni muislam),,zimejaa ukabila (zitto sio mchaga),na zimejaa ukanda kwa kuwa (zitto sio mtu wa kaskazin??)unless otherwise uje na ushahid wa haya mauza uza yako ama sivyo underline hayo maneno yangu..

WEWE UKIACHIA MBALI ARUSHA NIAMBIE WAPI UNA USHAWISH KITAIFA,KICHAMA??

ZITTO NI MIONGON MWA WATU AMBAO WAMEKIPIGANIA HIKI CHAMA KWA KIAS KIKUBWA NA KUJENGA TASWIRA CHANYA KWA CHAMA DHIDI YA PROPAGANDA MBALI MBALI ZA MAFISADI NA WAHUJUMU DEMOKRASIA NDAN YA CHAMA HIKI,KIPI KINACHOKUSUKUMA WEWE KUJA HAPA HADHARANI KUMCHAFUA??

LENGO LIMEFAHAMIKA NA LIMEFELI TAYARI,ZITTO KABWE USIWE MPUUUZ KAMA HAWA JAMAA,USITOKEE KUJIBU CHOCHOTE DHIDI YAO,NI WAZI KWAMBA MAJI YAMEWAFIKA SHINGON HADI SASA WAMEANZA KUWEWESEKA,

TUNATAKA KUONA SASA,HIKI SI WANASEMA NI CHAMA CHA DEMOKRASIA NA MAENDELEO??TUNATAKA SASA KUIONA DEMOKRASIA IKO WAPI??

KAMA NDAN YA CHAMA TUH WANASHINDWA KUHANDLE MADOGO KAMA HAYA WANAENDEKEZA UCHAWI NA MAJUNGU TUKIWAPA NCHI WATU HAWA MWISHO WAKE ITAKUAJE??

ZITTO KOMAA NAO WAJINGA WAJINGA NA WATU WASIO NA SHULE HAWA KAMA LEMA HADI KIELEWEKE,USIHOFU UMMA WA WATANZANIA UNAKUANGALIA KWA JICHO LA UHALISIA NA TUPO TUNATAKA KUSHUDIA MWISHO WA PICHA HILI NA UPI,

KOMAA NAO NDAN YA HIKO CHAMA HUKU UKISIMAMIA MISINGI YA CHAMA CHAKO,HAWA WAJINGA WAJINGA WAACHE WAJIDHARIRISHE NA KUJIPUUZISHA KAMA HIVI,,

LEMA KODI YA NCHI HII SISI NDIO TUNALIPA,HATA UFANYAJE HUNA HAKI YA KULALAMIKA UONGEZEWE POSHO,UONGEZEWE POSHO KWA KAZI GANI YA MAANA UNAYOIFANYA MJINGA WEWE??

THEN UNAJIITA ETI UNAPIGANIA MASLAHI YA WALALAHO,MASLAHI GANI??

Sasa ni kavu kavu!
Tena live.
Kumbe CHADEMA kuna members wanaotoa kali bila kutukana na wakaeleweka!
Hii ya leo kali.
 
Last edited by a moderator:
Mkuu Lema, pengine utusaidie kutupatia maana halisi ya 'Usaliti', 'Unafiki' na 'utu' kwa namna uelewavyo wewe.

Maneno haya kutoka kwako yananishangaza kidogo, kwa vigezo kuwa kwa yale unayofanya nawewe unaweza fuzu kuitewa Mnafiki na Msaliti asie na utu. Labda kama unatumia hii njia kujikosha baada ya wewe pia kutambua kuwa umeonyesha Usaliti mkubwa kwa Watanzania unaowawakilisha.

Lema inatakiwa uelewe haya;

Unatakiwa kujua kuwa hata kina KUBENEA wameshakuchoka, yeye si mmoja wa hao anaowasema? (Au woga ambao siku zote unashabikia ni sumu leo si sumu tena?), pitia hii https://www.jamiiforums.com/jukwaa-la-siasa/547535-mh-lema-anaivuruga-chadema.html

Watanzania wengi washakushtukia, unakiruvuga chama kwa siasa zako za kishabiki na kitoto wenzetu wanaita 'armature' (an insult ukiichukulia undani wake) pitia hii https://www.jamiiforums.com/jukwaa-...gwe-gavana-rahisi-kusababisha-mitafaruku.html

Inawezekana unawashambulia Shibuda na Zitto kwenye bandiko hili, vipi ni kwakuwa wewe Lema unapenda sana Posho hivyo umeamua liwalo na liwe? pitia hii https://www.jamiiforums.com/jukwaa-...bungeni-zitto-lema-katika-vita-ya-maneno.html

Au unataka kusema hizi posho zinamaanisha Uzalendo na Utu kwa Taifa? (Are you serious??). Zitto alisha litabiri hili na kueleza wazi (hakutumia unafiki) kuwa Siasa za Posho zitasababisha mjenge chuki na mmwite majina yote mabaya! www.jamiiforums.com/jukwaa-la-siasa/299635-zitto-sijahongwa-ni-siasa-za-urais-na-hasira-za-posho.html

Au hii ndiyo step ya kwanza ya kufanya Zitto aondoke Chadema? Maana inajulikana wazi kuwa kuna mkakati wa kumkatisha tamaa Zitto aondoke CHADEMA mapema kabla mwaka haujaisha ili mpumue ndani ya chama cha watu wa Kaskazini (viongozi wa juu). Inaturudisha kule kule mnako kukataa siku zote (Udini/Ukabila).

Pole zako Lema, watanzania wa leo si mabwege!

Siyo mabwege kama wewe uliyeonyesha u...bwe...ge wako hapo juu.
 
Mheshimiwa Lema,

Hakika mimi niseme maneno machache tu,

Kwamda wa miaka 8 niliyoanza kuhudumu katika siasa kali niseme wazi, kikwazo kikuu cha kuelekea mageuzi ya kweli katika nchi hii kupitia siasa za mageuzi ni Zitto Zuber Kabwe,

Narudia tena Zitto Zuber Kabwe ndie msaliti namba moja na ndie kiongozi wa migogoro yote kila itokeapo ndani ya Chadema,

Sisi tumemaliza kazi yetu sasa tumewaachia wafanyamamuzi,

Sasa mkimshindwa tutachukua jukumu la kihafidhina zaidi wenyewe


Haya maliza na majina ya wanaotakiwa kuchukua hatua lakini wanalala na kuhatarisha amani,maana kama kuna nyoka na mtu wa kumuua yupo ila hataki basi yeye ndio mbaya! !!!!!!!

I told you once mna shida kubwa huko ndani kwenu kuliko kelele za mitandaoni!!!!!!

Ni bahati mbaya ila msipokuwa makini mtajifunza kwa maumivu ya mioyo ya Watanzania wengi jambo ambalo gharama yake hamtoimudu!!!!!
 
Safari yetu ya kubadilisha utawala inaonekana kufika ukingoni na nifuraha ya kila Mtu mwenye hisia ya ukweli katika maisha na ninapotazama mbali sana ninaona jinsi ambavyo Usaliti na Unafiki unavyoangamiza Taifa ni bahati mbaya sana uwezi kuwaepuka katika harakati hizi lakini tukiwa makini tunaweza kuwathibiti .

Kama Chadema leo itashindwa kuwachukulia hatua wasaliti wa wazi wa kazi hii njema ni vipi Chadema itaweza kuitaka Serikali na Rais iwajibishe Viongozi wake katika ufisadi na wizi wa mamilioni ? Na Wananchi lazima wajue lengo kubwa na muhimu la Chadema kwanza liwe kubadilisha fikra na mitazamo na kuupa UMMA elimu na mamlaka na nguvu ya kusimamia Taifa lao katika kuhoji ,kudadisi na kukemea , kwani UMMA usipojua wajibu wake katika kusimamia rasilimali na Taifa lao , ukweli utabaki kuwa Nchi itabadilishwa na kufanikishwa na Jamii iliyoamua kuishi matendo dhahiri ya ukweli na haki na sio unafiki na usaliti .

Viongozi wote wa Siasa wanatokana na Jamii kwa hiyo jamii Thabiti inayo furahia UTU ni Nchi bora tutakayoijenga lakini Jamii yenye woga na hofu na Sifa itazaa Taifa lenye usaliti na Wanafiki . Usaliti na Unafiki unaliangamiza Taifa sana . Maombi na Dua za Watu wengi kuelekea 2015ni kutaka kuona Chadema inachukua Nchi , lakini Dua na Sala hizi zina Imani kubwa na Viongozi wa Chadema na sio rangi ya Chadema , hivyo ni muhimu Chadema kuchukua hatua sasa ya kusafisha Chama na kama hatua hiyo muhimu ya kuondoa Watu wenye rangi mbili italeta madhara katika Uchaguzi Mkuu wa 2015 kwamba tunaweza tusishinde dola basi madhara hayo ni muhimu kwani lengo letu lisiwe tu kwenda Ikulu bali kubadilisha fikra ya utawala katika kutenda na kuamua .

" Ni bora Simba wakali mia moja walioko Nje kuliko nyoka mdogo mmoja aliye ndani " Chadema lazima ifanye maamuzi sasa ya kusafisha Nyumba yake la sivyo itakuja kujuta katika siku za mwisho , wasaliti wote waondolewe hasa yule Kiongozi wao kwani hakuna genge la usaliti lisilokuwa na Kiongozi , kuna Watu wengi Vijana wamekuwa wahanga na ndoto zao kupotea katika Siasa kwa sababu waliongozwa vibaya na Kiongozi mkubwa anayeratibu usaliti ndani ya Chama .

Mtu huyu wote tunamjua ni matumaini yangu Usaliti wake sasa utafika kikomo kama Chama kitaamua kuwa na busara za kutosha katika kujenga siku njema zinazokuja . Mtu huyu amefanya mambo mengi mabaya katika Chama yanayohusu usaliti na amewaponza Vijana wengi na kuangamiza ndoto zao kwa sababu ya mambo yake binafsi .

" To me, the thing that is worse than death is betrayal. You see, I could conceive death, but I could not conceive betrayal." Malcolm X



Lema Godbless - Mp


Sometimes kuficha ujinga ni jambo bora sana kuliko kuja hadharani na kuzungumza vitu visivyo na mantiki,weledi na vilvyokosa mashiko kias hiki??

Umezungumza ukiwa umelewa au ukiwa na akili zako timamu??

Naona sasa mmeamua kutangaza vita RASMI,

KWA STYLE HII CCM ITAONDOKA VIPI MADARAKANI??

MISIMAMO YA KINA MALCOM X INAKUPOTOSHA SANA,MATTER OF FACT ZITTO KABWE HUMUWEZ HATA KAMA UMEAMUA KUJA RASMI KUMCHAFUA,AMEYAFNYA MENGI NA BADO ANAYAFANYA MENGI NDAN YA CHAMA NA KITAIFA,WE UMEFANYA NINI??

ANA FOLLOWERS NDAN YA CHAMA NA KITAIFA,WEWE UNA NIN??

UMEJIVUA NGUO KWELI KWA HILI,KWA UFUPI UMEPROVE KUWA WEWE NI KIHIYO NA KANJANJA...
 
YOTE hiyo ni sumu ya ccm,wamepandikiza mamluki CDM. Kuweni makini wanachadema.
 
Toa maneno ya kujenga chama,watu wako busy kushauriana wewe unasherehesha chorus!!!!
Nyie ndio mnapotosha chama,kila siku lugha za hovyo hapa leo inajitajika busara hapa sio ucheshi!!!

soma juu kuna post yericko vizuri, na hoja ya hapa ni usaliti sasa uchesh upi tena.
 
this is obviously personal attack from anonymous .
mungi muite lema aje ajibu hoja hapa! We huwezi kutetea vp tuhuma za jamaa ni za kweli kua lema kakopa hela za chama na hajarudsha?
''chadema since 2006 at age of 16''
 
Mkuu leo sisi wa Lumumba tuekaa viti vya VIP tukitazama mpambano na myukano ndani ya zizi la CHADEMA.
Mie naenda agiza popcorn na kuangalia episode hii inaendeleaje.
Tumeaonya kutofua nguo za ndani hadharani kwa afya hawasikii.
Sasa ndio inadhihirika hawa F4F wakikamata nchi, patakuwepo na idara maalum ya Majungu.

Mnaitana katika ushirika wenu wa wanga kwa kukiombea CHADEMA mabaya.Haitokei ,traitors wanashughulikiwa squarely.So just go home.Usivute kiti kusubiri
 
This is obviously personal attack from anonymous to the verified. We unaweza kuwa mwathirika wa the so called peeling back the mask!!

Ehee hee, inauma hee, safi sana. Na bado. Uzuri ni kwamba hawa wajinga wenu wana udhaifu mkubwa mno. Tutawaanika hapa hadi mtakapoacha ujinga wenu wa kumshambulia kiongozi wa chama kwa sababu tu hammpendi. Kama nyie ni wanasiasa kwa nini mnaogopa uchaguzi? Kwa nini msiache twende kwa wanachama waamue watu wanamtaka nani na waamue nani msaliti na nani ni mpiganaji wa kweli? Kama mlifikiri hiki chama ni cha kwenu mmekosea, tulishapita huko. Tutapigania haki zetu hadi tone la mwisho. Tuiteni majina yote.
 
mungi muite lema aje ajibu hoja hapa! We huwezi kutetea vp tuhuma za jamaa ni za kweli kua lema kakopa hela za chama na hajarudsha?
''chadema since 2006 at age of 16''

Aliyetoa hizo tuhuma athibitishe kwa ushahidi
 
maoni binafsi ya watu yataathiri vipi taasisi mkuu?

ya mwigamba yaliathirije taasisi? Leo npo na nyinyi hadi umisukule uwatoke. Tunataka cdm iwe na vjana wanaoweza kutetea demokrasia na kusimamia ukweli
 
Mheshimiwa Lema,

Hakika mimi niseme maneno machache tu,

Kwamda wa miaka 8 niliyoanza kuhudumu katika siasa kali niseme wazi, kikwazo kikuu cha kuelekea mageuzi ya kweli katika nchi hii kupitia siasa za mageuzi ni Zitto Zuber Kabwe,

Narudia tena Zitto Zuber Kabwe ndie msaliti namba moja na ndie kiongozi wa migogoro yote kila itokeapo ndani ya Chadema,

Sisi tumemaliza kazi yetu sasa tumewaachia wafanyamamuzi,

Sasa mkimshindwa tutachukua jukumu la kihafidhina zaidi wenyewe

Una uhakika na uyasemayo? soma hapa:

From @Zitto

Wana JF, kuna uzi umewekwa hapa na member anajiita Jason Bourne ambao unarusha shutuma zisizo na ushahidi wowote (maneno ya kuungaunga) dhidi yangu.

Hiki kinachoitwa uchunguzi ni hekaya ya kutungwa ambayo haina kichwa wala miguu na ninashangaa ni kwanini inaweza hata kufikiriwa kuwekwa hapa JF maana sheria za JF zinahitaji mtu aje na ushahidi kwa tuhuma nzito kama hizi.

Moja, Kuonyesha kuwa hii ni hadithi wanaongea mambo ya Buzwagi Juni 2008 wakati Taarifa ya Kamati ya Bomani iliwasilishwa Bungeni mapema kabla ya hapo. Buzwagi ni suala la mwaka 2007 na hizo hadithi zote za kutungwa wala haziendani na hali halisi.

Pili, Hekaya hii inataja namba za simu ambazo wala sijawahi kuwa nazo katika maisha yangu na hata pale walipopatia baadhi ya namba wameandika mambo ya uongo kabisa. Inasikitisha wana JF hata hawahoji hili.

Tatu, hizo Benki zinazotajwa wangeweka angalau bank statements basi kama ushahidi (mimi nawaruhusu kama wanao ushahidi huo badala ya kuchafua majina ya watu kwa nia zao chafu). Katika maisha yangu yote sijawahi kuwa na account iliyofikia kiwango kinachotajwa na wala sijawahi kuwa na account kupitia kwa mtu yeyote. Waje na ushahidi ili tuweze kujadili kitu chenye tija.

Nne, Benki za Ujerumani zinazotajwa ni uwongo mtupu, maana sijawahi kuwa na account huko. Wasiishie kutaja akaunti, walete ushaidi usio wa maneno.

Tano, mbaya sana wanataja watu wasiohusika na masuala haya kwa kuwachafulia majina na taasisi wanazofanyia kazi. Huyu dada Andrea Cordes masikini ni mdada wa watu innocent anaingizwa kwenye ujinga kama huu na hata sehemu anayofanyia kazi. Hii ni mbaya sana. Naomba JF isiruhusu mambo kama haya. Maadui zangu kisiasa wapambane na mimi wasionee watu wasio na hatia!

Moderators na administrators wa JF, msiruhusu hekaya kama hizi kuharibu jukwaa. Naomba tuanzishe jukwaa la watunga hadithi ili tuwape fursa ya kuandika hadithi kama hizi!

Zitto
 
Ukweli Usemwe:

Naona umekuja kujibu kwa id yako feki,

Njoo kwa jina lako halisi mkuu,

Mwandiga wanakushangaa
 
YOTE hiyo ni sumu ya ccm,wamepandikiza mamluki CDM. Kuweni makini wanachadema.

Hamna cha CCM. Mamluki tunajipachika wenyewe kwa woga ya baadhi ya wajinga. CCM ni wachovu mno sasa hivi wala hawana uwezo huo. Wangekuwa na uwezo wangeshatumaliza siku nyingi.
 
Sometimes kuficha ujinga ni jambo bora sana kuliko kuja hadharani na kuzungumza vitu visivyo na mantiki,weledi na vilvyokosa mashiko kias hiki??

Umezungumza ukiwa umelewa au ukiwa na akili zako timamu??

Naona sasa mmeamua kutangaza vita RASMI,

KWA STYLE HII CCM ITAONDOKA VIPI MADARAKANI??

MISIMAMO YA KINA MALCOM X INAKUPOTOSHA SANA,MATTER OF FACT ZITTO KABWE HUMUWEZ HATA KAMA UMEAMUA KUJA RASMI KUMCHAFUA,AMEYAFNYA MENGI NA BADO ANAYAFANYA MENGI NDAN YA CHAMA NA KITAIFA,WE UMEFANYA NINI??

ANA FOLLOWERS NDAN YA CHAMA NA KITAIFA,WEWE UNA NIN??

UMEJIVUA NGUO KWELI KWA HILI,KWA UFUPI UMEPROVE KUWA WEWE NI KIHIYO NA KANJANJA...


Malcolm K alikuwa mwanaharakati
CHADEMA ni chama kilichopo kwa mujibu wa sheria za nchi

inashangaza mtu anagombea posho anakuja kumtumia Malcolm X kudanganya watu humu
 
Ehee hee, inauma hee, safi sana. Na bado. Uzuri ni kwamba hawa wajinga wenu wana udhaifu mkubwa mno. Tutawaanika hapa hadi mtakapoacha ujinga wenu wa kumshambulia kiongozi wa chama kwa sababu tu hammpendi. Kama nyie ni wanasiasa kwa nini mnaogopa uchaguzi? Kwa nini msiache twende kwa wanachama waamue watu wanamtaka nani na waamue nani msaliti na nani ni mpiganaji wa kweli? Kama mlifikiri hiki chama ni cha kwenu mmekosea, tulishapita huko. Tutapigania haki zetu hadi tone la mwisho. Tuiteni majina yote.

Unatoa vitisho ukiwa nyuma ya keyboard kwa ID fake?Njoo front kwa jina lako kama kweli wewe ni tishio kiasi hicho.Usitafute sympathy kama ilivyo kawaida yako.
 
Status
Not open for further replies.
Back
Top Bottom