Usaliti na Unafiki unavyoangamiza Taifa - Lema

Usaliti na Unafiki unavyoangamiza Taifa - Lema

Status
Not open for further replies.
Itakuwa umewasaliti wanachama wako kama hujamtaja huyo mtu kwani Huwa nasikia sera ya Chadema ni uwazi na ukweli. Na katibu mkuu wenu amekuwa muwazi na Mkweli je huoni kuwa wewe ndiye mnafiki kwa sababu hujataja jina na wakati unamjua
 
Tatizo la CHADEMA huyo wanayemwita msaliti ana nguvu na wakifuata njia za sheria na demokrasia anaweza kuwashinda kirahisi sana akawa yeye ndo mwenyekiti.

Sasa ndo maana wanazunguuka zunguuka kujaribu kutafuta loop hole ya kumuondoa.

Qanamuogopa huyo 'msaliti' kuliko wanavyoigopa CCM...
 
Hivi unafikiri lema kulalama humu kuna saidia kumuondoa mnafiki kwenye chama zaidi ya kuendeleza malumbano yasiyo na tija? hivi kwanini lema aoneshe kuwa chadema kina lea wasaliti? kwanini asipeleke ushahidi wake kwenye vikao vya chama.

hawezi kwani wanayemtuhumu ndio anasimamia ukweli, katiba na maamuzi ya vikao vyao......kasimamia kutochukua posho, wakati wanachadema wabunge wote walisema hawatachukua posho

Katiba yao imebakwa na adui yao mkubwa aliyebaki ni zittto akna kafulila, shonza, mtela, mwigamba, marehemu wangwe n.k wooote waliondoka na same tuhuma juu ya CDM, si chama cha wanachama ni cha watu wachache na ubabe wao na nguvu yao

Itakuwa raha kwa uongozi wa sasa wa chadema kufanya lolote kumuondoa zitto kabwe ambaye anasimamia haki na ukweli......wakimwondoa wanapata raha,

Lema anaona kila mtu mjinga humu ANAJIANIKA VIBAYA SANA, na zitto yuko mioyoni mwa watu wapende wasipende.............matatizo yote ya nchi hii Lema anakuja na wasaliti wa taifa na chama

wasaliti nyie msiofanya uchaguzi kihalali na kupoteza matumaini ya wataka mabadiliko, CDM ni mbaya sana kuliko CCM at this point na view..................WATU WAZURI WOTE WALIO NDANI YA CDM wanaoisaidia jamii na taifa ndio wabaya wa CDM....something is wring here

Chacha wangwe alitaka ubia wa wananchi na ule mgodi wa dhahabu musoma, akasimamia hoja na kupinga ndani ya CDM na akaishia kufa............SOMETHING IS WRONG HAPA
 
Kweli nimeamini Zitto wewe ni mzito ya CDM ndo wanakuogopa hivyo hongera kaka hii inaonuesha wazi wanakogopa kukuface ndo maana wanatumia mafumbo mengi na misukule kukuchafua,Kua imara ninayo Imani kubwa.Mungu akujalie afya Tele.
 
mwigamba alitumia id fake, lema ametumia id yake mwenyewe.

ndo umejibu nini sasa! Kama kosa wote wameropoka jf na sio chamani.we kweli msukule hata kufikr huwezi.so lema angetumia fake id angekuwa na kosa? Poor u
 
Na ili tusirudi huko ni lazima tuchukue different approach ku-deal na elements zinazofanana na zile zilizoiua NCCR-Mageuzi.Ndiyo falsafa ya kumtoa nyoka mdogo ndani

Umetajwa kuwa ni mmoja wa wasaliti na umepokea hongo kupitia simu yako. Vichupa usivisahau mambo yako jikoni.

Kwi kwi kwi teh teh teh.
 
wanafiki ni wachokozi wa mijadala, halafu haooo wanakimbia, wanashindwa kutetea hoja zao, sasa kama si uchonganishi, uzandiki na unafiki nini?

Godbless J Lema, kama unasimamia ulichokiandika na kwa kuwa upo online, rudi utetee ulichoandika dhidi ya hoja za wasomaji wako, vinginevyo wewe ni troublemaker tu

Kwa akili zako finyu utakuwa umekaa pembeni unasoma michango ya wasomaji ukifurahi ukiamini umekomesha msaliti, lakini laiti ungetambua damage uliyofanya kwenye chama kwa kupanua mpasuko mlio nao, nasikitika sana kwa siasa zetu
 
Kwa hili Lema sikubaliani na wewe. Nafikiri cdm ni kwa ajili ya wote na sidhani kama watu wote wako sawa kila moja ana madhaifu yake. Nionavyo hapa ni hili la wewe kukorofishana na zitto kuhusu swala la posho kama ni kweli utakuwa umeenda kinyume. Zitto apokei posho wewe unapokea posho sidhani kama zitto amelalamika sehemu kuwa kwanini wabunge wa cdm wanapokea posho. Sasa kama wewe unapokea posho kwanini umseme mwenzako, wewe pokea lakini katika kujenga chama muwe kitu kimoja. Hapa kama ni kweli kisa cha kutoelewana na zitto ni posho na ndio maana umeandika basi nawe utakuwa na mapungufu.

Vijana wangapi wameadhiriwa na huyo kiongozi kama unavyodai, sawa ni wengi lakini siku zote hizo ulikuwa wapi kuwasemea mpaka baada ya kutofautiana kuhusu posho. Sio kila jambo lazima ulalamike hapa Jf nafikiri mngekaa kwenye kamati zenu na kila moja kutoa dukuduku lake baadae mnaelewana ndio namna ya uongozi. Usitegemee ndani ya chama mtakaa bila kutofautiana siyo rahisi hata hizo nchi kubwa zilizoendelea wanatofautiana ndani ya vyama vyao lakini baadae wanakaa na kuondoa tofauti zao.

Usitake kuleta chokochoko kitakachoibomoa moja kwa moja cdm kumbuka mwaka 2015 cdm wanategemea kuchukua nchi na hata isipochukua nchi inategemea kuwa na wabunge wengi ndani ya bunge. Nakuambia leo kuwa mkiibomoa cdm leo na mwaka 2015 mkakosa kuchukua nchi au kupata wabunge nusu ya bunge basi cdm ndio kwaheri hautaisikia tena. Kaa ufikirie usifikirie upande wako tu sawa tunajua ulikataa rushwa ya Jk kwa hilo tunakushukuru na kukuheshimu. Kaa na viongozi wako muongee lugha moja. Shibuda amefanya mangapi mbona hujaandika nakala kwa ajili yake. Shibuda amemtesa kada wa cdm dodoma hoteleni na akawa anajifanya kumpigia jk simu kumbe anaongea na mama wa mipasho nyama ya wazee. mbona hajatimuliwa kwenye chama mpaka leo?
 
nashukuru JF kwa kuifanya kazi ya kushika nchi kwa ccm kuwa rahisi,viongozi wa juu m4c wanakuja lia kwenye mitandao badala ya kuchukua hatua kwa mujibu wa katiba na sheria za chama.

Mbona Shibuda mnamjua kuwa ni mnafiki wazi wazi msichukue hatua yoyote?mmechelewa kama mamluki m4c wapo wengi hasa kwenye uongozi wa mikoa na wilaya
 
Tatizo kila asiye mmoja wenu akishauri humu mnashambulia kwa majina ya mnafiki,gamba,pandikizi,mara oonh hatred speech,sijui jealous!!!!!!

Mnataka kugeuka/kama bado much know and well experienced,mkishajiita kamanda basi wengine in uchafu tu mbele yenu!!!!

Jana nimewaambia kifo chenu ni kwa sababu mnaogopa kusema NO pale mnapokosea haswa kwa viongozi hata wakikosea live bila chenga mtataka kumpongeza,ili iwe nini????!!!!!

Kuna siku humu Dr. W. Slaa alinijbu post kwa kusema "tumia akili yako uliyopewa na mungu" then I asked myself huyu ndio kiongozi mkuu!!!!???? Lakini wafuasi walishabikia lugha ile!!!!!!

Jana tumeshinda tukisema kauli za juu ya posho sio sawa, Mungi ulikaa kifua mbele kutetea na wengine weeeengi sana; Rose Mayenga alianzisha uzi hapa hauna mantiki lakini ulishabikiwa na wafuasi saaana kumbe ni kuongeza mpasuko!!!!!!!

Sasa leo mnamalizia tu mzunguko ili furaha yenu itimie hata kama mnaenda nje ya track sababu ni makamanda wakuu endeleeni tu maana ukweli wa usoni kwenu sio sehemu ya maisha!!!!!!!

Ruttashobolwa yuko sahihi kabisa,ila bado mnampinga! !!!!!!!!!Kwa faida ya nani????!!!!

Inawezekana humo ndani kila kiongozi ana wafuasi wake ndio maana umoja wa kweli ni mashaka mashaka!!!!!!Yawezekana kiongoz mmoja haelewani na wenzake hivyo na wafuasi wamo vitani bila ya kuwa na common interest!!!!!!

Mtaona kama mnafuatwafuatwa lakini mjue mmebeba dhamana kubwa!!!!!!Kwa nini mmekuwa wagumu kiasi mnaingia hatari ya kujifunza kwa makosa????!!!



Just observations
 
Msimamo wa mbowe,slaa ni kuwa zitto ni msaliti. Hawawezi kumfukuza na wakiitsha uchaguzi huru na haki ztto anachukua kitengo. Ukweli mchungu ni kuwa zitto akfukuzwa chadema ndo mwsho wa wanachadema wenye akili kuwa cdm.watabaki wapuuzi tu na misukule
 
Mkuu Lema, pengine utusaidie kutupatia maana halisi ya 'Usaliti', 'Unafiki' na 'utu' kwa namna uelewavyo wewe.

Maneno haya kutoka kwako yananishangaza kidogo, kwa vigezo kuwa kwa yale unayofanya nawewe unaweza fuzu kuitewa Mnafiki na Msaliti asie na utu. Labda kama unatumia hii njia kujikosha baada ya wewe pia kutambua kuwa umeonyesha Usaliti mkubwa kwa Watanzania unaowawakilisha.

Lema inatakiwa uelewe haya;

Unatakiwa kujua kuwa hata kina KUBENEA wameshakuchoka, yeye si mmoja wa hao anaowasema? (Au woga ambao siku zote unashabikia ni sumu leo si sumu tena?), pitia hii https://www.jamiiforums.com/jukwaa-la-siasa/547535-mh-lema-anaivuruga-chadema.html

Watanzania wengi washakushtukia, unakiruvuga chama kwa siasa zako za kishabiki na kitoto wenzetu wanaita 'armature' (an insult ukiichukulia undani wake) pitia hii https://www.jamiiforums.com/jukwaa-...gwe-gavana-rahisi-kusababisha-mitafaruku.html

Inawezekana unawashambulia Shibuda na Zitto kwenye bandiko hili, vipi ni kwakuwa wewe Lema unapenda sana Posho hivyo umeamua liwalo na liwe? pitia hii https://www.jamiiforums.com/jukwaa-...bungeni-zitto-lema-katika-vita-ya-maneno.html

Au unataka kusema hizi posho zinamaanisha Uzalendo na Utu kwa Taifa? (Are you serious??). Zitto alisha litabiri hili na kueleza wazi (hakutumia unafiki) kuwa Siasa za Posho zitasababisha mjenge chuki na mmwite majina yote mabaya! www.jamiiforums.com/jukwaa-la-siasa/299635-zitto-sijahongwa-ni-siasa-za-urais-na-hasira-za-posho.html

Au hii ndiyo step ya kwanza ya kufanya Zitto aondoke Chadema? Maana inajulikana wazi kuwa kuna mkakati wa kumkatisha tamaa Zitto aondoke CHADEMA mapema kabla mwaka haujaisha ili mpumue ndani ya chama cha watu wa Kaskazini (viongozi wa juu). Inaturudisha kule kule mnako kukataa siku zote (Udini/Ukabila).

Pole zako Lema, watanzania wa leo si mabwege!
Ukitaka kutenda haki kwanini usiiweke na hii https://www.jamiiforums.com/jukwaa-...-dhambi-dhambi-ni-posho-inapokosa-utu-16.html au na wewe ni kati ya alio wataja....
 
Godbless J Lema

Naona umekuja na mipasho badala ya hoja watu wakiwambia chama chenu kina ubaguzi mnalalamika.
 
Last edited by a moderator:
hawezi kwani wanayemtuhumu ndio anasimamia ukweli, katiba na maamuzi ya vikao vyao......kasimamia kutochukua posho, wakati wanachadema wabunge wote walisema hawatachukua posho

Katiba yao imebakwa na adui yao mkubwa aliyebaki ni zittto akna kafulila, shonza, mtela, mwigamba, marehemu wangwe n.k wooote waliondoka na same tuhuma juu ya CDM, si chama cha wanachama ni cha watu wachache na ubabe wao na nguvu yao

Itakuwa raha kwa uongozi wa sasa wa chadema kufanya lolote kumuondoa zitto kabwe ambaye anasimamia haki na ukweli......wakimwondoa wanapata raha,

Lema anaona kila mtu mjinga humu ANAJIANIKA VIBAYA SANA, na zitto yuko mioyoni mwa watu wapende wasipende.............matatizo yote ya nchi hii Lema anakuja na wasaliti wa taifa na chama

wasaliti nyie msiofanya uchaguzi kihalali na kupoteza matumaini ya wataka mabadiliko, CDM ni mbaya sana kuliko CCM at this point na view..................WATU WAZURI WOTE WALIO NDANI YA CDM wanaoisaidia jamii na taifa ndio wabaya wa CDM....something is wring here

Chacha wangwe alitaka ubia wa wananchi na ule mgodi wa dhahabu musoma, akasimamia hoja na kupinga ndani ya CDM na akaishia kufa............SOMETHING IS WRONG HAPA

Umesahau akina Arfi na Safari licha ya kuwemo kwenye chama na watu wenye hadhi zao lakini wamewekwa picha tu. Cheza na Mtei wewe.

Na nnawaeleza hapa, hii haiishii kwa hao tu, Dr.W.Slaa pia saa hizi ni mguu ndani mguu nje, tumeshazihisi chokochoko humuhumu JF.

Kuna habari za kuaminika kabisa kutoka jikoni kuwa Slaa kakatiwa marupurupu kibao.

Kuna miaka ya nyuma Zitto aliambiwa hao huwawezi watakutenga tu, hakuelewa. Waswahili hunena, "kiranga komo".
 
Last edited by a moderator:
Ahaaaa, haa, Kamanda Lema umewatumia vijana wako weee umeamua uje mwenyewe mzimamzima, karibu sana. Jana imeongelewa sana hii makao makuu kwamba umeamua liwalo na liwe, utamvaa jamaa kwenye mitandao ikiwa ni maandalizi kuelekea kikao cha kamati kuu. Nilipuuza kumbe ni kweli umejipanga. Ni hivi:

i) Hakuna mtu mnafiki na msaliti kama wewe, hata kama hujijui kwamba wewe ni mnafiki. Ungekuwa sio mnafiki na zezeta hata issue ya mwigamba isingetugharimu kwa kiwango tunachokiona leo. Ungekuwa sio mpenda sifa issue ya Mwigamba ungeweza kuiwasilisha vizuri kwenye kikao chenu naye akaitwa na akachukuliwa hatua stahiki bila makelele. Lakini kwa unafiki na uzezeta wako uliona cha maana ni kupiga makelele kama vile umekamata mwizi na kuanza kurusha matofali na kukimbilia polisi bila kutafakari kwa makini athari zake za muda mrefu. Usingefanya hivi kwa sababu uwezo wako wa kufikiri ndio huo. Pole sana kamanda. Hatuna namna kwa sababu ndio watu tulionao itabidi tukuvumilie hivyohivyo ili tufike hiyo 2015.

ii) Kupenda kwako sifa ndio kunatuangamiza sana. Vurugu zote huku Arusha ni kwa sababu una wasiwasi na ubunge wako, kila mtu unayemuona anaweza akatamani ubunge unamzushia jambo. Tunajua next kwa Arusha ni Nanyaro, bahati nzuri huyu yupo smart sana na hutampata kwenye mitego yako ya kijinga. Na atagombea ubunge 2015 kwa ticket ya CDM na atakushinda kwenye kura za maoni-hilo unalijua vizuri sana. Mwenyekiti wetu (kama ataendelea) atajaribu sana kukuokoa ili upewe nafasi ya kugombea, lakini najua atagonga mwamba.

iii) Kwenye vikao huna hoja za kushawishi wajumbe. Umeshasema haya maneno kwenye kikao mara kibao lakini kila mara umeshindwa kuthibitisha juu ya hatari ya huyo unayemsema (sitomtaja hadi utakapothbutu kumtaja wewe mwenyewe). Na mara nyingi amekwambia utaondoka wewe kwanza kwenye CDM kabla yake kama ulivyoondoka NCCR na baadaye TLP. Mwenzako hajawahi kujiunga na chama chochote zaidi ya CDM. Wewe ulianzia CCM, ukaenda NCCR, TLP na kisha CDM. Na upo CDM kwa sababu ya ubunge, siku ukikosa ubunge utatimka tena.

iv) Nani asiyejua kwamba ulikuwa uuze ubunge kwa Lowasa lakini vijana wa Arusha wakakudhibiti hata kukutishia kukuua? Wewe unapenda hela kuliko chochote. Ndio maana huna aibu kung'ang'ania posho bungeni huku ukijua vizuri kwamba sera za chama zinakataza habari za posho ya kukaa. Nani msalti hapa? Mlimuingiza mkenge mwenyekiti wetu akarudisha gari kwa jazba. Siku mbili akakimbia na kupiga magoti kwa Katibu wa Bunge kuomba arudishiwe gari akilia kwamba ilikuwa siasa tu. Haya ni nani mnafiki na msaliti hapa? Mlikubaliana kususia posho, lakini mlikuwa wa kwanza kuzikimbilia na leo unapiga makelele kwa mdomo mkubwa muongezewe, nakuuliza ni nani mnafiki hapa? Au ulivyo kilaza hata maana ya neno mnafiki na msaliti hujui?

iii) Unajua vizuri sana taratibu za CDM za kushughulikia haya unayeyaongea, lakini kwa sababu upo dhaifu sana na huna uwezo wa kuwasilisha hoja kimantiki ikashawishi wajumbe ndio umeamua kuibukia huku baada ya kuona mabasha yako akina Ben wamekwama. Nawe utakwama tu kwa sababu ukweli siku zote hujulikana, kama ule wa kudanganya mambo ya katiba ulivyojulikana.

iv) Hata kama hujijui, ukweli ni kwamba wewe ni kikwazo kikubwa sana kwa watu makini kujiunga CDM. Hakuna mtu mwenye akili sawasawa anaweza kukuchukuliwa wewe kwa umakini wowote. Inashangaza kwamba mwenyekiti wetu alikuona wewe ndio mtu anayefaa kuwa waziri kivuli wa mambo ya ndani. Yaani wewe tukishinda 2015 ndio utapewa uwaziri wa mambo ya ndani?

Endelea kumwaga ----- wako, tutarudi na mengine kwa sababu tunakujua vizuri kuliko unavyojijua. Next ukiendelea nitatoa photocopy na kuscan nyaraka ya fedha ulizokopa chamani na ambazo hujarudisha hadi leo. Wewe endelea na ujinga wako wa kuchafua viongozi mitandaoni.
 
Msimamo wa mbowe,slaa ni kuwa zitto ni msaliti. Hawawezi kumfukuza na wakiitsha uchaguzi huru na haki ztto anachukua kitengo. Ukweli mchungu ni kuwa zitto akfukuzwa chadema ndo mwsho wa wanachadema wenye akili kuwa cdm.watabaki wapuuzi tu na misukule
Wapi kaburu...
 
Lawyer,

It is unfortunate wewe siyo mhudhuriaji sana wa hili jukwaa, ama we ni msomaji zaidi ya mchangiaji. Kama unavyoelewa kuna mada nyingi dhidi ya Lema siku za hivi karibuni, ambayo ilitaka kugeuza taswira sahihi na watu wakauamini uwongo kuwa ukweli.

Lema hajamtaja mtu, bali ametoa hili kama angalizo kwa chama akiwa verified. ni kweli kwamba hakumjua leo huyu msaliti.

Kwa kufanya alichokifanya Lema jamii inajua Lema ni mtu wa namna gani. Kukaa kimya wakati mwingine jamii inaweza kuaminishwa tofauti na ukweli.

Alichokifanya Lema ni kutoa elimu kwa jamii kuwa wanafiki na wasaliti siyo wakuvumiliwa hata kidogo. wanatakiwa kuondolewa kabla hawajaleta madhara. Ni jukumu la chama sasa kuchukua hatua.

Kuleta hii mada humu inasaidia jamii hasa GTs kutoa maoni yao juu ya hatua inayotakiwa kuchukuliwa dhidi ya wasaliti mahali popote siyo tu chadema, bali hata kwenye taasisi zingine za kujamii

Mkuu Mungi nikutoa wasiwasi tuu kuwa mimi ni mhudhuriaji mzuri hapa sema si changiii kila mada.

Lema hapa ametoa tuhuma kabisa na ameonesha kuwa chama kina lea wasaliti.
Je ni kweli chama kina lea wasaliti?
Lema kama ange kuwa anatoa elimu ange anza na maana ya usaliti na ange tupa njia za kupambana na wasaliti.

Lakini analo lifanya hapa ni kutoa tuhuma wakati ana nafasi za kusema kwenye chama.
wabunge wengi wa chadema na viongozi wakija humu hawatoi tuhuma bali kijibu tuhuma.

Lema amepotoka.
 
Last edited by a moderator:
Status
Not open for further replies.
Back
Top Bottom