Usaliti na Unafiki unavyoangamiza Taifa - Lema

Usaliti na Unafiki unavyoangamiza Taifa - Lema

Status
Not open for further replies.
Lema hajataja jina la mtu lakini umma unavyotaja majina hapa ni hatari
 
ukiona mzinzi,hatambui tabia zake za kubaka nimbaya huyo sio binaadam.

Lema huna maana,kwanini hayo unayonena hapa jf,usiyaseme kwenye vikao vya ndani?

Au nawewe nimwigamba mwinngine?unatofauti gani na wale wanafiki wanaoshindwa kusema mambo wakati mhusika akiwepo?

Huoni kutotaja jina la huyo msaliti,kunakushushia ujasiri wako wakutokuwa muoga?
 
ukanda na ukaskazini,ubagizi na uchu wa madaraka,chadema haiwezi kusimama kama itakuwa ya kilimanjaro na Arusha,Zitto tumekisubiri kwa hamu 2015 ili uendelee kituunganisha vijana ukiwa mwenyekiti wa chadema.. Taifa hakuna wa kukuzuia,hawa mamluki waliotoka CCM,NCCR,CUF,TLP na UDP waikukatishe tamaa,chapa kazi za ujenzi wa chama.waache waropoke maana wameshikwa pabaya.Nakuomba isiwajibu chochote,si hadhi yako,tuache tuwaelimishe hawa wauaji.
 
Mheshimiwa Lema,
Kutokana na ujumbe wako huu, ni wazi ndani ya CHADEMA kuna matatizo ambayo ili chama kisonge mbele, kinahitaji kuyashughulikia.

Kwa mtu yeyote anayejua demokrasia ya kweli, matatizo yatokanayo na misimamo tofauti ndani ya vyama, hutatuliwa kwenye sanduku la kura.

Kama ndani ya CHADEMA kuna wasaliti, basi njia bora kuliko zote na ambayo historia inatuonyesha ndio mwarobaini mzuri, ni kuitisha uchaguzi ili wanachama waamue kama hao watu ni wasaliti au ni wakombozi. Ni wanachama tu wana mandate ya kuamua nani awe kiongozi kwenye vyama vinavyofuata misingi ya kidemokrsia.

Waziri mkuu wa Uingereza, Thatcher, alipokuwa challenged na wasaliti ndani ya chama mwaka 1989, aliitisha uchaguzi wa wa chama na akashinda na wasaliti wakapotea.

Mwaka 1990 ukatokea usaliti mwingine na safari hii Tatcher akashindwa na wasaliti wake na Major akachaguliwa kuwa PM.

Kwa maoni yangu mimi, kama ndani ya CHADEMA kuna usaliti, basi ni kuwaambia hayo makundi kukutana kwenye kisanduku cha kura ili wanachama wawaondoe wale ambao wanachama wanaona hawafai.

Lakini hii yakuitana wasaliti kwrenye mitandao, sidhani kama itakisaidia chama hata kidogo. Kibaya zaidi mtawatisha hata wale watu wazuri ambao wangependa kuungana na CHADEMA 2015. Hakuna mtu makini anayependa kwenda chama ambacho kutofautiana mawazo unageuka kuitwa msaliti.
Hitaji la CCM ambalo CDM walilishtukia. Utashindana kwa kura na mtu mwenye uwezo na nia ya kuwanunua wapigakura wote? If that is what you call democracy, wacha CDM iende kidikteta. Haya mapesa aliyowarushia kina Ben yalikuwa na lengo gani? Zitto is ambitious, and he has every right to be, but he should move rationally.
 
Ndugu Lema
Ni vizuri kuchukua hatua kuliko kulia lia
1. Peleka taarifa kwa uongozi wenu
2. Mtaje nani huyo ili umma ujue
 
Mie nimekujibu tu ulivyotumwa uweke hapa. Kawapelekee walio kutuma wakutafsirie, huna haja ya kuleta maneno ya kashfa sababu tu umeshindwa hoja. Si lazima wote mpost. Wengine kuweni wasomaji inatosha.

Unataka kusema nini maana naona unahara tu..
 
Saa nane na sifa ya ushika pembe wakati Lema anakamua maziwa.
your the full coward like a women
 
Nasema tena lema umepotoka na katika haya unachangia kukivuruga chama.

Sasa umeleta mjadala mwingine ambao pengine hauna tija hapa.
Viongozi wenzio na wabunge wanakuja humu kujibu tuhuma si kuleta tuhuma.

Lema huu ni ujinga tuu na hausaidii chama kabisa bali mnatukera wanachama.
 
ukanda na ukaskazini,ubagizi na uchu wa madaraka,chadema haiwezi kusimama kama itakuwa ya kilimanjaro na Arusha,Zitto tumekisubiri kwa hamu 2015 ili uendelee kituunganisha vijana ukiwa mwenyekiti wa chadema.. Taifa hakuna wa kukuzuia,hawa mamluki waliotoka CCM,NCCR,CUF,TLP na UDP waikukatishe tamaa,chapa kazi za ujenzi wa chama.waache waropoke maana wameshikwa pabaya.Nakuomba isiwajibu chochote,si hadhi yako,tuache tuwaelimishe hawa wauaji.

Hata mimi nataka Zitto awe mwenyekiti ili awanyooshe wale wachaga. Ila kwa bahati mbaya sana zitto ni mkongo na wenye chama ni wakikuyu huwa hawafungamani.
 
Last edited by a moderator:
ukanda na ukaskazini,ubagizi na uchu wa madaraka,chadema haiwezi kusimama kama itakuwa ya kilimanjaro na Arusha,Zitto tumekisubiri kwa hamu 2015 ili uendelee kituunganisha vijana ukiwa mwenyekiti wa chadema.. Taifa hakuna wa kukuzuia,hawa mamluki waliotoka CCM,NCCR,CUF,TLP na UDP waikukatishe tamaa,chapa kazi za ujenzi wa chama.waache waropoke maana wameshikwa pabaya.Nakuomba isiwajibu chochote,si hadhi yako,tuache tuwaelimishe hawa wauaji.
ha ha tangu lini maiti ikaunganisha vijana atangulie kuzimu tutamkuta vijana hatutaki misukule ya CCM yeye aliuza ukanda wa kanda ya ziwa kwa NCCR mageuzi kiwavi huyo
 
Mkuu huhitaji eli ya juu sana kujua nani msariti ndani ya chama cetuu na tumemvumilia sana...

mkuu yegella, inawezekana kweli kuna msaliti lakini si muda muafaka kuongelea weakness wakati bomu la msaliti mwigamba!
 
Hata mimi nataka Zitto awe mwenyekiti ili awanyooshe wale wachaga. Ila kwa bahati mbaya sana zitto ni mkongo na wenye chama ni wakikuyu huwa hawafungamani.

una ka asili ka ubaguzi wewe ....hiyo ni mipaka tu ya wakoloni weupe nyie weusi mnaendeleza ubaguzi mamvo leo kuna wamakonde msumbiji ...
 
Last edited by a moderator:
Naamini katika cdm
lema ni miungoni mwa positive thinker
je kwenye hili umefikiria positively?
 
Lazima ifike muda watu watambue kuwa akili na busara zinahitajika sana ili kufanya nchi yetu isonge mbele. Chadema chini ya hawa akila Lema they dont seem kuelewa upinzani ni nini hasa na unatakiwa uwe vipi??

Lema, pole sana ukidhani umeandika kitu cha maana sana hapo juu kumbe pumba zile zile za akina slaa na mbowe na akina ben saa nane ( the puppet)

Kwanza, taja jina na weka wazi msaliti ni nani? maana inajulikana hauna ushirikiano na urafiki mzuri na zito zuberi kabwe, inajulikana

wewe , salaa, mbowe na wenzenu mmejitahidi kuwafanya wanachadema wengine waonekane mbumbumbu na hamnazo simply kwa sababu wamewaaamini mno, na kuwapenda, kwani CCM imewachosha, lakini mmekaa ki-NGO zaidi, kikanda, kikabila kila kukicha chuki na asilimia 90 ya mazungumzo yenu ni ugomvi wa chama chenu na si kuiondoa ccm inaleta nini?

1. ugomvi wa chama chenu unapoonekana kwa watu wa nje unawavunja moyo hasa wakichukulia historia za cuf na nccr mageuzi

2. ugomvi wa ndani unawarudisha nyuma na kuleta sintomfahamu nyingi kiasi cha kuwa vitani kila mmoja anarudi nyuma maana unaweka viulizo nani wa KUAMINIWA??

3. Unaendeleza ugonjwa wa yaleyale ya mwigamba ya kusemea mtandaoni hivyo basi inaonyesha kuwa

a/. hauna ubavu wa kuwa face hao unaowaita wasaliti ndani ya chama simply kwa sababu UNAOWAITA WASALITI SIO WASALITI ILA WANASIMAMIA HAKI NA UKWELI

b./ umekuja na hoja za wasaliti ukijua JF itaku support kwani JF wengi ni wanachadema, umesahau kuwa ni sehemu ya ukweli na uwazi, WEWE MBUNGE UKILIA HIVI, mwita maranya afanyaje????

c/. mnaowaita wasaliti hamuwezi kuwaondoa kwenye vikao vya chama maana watawashinda kwa hoja za katiba ya chama, kwa mfano HAIWEZEKANI KIJANA KAMA WEWE, SMART, NA AKIL ZAKO unakuwa wa KWANZA KUCHEKEA KUTOFANYA UCHAGUZI NA KATIBA YA CHAMA KUBAKWA kisa uonekane mzuri kwa mbowe na slaa?? mkipewa nchi mtafanyaje??

Hii dalili ya kusemea mitandaoni kwa mtu mkubwa kama wewe ni UDHAIFU na kwa akili zenu mnajua wengine hatuoni vile...na ndio maana mtaishia kutukuzwa na kupigiwa makofi na washabiki na sio umma......utasifiwa na vilaza na waliopofushwa na mahaba yaliyotokana na chuki kwa ccm na sio reality za kuwa nyie ni wakombozi

Lema, SOMA KWA NGUVU HAPA, HATA ZITTO MKIMTOA LEO NDANI YA CHADEMA, ATABAKAI KUWA ZITTO, zitto ni rais anayeishi mioyoni mwa watu, anapendwa, anaogopwa na mafisadi, anasimamia hoja zake, ana uthubutu NDIO YUKO HIVYO, nyakati zile unaendesha ujambazi arusha yeye alikuwa anasoma degree, anaendesha siasa chuo kiku...hajaanza leo....certainly ndani ya chadema watu wa caliber ya zitto hamna na wengine mmewaua au kuwafukuza

Zitto ni bright, tough na focused, hategemei siasa wala CDM yenu ambayo kila wakati mmepaka majina yote mabaya...Lema ,zitto angekuwa fisadi au msaliti hao CCM wangeisha muumbua.........hoja za uswis, hesabu za mashirika ya umma, buzwagi, kutaka kumtoa waziri mkuu, kutaja mishahara ya viongozi, na hoja zingine ndio zinazoifanya sio zito tu CHAMA KIZIMA CHA CDM KIONEKANE KINA WATU makini, lakini kuna uozo wa wewe, sugu na mtei ambao akili zenu mnazijua wenyewe

Yesu alisema, ikiwa ufalme utajifitini hautasimama...kamwe

we have plenty of problems IN THIS COUNTRY which need your attention and your solutions…. wewe UNAONGELEA WASALITI NDANI YA CHAMA??? Hao wasaliti umewajua lini?? wanaogopwa nini mpaka leo hii wasitolewe??

Hivi lema unajua chadema kinapendwa na hata wasio wanachadema?? fanyeni kitu kuwaaminisha watanzania mnaweza Zitto anafanya hivyo, Lissu anafanya hivyo, hata Slaa alivyokuwa mbunge alifanya hivyo...nyie wengine mnafanya nini??? HATUONI

Leo Lema ukifa utakumbukwa kwa lipi?? kuchukua jiwe na kumponda nalo mwigamba?? kufungwa jela?? kutukana matusi kuwa ile mimba ya Lowassa?? why u guys dont evaluate urself ila MNAOGOPA KIVULI CHA ZITTO?? where is nassari where is msigwa, wabunge woooooooote wa CDM ambaye ana international status, anayeweza kuongea kitu akaeleweka na kukubalika ni Zitto peke yake ndani ya CDM...................yet is your no. 1 enemy

utasema hooo sijataja hilo jina Lema, YOU ARE INFERIOR na ukiwa INFERIOR UTAJIONA UKO CHINI NA UTATAFUTA SUPPORT YA INFERIOR WENZAKO kumtafuta mchawi ni nini??

Kama aliyoyasema Mwigamba juzi ni usaliti, wenye akili tuna majibu………………kama post hii umeituma ukiwa na akili timamu, jiuzulu ubunge mkuu.

Lema, kila kitu kina mwisho wake, endeleeni na haya mnayoyafanya nakutakia maisha marefu ila UTAONA MWISHO WAKE, sio mzuri kwa chama.

Zitto kama hamumtaki amueni muondoeni kwenye NGO yenu, ATAISHI HE IS GRADUATE na anaweza kujisimamia. Lema ukiondolewa hapo kwenye siasa za chadema unazobebwa na wenye ufahamu mdogo na nguvu za akina mbowe, huna pa kwenda na hakuna atakayekuelewa.

Chadema, mliamua kwa pamoja hamtaki Posho ( sitting allowance) mmeanda bungeni Zitto katekeleza mliyoyaamua WENGINE, akiwem o wewe na Mbowe mmeshindwa……..Then ZITTO M’BAYA???????

Watchin u​

Huna adabu kabisa Mzee Mtei sio wa kumsema kiwepesi hivyo
 
Safari yetu ya kubadilisha utawala inaonekana kufika ukingoni na nifuraha ya kila Mtu mwenye hisia ya ukweli katika maisha na ninapotazama mbali sana ninaona jinsi ambavyo Usaliti na Unafiki unavyoangamiza Taifa ni bahati mbaya sana uwezi kuwaepuka katika harakati hizi lakini tukiwa makini tunaweza kuwathibiti .

Kama Chadema leo itashindwa kuwachukulia hatua wasaliti wa wazi wa kazi hii njema ni vipi Chadema itaweza kuitaka Serikali na Rais iwajibishe Viongozi wake katika ufisadi na wizi wa mamilioni ? Na Wananchi lazima wajue lengo kubwa na muhimu la Chadema kwanza liwe kubadilisha fikra na mitazamo na kuupa UMMA elimu na mamlaka na nguvu ya kusimamia Taifa lao katika kuhoji ,kudadisi na kukemea , kwani UMMA usipojua wajibu wake katika kusimamia rasilimali na Taifa lao , ukweli utabaki kuwa Nchi itabadilishwa na kufanikishwa na Jamii iliyoamua kuishi matendo dhahiri ya ukweli na haki na sio unafiki na usaliti .

Viongozi wote wa Siasa wanatokana na Jamii kwa hiyo jamii Thabiti inayo furahia UTU ni Nchi bora tutakayoijenga lakini Jamii yenye woga na hofu na Sifa itazaa Taifa lenye usaliti na Wanafiki . Usaliti na Unafiki unaliangamiza Taifa sana . Maombi na Dua za Watu wengi kuelekea 2015ni kutaka kuona Chadema inachukua Nchi , lakini Dua na Sala hizi zina Imani kubwa na Viongozi wa Chadema na sio rangi ya Chadema , hivyo ni muhimu Chadema kuchukua hatua sasa ya kusafisha Chama na kama hatua hiyo muhimu ya kuondoa Watu wenye rangi mbili italeta madhara katika Uchaguzi Mkuu wa 2015 kwamba tunaweza tusishinde dola basi madhara hayo ni muhimu kwani lengo letu lisiwe tu kwenda Ikulu bali kubadilisha fikra ya utawala katika kutenda na kuamua .

“ Ni bora Simba wakali mia moja walioko Nje kuliko nyoka mdogo mmoja aliye ndani “ Chadema lazima ifanye maamuzi sasa ya kusafisha Nyumba yake la sivyo itakuja kujuta katika siku za mwisho , wasaliti wote waondolewe hasa yule Kiongozi wao kwani hakuna genge la usaliti lisilokuwa na Kiongozi , kuna Watu wengi Vijana wamekuwa wahanga na ndoto zao kupotea katika Siasa kwa sababu waliongozwa vibaya na Kiongozi mkubwa anayeratibu usaliti ndani ya Chama .

Mtu huyu wote tunamjua ni matumaini yangu Usaliti wake sasa utafika kikomo kama Chama kitaamua kuwa na busara za kutosha katika kujenga siku njema zinazokuja . Mtu huyu amefanya mambo mengi mabaya katika Chama yanayohusu usaliti na amewaponza Vijana wengi na kuangamiza ndoto zao kwa sababu ya mambo yake binafsi .

“ To me, the thing that is worse than death is betrayal. You see, I could conceive death, but I could not conceive betrayal.” Malcolm X



Lema Godbless - Mp

KWANZA, Nikupongeze na jitihada zako za kuelemisha watanzania wajitambua kupitia haki zao za kiraia na kikatiba. Maana umefanya kazi kubwa na ya kupigiwa mfano katika Mkoa wa Arusha na Taifa kwa ujumla.

PILI ni kupongeze kwa kutoa picha halisi ya safari yetu ya kulikomboa taifa letu kwa mara ta pili maana watanzania wengi nikiwemo na mimi hawana matumaini na mioyo yao imekusosa furaha na matumaini (Kwa mujibu wa tafiti mbalimbali)

Lakini pamoja pongezi hizo mimi nadhani lazima Viongozi wa CHADEMA wote na kama Chama lazima muweke utaratibu wa kuongea mambo ya msingi ndani ya Chama na ndani ya vikao halali. Tunajua na kila mmoja anatambua usaliti unavyokinyemelea chama lakini kwa maoni yangu si afya sana kama kiongozi naye akatoka nje akaanza kulalamika matatizo ya ndani. Waswahili wanasema ukiona Wanandoa wanatukanana upenuni hadharani ujue wameshabishana na kushindwa kuyamaliza ndani.

Naamin hakuna kipindi kigumu na kinachotakiwa kutumia busura zaidi kama hivi sasa. Nishauri tu kwa uongozi ni vyema mkafanya utafiti wa ndani juu ya mambo yafuatayo:-

Kutazama madhara na faida ya kufanya uchaguzi wa ndani kabla au baada ya uchaguzi mkuu kwa kuzingatia mchakato wa Katiba Mpya ya Tanzania.

Pili, Ni kwa kiwango gani Kanda za uongozi mlizozianzisha zinaweza kujisimamia (kiorganaizeshi na kioperesheni) kwa kufanya chaguzi zao za ndani, kukijenga chama kuelekea kwenye uchaguzi mkuu.

Then mnatoka na dira na mkakati wa pamoja kuelekea kwenye ukombozi wa uchumi na kijamii katika nchi yetu.

Nawasilisha.

MFUKUZI

Helsinki Finland.


 
Mh Lema,tumia kauli ya"hakuna dhambi kubwa na mbaya kama uoga" mtaje msaliti huyo ajulikane.
 
Status
Not open for further replies.
Back
Top Bottom