Usaili wa nafasi Jeshi la Polisi mkoa wa Dar es Salaam unashangaza

harunimaiga

Member
Nov 13, 2022
26
47
Usaili wa nafasi za kazi jeshi la polisi umeanza October 31,2032. Mikoa yote nchi nzima. Baadhi ya mikoa wamemaliza usaili kwa ngazi zote, lakini mkoa wa Dar es Salaam bado.

Usaili ufanyika ngazi ya wilaya na mwisho ni mkoa, ambapo kikawaida mitihani ya mchujo ufanyika katika ngazi ya wilaya na wanaofuzu ndio uja kufanya usaili mkoani.

Hii imekua tofauti kwa mkoa wa Dar es Salaam, ambapo waliotuma maombi mikoa yote ya kipolisi (wilaya) wamefanya mitihani ambayo ilikua ni kama ya mchujo lakini hakuna alochujwa. Vipimo vimefanyika lakini Hadi sasa waombaji hawajui majibu ya afya zao kama zitawaruhusu kuendelea na mchakato wa usaili na hatimae kujiunga na mafunzo ya Jeshi la Polisi.

Inashangaza, kwani jumla ya waombaji Hadi sasa ni 1149 na nafasi ziko 118 tu. Je mchakato.

Najiuliza!
1. Inakuaje waombaji wafanye vipimo na mitihani ya mchujo wilayani, lakini hawajatoa majina ya waliovuka ngazi ya wilaya?

2. Kiujumla usaili umeisha,wanapanga kuwapeleka waombaji wote uwanjani kabla hata ya kutoa majibu ya vipimo. Unampelekaje mtu uwanjani na haujapata uhakika WA afya yake.

3. Nafasi ziko chache, waombaji ni wengi na wameacha shughuli mbalimbali za kiuchumi kwa ajiri ya usaili lakini wahusika hawajali upotevu muda kwa watu hawa. Leo ni takribani siku saba(7) Toka kuanza usaili. Mikoa mingine wamemaliza ila Dar es salaam Bado wanajivuta. Hii sio sawa.

Changamoto zingine ambazo najiuliza kweli huu ni usaili wa jeshi au kikundi Cha wakulima?

1. Moja ya sifa ya kuomba nafasi hizi,lazima mwombaji awe na Cheti cha Jeshi la Kujenga Taifa (JKT) lakini cha kushangaza kuna watu hawana vyeti na Bado wanaohusika na usaili hawajawapunguza Ili kurahisisha zoezi.

2. Usaili umeanza October 31 lakini kuna mtu anafika November 2, na Bado wahusika wanamtafuta mtu huyo kumfanyia vipimo au mitihani. Unajiuliza Ina maana jeshi lishakua la kubembelezana siku hizi?

MAWAZO YANGU TU
 
Kweli watu hawapendi kazi za upolisi kiasi hiki kwa jobless ya dar nlitegemea number iwe kubwa zaidi ya hapo
 
Kweli watu hawapendi kazi za upolisi kiasi hiki kwa jobless ya dar nlitegemea number iwe kubwa zaidi ya hapo
nan kakuambia hawapendi, hiyo ni idadi ya waliopita usahili ila walioomba ni zaidi ta 500 kwa dar tuu
 
Back
Top Bottom