Nafasi za Ajira Jeshi la Polisi Tanzania Oktoba, 2023

Jamii Opportunities

JF-Expert Member
Feb 10, 2014
4,438
1,387
Mkuu wa Jeshi la Polisi Tanzania anatangaza nafasi za ajira kwa waliohitimu mafunzo ya
kujenga Taifa (JKT) na Kujenga Uchumi (JKU), waliopo kwenye makambi na nje ya makambi
wenye elimu ya Shahada, Stashahada, Astashahada, Kidato cha sita na Kidato cha nne.

1. Sifa za Waombaji
a) Awe raia wa Tanzania kwa kuzaliwa.
b) Awe amehitimu kidato cha nne au cha sita kuanzia mwaka 2017 hadi 2022.
c) Kwa waombaji wa kidato cha nne na sita wawe na umri kuanzia miaka 18 hadi 25.
d) Kwa waombaji wa kidato cha nne wawe na ufaulu wa daraja la kwanza mpaka la nne
(Division I – IV). Kwa waombaji wenye ufaulu wa daraja la nne (Division IV) wawe na ufaulu wa alama (Point) 26 hadi 29.
e) Kwa waombaji wa kidato cha sita wawe wamesoma masomo ya sayansi na ufaulu wa daraja la kwanza mpaka la tatu (Division I – III)
f) Wahitimu wa Shahada, Stashahada na Astashahada wawe na umri kuanzia miaka 18 hadi 29.
g) Awe na urefu usiopunguwa futi tano na inchi tano (5’5”) kwa wanaume, na futi tano inchi mbili (5’2”) kwa wanawake.
h) Awe na kitambulisho cha taifa au namba ya utambulisho kutoka Mamlaka ya Vitambulisho vya Taifa (NIDA).
i) Awe na afya njema kimwili na kiakili iliyothibitishwa na daktari wa Serikali.
j) Awe hajaoa/kuolewa au kuwa na mtoto.
k) Awe hajawahi kutumia madawa ya kulevya.
l) Awe tayari kuhudhuria mafunzo ya awali ya taaluma ya Polisi.
m) Awe hajaajiriwa au hajawahi kuajiriwa na taasisi nyingine ya Serikali.
n) Awe tayari kufanya kazi za Polisi mahali popote Tanzania.
o) Awe tayari kujigharamia katika hatua zote za usaili endapo ataitwa
p) Asiwe na alama za kuchorwa mwilini (tattoo).
q) Asiwe na kumbukumbu za uhalifu.
r) Kwa waombaji wenye elimu ya kiwango cha Shahada (NTA level 8), Stashahada (NTA level 6) na Astashadaha (NTA Level 5 au NVA Level 3) wanatakiwa wawe na fani zilizoainishwa kwenye tangazo.

2. Utaratibu wa kutuma Maombi

1. Waombaji wote wanatakiwa waandike barua za maombi wao wenyewe kwa mkono (Handwriting) bila kusahau namba za simu, na watumie anuani ya Mkuu wa Jeshi la Polisi S.L.P 961 DODOMA.

2. Waombaji wote waambatanishe nakala zifuatazo:
a) Nakala ya cheti cha kuzaliwa
b) Nakala ya kitambulisho cha Taifa cha NIDA au namba ya NIDA
c) Nakala ya cheti cha kuhitimu mafunzo ya JKT/JKU kwa walio nje ya makambi.
d) Nakala za vyeti vya taaluma (Academic Certificates).
e) Nakala za vyeti vya kuhitimu mafunzo ya sekondari (Leaving Certificate).
3. Kwa waombaji wa kidato cha sita na cha nne ambao wamehitimu mafunzo ya JKT/JKU waliopo nje ya makambi (uraiani) maombi yao yapelekwe kwa Makamanda wa Polisi wa Mikoa waliopo na sio Makao Makuu ya Polisi Dodoma.

4. Kwa waombaji wa kidato cha sita na cha nne waliopo kwenye makambi ya JKT/JKU maombi yao yawasilishwe kwa Makamanda wa Polisi wa Mikoa kupitia kwa Wakuu wa Kambi.

5. Kwa waombaji wenye elimu ya Shahada, Stashahada na Astashahada zilizoainishwa kwenye tangazo hili wanatakiwa kupakua (download) na kujaza fomu maalum (Kiambatisho ‘B’) inayoonyesha taarifa zake binafsi. Fomu hiyo imeambatanishwa kwenye tangazo na inapatikana kwenye tovuti ya Polisi. Utumaji wa fomu hiyo uwe kwa njia ya ‘excel’ na usiwe kwa njia ya kuskani (pdf) isipokuwa barua za maombi na vyeti ndio viskaniwe (pdf). Kwa waombaji wa Tanzania Bara Maombi yatumwe kupitia barua pepe admin.phq@tpf.go.tz na kwa waombaji wa Zanzibar yatumwe kupitia barua pepe ajira.znz@tpf.go.tz. Maombi yatakayotumwa kwa mkono au kwa njia ya Posta hayatopokelewa.

6. Mwisho wa kupokea maombi ni tarehe 16/10/2023.

Imetolewa na:
Mkuu wa Jeshi la Polisi Tanzania,
Makao Makuu ya Jeshi la Polisi,
S.L.P 961,
DODOMA.
09/10/2023

Screenshot 2023-10-15 115218.png
Screenshot 2023-10-15 115235.png
Screenshot 2023-10-15 115250.png
Screenshot 2023-10-15 115303.png
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom