DOKEZO Kuna viashiria vya Rushwa katika mchakato wa kuomba ajira Jeshi la Polisi Mkoa wa Songwe

Hili ni dokezo maalum toka kwa mwananchi mtumiaji wa JF mwenye nia ya kuusaidia umma kuwa na taarifa 'maalum'
A

Anonymous

Guest
Hivi karibuni Jeshi la Polisi lilitangaza nafasi za ajira katika mikoa tofauti, kilichokuwa kinafanyika ni wale tunaohitaji kuomba tulitakiwa kufanya hivyo kupitia ngazi ya Mkoa.

Mkishafanya maombi ya kazi mnafanyiwa Usaili chini ya Jeshi la Polisi likiongozwa na Kamanda wa Polisi Mkoa kisha baada ya hapo majina yanapelekwa kwenye Kamati ya Usalama Mkoa chini ya Mwenyekiti wake ambaye ni Mkuu wa Mkoa husika.

Sasa kilichotokea upande wa hapa Mkoani kwetu Songwe ni kuwa tangazo lilitolewa kama kawaida, tukajitokeza kufanya usaili na kupita katika mchakato wa Polisi.

Tuliofanya usajili usaili na majina yetu kupitishwa kwenda kwenye Kamati ya Usalama Mkoa wa Songwe tarehe 13 Novemba, 2023 ambayo ilikuwa ni siku ya Jumatatu kuanzia Saa 2:00 Asubuhi ni hii hapa kwenye chini, unaweza kujionea mwenyewe…
WALIOITWA KUFANYA USAILI0001 (1)_page-0001.jpg

Baada ya hapo majina yetu 32 yakapelekwa kwenye Kamati ya Usalama Mkoa wa Songwe, baada ya mchakato majina 12 yakachujwa na kuondolewa kwa kuonekana hawakidhi vigezo vya kuendelea na mchakato wa kwenda kwenye mafunzo rasmi ya Jeshi la Polisi.

Hivyo, majina yakabaki 20 lakini ajabu ni kuwa orodha ya mwisho kabisa ya majina ambayo imepatikana na wahusika wanatakiwa kwenda hatua ya mbele kwa maana majina yao kutumwa Makao Makuu yamekuwa 42.

Kamati hiyo chini ya Mwenyekiti wao wameoneza majina mengine 22 ambayo hayakuwepo kuanzia katika mchakato wa awali, kwa ufupi kuna watu 22 wameongezwa na hatujui wametokea wapi.

Baadhi ya Vijana ambao wapo tayari kusaidia Taifa lao wakiwa wamepitia JTK wameondolewa kwenye mchakato wa maombi, kama wameondolewa kihalali ni sawa, lakini vipi kuhusu hao 22 walioongezeka wametoka wapi? Kwa nini waingizwe kwa siri? Hii inatoa picha gani kwa mchakato huu katika mikoa mingine?

Hii hapa orodha mpya ambayo inatarajiwa kutumwa Makao Makuu ikiwa na majina 22 ambayo hayakuwepo awali...
MAJINA YA  USAILI FORM   FOUR_page-0001.jpg

Naomba Serikali Kuu, Rais Samia Suluhu Hassan, Makamu wa Rais na Waziri Mkuu pamoja na IGP na Usalama wa Taifa wafuatilie hiki kilichotokea Songwe.

Inawezekana mazingira kama haya ndio yanafanyika mikoa mingine mingi na mwisho wake tunapata Jeshi la Polisi ambalo linakuwa na mapungufu mengi wa kuwa mchakato unakosewa kuanzia huku chini.
 
kwaiyo [mention]Ritz [/mention] alitoa rushwa ya ngono
 
Back
Top Bottom