Usafiri enzi zile Mwanza yetu

Usafiri enzi zile Mwanza yetu

Wadau wa rock city enzi zile mnakumbuka Mwanza hapakuwa na usafiri wa vipanya kama leo. Vipanya vilikuwa Mabatini na Kirumba tu lakini Igombe kulikuwa na min bus zikiitwa Toto Tundu, Mayeji na Jalijalalam, Igoma kulikuwa na Last Boy na Mkuyuni air Jordan.

Vipi, kile kikundi cha taarabu cha Mabruki ukoma bado kipo or?
 
UnaKumbuka bin sadoti express ya kwenda pasiansi nauli shiling 3.

Nimepanda magari ya Sadoti enzi hizo dereva akiwa 'kaka Mafyale'.. bahati mbaya sana huyu mzee alifilisika vibaya na kwa sasa amezeeka kweli.

Kuna express moja ilikuwa inapiga route za Mwaloni - mjini inaitwa MAJIRA...
 
...nilifunga safari mpaka mwanza kutafuta raba pale mabatini,bei niliyoikuta nikalaza taratiiibu...
 
Vipi, kile kikundi cha taarabu cha Mabruki ukoma bado kipo or?

igogo haiendelei mzee sasa hakuna ukumbi tena wa burudani wala kikundi cha muziki ukumbi wa jitegemee ulishajiishia siku nyingi
 
Kumbe nyie wote mliotoa comment mpaka sasa hivi ni wa juzi tu. Miaka ile ilikuwa hakuna cha minibus wala nini. Tulikuwa tunapanda zile peugeot za kizamani mnarundikwa kama ndizi humu. Station wagon moja ilikuwa inaweza kubeba hadi abiria 8. Zilipotoka hizo ndio zikaja express. I love Mwanza mji niliokulia.

Tiba
.nyie watoto sana i see.kipindi chetu tulipanda punda
 
Mkuu Chizi Fureshi umenikumbusha DJ Bush Doctor,jamaa alikufa kwa homa ya uti wa mgongo wimbo wa Ice baby ulimpaisha
 
Du!!!!! Watu mnakumbuka mbali sana,wakati wa chai maharage?

Tumezisahau siku nyingi saaaaaaaaaaana kwa sasa zipo zanzibar tu
 
Subisubi- Mwaloni-mjini/stand ya taxi.
Simba mtoto- Mkuyuni- stand ya Tanganyika
 
Kweli Tiba hao hawakuona yale maisuzu yakiitwa Santamaria
na baadae mtama kwa watoto enzi hizo njia ya pasiansi

Nani alipanda basi la mdundiko na machimukenda, express za kugombania ukishindwa sana unaanza mdogo mdogo town hadi nyamanoro, hadi ufike umepaukaaaa, kweli mwanza imetoka mwanza
 
Last edited by a moderator:
Dj Yusuph (R.IP) na wadogo zake akina Harry na disco lao, Baadae tukahamia club ya matata na dj Bush Doctor akisaidiwa na Dj Richie Dillon!

Club ya Matata hapa unamaanisha Magnum club pale Kirumba mbele kidogo ya Furahisha? Mwanza imetoka mbali jamani!
 
Miaka y 1980-90 kilikuwa na mabasi kama Bajiberi, Nzegenuka
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom