North Korea ni kweli ni taifa lenye zana nyingi za kijeshi,na hivi karibuni ame advance sana kutoka uwezo mkubwa wa mizinga hadi sasa kwenye makombora,huyu Bwana anajitapa kuwa na uwezo mkubwa wa jeshi,hilo ni kweli,makombora yake ya Taepodong ambayo ni version mpya ya scud missile anayategemea sana.But all in all hayo makombora yake yoote hayaweZi fua dafu kwa marekani na washirika wake,nakuhakikishia hakuna kombora litafika USA,
Why?.
1.MArekani ameweka mifumo bora zaidi ya ulinzi wa makombora yani Anti ballistic missiles za aina tofauti tofauti maeneo mbali mbali kuizunguka marekani,kuanzia tuu south korea pale marekani kashafunga Terminal High Altitude Area Defense,ambazo zitatungua makombora ya North Korea,achana na patriots,na arow system alizounda kwa ushirikiano na Israel,
Je North Korea atatumia nini?
Jibu ni EMP weapon.
Yani Electromagnetic pulse weapon,
Hili ni bomu la nyuklia ambalo likiwa detonated/lipuliwa nje ya orbit au kwenye orbit ya dunia basi huyuma miale flani ambayo itaharibu vifaa vyote vya electronic plus kuzima na kuharibu mitambo yote ya umeme,wachambuzi wa mambo tunajua hili bomu likipigwa basi tutatudi zama za mawe.
Hili bomu halina madhara kwa binadamu yani maana ya kuwalipua na kutoa moto yani kama ivyo,yani mnashangaa gafla tuu umeme na simu hazifanyi kazi.hata gari haiwaki tena.
North korea ana satellite zake kwenye lower earth orbit south trajectory amabapo ni karibu na USA,mk 3 na MK 4, hofu ni kuwa je huyu kim jong un aja attach Nuclear bombs huko?
Mkuu mimi natofautiana kidogo na maoni yako, kitu cha kwanza Wakorea siyo wajinga kusema wanaweza kurusha makombora yao kama projecticle za kawaida ambazo flight path zake ni highly predictable - Koreans knows how to defeat/beat American anti missile MISSILE in other words American Intergrated Defence System can be beaten, hivi kweli Wakorea wapoteza mabillion ya fedha zao kwenye Research and Development za kuhunda Balistic Missiles zinazoweza kuwa intercepted kirahisi na system za Wamerikani? Come on - Korean Rocket Scientists are no VILAZAS kumbuka hakuna Physics za Kimerikani au Physics za Kikorea zote zinafuata Same basic principles hisipokuwa what counts is how you tinker around na systems zako ku-defeat adui yako basi - hii dhana iliyo jengeka hapa kwamba somehow Wamerika wanatumia nadharia za kisayansi za kutoka mbinguni ambazo Mataifa mengine awana uwezo wa kuzitumia au kuziboresha zaidi hiyo si kweli hata kidogo - hizo ni lugha za wanasiasa na wanajeshi siyo Scientific Community hao ndiyo wanajua ukweli na hawasukumwi na itikadi za ukomunism/socialism na Capitalism au nadharia ya vita baridi - wanasayansi mara zote usema ukweli na mimi nawaeleza ukweli.
Naona hapa unasema Wakorea hawawezi kuhunda ICBMs zinazo weza kuruka mpaka Marekani bila ya kuwa intercepted in mid flight na System za Kimerikani - who told you that? Wakorea wana mbinu nyingi za kudeliver Thermonuclear Payloads mpaka kwenye aridhi ya USA mojawapo ikiwa ni hiyo ya kutumia ICBMs zenye uwezo wa kubadirisha badirisha mwerekeo na hivyo kuwa viguma kuzi track down na kuzi-intercept, mbinu nyingine ambayo ni more deadly ni hii ya kutumia submarine zinazo endeshwa na Dizeli injinis zikishirikiana na electric motors, submarine za type hii hazina kelele hata kidogo, si rahisi kugundurika sina ahakika kila submarini wame-install tubes ngapi zi kufyatulia SLBM lakini aziwezi kuwa chini nane - Wakorea watakacho fanya ni kusafirisha submarini hizo mpaka karibu na West Coast ya USA wakipata amri ya kuvurumisha
Submarine
Lauched
Ballistic
Missiles miji yote ambayo ipo within range ya missiles itateketea kutokana na makombora hayo ya nuclear, kumbuka range ya makombora hayo ni kuanzia 1500Km mpaka 2500Km - je, umbali wa kutoka West Caost Mpaka East Coast ya USA ni wa umbali gani - watu watasema hii haiwezekani Amerika ina ulinzi mkali ukiwauliza ilikuwaje tena ndege nne za abiria kuendelea kubaki kwenye anga lao huku zimezima transponders, wamepata taarifa kwamba zimetekwa na magaidi, zinabamizwa moja baada ya nyingine kwenye majengo muhimu lakini jeshi la anga la marekani hawafanyi lolote - je, makombora ya Wakorea si ndiyo yataleta balaa zaidi.
Haya tuje kwenye kwenye
THAAD System unazo sema kwamba hakuna kinacho weza kukatiza katika anga zake - una ukweli gani na unacho kisema hapa? - Binafsi sisemi mengi tafuta kwa wakati wako usome kwa umakini makombora ya Urusi na Uchina aina ya Hypersonic speed Missiles e.g Russian
3M22 Zircon na
Chinese WU-14 kama kweli system ya
THAAD ina uwezo wa kutrack na kuharibu silaha hizo hatari in realtime - tafuta taarifa hizo kutoka huko huko Marekani usikie Wanasayansi, Majenerali na watu wengine weledi wanasema nini kuhusu makombora hayo hatari ya Warusi - version ya kwanza ilifanyiwa majaribio na kufanikiwa ku-hit target zilizo kuwa ambali wa zaidi ya 2,600Km at hypersonic speed,version mpya ya short range imefanyiwa majaribio mwezi March kama sikosei, kama unafikiri THAAD ina uwezo wa ku-defeat a vehicle travelling at Mach5/6 think again - Taifa la Marekani na Washirika wao wako overly worried na makombora hayo hatari ambayo awana kinga ya kuyadhibiti, hivi sasa Amerika nao wako mbioni kufuata nyayo za Warusi na Wachina lakini they still have a long way to go.
Nimalizie kwa kugusia EMP weapons/generators, mkuu mtu yeyote aliyesoma Solid State Physics na Electronics anajua EMP haziana uwezo wa kuharibu system/circuits zinazo tumia
Thermoionic Valves, EMP uharibu systems zinazo incorporate semi conductors siyo valves ndiyo maana watu weledi kwenye mission critical systems ziwe silaha, fixed wing planes au choppers wanaweka systems ambazo haziwe kuharibiwa na EMP weapons/generators, Koreans knows that fact si mbumbumbu - huo ndio mchango wangu.