Urais wa ZZK 2015 Kupitia Chadema: Kwa nini Wanatetemeka!, Kuweweseka! na Kutishika?!.

Status
Not open for further replies.
Nashangaa mnavyohangaika na ZZK na nia yake ya kuweka hadharani dhamira ya kuutaka urais! Yeye kaweka kwenye fb ya kuwa atamuunga mkono mgombea yoyote atakayeteuliwa na chama chake na yeye atamuunga mkono kwa kumfanyia kampeni! Akimaanisha kwamba si lazima yeye awe mgombea urais! Nia akisisitiza ya CHADEMA kushika dola 2015. Na kama ikiwa hivyo itachagiza attention ya umma kipindi cha uchaguzi kuwa upande wa chadema!
 
Ni swala lililo wazi kuwa kama upo kundi moja na Zitto iwe kichama ama kimaslahi yoyote - kama kuna mkanganyiko wowote ule na upo against yeye (ZZK); Then hustahili kabisa kuwa comfy, ni lazima uwe juu juu na tayari kwa counter attack! Ana nguvu na uwezo huo wa kujipandikiza katika mawazo na bongo za mtu ambaye yupo kinyume na yale ambayo yeye anaamini ama kusimamia.

Hata ni ajabu pale comments nyingi za wampingao zinapokuwa zinamchukulia ni 'ki dagaa' na hali matendo, chuki na nguvu zao dhidi yake ni stahili kwa 'papa'. Zitto haeleweki kabisa sababu ya u 'unpredictability' wake uendanao na nyakati, ila you can't stop admiring his dare and guts!

Nakubaliana na Mchambuzi kuwa "Habari za Zitto zinatawaliwa na hoja nyepesi kwa suala ambalo ni ZITO"
 
Last edited by a moderator:
İ doubt you,do you really know yourself?what you write outrightly shows that you are Pro El and Zzk utajibeba .
Kwenye kuandika, kuna wenye uwezo wa kusoma maneno yaliyoandikwa na mwandishi, na mwisho wa uwezo wao na kusoma tuu maandishi!. Kuna wengine wana uwezo wa kusoma maandishi na kuijua maana ya the motive behind hayo maandishi!, kama Adam na Eva/Hawa Walipokula lile "tunda"!.
 
Kuhusu wagombea hawa wawili ni muhimu pia utazame michango ya wanabodi wengi sana hawampendi Zitto na sababu zake zimeelezwa. Pamoja na hayo hatuwezi kudai hakuna Udini, Ukabila wala Ukanda ikiwa sisi wenyewe tunashindwa kuonyesha takwimu ama utafiti wetu wenyewe ktk matokeo kama haya. Na tunashindwa pia kuziba midomo yetu kuonyesha Udini, Ukanda na hata Ukabila..

Siku zote mimi nasisitiza sana kupokea na kuyasikia malalamiko ya WATU wengine, halafu tunajiuliza kwa nini watu wanafikiria hivyo, Je kuna dalili zozote zinazoashiria Udini Ukabila na Ukanda? Tunafanya utafiti wetu na kurudi na majibu na sii tunavyofiiria toka kichwani. Hakika hapa JF tu Upo Udini, Ukabila na Ukanda japokuwa wanaoandika humu sio viongozi wa Chadema lakini chama hakijengwi na viongozi bali wanachama. Ukizungumzia mikoa ya kusini na pwani utawasikia wana Chamdema wakitukana matusi ya nguoni, Ukizungumzia Uislaam utayasikia matusi, Tukizungumzia makabila ya watu wa Pwani utawasikia watu wakisema vibaya kuhusu kabila la rais. Ni tabia mbovu sana ya wana Chadema ku generalise hili lipo na wala tusilipinge maana hata mimi hunikwaza sana naposoma hoja za baadhi ya wana Chadema.

Pasco, mimi naelewa sana hoja yako ya msingi, pamoja na makundi kumi unayojaribu kuchambua. You are right kufanya uchambuzi huo. UDINI, UKABILA, UKANDA, nk, yapo, they will be there to stay. bahati nzuri kuna kundi lingine ambalo unaona ndio zuri, unajiweka na wewe mwenyewe. which is so good Ninachosema na labda kusisitiza sana ni KUTOKUYAPAKA RANGI NA KUYATANGULIZA KATIKA JUHUDI ZETU ZA KUANGALIA SAFARI YETU KAMA WATANZANIA. ! Unajua kila jambo linaanzia mahala fulani. Kama ni chama, kuna mtu mmoja atapendekeza wazo na wengine watamwunga mkono. Mtu yule anayeanzisha wazo ni lazima atakuwa na Dini fulani, kabila fulani, Kanda fulani, Huu ndio ukweli. Na wakati anaanzisha wazo ni lazima atakuwa mahali fulani, ama Mbeya, Arusha, Ruvuma, Musoma nk. Watu wanaomzunguka mwanzisha wazo huyo, watakuwa ama wa kabila lake, ukanda wake, dini yake nk, Lakini taratibu, wazo hilo litaanza kuungwa mkono na watu wengine, Dini, kabila lingine, kanda nk. It takes time kwa mtu mwingine kuunga mkono wazo. Naomba tuwasamehe na tuendelee kuwaelimisha wale wanaotukana, kwasababu kila mtu ana namna yake ya kuhimili hoja. Sisi hatutakiwi kufuata wale wanaotukana, kwanza hatujui tunajibizana humu na watu wa maadili gani ( wachache) maana namini wengi ni wasomi na ni watu wenye uelewa. Pasco hayo ya dini, ukabila, ukanda, yaliibuka tu mwaka 2010 pale kiongozi mmoja wa juu aliposhikwa na wasiwasi wa kukosa post kubwa kwa kudhani watu wangechagua kwa kufuata udini, ukanda, ukabila. Lakini naomba nikuhakikishie kuwa Rais hakuchaguliwa na watu wa kabila moja au dini moja, au ukanda mmoja. Na kama hii haitoshi, tukumbuke CUF walivyopata shida kupenyeza hoja, waliitwa CHAMA CHA UDINI, na maneno yote mengine mabaya ili tu kuwashawishi wananchi kuwa hao si watu wazuri. Sasa tumejikuta wananchi tunaingia katika malumbano ambayo hayakuwa ya lazima katika kipindi hiki. Hata hilo la ZZK, huenda watu wanalitumia ili kuvuruga tu mwelekeo na vuguvugu la kisiasa linaloendelea. MIMI SIAMINI KAMA TANZANIA TUNA UDINI, UKABILA, UKANDA, KIHIIIIIIIVYO ! Hata we Pasco kweli linakuingia akilini ? CDM ni chama cha wakristo ? CUF ni chama cha waislam ? Na CCM ni chama cha watu gani ?
 
Pasco nimepata habari za kuaminika kuwa, mambo yakitulia CCM, Zitto atahamia huko muda si mrefu kuongeza nguvu kambi ya Lowassa na mpango umeandaliwa na Jk na namna ya kumpokea.

Ni Bora gamba ZZK utoke, CHEDEMA tumekuchoka...
Pasco ,Who the Hell is ZZK, Hatumtaki, hivi hamumpelekeagi Mirejesho yetu humu ndani????????
 
Last edited by a moderator:
Nimeyaweka makundi ya watu!, au ulitaka nitaje na majina kabisa?.
Haya ni makundi ambayo wana JF wanaingia sio?

Ok, mii naangalia hapa kwenye kundi la Mwisho.....WAKWELI. ZZK ni mkweli kama wewe, lakini unaweza ukawa mkweli mpayukaji.....kama ZZK alivyo hivi sasa.

Kweli unaweza kuwa mpayukaji MKWELI? kwamba unapayuka mambo hovyohovyo lakini wewe ni MKWELI?
Ukweli unaoogelewa hapa ni ukweli wa personal decisions ndani ya Politics na sio Ukweli katika kusimamia issues.

Kama ni katika personal decisions ndani ya game, ZZK hajaonyesha UKWELI wowote. historia inamuondoa kwenye kundi hilo.
Kama ni kusimamia UKWELI katika national interests, hapo si haba, ameweza, kama kuna alipojikwaa ni padogo...hapa-count kivile wanasema vijana.

Haya maneno ya kwamba ZZK ni mtaji wa CHADEMA, na kwamba chama kinamhitaji zaidi kuliko yeye anavyokihitaji, nadhani ni nadharia ambayo ipo ndani ya Upenzi wako kwa ZZK.
Je, CHADEMA isipo m-contain ZZK kama unavyosema, nini kitatokea? will he raise or fall, will CHADEMA raise or fall?

Point blank.......Nakubaliana na wewe, ZZK kuonyesha nia ni sahihi, kutangaza kugombea sio sahihi at this point in time

Anyway......Mamvi is our next president....hahahahahahaa!!.........I support you on this broda.
 
Huu ni wakati wa kujenga chama na CCM wangependa sana makundi ya Urais yawe kama kwao ili CDM isambaratike-Mzee Mtei.

Wanachadema wote wenye mapenzi mema na chama chetu nawaomba kwa moyo mkunjufu kabisa kwamba inatosha sasa kuendelea kumjadili zitto na hoja yake ya uraisi. Kama kuna hoja nyingine tujadili lakini hii ya uraisi ni kama inaelekea kutushika akili zetu na tunapoteza muda kuizungumzia wakati tuna majukumu mengine muhimu ya kukijenga na kukiimarisha chama.

Mimi naona hapa wapambe wa zitto ambao wengi wao si wanachadema wamefanikiwa kutu divert kutoka katika hoja yetu ya msingi sasa tumebaki kubishana nao juu ya suala hili moja kila siku. Hivi hamuoni wengi wanaoongoza kuleta mijadala ya zitto na uraisi hapa JF ni wanaccm na wanachadema wenye maslahi binafsi na zitto?

Mimi hii ndiyo post yangu ya mwisho kwa sasa juu ya uraisi wa zitto,nawaombeni sana makamanda huu mtego mmenaswa bila kujua na sasa mnamfanyia kampeni mtu binafsi huku mkikisahau chama. Sasa ni muda wa kukizungumzia chama na namna bora ya kujikita kwa wananchi, tuendelee na moto uliokwisha washwa wa kuipeleka chama huko vijijini kama tulivyokwisha anza.
 
Pasco na Zitto hawajakutana barabarani....mtapiga kelele huku mkipoteza energy zenu. Anyway, kuna watu wanaweza kujikuta wanapunguza uzito kwa ajili ya hili suala. Mwenye kuneemeka na hii strategy mwache aneemeke ila wananchi wa Tanzania wanajua ni kiongozi gani wanayemhitaji.Hakuna cha TB Joshua au Jasho, watanzania ndiyo watajiamulia wenyewe (especially kipindi hiki nchi ikiwa inayumba)
 
Mkuu Joka Kuu, kwanza nakushukuru kwa objectivity yako na frankness kumhusu ZZK. Kwa vile nafahamiana na ZZK, naanza kuchelea kujibu baadhi ya post humu nikaonekana nimetumwa na ZZK hivyo mimi ni mouthpeace yake!.

Katika hayo uliyoyasema, kosa la ZZK ni lile lile kuwa mkweli tuu much hivyo kujikuta anashindwa kufanya baadhi ya mambo ambayo Chadema kama chama wanayafanya ila kwake ni kinyume cha dhamira yake. Imetokea tuu mimi kujikuta nina side na ZZK kila anapo tofautiana na Chadema. Kwenye kutoka nje, he did what was best kutokuja kabisa!, angekuwa ni msaliti kama ange turn up na asitoke nje!.

Hili la Chadema, kujifanya kutomtambua rais, nililisema sana hapa Chadema Yakubali Yaishe! Yamtambua Rais kimya kimya!, Yampongeza!. baadae Marehemu Regia akanitaka niombe radhi hapa,Pasco Tuombe radhi CHADEMA-Umemwelewa Vibaya Hon Mbowe na mimi kibinaadamu niliomba radhi hapa,Nawaomba radhi wana CHADEMA, nilimwelewa vibaya Mhe. Mbowe ila ukweli unabaki unasimama kuwa Chadema ilijifanya haimtambui rais kwa kauli "expresilly" na mpaka leo haikuwahi kuifuta kauli ile, huku imanafanya matendo "impliedily" yanayothibitisha kumtambua rais!. Hili la kumsusia JK, Dr. Aliendelea nalo, hata JK alipojitoa kuja msiba wa Regia pale Tabata, Dr akawa hapatikaniki, JK akatia timu mpaka Kilombero hapa lazima wangekuta, mpaka masizishi yalikwisha bila kusalimiana!, Kwa nini Dr. Slaa Amenuniana na JK?! - Chadema wakakaribishwa "chai" Ikulu, Dr. akagoma, hatimaye mbio za sakafuni zilimalizikia ukiongoni, jamaa walikutana, wakashikana mikono waka hug hostilities zikamalizika, Chadema sasa inashirikiana vizuri na serikali katika baadhi ya mambo, lakini kauli ya "hatumtambui rais" bado imesimama!. Kwa vile ukweli daima husimama, na kwenye siasa, The end justifies the means, pamoja na yote Chadema iliyoyafanya kwenye kususa, at the end of the day, all was wrong, and ZZK ndio yuko right!.

Hata ule msimamo wa ZZK kuhusu ununuzi wa mitambo ya Dowans au kuitaifisha, he was 100% right!. Stta, Mwakyembe and their team are dam wrong!, and belive me, tozo ya ICC lazima tutailipa!, at the end of the day, ni sisi Watanzania, mimi na wewe ndio tutailipa the last price and feel the pinch!.

Hata hivyo pamoja na kumsupport ZZK, lazima pia nikiri, ZZK ni binadamu tuu kama wengine hivyo na yeye anayo madhaifu yake, mfano uongozi ni team work, na ZZK is not a good team player ndio maana haonekani kwenye hadhara za M4C na huu ni udhaifu wa ZZK na nimeishamwambia hapa Urais wa ZZK 2015: Ngoma Ikivuma Sana...!.

All and all, pamoja na yote haya, wanaChadema, haswa manazi wa Chadema, lazima wa change their atitutes towards some issues nazo nimezizungumza hapa Kuelekea 2015: Chadema Kuchukua Nchi Kwa Kishindo!... Only If...!
P.
Pasco,

..nadhani unazungumza zaidi kama a legal scholar.

..kitendo cha CDM kumsusia Raisi hakikuwa na lengo la kumuondoa JK madarakani.

..lengo na mkakati wa CDM ulikuwa ni kupelekea ujumbe kwa CCM na utawala wao kuhusu suala zima la Katiba yetu na tume ya uchaguzi.

..binafsi naamini kitendo cha CDM kususia hotuba ya Raisi, na baadaye pressure waliyoweka ndiyo imepelekea kuundwa kwa tume ya katiba.

..wewe umejaribu kulieleza tukio lile kwa mtizamo wa kisheria, lakini nakuhakikishia kitendo kile kina ujumbe tofauti kabisa kwa mwananchi wa kawaida na wanasiasa.

..sasa labda nikuulize: je, kitendo cha Zitto kususia kitendo cha CDM kumsusia JK, kimemjenga au kimemboa Zitto, katika macho ya wapenzi wa CDM??

..kuhusu Dr.Slaa kususa kuonana na Raisi, au hata kumkwepa, naamini ilikuwa ni mbinu nzuri ya kuwachanganya CCM, and keeping them guessing about what was going to be Dr.Slaa next step. kitendo cha Raisi na Amiri Jeshi mkuu kuacha shughuli zake, na kuanza kumvizia Dr.Slaa toka D'Salaam mpaka Kilombero, ili mradi tu apige picha naye wakichekeana, siyo jambo dogo kisiasa.

..kuhusu msimamo wa Zitto kuhusu Dowans, again una tendency na kujichimbia kwenye taaluma ya sheria. tatizo hapa siyo Zitto kuwa 100% right in his legal interpretation, tatizo ni Zitto kutoaminika, kutokuwa na credibility, na hilo ni tatizo kubwa sana kwa mwanasiasa.

..kwa maana nyingine, Zitto alishajichafua machoni mwa wapenzi wa CDM kiasi kwamba wakakosa imani naye, na kutokuwa tayari kumsikiliza pamoja na kwamba aliyokuwa akiyasema yalikuwa ya msingi, na yamekuja kuwa kweli.

..mwisho, kuna mambo ambayo Zitto huyafanya and ppl go like, WHAT?? hapa nazungumzia kauli zake kwamba atamsaidia Kafulila bila kujali kwamba amefukuzwa na CDM. pia kuna yale matamko aliyoyatoa, in the middle of Dr.Slaa's presidential campaign, kwamba yeye Zitto atagombea Uraisi 2015!!! Au, alipoamua kugombea nafasi ya mwenyekiti wa CDM huku akipingana na FREEMAN MBOWE ambaye ni mmoja wa WAASISI wa CDM? Hata Mwalimu Nyerere alipogombea uenyekiti wa Tanu, hakukurupuka tu, bali alifanya hivyo baada ya mambo yote kuwekwa sawa kuhakikisha kwamba TANU haiwezi kuathirika kutokana na kitendo hicho.

..Ushauri wangu kwa Zitto ni kwamba huu ni wakati wa kujenga chama, siyo wakati wa kuendekeza ajenda binafsi.
 
Last edited by a moderator:
Mkuu SG8, kipengele cha umri wa kugomba ulikuwa miaka 30 mpaka katiba ya mwaka 1977 walipoweka miaka 40. Katiba ya 2014 tutarudi mpaka miaka 35. Nawaombeni wana Chadema msilete mchezo wa ki CCM wa hide 'n' seek kwenye urais.

Hoja zangu zote ziko based on face value, hayo ya ndani ya chama, ni ya kwenu, huna haja ya kuyatoa nje ili kum discredit ZZK. Kama viongozi wa Chadema ndio kama wewe, siri za ndani, unazianika humu!, nawahurumia sana Chadema, safari bado ni ndefu na 2015, kiukweli kazi mnayo!.
Kwa sisi waandishi wa habari, ukiulizwa swali na kutojibu, huko kutojibu tuu pekeyake pia ni jibu!.
P.
Pasco
Ifike wakati sasa tuseme ukweli. Haya niliyoyasema hapa sio mambo ya ndani kiasi hicho ila nataka nyie mnaodhani sisi tunamwogopa ZZK mjue kwamba tuna hoja za msingi. Ningeweza kukutumia PM lakini niliamua kuweka hapa kwenye mjadala kwa sababu ya kuweka rekodi sawa. Mnaambiwa kila siku kwamba kuna watu wanatumika lakini hamtaki kusikia. Nadhani unakumbuka yale mawasiliano ya ZZK na Mwandishi wa Mwananchi na yale yaliyowekwa wazi kupitia gazeti la Mwanahalisi. Sikumbuki kama ZZK alishakanusha uhusika wake.
Habari ya kwamba natoa siri nadhani hujanitendea haki kwa sababu nilitaka ujue kwamba wapo watu waliopo nje ya makundi hayo uliyoyataja na sio kwamba tunaogopa au tunamwonea wivu la hasha. Tuna mashaka na mwenendo wake. Naeudia tena fanya utafiti wako bila bias ili ujue kwamba huyo unayempigia debe sasa sio maarufu tena, hata kwenye top ten ya Chadema kwa sasa hayumo. Hata yule Issa Mohamed Makamu toka Zanzibar ni maarufu zaidi yake.

Na mwisho kabisa niweke sawa jambo moja hapa jukwaani sizungumzi kama Kiongozi wa CDM, nazungumza kama SG8 nikiiwakilisha nafsi yangu
 
Mkuu wangu kama wewe ni kiongozi ndani ya CDM na umeyaandika haya, basi sisi wasomaji ndio tutakuhumuni maana tayari wewe mwenyewe umesha onyesha upo kimakundi..Hivi unataka kunambia upande wapili hawakuwa na makosa? hivi kweli unataka sisi tuamini ZZK alifanya mabaya yote yale na leo bado yupo ktk madaraka?..

Something is very wrong nakuomba sana wakati mwingine jukwaa kama hili tuachie sisi tujadili badala ya kiongozi unatuonyesha jinsi msivyo mheshimu ZZK naibu katibu wa chama na pengine kuna ukweli nyie ndio mnaomtenga. Kumradhi sana lakini imebidi niseme haya, simuungi ZZK mkono wala yeyote anayepingana naye diplomacy ndani ya chama na usiri wa mambo ya chama ni muhimu saa ktk kukilinda chama..
Binafsi nadhani kwa kuendelea kumjadili huyu mtu ni kukubaliana na hoja za nbaadhi ya watu wanaodhani tunamwogopa au kumwonea ZZK. Nilichosema ni maoni yangu na kile nilichokiona na ninachoendelea kukiona. .
 
Binafsi nadhani kwa kuendelea kumjadili huyu mtu ni kukubaliana na hoja za nbaadhi ya watu wanaodhani tunamwogopa au kumwonea ZZK. Nilichosema ni maoni yangu na kile nilichokiona na ninachoendelea kukiona. .
Sawa tupo pamoja lakini kuna maswala unaacha kama yalivyo majukwaani ukiwa kiongozi unayamaliza huko huko maofisini..Kama hafai mnamwodoa madakani lakini sii majungu kutuaminisha wakati mke unalala naye. Tuachie sisi kina Mkandara tuchambue tunayoyaona na mnatupeleka wapi...
 
Sawa tupo pamoja lakini kuna maswala unaacha kama yalivyo majukwaani ukiwa kiongozi unayamaliza huko huko maofisini..Kama hafai mnamwodoa madakani lakini sii majungu kutuaminisha wakati mke unalala naye. Tuachie sisi kina Mkandara tuchambue tunayoyaona na mnatupeleka wapi...
Point noted with thanks!!!! Ndio maana ya JF, mimi ni muumini mzuri sana wa kukubali kukosolewa na kujisahihisha!!!
 
Pasco
Ifike wakati sasa tuseme ukweli. Haya niliyoyasema hapa sio mambo ya ndani kiasi hicho ila nataka nyie mnaodhani sisi tunamwogopa ZZK mjue kwamba tuna hoja za msingi. Ningeweza kukutumia PM lakini niliamua kuweka hapa kwenye mjadala kwa sababu ya kuweka rekodi sawa. Mnaambiwa kila siku kwamba kuna watu wanatumika lakini hamtaki kusikia. Nadhani unakumbuka yale mawasiliano ya ZZK na Mwandishi wa Mwananchi na yale yaliyowekwa wazi kupitia gazeti la Mwanahalisi. Sikumbuki kama ZZK alishakanusha uhusika wake.
Habari ya kwamba natoa siri nadhani hujanitendea haki kwa sababu nilitaka ujue kwamba wapo watu waliopo nje ya makundi hayo uliyoyataja na sio kwamba tunaogopa au tunamwonea wivu la hasha. Tuna mashaka na mwenendo wake. Naeudia tena fanya utafiti wako bila bias ili ujue kwamba huyo unayempigia debe sasa sio maarufu tena, hata kwenye top ten ya Chadema kwa sasa hayumo. Hata yule Issa Mohamed Makamu toka Zanzibar ni maarufu zaidi yake.

Na mwisho kabisa niweke sawa jambo moja hapa jukwaani sizungumzi kama Kiongozi wa CDM, nazungumza kama SG8 nikiiwakilisha nafsi yangu
Mkuu Jeradi, nimekusikia, nimekuelewa, na kukubali. Nakiri kwa haya uliyoeleza kuhusu ZZK, nakiri kumbe ufahamu wako is the judgement based on the cover of the book only!, nitatafuta time nikisome kitabu chenyewe, na kama ni kweli, kwanza tunamlipua humu humu na kisha tunampotezea!, JF hatukopeshi, na mimi kwa vile kila siku nahubiri sina chama, pia sina permenent friendships na any politicians, we just have common interest!. Japo ZZK namkubali sana, hoja zako kumhusu sio za kupuuziwa hata kidogo!.
Thanks kwa inside info!.
P.
 
  • Thanks
Reactions: SG8
Thanks Mkuu COMRADE CHRIS HANI, ukikubali kuwa mkweli, lazima uwe tayari kukubali matokeo including to pay the price!. Miongoni mwa gharama ni kuchukiwa "an anemy of the people"!. Humu jf nimeisha zoea kubezwa, kutukanwa, kudhihakiwa but at the end of the day, kweli itasimama!.

....Salute kamanda pasco!! amini....silent majority wana ushujaa wa kumeza vidonge vyote vichungu vya ukweli..na wako na wewe ktk hili na mengine, kama walivyo na wakweli wengine..kwa wale wenye kuwabeza...from u, na wakweli wengine ni... "sword on dem throat"...!tuendelee kuipeleka jf ktk uhalisia wake wa great thinkers forum...na si kwingine....again..salute !!
 
Wanachadema wote wenye mapenzi mema na chama chetu nawaomba kwa moyo mkunjufu kabisa kwamba inatosha sasa kuendelea kumjadili zitto na hoja yake ya uraisi. Kama kuna hoja nyingine tujadili lakini hii ya uraisi ni kama inaelekea kutushika akili zetu na tunapoteza muda kuizungumzia wakati tuna majukumu mengine muhimu ya kukijenga na kukiimarisha chama.

Mimi naona hapa wapambe wa zitto ambao wengi wao si wanachadema wamefanikiwa kutu divert kutoka katika hoja yetu ya msingi sasa tumebaki kubishana nao juu ya suala hili moja kila siku. Hivi hamuoni wengi wanaoongoza kuleta mijadala ya zitto na uraisi hapa JF ni wanaccm na wanachadema wenye maslahi binafsi na zitto?

Mimi hii ndiyo post yangu ya mwisho kwa sasa juu ya uraisi wa zitto,nawaombeni sana makamanda huu mtego mmenaswa bila kujua na sasa mnamfanyia kampeni mtu binafsi huku mkikisahau chama. Sasa ni muda wa kukizungumzia chama na namna bora ya kujikita kwa wananchi, tuendelee na moto uliokwisha washwa wa kuipeleka chama huko vijijini kama tulivyokwisha anza.

..Mkuu hilo ndilo lilikuwa lengo kuu la Zitto na waliomtuma.
 
Zito is just another hopeless man! Sijui kama anajua watu wanamjua kwa undani na wanamhifadhi tu. This guy is one of the corrupt guys na details zote za mahusiano yake na RA na Lowassa hasa kuanzia kwenye Richmond yako wazi. Alihusika sana kutuliza swala la Richmond, vikao vya wapi walikuwa wanakutana, watu waliokuwa wanatumika kuandaa vikao, fedha zilivyotolewa, watu waliohusika including Sitta, Lowassa, RA and Makamba ni very clear. Zitto alivuta zaidi ya 500m na ndizo alizotumia kununulia Hamma na kampeni za 2010 + msaada kwa Kafulila. What Chadema is actually doing ni kucheza na politics, kumstahi ili kukilinda chama for the time being, nothing more! Zitto mwenyewe anafahamu hili na yuko mguu ndani - mguu nje. Ndio sababu za kutoshiriki shughuli na kutekeleza maamuzi ya chama vilivyo.
 
Pasco,

Hongera kwa jitihada za kujaribu kutuelimisha.I pray to God and Give you more wisdom beyond reasonable doubts on this.

The Issue is not Zitto to become a Leader.Am also very concern on this.

1. Chadema has a Vision,and according to the low of leading,leaders are the Pillars of carring a vision.
what do i mean,

a. They have to lift the Vision together through both pillars.
b. They have to speak one thing to bring the togetherness
c. They have to move together for the best
d. They have to see and foccus to one direction so that to persue the enemy.

But all in all one should lead all this, therefore ROYALITY has to be applied,without being royal to one another it is difficult to please God whom we all depend.

For this really the approach is not right,so kindly may you be good adviser,don't let him loose the special gift he has.Because You can not please God with such altitude.

Currently I know every leader of CHADEMA their together planning the strategies of overcoming the enemy,it is not the right time to talk about being a Presidential candidates.
what he has to do let him prepare in silent mode and when the time comes He can speak out,with all the authority,power and blessings.

friends it is time to seek the mercy of GOD for KNEW TANZANIA stop bringing topics which will take out from this direction.
There is always right time for Everything and Everyone.

He can become the President let him worry not,But now he is ONE OF THE PILLARS OF CHADEMA VISION LET HIM BE ONE AND ROYAL TO HIS TOP LEADERS AND MOVE WITH THEM IN THE SAME BOAT.
 
Pasco,

Hongera kwa jitihada za kujaribu kutuelimisha.I pray to God and Give you more wisdom beyond reasonable doubts on this.

The Issue is not Zitto to become a Leader.
Currently I know every leader of CHADEMA their together planning the strategies of overcoming the enemy,it is not the right time to talk about.
Mkuu Josephine, leo nilikuwa nafanya rejea ya uzi huu, ndipo nikakutana na posti yako hii!,
I hope kinachoendelea sasa sio sehemu ya hizo strategies of ivercoming the enemy!.

Pasco.

Kwa wengine, chunguzeni kwa makini Why ZZK?!, angalia hao wanaomshutumu wako kundi gani kati ya makundi 10 haya!.

P.
 
Status
Not open for further replies.
Back
Top Bottom