Erythrocyte
JF-Expert Member
- Nov 6, 2012
- 117,703
- 218,249
Nimefuatilia Hotuba za viongozi karibu wote wa CCM na serikali wa sasa na wastaafu, sijasikia hata mmoja anayesema kwamba Lowassa aliwahi kuhamia Chadema na kugombea Urais kupitia Chama hicho 2015.
Bado sijajua kama wanaogopa kusema au wanaona aibu, hata Warioba anayesifiwa kwa hotuba yake kwenye msiba huo, hakusema baada ya Lowassa kukatwa na ccm 2015 alienda wapi, wala hakusema kilichotokea, aliishia tu kusema Lowassa alikatwa 1995.
Bali kinachofichwa ni kwamba Lowassa alijiunga na CHADEMA august 2015 na kugombea Urais na kushinda kwa kishindo , kabla ya kunyang'anywa Ushindi wake kwa msaada wa "ofisi" ya Masaki iliyoongozwa na watu watatu ambao tutawataja hadharani baada ya mazishi (Liwalo na liwe)
Baada ya dhuluma hiyo " watu wa system " waliofichua uchafu wote uliotendwa hadi Lowassa kuporwa ushindi wakakamatwa na kutupwa gereza la KEKO , bila kufikishwa Mahakamani, japo waliachiwa baada ya miaka mingi , huku wachache wakifa kwa presha na visukari, CCM inafanya siasa za kishamba sana !(HAKUNA ASIYELIJUA HILI)