Chama cha haki na kilichokubalika kwa Mungu, mtu, au taasisi kupitia dini akipinge, ni kujichosha tu! CHADEMA ina kibali bwana!

Nsanzagee

JF-Expert Member
Jun 28, 2023
1,939
4,119
Chadema inayo mambo madogo madogo ya kujirekebisha hasa kupitia wafuasi wake ambao hujikuta wakitoa maneno yaliyokosa hekima, busara, wala mwelekeo huo wa kukubalika

Niliandika uzi uliotambulikana kuwa, Chadema ni chama cha wahuni?

Katika maelezo yangu nilitahadharisha kauli za wafuasi wa Chadema, sambamba na baadhi ya viongozi kwa kidiriki kwao kuwaita wananchi ni wajinga, sababu wanaitikia kwa wingi mikutano ya katibu mwenezi wa CCM ndugu Makonda

Ni mwaka 2015 tu ambapo sikukipigia Chadema kura yangu kwa sababu zangu binafsi na za mhimu, kwa maana nyingine, mimi ni mpiga kura wa Chadema, ila sikubaliani kabisa na kuitwa wajinga Watanzania wenzangu kwa makosa ya kisiasa!

Wanajamvi, naandika uzi huu nikiwa nagahamu fika kwamba, yapo matarajio ya wanasiasa kuihusu Chadema kwamba, kwa yaliyotokea na kwa wanavyokitendea, wanaamini chama hiki kitakufa na ama kupoteza nguvu zake kabisa

Lakini pia, wapo viongozi mbali mbali wa dini, kwa kuongozwa na hisia za Kisiasa, ambapo stawataja kwa majina yao, nao wanaamini kwamba, kwa kutumia majukwaa yao ya kidini, na mihadhara mbalimbali, wanakipondea chama hiki kwa mabaya pasipo sababu zozote za msingi, huku wakiamini kuwa, kwa matamko yao hayo, Chadema itakataliwa na watu, kumbe bado wanaendelea kukipalilia ili king'are zaidi

Nani asiyejua, kulikuwepo vyama fulani vilivuma kwa kishindo, ila kwa sababu havikuwa na kibali, fitina hizi hizi ambazo hata sasa vinafanywa kwa Chadema, viliviangusha kwa mapema zaidi

Chama kilichokubalika kwa Mungu, mbinu zozote hazitafanikiwa kukivunja, utaingiza mambo ya kidini nayo yatagonha mwamba, utakihujumu kwa namna zote ujuavyo, bado utagonga mwamba! Hii ndiyo Chadema buana!

Sasa, kwa tunayoyaona huko Mbeya, tuliyoyaona huko Mwanza na Dar, kuna atakeyebisha kwamba Chadema ni chama chenye kibali?

Nikushawishi kijana mwenzangu mpenda maendeleo, achana na CCM, waachie mafaili yao na uhamie Chadema ili TANZANIA ikomboke

Chadema ni nuru ya Tanzania
 
Screenshot_2024-02-20-14-02-29-1.png
Screenshot_2024-02-20-17-45-58-1.png
 
Chadema inayo mambo madogo madogo ya kujirekebisha hasa kupitia wafuasi wake ambao hujikuta wakitoa maneno yaliyokosa hekima, busara, wala mwelekeo huo wa kukubalika

Niliandika uzi uliotambulikana kuwa,Chadema ni chama cha wahuni?

Katika maelezo yangu nilitahadharisha kauli za wafuasi wa Chadema, sambamba na baadhi ya viongozi kwa kidiriki kwao kuwaita wananchi ni wajinga, sababu wanaitikia kwa wingi mikutano ya katibu mwenezi wa CCM ndugu Makonda

Ni mwaka 2015 tu ambapo sikukipigia Chadema kura yangu kwa sababu zangu binafsi na za mhimu, kwa maana nyingine, mimi ni mpiga kura wa Chadema, ila sikubaliani kabisa na kuitwa wajinga Watanzania wenzangu kwa makosa ya kisiasa!

Wanajamvi, naandika uzi huu nikiwa nagahamu fika kwamba, yapo matarajio ya wanasiasa kuihusu Chadema kwamba, kwa yaliyotokea na kwa wanavyokitendea, wanaamini chama hiki kitakufa na ama kupoteza nguvu zake kabisa

Lakini pia, wapo viongozi mbali mbali wa dini, kwa kuongozwa na hisia za Kisiasa, ambapo stawataja kwa majina yao, nao wanaamini kwamba, kwa kutumia majukwaa yao ya kidini, na mihadhara mbalimbali, wanakipondea chama hiki kwa mabaya pasipo sababu zozote za msingi, huku wakiamini kuwa, kwa matamko yao hayo, Chadema itakataliwa na watu, kumbe bado wanaendelea kukipalilia ili king'are zaidi

Nani asiyejua, kulikuwepo vyama fulani vilivuma kwa kishindo, ila kwa sababu havikuwa na kibali, fitina hizi hizi ambazo hata sasa vinafanywa kwa Chadema, viliviangusha kwa mapema zaidi

Chama kilichokubalika kwa Mungu, mbinu zozote hazitafanikiwa kukivunja, utaingiza mambo ya kidini nayo yatagonha mwamba, utakihujumu kwa namna zote ujuavyo, bado utagonga mwamba! Hii ndiyo Chadema buana!

Sasa, kwa tunayoyaona huko Mbeya, tuliyoyaona huko Mwanza na Dar, kuna atakeyebisha kwamba Chadema ni chama chenye kibali?

Nikushawishi kijana mwenzangu mpenda maendeleo, achana na CCM, waachie mafaili yao na uhamie Chadema ili TANZANIA ikomboke

Chadema ni nuru ya Tanzania
Chadema ndio mkombozi wa watanzania tupo pamoja na CDM kwa hali na mali!
 
Back
Top Bottom