Urais wa ZZK 2015 Kupitia Chadema: Kwa nini Wanatetemeka!, Kuweweseka! na Kutishika?!. | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Urais wa ZZK 2015 Kupitia Chadema: Kwa nini Wanatetemeka!, Kuweweseka! na Kutishika?!.

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Pascal Mayalla, Oct 15, 2012.

Thread Status:
Not open for further replies.
 1. Pascal Mayalla

  Pascal Mayalla JF-Expert Member

  #1
  Oct 15, 2012
  Joined: Sep 22, 2008
  Messages: 24,560
  Likes Received: 18,289
  Trophy Points: 280
  Wanabodi,

  Preamble: Tangu ZZK alipotangaza wazi nia yake ya kugombea urais wa 2015 kupitia Chadema, nimenote humu jf, watu wanatetemeke, kuweweseka na hata kutishika eti ZZK ni mamluki na kitendo cha kuitangaza nia hiyo, kuna lengo la kukisambaratisha Chadema!. Maudhui ya mada hii ni kuwachambau makundi 10 yanayomsupport au kumpinga ZZK na uamuzi wake huu. Naomba nikiri, kichocheo kilichonifanya kuanzisha uzi huu ni mada ya Mchambuzi ...

  Utangulizi.
  To start with, naomba kwanza ku declare my interest!. Namsupport ZZK kuonyesha nia na sio kutangaza rasmi nia hiyo!.
  Tofauti ya kuonyesha nia mapema na kutangaza rasmi nia mapema ni hizi zifuatazo!.
  Kuonyesha nia: Kubehave ki "presidential hopeful" ili kujenga nia "will" utakayoitumia kama "power" ili kukipata unachokitaka. (Where there is a will, there is a way!"). Faida ya kuonyesha nia mapema ni kukipa chama na sisi wananchi fursa ya kukupima ili muda muafaka ukifika, Chama ndicho kikushauri kijana chukua fomu gombea, unaonekana unatufaa.
  Kutangaza rasmi nia: Ni kitendo cha kujitangaza rasmi nia kuwa mtu utagombea urais wa Tanzania mwaka 2015. Kwa utaratibu wa sasa, mtu huwezi kutangaza utagombea urais, ten a ukatangaza wazi mchana kweupe kwenye kadamnasi ya watu!, kwa sababu, wagombea ni wa vyama!. ZZK hakupaswa kutangaza wazi ki vile, this was a mistake, mimi ZZK ni rafiki yangu, na pia nimeshamwambia maoni yangu kwenye hili. Kwa jinsi alivyotangaza is as if alishafikia uamuzi hivyo kutishia kuwa Chadema isipomsimamisha yeye, patachimbika!. Hili nimelieza wazi katika mada yangu ya Urais wa ZZK 2015: Ngoma Ikivuma Sana...!.

  Baada ya kutoa utangulizi huo, sasa naomba nije kwenye hoja yangu haya makundi 10 ya watu wanao muunga mkono ZZK na wanaompinga ZZK wako wenye busara, wako waoga, wako wadini, wako wa wakabila, wako wa ukanda, wako wanafiki, wako waumini, wako wafuasi, wako washabiki, wako wakweli.
  • Waoga: Hili ni kundi la kwanza na ndilo kundi kubwa, hawa wanampinga ZZK kwa uoga tuu usio na sababu zozote za msingi. Hawa ni wale waliozoea mazoea, hivyo hiogopa mabadiliko yoyote yawe positive au negative, kwao ni uoga tuu!. Kwa vile ZZK ni mwana Chadema, na mwana chama yoyote anayo haki ya kugombea nafasi yoyote ya uongozi ndani ya chama na ndani ya nchi. ZZK ameitumia haki hiyo kuelezea nia yake bila kuvunja sheria, tararibu wala kanununi yoyote ya chama. Natoa mwito kwenu nyie enyi waoga, open up be ready for changes for the better!. Ukombozi wa nchi hii utaletwa na wele tuu wenye kukubali mabadiliko na sio ving'ang'anizi!.
  • Wadini:Kama ilivyo kwa Tanzania, nchi kama nchi haina dini, ila watu wake wa na dini zao!. Wadini ni wale ambao, wanajiona dini zao ni bora zaidi ya dini za wengine, hivyo yoyote asiye dini yao, wao wanamuona huyo sio!. JK ni Muislamu, appointment powers zake hazina any terms of refence hivyo huweza kuteau mtu yoyote kutoka positio yoyote na kumgeuza kuwa ni mtu wa top office bila reference yoyote. Wale wanaotaza ma kwa jicho la udini, wakijuiliza kwa nini fulani kapewa nafasi fulani kwa sifa zipi na vigezo vipi, wakifikosa na kuja kuangalia dini ya mhusika, basi watamlebo JK ni mdini, hata kama baadhi ya wateule hawa wanaso sifa na wangestahili nafasi his regardless wao ni dini gani!. Ndio maana kwa baadhi ya teuzi za JK tukubali tukatae anatea as he pleases lakini kwa wengine, dini ni kigezo!. Chadema nacho kama chama hakina dini, ila wanachama, wafuasi wake na washabiki wake wote wana dini zao. Kwa hao wadini wa Chadema kwao,nafasi za juu kabisa za uongozi wa Chadema, lazima zishikwe na watu wa dini fulani!, ZZK alipogombea uenyekiti kiliwaka na mwenyewe akanywea!. Uchaguzi unakuja tena na this time tutamchagiza Prof. Safari kugombea Uenyekiti, nashauri subirini muone kitakachotokea!. `Vivyo hizo wako wanaompinga ZZK kwa dini yake, hawa watampinga Mkandara, Watampinga Arfi na Watampinga Prof. Safari kugombea top position yoyote kwa sababu tuu ya dini zao. Hawa wapo, tukubali tukatae!. Dawa yao hawa sio kuwabadilisha, bali kuyalazimisha mabadiliko, ili hayo mabadiliko ndiyo yawabadilishe na huo udini wao uwawashe kama koti la chawa na kujikuta wanalazimika kulivua!.
  • Wakabila: Hili nalo ni kama lile la udini, Tanzania kama nchi, haina kabila, ila wananchi wake makabila yao, viongozi nao wana makabila yao. Ukabila ni ile hali ya kuona mtu wa kabila lako ndio bora zaidi. Enzi za Nyerere, kwa vile alitoka Musoma, watu wa Musoma, wakajikuta wana upper hand Ikulu na kwenye Majeshi ndio maana tuliwashuhudia kina Musuguri, Mwita Marwa, Waitara etc, huku kule Ikulu kina Apiyo etc. Waziri fulani akiwa wizara fulani, inatokea wengi wa wakuu wa taasisi za wizara hiyo ni kabila lake!. Hata JK baada ya kuingia ikulu, wako watu fulani wa kabila lake, ndugu au jamaa zake, wamefika hapo walipo kwa kubebwa tuu!, tena angalau wengine baada ya kubebwa, "ukibebwa bebeka" wamebebeka na ku perform!. Wako waliobebwa, lakini hawabebeki, they are non performers kabisa, lakini wanaendelea kuwepo tuu na sana sana ni kuhamishwa tuu huku wakiendelea ama kuto perform, au kuborongo ila wapo!. Chadema nacho kama chama, hakina kabila, ila wanachama na viongozi wake wana makabila yao!. Hakuna asiyejua kuwa kuna viongozi wenu wakuu wamefikaje hapo walipo!. Hakuna asiyejua kuna mtu yuko bungeni na bintiye na mkwewe kwa sababu tuu ya kabila na nasaba!. Sasa kuna wanaompinga ZZK kwa sababu tuu ya kabila lake!. Wangwe alipotamka kugombea uenyekiti, kilichofuatia sote tunakijua!. Chadema ni chama cha kitaifa, kiko over and above ukabila, hivyo tutahakikisha nafasi za juu za uomgozi, zinashikwa na wenye sifa regardless ni wa makabila gani, ndio maana nitamchagiza tena ZZK agombeaa sio tuu urais, bali aanzie Uenyekiti wa Chadema ambao unautangulia urais na hauna kizingiti cha umri!. Na kuna ukabila mbaya kabisa usiotamkwa wazi, lakini umo mioyoni mwa wenye ukabila,"eti watu wa makabila fulani fulani, kamwe hawawezi kushika urais wa nchi hii!". Tutaukomesha!.
  • Ukanda: Huu ni kama ulivyo udini, na ukabila, Tanzania kama nchi, haina kanda fulani ambazo ni preferencial, maeneo yote ni sawa mbele ya taifa!. Ila lazima tukubali, tukatae, kuna maeneo fulani, watu wake wameneemeka zaidi kuliko maeneo mengine!. Sasa kuna baadhi ya watu wa maeneo haya yaliyoneemeka, hujiona wao ni bora zaidi kuloko watu wa maeneo mengine, hivyo kufikia stage ya kujiona wao wanastahili preferential treatment kwenye kila kitu, hali inayopelekea wale watu wa maeneo ambayo hayajaneemeka sana, kujiona wako sidelined au marginalized!. Ili kujionyesha na wao wapo, ndio hivi sasa wanajitutumua!. Hakuna ubishi Kaskazini kuna neema kuliko kwingine kote!. Chadema nayo ime gain stronger momentum maeneo kuliko maeneo mengine ambayo its gaining now!. Hili limewapelekea baadhi ya manazi kujidhania nafasi fulani za uongozi its their rightful kutokana na kanda yao!, ndio maana utasikia safari hii rais lazima atoke kanda fulani!. Kwa vile ZZK hatoka Kaskazini, kuna wanaompinga kwa hilo tuu na hawa wakanda, hata akiibuka Prof. Mwesiga Baregu au Prof. Safari ambao wanazo sifa zote kugombea uenyekiti au urais, nao watapingwa tuu!. Ili kuiondoa hii dhana potofu ya ukanda, tunataka kushuhudia nafasi za juu zikishikwa na watu wenye sifa, regarless wanatoka kanda gani sambamba na haki za kugombea, na hata ikitokea top positions zote zikashikwa na watu wa kabila moja kanda moja, lakini watakuwa wamezipata kwa merits za sifa na uwezo, na sio kwa ukanda na ukabila wao!.
  • Wanafiki: Hawa ni watu wanaujua uwezo wa kiukweli wa ZZK kma rais na amiri jeshi mkuu, lakini kwa sababu, wamezoe kujikomba komba kwa watu wao, wanajifanya kumpinga tuu ili wasionekane watovu wa nidhamu!. Vivyo hivyo kwa wanamsupport ZZK, kuna wale wanaomsupport na kumchagiza ili kuona Chadema inasambaratika. Wengi wa hawa hawana nia ya dhadi ya mageuzi, bali wanataka ZZK apunguze kitisho cha lanss;ide victory ya Chadema come 2015 (if it will change!).
  • Washabiki: Miongoni mwa wanaomsupport ZZK, wako wanaomsupport au kumpinga kwa ushabiki tuu, kama walivyo mashabiki wa simba na yanga. Hata ZZK aboronge vipi, wao kama mashabiki, watamchagiza tuu na kumshagilia mpaka mwisho. Na kwa wasio mashabiki, hata afanye mema vipi hawa watambeza tuu. Uzuri wa ushabiki ni mapenzi tuu na sometimes hauna sababu zozote za msingi za kupenda au kuchukia!. Mfano kuna wanaoipenda yanga kwa sababu fulani na kuna wanaipenda yanga kwa bila sababu yoyote!. Kuna mashabiki wa Yanga ambao wao hawaimaind Simba lakini kuna mashabiki wa yanga wanaichukia Simba bila sababu yoyote!. Mfano mimi siipendi kabisa rangi yoyote ya kijani na manjano!, kitu chochote chenye kijani na manjano kinanichefua, hivyo kujikuta naichukia Yanga kwa sababu tuu ya rangi hizo, kama yanga wangebadili rangi na kuwa blue na nyeupe, nisinge ichukia Yanga!. Vivyo hivyo ZZK ana washabiki wake na wengine wana mashabiki wao wengine, hivyo kuna wanaimpinga ZZK kwa ushabiki tuu lakini hawana hoja zozote valid ni kwa nini ZZK or why not ZZK!.
  • Waumini: Waumini ni stage ya juu zaidi ya washabiki, hawa wana muaminia na kumkubali. Kuna watu wanamuaminia ZZK na kumkubali hivyo kumuunga mkono!. Katika kumuaminia na kumkubali, pia kuna watu wana waaminia na kuwakubali wengine wote wenye uwezo wa urais. Miongoni mwa waumini hawa, wale ambao wanawaaminia wengine ambao sio ZZK, watampinga ZZK kwa uwezo wao wote na hiyo upinzani wao ni justified kwa wanachokiamimni.
  • Wafuasi: Hawa ni zaidi ya washabiki na waumini, hawa ni followers wa ZZK ambao watamfuata popote atakapokuwepo ndipo nao watakuwepo. Followers mwanzo walikuwa washabiki, waka graduate na kuwa waamini, waka pata masters kwa kumfuata na kujiunga Chadema. Kwao hawa ZZK ndio everything!. Sambamba na hao, pia figures nyingine za Chadema, nao wanao wale wanaowafuatilia, hawa ambao sio wafuasi wa ZZK, hawa kwa vyovyote vile, watampinga ZZK au mwingine yoyote atakayejitokeza. Huu ufuasi ukivuka mipaka unageuka kuabudu!. Wako wafuasi wanao waabudu wale viongozi wao na kuwaona kama miungu!. Sasa ikitokea mtu akajitokeza kuwapinga hawa miungu watu ndani ya Chadema, mtu huyo atachukiwa na kubatizwa kila aina ya jina "katumwa", "msaliti", "pandikizi" etc, etc!. Baada ya uchaguzi wa 2010, kuna watu waliaminishwa mgombea wa Chadema alishinda, NEC wakauchakachua ushindi ule na kumtangaza mgombea wa CCM!. Sasa wengi wa hawa mashabiki, waumini na wafuasi, wanaamini na waabudu, tayari wanaye mgombea wao kwa 2015 na sio ZZK!, kitendo cha ZZK kutangaza nia, kimawatetemesha, wanatishika na kuweweseka humu jukwaani kila kukicha!. Mimi nilibahatika kuzungumza off-the record na mgombea fulani hivyo naujua msimamo wake, ndio maana nikawashauri, ...
  • Wenye Busara: Hawa ni wale ambao wanazo akili za kiutu uzima, hawa wanaelewa ushindi wowote, hupatikana kwa team work na sio individual ambitions za kuitwa rais!. Hawa wanapiga mwenendo wa ZZK kutangaza kugombea kwa sababu baadhi ya matamshi na maamuzi ya ZZK, yanaongozwa na feelings, emotions na ego, sio kwa critical thinking na tafakuri makini, hivyo huwa ni maamuzi ya papara na yasiyo na tija yoyote kwa mustakabali wa Chadema. Hawa wanampinga ZZK bila chuki, wanaamini ni ujana na utoto, akikua atatulia. Wengi katika kundi hili ni ma great thinkers, ZZK kama ana masikio, atakuwa amewasikia!.
  • Wakweli:Hili ndilo kundi la mwisho na lina watu wachache. Hawa ni wale ambao wanampinga ZZK kwa sababu za ukweli au wanamsupport ZZK kwa sababu za ukweli. Ukweli daima huwa ni mchungu, ukweli huwa unauma, ukiwa mkweli daima utachukiwa na sometimes you may pay the price!. Sometimes ukiwe mkweli mno, hili ni kosa kwa siasa zetu zilizogubikwa unafiki, majungu, fitna na mambo kibao ya kiajabu ajabu!. Kosa kubwa la ZZK ni kuwa mkweli daima!. Mimi pia niko kwenye kundi hili, nafahamu kwa sasa ZZK ndie mtaji mkubwa zaidi Chadema kuliko mtu mwingine yoyote!. Nahisi hata ushindi wa wale vijana wa Kigoma, he has a hand!. Yako mambo mengi huwa ninayaandika humu, huwa naishia kupingwa!. Sifa kuu ya ukweli siku zote husimama!. Kwa vile Chadema wamejipanga kushinda 2015, ziko hoja ambazo ni za ukweli na lazima Chadema wasimame nazo ikiwemo ya kutompuuza ZZK hata kidogo na kuendelea kumwacha akipayuka payuka, he needs to be contained more kuliko hivi alivyo let loose!. Chadema ndiyo inayomuhitaji zaidi ZZK kuliko ZZK anavyoihitaji Chadema!.

  Hitimisho.
  2015 inakuja, kuna vyama vinajipanga kuchukua nchi huku vingine vinajipanga kutetea viti vyao. Katika
  kutimiza azma hiyo, viko vyama vinajipanga kimipango mkakati huku vikieleza vitafanya nini, na kuna
  vyama vinaendeleza mahubiri, kucheza makida makida na kuchezea shilingi chooni!. Siku ya siku ikifika,
  hatutaki watu waje kutulilia tena humu as if hawakuambiwa!. ZZK ametangaza tuu nia, msitetemeke,
  msiweweseke wala msitishike, just do the right thing and and in doing that right thing, make sure you do it
  right!.

  Naomba kuwasilisha.

  Asante.

  Pasco.
   
 2. M

  Molemo JF-Expert Member

  #2
  Oct 15, 2012
  Joined: Sep 24, 2010
  Messages: 13,287
  Likes Received: 580
  Trophy Points: 280
  Huu ni wakati wa kujenga chama na CCM wangependa sana makundi ya Urais yawe kama kwao ili CDM isambaratike-Mzee Mtei.
   
 3. POMPO

  POMPO JF-Expert Member

  #3
  Oct 15, 2012
  Joined: Mar 12, 2011
  Messages: 6,694
  Likes Received: 14
  Trophy Points: 135
  Pasco nimepata habari za kuaminika kuwa, mambo yakitulia CCM, Zitto atahamia huko muda si mrefu kuongeza nguvu kambi ya Lowassa na mpango umeandaliwa na Jk na namna ya kumpokea.

  Ni Bora gamba ZZK utoke, CHEDEMA tumekuchoka...
   
 4. M

  Mkeshaji JF-Expert Member

  #4
  Oct 15, 2012
  Joined: Jan 7, 2011
  Messages: 4,264
  Likes Received: 7
  Trophy Points: 0
  Jamani eeeh!
  Si msubiri basi hiyo 2015 ifike mkachukue fomu na mgombee kupitia kama ni chama au mgombea binafsi.

  Tumechoshwa na khabari za mtu mmoja kila siku.
  By the way, who is he?

  Ngoja nikaage mwili wa kamanda saa hizi.
   
 5. Shinto

  Shinto JF-Expert Member

  #5
  Oct 15, 2012
  Joined: Dec 6, 2010
  Messages: 1,781
  Likes Received: 6
  Trophy Points: 0
  ZZK ni ndege wa rangi tofauti kwenye kundi la CHADEMA ya leo! Dini, Kanda, kabila vinahusika!
   
 6. Kachanchabuseta

  Kachanchabuseta JF-Expert Member

  #6
  Oct 15, 2012
  Joined: Mar 8, 2010
  Messages: 7,290
  Likes Received: 11
  Trophy Points: 135
  Mkuu Pasco Mayalla

  Pole sana nilikuwa sijakujibu muda mrefu maana naona kila siku anaangaika kwa ajili ya Zitto
  Mimi ni CCM damu lakini nakuhakikishia kuwa Zitto anatumika wewe subiri true colour will show.......
  Kama ilivyokuwa kwako baada ya kugundulika kuwa wewe ni mwanaCCM mwenzetu ukawa unasema
  wewe ni independent advicer mara Political Analysist lakini yote kwa yote hakuna chochote na wewe your
  true colour show at the end

  Last:.................... Pasco Njaa Mbaya tujenge taifa letu tuache siasa za majungu................
   
 7. M

  Mkeshaji JF-Expert Member

  #7
  Oct 15, 2012
  Joined: Jan 7, 2011
  Messages: 4,264
  Likes Received: 7
  Trophy Points: 0
  Wakati mwingine unaongea (I mean unaandika) vitu vya maana sana.
   
 8. rosemarie

  rosemarie JF-Expert Member

  #8
  Oct 15, 2012
  Joined: Mar 22, 2011
  Messages: 6,767
  Likes Received: 1,023
  Trophy Points: 280
  mkuu unahangaika sana na issue ya zito,mbona ulishasema wewe sio chadema sasa kelele nyingi za nini,by the way muda wa kutangaza nia bado sana,hata huyu Rais aliyeko madarakani hajamali hata nusu ya kipindi chake,nafikiri tutulie tusubiri end of 2013 pale ndio unaweza kuja na ushawishi wako wa kinafiki
   
 9. W

  WEMBE WENGE Senior Member

  #9
  Oct 15, 2012
  Joined: Mar 6, 2011
  Messages: 127
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  Pasco
  usitupotezee muda kanywe nae chai.
  Ukiona mtu anakimbilia ikulu muogopeni kama ukoma (j.k. Nyerere, .....)
   
 10. Viol

  Viol JF-Expert Member

  #10
  Oct 15, 2012
  Joined: Dec 15, 2009
  Messages: 18,982
  Likes Received: 1,087
  Trophy Points: 280
  njaa noma
   
 11. Safari_ni_Safari

  Safari_ni_Safari JF-Expert Member

  #11
  Oct 15, 2012
  Joined: Oct 5, 2007
  Messages: 22,458
  Likes Received: 5,844
  Trophy Points: 280
  Pasco,

  Kwa hiyo wewe mathalan una binti ana miaka 15 halafu mtu akakwambia kuwa akifikisha miaka 18 atakuja kumposa utajisikiaje? Kwa nini asisubiri mtoto afikishe hiyo miaka 18(umri wa mtu mzima) ndio aje kuposa?
   
 12. W

  WEMBE WENGE Senior Member

  #12
  Oct 15, 2012
  Joined: Mar 6, 2011
  Messages: 127
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0

  msisahau mbinu na mikakati ya mrema wa NCCR enzi zile zilikuwa kama hivi. lengo likiwa kuua upinzani. na huyu jamaa naona nyota ni zilezile. alitengenezewa umaarufu na dola kisha akadiffect watu wakamuona mpinzani kumbe geresha. acha na huyu jamaa naona anaelekea kulekule. hata magamba wenye serikali hawaongelei urais yeye anatoka wapi? huyu kifaa jinamizi jamani. Labda tumuulize analipwa ngapi. maana hata hao magamba wanavyomapimbisha utashangaa.
   
 13. nngu007

  nngu007 JF-Expert Member

  #13
  Oct 15, 2012
  Joined: Aug 2, 2010
  Messages: 15,871
  Likes Received: 56
  Trophy Points: 145
  Kwani ni Nani Anatetemeka? ni Nani Anaweweseka? na ni Nani Anatishika?
  Ni wewe ndie Unayeweka UPUUZI wa UDINIl UKABILA kwenye MASUALA ya ZITTO KABWE Ni wewe ndie Unayeweweseka kama ZITTO KABWE si kiongozi asiyefaa...

  Embu tueleze ni tangu lini ZITTO KABWE amefanya MIKUTANO ya KUZUNGUKA nchini kama VIONGOZI wenzake wa CHADEMA kutafuta WANACHAMA WAPYA zaidi ya KUZUNGUKA kwa NDEGE na MTUKUFU RAIS? au MAMA SPIKA?

  EMBU TUAMBIE ni lini AMEONGELEA kuhusu CHADEMA zaidi ya kuongelea U-MIMI KUGOMBEA URAIS? Sasa ni kwanini Unamkumbatia MBINAFSI; MPEKEE; MCHOYO; ILI AKIVURUGE CHAMA cha UPINZANI kinachoitwa CHADEMA?

  Wa CCM wapo WENGI wanaotaka kugombea URAIS; lakini UMESIKIA wanaongelea UDINI; UKABILA ? ni Kwanini wewe UNAONGELEA UPUUZI HUO? INAONYESHA JINSI ULIVYOFILISIKA KISIASA...  What I'm telling you is this; Remember what Julius Nyerere Once Said... And then the harder they come...The harder they fall...One and for all

  Did you know what kind of people NYERERE was referring to????
   
 14. Mwana Mpotevu

  Mwana Mpotevu Platinum Member

  #14
  Oct 15, 2012
  Joined: Sep 7, 2011
  Messages: 3,294
  Likes Received: 333
  Trophy Points: 180
  nahisi ni kwa mara ya kwanza leo nimekupa LIKE yangu na UNASTAHILI kwa jibu hili. Sina nyongeza kwa Pasco
   
  Last edited by a moderator: Jan 4, 2016
 15. TOWNSEND

  TOWNSEND JF-Expert Member

  #15
  Oct 15, 2012
  Joined: May 8, 2011
  Messages: 2,597
  Likes Received: 48
  Trophy Points: 145
  Hivi kweli pasco una njaa ya kihivyo ....mbona huwa nakuona wa maana kumbe upo hivyo imekuwaje ukawa na njaa ya kijinga hivyo naaamini hata kwa mungu haya sio mawazo yako tangu nimejiunga jf sijawahi ona upuuzi kama huu
  angalia nyuma tizama ndugu zako jamaa zako angalia shida walizo nazo leo watz ...dawa hakuna kwa ujumla shida ni nyingi au na wewe unataka uwe ndani ya safari za jk kama michuzi?
   
 16. Kimbunga

  Kimbunga Platinum Member

  #16
  Oct 15, 2012
  Joined: Oct 4, 2007
  Messages: 13,011
  Likes Received: 1,816
  Trophy Points: 280
  Yero hiii inategemea wewe unatoka pande ipi? Kule kwetu mtu anachumbia mimba! Je likizaliwa dume?
   
 17. Safari_ni_Safari

  Safari_ni_Safari JF-Expert Member

  #17
  Oct 15, 2012
  Joined: Oct 5, 2007
  Messages: 22,458
  Likes Received: 5,844
  Trophy Points: 280
  Unaiwowa hiyo dume
   
 18. Takalani Sesame

  Takalani Sesame JF-Expert Member

  #18
  Oct 15, 2012
  Joined: Jun 24, 2008
  Messages: 588
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 33
  Ikulu kuna nini?
   
 19. l

  lengijave Senior Member

  #19
  Oct 15, 2012
  Joined: Apr 4, 2012
  Messages: 116
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Mr.Pasco,
  Pole na majukumu na nimeona vile umeandika na kwa sababu kila mtu ana upeo wake mi ninaona ni vizuri nikichangia tofauti na wewe,Kitu ambacho sipendi vile anafanya,kwanza kabisa ni sawa na kuvunja katiba ya mambo ya uchaguzi:
  Kwa mfano katiba inasema kwamba mtu ili agombee uchaguzi lazima awe na miaka 40 sasa yeye 2015 bado atakuwa haja fikisha:sasa we huoni ni kukosa busara au kama kuna watu ameongea nao kwamba watabadilisha katiba kwa manufaa yake mwenyewe,ni hekima angengoja kwanza katiba abadilike ndo aanze kutangaza:pia si vizuri kwa kila mwanachama kutangaza nia kabla muda wa kutangaza haujafika:sababu anaweza hata akadhuriwa mambo mabaya hata kabla,ni vizuri angefanya kama ni ndoto, wakati ukifika anagombea,ni sawa na kwenda kwenye vyombo vya habari useme nataka nimuoe fulani wakati hata huja onge nae,Pia kuna maswala hayapo kikatiba lkn yanaweza kumuangusha,mfano Zitto bado hajaoa na vyama vingine vitapata cha kusema we huoni ni vizuri angejipanga yeye mwenyewe arekebishe mambo madogo madogo kabla ya kutangaza nia?
   
 20. Pascal Mayalla

  Pascal Mayalla JF-Expert Member

  #20
  Oct 15, 2012
  Joined: Sep 22, 2008
  Messages: 24,560
  Likes Received: 18,289
  Trophy Points: 280
  Mkuu Pompo. Hili nimelizungumzia pale number 10. Kama habari zako ni za kuaminika, then hizo ni habari za kweli. Sifa kuu ya ukweli, huwa unasimama!. Mpaka ukweli huu utakapothibitika na kusimama ndipo, nitakuamini kuwa kijana anakuja kuimarisha kambi ya mgombea wangu!.
   
Thread Status:
Not open for further replies.
Loading...