Record kubwa sana inaonyesha kuwa wanasiasa wanaokuwa na ndoto za urais kwa muda mrefu hushindwa kufanya majukumu yao vizuri wanapopata nafasi za kuwa rais na mara nyingi huvuruga sana nchi zao. Sababu mojawapo kubwa ya kushindwa huko ni kutokana na kuwa mara nyingi huwa hawana ajenda ya nchi bali ajenda yao. Sababu nyingine ni kuwa njia wanazotumia huwafanya wakose washauri wazuri kwa vile huwa wamahsvurugana na watu ambao wangewashauri vizuri.
Richard Nixon (aligombea kwa zaidi ya miaka kumi), Kikwete (alijiandaa kwa zaidi ya miaka kumi+), Bush (alijiandaa kwa miaka minane tang baba yake alivyoshindwa na alitumia pesa nyingi sana kuupata).
Mara zote marais wanaohappen kuwa na ufanisi mkubwa ni wale walioombwa na mashabiki wao kuwa wagombee, na wakapewa support kubwa sana na vyama vyao; wengine huchaguliwa kwa bahatio bahati tu kwa vile walikuwa katika position fulani wakiwa hawategemei kupata nafasi hiyo. Utaratibu mzima wa wao kujiandaa kugombea huwa ni muda mfupi sana. Mifano ipo ya kutosha kwa watu wa aina hiyo
Kuanzia mwaka jana (au kabla ya hapo- wakati ulituarifu kuwa Kikwete alipendekeza wewe ndiwe uwe rais ajaye), Mheshimiwa Zito umekuwa vocal sana katika kutangaza nia yako ya kugombea urais na mara kadhaa umekwaruzana na wenzako ndani ya chama chako kwa sababu hiyo tu. Kadri siku zinavyokwenda umekuwa unaongeza kasi hiyo ukiwa labda na lengo la ku-preempt watu wengine ndani ya chama chako wasigombee nafasi hiyo. Utaratibu unaotumia, hauna tofauti sana na utaratibu uliotumiwa na Kikwete wakati akitaka kugombea uraisi, na leo hii sote tunajua kuwa Kashindwa kazi hiyo. Ingawa leo hii tunamwona Kikwete ni dhaifu, lakini kila mtu anajua jinsi alivyokuwa thabiti kama wewe ulivyo leo wakati yeye akiwa waziri wa fedha ambapo alibana kabisa mismaha ya kodi na kuwabana sana wafanyabishara waliokuwa wakikwepa kodi. Kwa hali hiyo, kuwa makini kuwa hatua unazofanya sasa hivi zinaweza zisiwe productive kwako binafsi, na huenda kwa chama chako. Usitake swala la Zito na Urais ndiyo iwe headline kila siku, kwa sababu ikitokea kuwa hutateuliwa na chama chako kwa njia halali kabisa, utakuwa umetia doa kwa chama chako.
Kiongozi mzuri ngazi ya Urais siyo tu yule ambaye yuko vocal bungeni kupambana na serikali, bali ni yule aliyekuwa na busara za kutosha kuangalia mambo kwa mapana kwa faida ya jamii yake. Unapokuwa unajaribu kuwagawa wanachama wa chama chako kwa ajili ya uraisi ni dalili ya kupungukiwa busara hiyo.