Urais, Halima, Nassari na Kigoma

Urais, Halima, Nassari na Kigoma

Status
Not open for further replies.
mkuu nadhani hujamwelewa zitto, yeye hapingi kilichoandikwa gazetini ila anataka kudhibitisha kilichoandikwa kwa kuleta video, hivyo kifupi yupo pamoja na mwandishi. Ndio maana wadau wanasubiri video ili waone nani mwongo kati ya Zitto na gazeti v/s Nassari,mdee,Filikunjom na Estar kwa upande mwingine.!
veve iko gamba veve...eeeh?
 
....hahahahaha..mkuu bado hujamaliza editing..?..peleka pale nyumba ya vipaji..wakueditie...kama mlivyokutana siku ile na kupanga juu ya hilo tamasha...
 
Wewe unapenda mtu na sio chama.Go to hell.

Hell nimeshakwenda na nimerudi baada ya kuona viongozi legelege kama Kikwete wanavyotesa Watanganyika. Unataka upendwe wewe na upewe urais?
 
hivi zitto wewe kijana mwenzangu na nakumbuka siku unatolewa bungeni sijui ulifanyaje enzi za mzee sitta pale muhidhir alipokwaluzana na wewe nakumbuka nilikuwa form five siku ile nililia sana kwa jinsi nilivyokuwa nakupenda kama mbunge machachari pale bungeni na mwenye msimamo na mwenye mapenzi ya kweli na chadema ila kwa hii hali inayotokea unaniweka dilema sn mh,hv kweli zitto ukisimamishwa ugombee urais kweli zitto na Mungu anakuona unao umarufu wa kutuletea wabunge wengi kama alivyofanya Dr slaa?
 
Akili yako imekupoteza, ikiwa unadhani zito anafaa kuwa rais wa jmt asubiri atimize miaka 55, wakati anasubiri akitumikie chama kufa kupona, ni sisi tutamtunukia hiyo top position nchini, ama la anakwisha kisiasa kwa stail ya mutamwega.
Thubutu, Nadhani hujajua tuko kwenye mchakato wa kuruhusu wagombea binafsi, na hivyo hata bila ya chadema nyota ya Zito itaendelea kuzizima in whatever means.
 
Karibu jamvini!!! Ila ni utamaduni wetu Kupiga HODI unapokuja kama mgeni.
Mhhhhhhhh!!!!!namkubali sana mh.Zitto na ndie mgombea rais kijana mpya wa 2015,hata mkileta majunguhili taifa ni la vjana kwa ajili ya mustkabali wa taifa lao.
 
Nilikuwepo uwanjani pale lake Tanganyika Kigoma, kilichoandikwa ndicho nilichosikia pia. Videos zitawekwa hapa na zitathibitisha.

Siwezi kuwaandikia mwananchi kwani mimi silalamiki kuhusu habari hiyo. Wenye kuilalamikia habari wameandika.

Mimi ninaamini gazeti la Mwananchi ndio gazeti pekee huru la kiswahili hapa nchini. Ndio gazeti pekee ambalo umiliki wake hauna maslahi na waandishi na wahariri wake ni mahiri, hawana njaa na hawapindishwi. Ndio maana huandika ukweli muda wote na wanapokosea hawasiti kurekebisha. Ndio maana ni gazeti linasomwa kwa wingi kuliko magazeti yote nchini. Hakuna gazeti linalofikia hata nusu ya mwananchi kwa kusomwa. Hivyo Mwananchi linaaminika na umma.

Najua kuna watu wana chuki binafsi na mwananchi kama gazeti na wahariri wa mwananchi kama binaadamu. Hayo wayamalize wenyewe huko walikochukiana.

Subirini video ndio tutajua habari ile imepikwa au ni ya kweli. Kwa tuliokuwepo uwanjani tunajua nani alisema nini.

Hizo video zinachelewa wapi? Ziweke haraka zituondolee mashaka ya kuchakachuliwa
 
Mbunge wa kigoma kaskazini, Naibu katibu Mkuu (CHADEMA) Zitto Kabwe.

Katika gazeti la Mwananchi la tarehe 23 Julai 2012, kulikuwa na habari yenye kusomeka 'Wabunge wamsafishia Zitto njia ya Urais 2015'. Habari hii imeleta mjadala mara baada ya kutoka na kusomwa. Mjadala umekuzwa zaidi baada ya Wabunge ndugu Halima Mdee na ndugu Joshua Nassari kukanusha maneno waliyonukuliwa kusema. Napenda kusema masuala yafuatayo.

Moja, Waheshimiwa Wabunge Halima Mdee, Joshua Nassari, Kangi Lugola, Esther Bulaya, Deo Filikunjombe, Raya Ibrahim, Amina Mwidau na David Kafulila walihudhuria tamasha la vijana wa Kigoma All Stars kwa kualikwa na Mratibu wa kundi hilo Mwasiti Almasi.

Wabunge wengine walialikwa lakini hawakutokea wakiwemo Joseph Mbilinyi,…

Mbunge wa kigoma kaskazini, Naibu katibu Mkuu (CHADEMA) Zitto Kabwe

Katika gazeti la Mwananchi la tarehe 23 Julai 2012, kulikuwa na habari yenye kusomeka 'Wabunge wamsafishia Zitto njia ya Urais 2015'. Habari hii imeleta mjadala mara baada ya kutoka na kusomwa. Mjadala umekuzwa zaidi baada ya Wabunge ndugu Halima Mdee na ndugu Joshua Nassari kukanusha maneno waliyonukuliwa kusema. Napenda kusema masuala yafuatayo.

Moja, Waheshimiwa Wabunge Halima Mdee, Joshua Nassari, Kangi Lugola, Esther Bulaya, Deo Filikunjombe, Raya Ibrahim, Amina Mwidau na David Kafulila walihudhuria tamasha la vijana wa Kigoma All Stars kwa kualikwa na Mratibu wa kundi hilo Mwasiti Almasi.
Wabunge wengine walialikwa lakini hawakutokea wakiwemo Joseph Mbilinyi, David Silinde, Amos Makala, Vicky Kamata na Peter Serukamba. Wabunge hawa hawakualikwa na mimi na wala sikufanya mazungumzo nao yeyote ya awali au kuwaambia au kukubaliana nini cha kuzungumza au hapana. Tamasha lilikuwa la muziki na halikuhusika kabisa na siasa.

Waheshimiwa wote walipewa nafasi ya kusalimia na wote walizungumza. Wabunge waliozungumza kwa muda mrefu kidogo ni ndugu Halima Mdee, Joshua Nassari, Deo Filikunjombe na Kangi Lugola.

Hotuba za Wabunge wote zilirekodiwa kwenye video neno kwa neno na Video hizo zitawekwa wazi kwenye blogu yangu kama sehemu ya documentary ya tamasha lile la kihistoria.

Pili, sikuhusika kwa namna yeyote ile na kuandikwa kwa habari hii iliyozusha mjadala. Wala sikujua kama habari hii ingeandikwa maana katika ziara ile sikuita mwandishi hata mmoja maana nilitaka liwe tukio la Kigoma tu.

Kama mwandishi kaandika ambayo wabunge hawa hawakuyasema basi itaonekana kwenye videos hizo. Wabunge wenyewe wanajua kwenye nafsi zao nini walisema Kigoma na kipi kiliwasukuma kusema walioyasema Kigoma. Nisingependa kuhusishwa kwa njia yeyote ile na matamshi yao, habari iliyowanukuu na hata makanusho yao. Maana mwisho wa siku ukweli ndio utasimama.

Suala la Urais lisitupotezee muda kwani kuna mambo mengi sana ya kujadili kuhusu nchi yetu. Taharuki ambazo watu wanazipata masuala ya urais yanapotajwa zinashangaza sana.

Chama changu bado hakijatangaza rasmi mchakato wa kupata mgombea Urais. Hivi sasa chama hakina mgombea Urais mpaka hapo mchakato utakapotangazwa ambapo wanachama wataruhusiwa kuomba kupeperusha bendera ya chama. Mwanachama wa chama chetu atakaye kubalika na jamii na wajumbe wa mkutano wa uteuzi ndiye atakuwa mgombea wetu. Kwa sasa hayupo na hivyo tusipoteze muda kujadili jambo hili.

Mzee Thabiti Kombo alituachia usia tunapokuwa tunazungumza. Alisema 'weka akiba' sio akiba ya fedha, bali ya akiba ya maneno. Tuweke akiba ya maneno. Tusimalize yote.
 
ccm inatumia mtaji huu mtaji wa zito kusahaulisha mambo ya dr ulimboka na upuuzi wa mwigulu nchemba be careful
 
Suala la Urais lisitupotezee muda kwani kuna mambo mengi sana ya kujadili kuhusu nchi yetu. Taharuki ambazo watu wanazipata masuala ya urais yanapotajwa zinashangaza sana.

Chama changu bado hakijatangaza rasmi mchakato wa kupata mgombea Urais. Hivi sasa chama hakina mgombea Urais mpaka hapo mchakato utakapotangazwa ambapo wanachama wataruhusiwa kuomba kupeperusha bendera ya chama. Mwanachama wa chama chetu atakaye kubalika na jamii na wajumbe wa mkutano wa uteuzi ndiye atakuwa mgombea wetu. Kwa sasa hayupo na hivyo tusipoteze muda kujadili jambo hili.

Mzee Thabiti Kombo alituachia usia tunapokuwa tunazungumza. Alisema 'weka akiba' sio akiba ya fedha, bali ya akiba ya maneno. Tuweke akiba ya maneno. Tusimalize yote.

Hapo kwenye red, hiyo ni jana, leo bungeni Zitto anafanya flip-flop!
 
sawa ukipata mda pitia link http: https://www.jamiiforums.com/jukwaa-...using-ramadhan-semtawa-kuivuruga-chadema.html ambayo tunapata wasi wasi kuwa unamtumia huyu bwana.hizi ni baadhi ya makala anazoandika huyu....hizo video umeshaweka kwenye blog yako? nakuomba na hapa uziweke..

urafiki wako na davidi Msacky unatajwa kuw nae yuko nyuma ya project hii ya uchonganishi ndani ya chama (chadema)...unasemaje juu ya hili?

ni kweli wewe unatumiwa na ccm kukivuruga chama?(chadema)

bila shaka najua zito na denis msaki ndo wamefanya haya
 
Kwa kweli Zito ukicheza karata yako vibaya 2015 ndio utakuwa mwisho wako kisiasa.. waulize akina Augustino Mrema watakuambia...siasa uchwara hizi..kuwa makini kaka.
 
Hivi hili tamasha lingefanyika KARATU, na wabunge hawa hawa wakasema SLAA ni jembe na anafaa kuwa rais 2015 na gazeti la mwananchi likaripoti kungekuwa na kelele zote hizi?
Free World sidhani kwamba kuna sababu yoyote ya msingi kuanza kutabiri kwamba nini kingetokea ama nini kitatokea.
Na hii isiwe sababu ya kuwafanya watu wasijadili hiki kilichotokea, na bahati nzuri si mara ya kwanza kwa kamanda Zitto kutangaza nia ya kugombea uraisi, na hata hivyo anazo haki zote za kugombea nafasi hiyo kwa mujibu wa katiba yetu.

Zogo hili lote ni kutokana na hii tabia ya kuweka mbele agenda ya uraisi kila mara. Inakumbukwa wakati wa uchaguzi mkuu 2010 alidokeza juu ya yeye kugombea uraisi mwaka 2015, wakati wa uchaguzi mdogo wa arumeru mashariki pia akaibuka na agenda hii ya uraisi. Kama nilivyosema awali hazuiliwi kugombea lakini anatakiwa awe mwerevu na makini sana kujua ni wakati gani wa kuanza kampeni za kuelekea ikulu.

Siku Dr. Slaa, ama Freeman Mbowe atakapotangaza kuwania uraisi, awe karatu ama hai, kama hautakuwa muda muafaka wadau hawatosita kutoa maoni yao, yawe ni ya kukosoa ama kuunga mkono. Sasa timing yake ndio itasababisha critics kuwa wengi ama wachache kwakuwa hakuna mtu yeyote anayeweza kuungwa mkono na watu wote.
 
Last edited by a moderator:
Katika swali hili binafsi yangu nipo upande wa Zitto kwa sababu naamini kabisa na Umri wangu huu ya kuwa hawa vijana Halima Mdee, Joshua Nassari, Deo Filikunjombe wameyasema yaliyoandikwa magazetini ktk uwanja wa starehe. Na badala yake kundi linalomchukia Zitto ndilo limezua habari hii kuipindisha na pengine kuwatishia hawa vijana..

Nitasema kwa nini.. Katika matamasha ya Kibongo, mikutano na mihadhara inawezekana kabisa watangazaji wakazungumza maneno haya kama sifa, kumpamba mtu wao kwa udhi, marashi na manukato ili mradi kuonyesha mapenzi yao kwa mtu huo. Hata mimi leo nikipewa mike jukwaa la JK itakuwa sii rahisi kwangu kumponda na wala sintopewa nafasi hiyo kama wanajua nitamponda..

Hawa vijana wamekwenda ktk sherehe ile kwa furaha na support ya Zitto hivyo kuna uwezekano mkubwa wamemsifia.. Wao wanayakana yaliyoandikwa magazetini lakini mbona sijamsikia Mtu akiwauliza wao WALISEMA NINI?..mimi nawaomba hao kina Mndee, Nasari na Filikunjombe waweke nao kwa maandishi kwanza kabla ya ushahidi maneno waliyohutubia maana tayari salaam nilizopata toka Kigoma zinapingana na maneno yao vile vile..

Hali hii inatisha zaidi sana ndani ya Chadema na hakika naona CCM wanafanikiwa sana kupandikiza mbegu za chuki kwa Zitto kama walivyoweza kuhusu Uislaam na Chadema. Mtanisamehe sana, lakini wanafanikiwa sana na kwa kasi kubwa ajabu.. Jamani hata mimi binafsi sikubaliani na Zitto ktk maswala mengi ya kiutawala hasa pale anapofikiria kwamba anaweza kuunda yeye relationshiup na CCM ktk maswala ambayo yanahitaji situation ya kisiasa itakayo lead to BIPARTISANSHIP - yaani hali ya kisiasa ambayo kwamba chama tawala na chama cha Upinzani wanafikia makubaliano (muafaka) baada ya kupata common ground juu ya maswala muhimu sana kwa Taifa hata iwe madini au gas... Ni makubaliano baina ya vyama kisiasa na sio mtu mmoja au wawili kutumiwa na chama tawala wakidhi sera zao.

Na sii kabisa jinsi gani Zitto anafikiria kama independent mp, anavyolitazama swala la uongozi wa CCM au JK. Anachanganya sana kupewa nafasi za uawaziri kivuli na kuunda relationship na chama tawala kk utekelezaji wa sera ambazo hazikubaliwi na upande wa chama chake. Yeye anachotazama ni kujenga Reli - sawa, kujenga bomba la gas - sawa haya ndio tunayataka lakini anashindwa kuelewa CCM wana mipango gani, usiri gani maana sera ni pamoja na upatikanaji wa fedha, uendeshaji, utekelezaji na kwa malengo gani. Hadi leo hii Barricks hawalipi kodi za corporate na wala hakuna dalili kwamba watakuja kulipa..Tukiwauliza CCM wanasema Mbona Zitto alishiriki ktk kuunda sheria - Tuliwashirikisheni haikuwezekana sasa tufanyeje?

Na ndio maana husema Zitto mtu safi sana lakini sii MWANASIASA.. Tofauti na mwenzake January mwanasiasa na ndio maana aliwaruka siku ya kura za maoni juu ya kutokuwa na imani na Waziri mkuu. Siku zote mwanasiasa utatetea itikadi na sera za chama chako ndio ziwe na solution ya kutatua matatizo kinyume cha hapo ipatikane bipartisan, sio uipitishe solution ya Upinzani wakati chama chako bado kina imani na waziri mkuu.

Zitto akiweza kuijigadhari na hili, kujijenga zaidi kisiasa na kuelewa nini umuhimu wa kuamini malengo ya chama chako dhidi ya chama tawala au vyama vinginevyo basi atakuiwa ameiva kuweza kuongoza maana sina mashaka naye ktk utendaji, sina mashaka na ari, nguvu na sababu za vijana wetu ktk kulijenga Taifa lakini nina mashaka sana IMANI zao Kisiasa. Sidhani kama wameisha iva kisiasa na pengine hawajui hata maana wala umuhimu wa SIASA ktk utawala..Kwao ukisha jua kuendesha gari huna sababu ya kuelewa road signs cha muhimu zaidi ni kuendesha gari mengine yatajipanga.. Hiyo safari hamtafika..
 
Hapo kwenye red, hiyo ni jana, leo bungeni Zitto anafanya flip-flop!

Hapo ulipo underline, yaani kapoteza muda ule ule aliosema kuwa tusipoteze kulijadili na hiyo ni jana tu!
 
  • Thanks
Reactions: FJM
Nilikuwepo uwanjani pale lake Tanganyika Kigoma, kilichoandikwa ndicho nilichosikia pia. Videos zitawekwa hapa na zitathibitisha.

Siwezi kuwaandikia mwananchi kwani mimi silalamiki kuhusu habari hiyo. Wenye kuilalamikia habari wameandika.

Mimi ninaamini gazeti la Mwananchi ndio gazeti pekee huru la kiswahili hapa nchini. Ndio gazeti pekee ambalo umiliki wake hauna maslahi na waandishi na wahariri wake ni mahiri, hawana njaa na hawapindishwi. Ndio maana huandika ukweli muda wote na wanapokosea hawasiti kurekebisha. Ndio maana ni gazeti linasomwa kwa wingi kuliko magazeti yote nchini. Hakuna gazeti linalofikia hata nusu ya mwananchi kwa kusomwa. Hivyo Mwananchi linaaminika na umma.

Najua kuna watu wana chuki binafsi na mwananchi kama gazeti na wahariri wa mwananchi kama binaadamu. Hayo wayamalize wenyewe huko walikochukiana.

Subirini video ndio tutajua habari ile imepikwa au ni ya kweli. Kwa tuliokuwepo uwanjani tunajua nani alisema nini.

Mheshimiwa Zito Kabwe wewe ni mwanga, nuru na tumaini la wengi lakini unabahati mbaya kuwa mara kwa mara umejikuta upo kwenye firing line/point and it looks like you are a soft target of many many enemies of your own make.

Watu wanaonekana wamekufahamu sijui kama wamekupatia kuwa wewe ni dhaifu sana na hasa ukiamua kukabiliana nao katika tofauti zenu. Na kwa kuwa wanaona wanakushinda na kila wakati wanakuchochea ugombane na watu unaodhani ni maadui zako hawa watu wataendelea kukutafuta na kukuchochochea ugombane na watu wengi kwa matukio ambayo unayaandaa mwenyewe. Kwa kuwatetea mwananchi visa hivi vinakurudia kuwa wewe ni sehemu ya yaliyoandikwa, mimi sinasababu ya kuamini haya na sitakaa niamini lakini mhariri makini angeona mambo mengi ni ya kilevi na hayakuwa na maana kuyaandika kama magazeti mengine yalivyofanya siyo kwamba watu wao hawakuwapo kwa hiyo wanaweza kuwa makini kama unavyowasifiwa lakini kwa hili umepotoka kuwapa alama ya ufaulu katika fani hii bila kuwa na mashaka yoyote.

Mimi sikutegemea kuwa ungetokeza katika jamii forum kujibizana katika na watu hawa katika jambo dogo hili naomba nikupe angalizo wiki iliyopita mchezaji maarufu wa chelsea Ashley Cole alifungua account ya twitter kilichomtokea baada ya kuanza kutwitt dunia inakifahamu, naona katika mabadilishano ya baadhi ya kejeli zinazotolewa humu ndani umepoteza passion na unaanza kujibizana ovyo kwa kutumia maneno ambayo si ya Rais mtarajiwa kwa mfno neno porojo. Nakusihi tena jihadhari usikubali kupata makovu ambayo baadaye yatakuwa yadi stiki ya kupima utu wako na uraisi, kauli uliyoitoa bungeni leo wachawi wako wanaona unautaka uraisi kwa udi na uvumba kauli ya Nyerere ya watu wanaoitafuta ikulu kwa namna hiyo itaweza kutumika vibaya juu yako.


Huna sababu ya kutuletea habari za video kwa watu ambao waliact under influence of alcohol achana na hii agenda it does not add value sana sana inapanua misunderstanding


NI MIMI SHABIKI WAKO
 
Ndugu wanajamvi naomba niseme kabisa kuwa wote waliyoyakataa maneno yao waliyoyatamka kule Kigoma pale Lake TANGANYIKA stadium ni wanafiki.Kwa kuwa mimi nilikuwepo pale uwanjani na ninavideo la tukio lote,Nimeanza kuupload japo ipo slow but ukweli utajulikana.Nassary ni mnafiki na akizeeka atakuwa mchawi kwa sababu anakataa maneno aliyeyasema mwenyewe mbele ya umati wa watu.Zitto,usipoweka video kwa kumlinda Nassary na wanafiki wenzake mimi nitaweka.Sasa sijui walikuwa wamelewa ile siku pale jukwaani!
 
I fail to understand why people always panic whenever Zitto Kabwe is associated with the presidency. Tatizo ni nini hasa? Zitto amesaliti vipi chama chake kwa kuutaka urais? Na kuna ubaya gani Zitto akigombea uRais au akiwa Rais? In my opinion more than any other politician Zitto has proved that he has the skills, capability,vision, knowledge and experience to lead this country. Yes he is outspoken and he will not hesitate to speak his mind. Through his character we have been able to understand and know him better than any other politician. Tunaelewa na kujua msimamo wake. After all he has done for this country, we instead choose to smear him with slander and call him all sorts of names...eti msaliti? Msaliti? Amemsaliti nani na kivipi? Nyinyi mnaomutia majina, what have you done for your country? Yaani with all the issues confronting this country, we choose instead to focus on who said what about Zitto and the presidency. Hivi tumekuwa watu wa aina gani? Yaani mna sakama mtu just because gazeti lime quote matamshi ya wabunge wenzake? Bro Zitto wewe endelea na mapambano!

It looks you know very little as far as politics is concerned. Wait and see!
 
Status
Not open for further replies.
Back
Top Bottom