Urais, Halima, Nassari na Kigoma

Urais, Halima, Nassari na Kigoma

Status
Not open for further replies.
Hivi Video ikiwekwa hapa itakuaje? Nitasikitika sana kuona mbunge yeyote kijna anafanya mambo waliyofanya wazee wetu zamani kuwaghilibu wenzake. Kuna hatari ya watu kupata aibu ya Mwaka.Na mimi safari nashabikia video iwekwe.
 
Wakati makamanda wakiwa busy kukijenga chama, hatujamuona Zitto akifanya hivo! Hii inanipa mashaka kama bado tuko nae huyu kamanda!pili, Zitto alihusika sana kukihujumu chama wakati wa uchaguzi mkuu na hii kupelekea chama kupoteza majimbo mengi kigoma!tatu, atueleze amepata wapi utajiri alionao wa kutembelea hammer na kujenga ghorofa la kifahari dodoma? Soon tutaweka wazi baadhi ya rushwa alizopewa Zitto kutoka mashirika ya Umma!
 
Kazi tunayo sana watz. Kupata kiongozi ambaye yupo yupo ladhi kufa kwajiri ya wananchi. Mimi kama kijana bado nina wasiwasi na hawa vijana wenzetu ambao wapo kwenye siasa kama wanania ya dhati kuleta mabadiliko au wanatumia mgongo kujinufaisha.
Je kunamtu anaweza simama kwamba ni msafi 100% kati ya hao wote wasemwao kila siku kwenye magazeti yetu? Wanatumia magazeti na redio mbalimbali kujitangaza na kutufanya sisi raia kutopata nn wanakitaka.

Kwani wanashindwa nn kupambana na matatizo tulio nayo leo hii, Madaktari, Walimu, Madini yetu yana chukuliwa bila manufaa yeyote, mbuga zetu ndo balaa kabisa halafu tunakaa na kusema mambo ya Uraisi kweli? Wanasema lisemwalo lipo nakama halipo basi laja.

Hivi tunafaida gani yakuwa na madini, gesi, mafuta (wanasema wanafanya uchunguzi wakati wanachukua na kupeleka nje), Hakuna uzalendo kabisa ktk nchi hii. Mimi nalia na wananchi wa vijijini ambao wanadanganya sana kwa maneno matamu wakati hakuna msaada wowote.

Ni kweli mkuu.Pole sana....
Politicians should be listeners. They should align their 'convictions' with the will of the people. Liars are worse than mass murderers.
 
[TABLE="width: 100%"]
[TR]
[TD] [/TD]
[TD] Nisihusishwe na Matamshi na Makanusho wa Wabunge walokuwa Kigoma

by zittokabwe[/TD]
[/TR]
[/TABLE]
Katika gazeti la Mwananchi la tarehe 23 Julai 2012, kulikuwa na habari yenye kusomeka 'Wabunge wamsafishia Zitto njia ya Urais 2015'. Habari hii imeleta mjadala mara baada ya kutoka na kusomwa. Mjadala umekuzwa zaidi baada ya Wabunge ndugu Halima Mdee na ndugu Joshua Nassari kukanusha maneno waliyonukuliwa kuyasema. Napenda kusema masuala yafuatayo.

Moja, Waheshimiwa Wabunge Halima Mdee, Joshua Nassari, Kangi Lugola, Esther Bulaya, Deo Filikunjombe, Raya Ibrahim, Amina Mwidau na David Kafulila walihudhuria tamasha la vijana wa Kigoma All Stars kwa kualikwa na Mratibu wa kundi hilo Mwasiti Almasi.

Wabunge wengine walialikwa lakini hawakutokea wakiwemo Joseph Mbilinyi, David Silinde, Amos Makala, Vicky Kamata na Peter Serukamba. Wabunge hawa hawakualikwa na mimi bali nilisaidia 'logistics' tu. Lengo la kushauriana na Vijana wa Kigoma All Stars kuwaalika wabunge kutoka vyama mbalimbali lilikuwa ni kuonyesha umoja na mshikamano wa nchi bila kujali vyama vya siasa.

Wabunge wote walioalikwa waliambiwa hii ni shughuli ya muziki na wala sikufanya mazungumzo nao yeyote ya awali au kuwaambia au kukubaliana nini cha kuzungumza au hapana. Tamasha lilikuwa la muziki na halikuhusika kabisa na siasa. Ni bahati mbaya sana kuwa kuna matamshi ya kisiasa yalitamkwa katika shughuli ile.

Waheshimiwa wote walipewa nafasi ya kusalimia na wote walizungumza. Wabunge waliozungumza kwa muda mrefu kidogo ni ndugu Halima Mdee, Joshua Nassari, Deo Filikunjombe na Kangi Lugola.

Hotuba za Wabunge wote zilirekodiwa kwenye video neno kwa neno na video hizo zitawekwa wazi kwenye blogu yangu kama sehemu ya documentary ya tamasha lile la kihistoria.

Pili, sikuhusika kwa namna yeyote ile na kuandikwa kwa habari hii iliyozusha mjadala. Wala sikujua kama habari hii ingeandikwa maana katika ziara ile sikuita mwandishi hata mmoja maana nilitaka liwe tukio la Kigoma tu. Mimi kama mlezi wa KigomaAllStars na vijana wenyewe tulijikita katika 'shukrani Kigoma' kwa watu wa Kigoma.

Kama mwandishi kaandika ambayo wabunge hawa hawakuyasema basi itaonekana kwenye videos hizo. Wabunge wenyewe wanajua kwenye nafsi zao nini walisema Kigoma na kipi kiliwasukuma kusema walioyasema Kigoma.
Nisingependa kuhusishwa kwa njia yeyote ile na matamshi yao, habari iliyowanukuu na hata makanusho yao. Maana mwisho wa siku ukweli ndio utasimama.

Suala la Urais lisitupotezee muda kwani kuna mambo mengi sana ya kujadili kuhusu nchi yetu. Taharuki ambazo watu wanazipata masuala ya urais yanapotajwa zinashangaza sana.

Chama changu bado hakijatangaza rasmi mchakato wa kupata mgombea Urais. Hivi sasa chama hakina mgombea Urais mpaka hapo mchakato utakapotangazwa ambapo wanachama wataruhusiwa kuomba kupeperusha bendera ya chama. Mwanachama wa chama chetu atakaye kubalika na jamii na wajumbe wa mkutano wa uteuzi ndiye atakuwa mgombea wetu. Kwa sasa hayupo na hivyo tusipoteze muda kujadili jambo hili.

Mzee Thabiti Kombo alituachia usia tunapokuwa tunazungumza. Alisema 'weka akiba' sio akiba ya fedha, bali ya akiba ya maneno. Tuweke akiba ya maneno. Tusimalize yote.

zittokabwe | July 25, 2012 at 9:07 AM | Categories: Uncategorized | URL: Nisihusishwe na Matamshi na Makanusho wa Wabunge walokuwa Kigoma « Zitto na Demokrasia
 
Zitto unajichanganya wewe mwenyewe. Amua kama wewe ni moto au baridi . Usiwe vuguvugu na mnafiki. Binafsi nakuona una uwezo wa kawaida tu. You are not a presidential material period. Na kwa wananchi nashangaa sana katika CHADEMA yaani Zito hata hamfikii hata kwa 50% Rissu wala 70% ya Mnyika. Asubiri aone kipindi cha uchaguzi atatemwa na sehemu zote si wa CCM wala wa CHADEMA maana hiyo ndiyo faida na hasara ya ukahaba wa kisiasa!
 
Yaani hata sasa Zitto ameonekana kuongea Bungeni kwa unafiki sana. Eti anamtaja January kuonyesha kuwa ni mtetezi wa Vijana. Zitto ni mbaya sana na ni mchonganishi. Mtu anayetaka kupata cheo kwa nana yeyote hata kuuza chama chake ni wa hatari sana. Hafai huyi jamaa. Kuna wengi sana wenye uwezo zaidi yake. Ebu mlinganishe hata na Rissu muone ambavyo huyu msanii asivyofua dafu.

Swali la kumuuliza ni hili. Kwa nini kila siku uwe wewe Zitto wa kulaumiwa katika matukio ya kuizunguka CHADEMA? Mbona hatujasikia haya kwa wengine akina Mbowe, Rissu, Mdee na Mnyika
 
Katika wanasiasa ninao waheshimu na kuweka matumaini makubwa ya mstakabali mzima wa Tanzania tunayoitaka ni wewe, Zitto Zuberi Kabwe..

Nakuomba upuuzie upumbavu na upuuzi wa hawa magamba wanaopandikiza watu kwenye Media maana nia na dhamira yao ni wewe ukasirike, upanic na uanze kupayuka na kuongelea mikakati na mipango yako ili wajue namna ya kukuangusha...

ZITTO WEWE NI ZAIDI YA MWANASIASA, wewe ni hazina ya chama na Taifa kwa ujumla..."Unapobishana na Mlevi na wewe utaonekana umelewa" SONGA MBELE ZITTO.
 
unajua mh. watu tumetrace nyuma huko yaani habari zako kwenye gazeti la mwananchi zinaandikwa na mwandishi mmoja (Ramadhani Semtawa)..na zote huwa zinazua mgogoro mkubwa sana kwenye jamii....leka tutigite imefanyika karibu siku 6 zimepita alikuwa wapi kuandika? na je ni kweli umemuweka mfukoni huyu mwandishi?...

Hapo kuna maswali mengi kushinda majibu, ITAJULIKANA TU!
 
Hivi kwa nini Mh. Zitto umeona ni busara kutumia mdua wa kujadili bajeti ya wizara ya sayansi na teknolojia kuchomekea masuala ya tamasha la Kigoma na suala la wewe kugombea urais?
 
Zitto anaendesha farasi wawili subiri wafike njia panda TUSHUHUDIE UPASUKAJI WA MSAMBA WAKE HADHARANI!
 
kasema bungeni.Yupo detemined kuwa anautaka urais.Nitakuwa na furaha kama uongozi wa CDM nao wanaridhia hilo.Ila wenye nguvu CDM ni wanachama kwani hao ndio hupigania kura na kuzilinda kwa nguvu sana.

Problem ninayoiona ni kwamba kama katiba itakuwa tayari CDM wakishinda halafu ccm wakaamua tangaza ntu wao na mgombea wa CDM akiwa si makini anaweza kataa kupeleka suala mahakamani.Sijui katika itaweka vipi hii sheria ya kupewa pinga matokeo mahakamani.Kama itakuwa ni mgombea husika na si chama.Labda determination Ya zitto iwe kubwa zaidi akiona mlango wa ikulu na hivyo kupambana kwa maslahi ya pamoja chama na yeye binafsi huku kama kawa pakiwa na maslahi kiduchu kwa wananchi.

Bado nasema kuna wengi katika cdm ambao bado ni mamluki,ila nawahurumia kwa vile bado uhakika wa kukuta malipo yao katika CCM yanaweza yasiwepo.Mazingira si predictable ingawa unpredictability inalala katika dimensions za kuanguka kwa CCM
 
Zitto ana kiburi na anajua sababu ya kiburi hicho! Hashauriki,hasikilizi na hata watu wa Kigoma wamefanywa majuha yaani yeye ndio anayejua nini awafanyie wana Kigoma regardless maoni binafsi ya wananchi!

Yaani huyu ndio dikteta wa Kigoma akisaidiwa na Dola kumpamba aonekane bora!
 
Ungemwangalia zitto usoni wakati anaongea bungeni muda mfupi uliopita, unaweza kusoma kabisa ramani ya unafiki yenye makao makuu ya roho mtakakitu!

Mbowe kwa nini mnamchezea huyu mtu wakati ni hatari sana?
 
Penye wengi pana mengi pia lakini pia naamini hakuna uwongo uliyo uwongo mtupu kwasababu uwongo unatokana na ukweli ila unapindishwa kidogo kwa maslahi binafsi.Naamini Zitto ni mtu hivyo atajirekebisha ili aendano na matarajio wa pro-chadema na mategemeo ya watanzania kwa ujumla.
 
Katika wanasiasa ninao waheshimu na kuweka matumaini makubwa ya mstakabali mzima wa Tanzania tunayoitaka ni wewe, Zitto Zuberi Kabwe..

Nakuomba upuuzie upumbavu na upuuzi wa hawa magamba wanaopandikiza watu kwenye Media maana nia na dhamira yao ni wewe ukasirike, upanic na uanze kupayuka na kuongelea mikakati na mipango yako ili wajue namna ya kukuangusha...

ZITTO WEWE NI ZAIDI YA MWANASIASA, wewe ni hazina ya chama na Taifa kwa ujumla..."Unapobishana na Mlevi na wewe utaonekana umelewa" SONGA MBELE ZITTO.

mkuu nadhani hujamwelewa zitto, yeye hapingi kilichoandikwa gazetini ila anataka kudhibitisha kilichoandikwa kwa kuleta video, hivyo kifupi yupo pamoja na mwandishi. Ndio maana wadau wanasubiri video ili waone nani mwongo kati ya Zitto na gazeti v/s Nassari,mdee,Filikunjom na Estar kwa upande mwingine.!
 
Zitto anakimbilia uraisi. Je ataweza? Jamaa anajifanya anajua wakati hajui kitu. Mdomo tu mkubwa kuongea.
 
Mh Zitto,

Kwanza napenda kukupa pole sana kwa haya yote mimi sijaona jambo lolote baya ulilotenda maana tuliokuwepo tulisikia na kuona nini kilifanyika pale uwanjani.Tatizo lililopo ni wahariri wetu na headlines zao za front page .Vilevile kuna watu wanaodhani kuwa chaguo lao ndio chaguo la wote. ACTIONS SPEAK LOUDER THAN WORDS.Kuna watu hawasemi kuwa wanataka urais ila matendo yao yanadhihirisha hivyo. Kwa jinsi ninavyokuelewa you've always kept your word (I stand to be corrected) na kama jambo halikuhusu umekua ukiendelea na shughuli zako bila kumbughudhi mtu(watu).

Huu Urais muda bado na kama ulivyosema watu wajadili mustakabali wa Taifa hili kwa sasa maana ndio jambo linalotekelezeka leo huu urais mpaka 2015 ni safari ndefu .Ni bora watu wangeheshimu maelezo yako ndio waseme mengine. JIPE MOYO HAYA NI MAPITO NA HUWEZI PENDWA NA KILA MTU.
 
Status
Not open for further replies.
Back
Top Bottom