Urais, Halima, Nassari na Kigoma

Urais, Halima, Nassari na Kigoma

Status
Not open for further replies.
Kwa vile Zitto hupita hapa jamvini, ajitokeze ajibu tuhuma hizi. Hata hivyo, Zitto kisiasa bado ni mteke ingawa kuna watu wanampigia ndogo ndogo ateuliwe kugombea urais. Kimsingi, CDM haijatangaza nani atakayebeba bendera yake kwenye mbio za urais zaidi ya kuweka mazingira mazuri. Zitto kama yupo nyuma ya hiki kinachovumishwa kuwa anafaa ajue anajimaliza na kudhoofisha chama chake. Kwanini asingoje uamuzi wa chama? Pia angejikita kwenye kujisafisha kuhusiana na kashfa yake ya kushirikiana na Usalama wa Taifa kuhujumu demokrasia. Ziliwahi kutolewa tuhuma hizi na Zitto hakujitokeza kuzijibu kiasi cha kufanya watu waamini kuwa zilikuwa za kweli na aliogopa kuumbuliwa zaidi.
 
Wewe @MkeYa Muzungu
Kama wewe ni mwanahabari wa kweli hebu Weka hapa hiyo habari dhidi ya Mbowe ambayo unadai ilitungwa na Zitto.
Binafsi nakuwa mzito sana kuamini kuwa Zitto ninjuaye mimi anaweza kuwa na mipango ya siri ya kiharamia kama mlivyoeleza. Nijuavyo mimi mbio za urais huanza pale unapopendekezwa na idadi kubwa ya watu toka maeneo mbalimbali ya nchi, na si mkoa utokao tu.
Finally i wish iw wasnt true!
 
Zito ana uwezo wa kujenga hoja vizuri sana. tatizo ni hiyo kasoro ya superiority complex aliyo nayo. He believes he is knowledgeable than anybody. katika mambo haya ya vyama team work is very important for a success. Apunguze power mongering. Sawa kila mwanadamu ana hulka ya kutaka madaraka, lakini not at the detriment of the many. kama hakuna hatua za makusudi ataiua CDM, na CCM watampokea kwa kumbeza!!

To sum up your good analysis, Zitto is a brilliant individualist.
 
Wewe Mkeya Muzungu
Kama wewe ni mwanahabari wa kweli hebu Weka hapa hiyo habari dhidi ya Mbowe ambayo unadai ilitungwa na Zitto.
Binafsi nakuwa mzito sana kuamini kuwa Zitto ninjuaye mimi anaweza kuwa na mipango ya siri ya kiharamia kama mlivyoeleza. Nijuavyo mimi mbio za urais huanza pale unapopendekezwa na idadi kubwa ya watu toka maeneo mbalimbali ya nchi, na si mkoa utokao tu.
Finally i wish iw wasnt true!
PakaJimmy hakuna mtu mnafiki ndani ya CDM kama Zitto......ni mpenda sifa pia ! Binafsi kweli nakerwa sana na hizi habari za Zitto kila kukicha manake kweli ni kupoteza muda kwa mtu ambae tulidhani kuwa ni mtetezi wa wanyonge....ifike mahali tumsusie na hizi habari zake za kijinga kila siku ! Asituvurugie chama bana kama vipi aondoke aone kama CDM itapungukiwa na chochote !
 
Last edited by a moderator:
Dogo anatumiwa huyu. Na anafahamu kama hawezi pata. Na kama angekuwa mwadilifu angekuwa keshajitokeza na kusema ukweli kama yeye hatogombea. Wanamdanganya sana na anapoteza muda wake.
 
Wewe ndio mnafiki,kama umechoka na stori za zitto mbona umeanzisha topic nyingine ya zitto?si ungechangia katika hizo zilizo janazana humu JF.
 
Kwa sasa huyu jamaa ni kete ya kisiasa ya magamba, kwamba wafanye kila wawezalo ajitoe au afukuzwe ili ile kuwaaminisha waislam kuwa cdm ni chama cha kidini na ukanda. Akili kichwani
 
Hakunaga CDM kama Zitto...Nngependa 2015 ugombee urais ka itawezekana, sio kuja kuongozwa na vibabu...
 
Shida ya zitto analewa sana sifa nilwahi kuongea kwa muda mref wakati wa uchaguzi mdogo wa udiwan kirumba hapa mwanza vijana walikua wakimshabikia agombee urais atapata urais kwan anakibalika na umati ilikua mkubwa sana alionekana kuhamanika na kuvimba bichwa na saikolojia yake kwa kumtazama ilisadifu kilichomo ndani yake,zitto ajipange atapotea wakongwe wanazingatia itifaki hamuoni dr.slaa
 
Megwa

QUOTE=majebere;4311013]Wewe ndio mnafiki,kama umechoka na stori za zitto mbona umeanzisha topic nyingine ya zitto?si ungechangia katika hizo zilizo janazana humu JF.[/QUOTE]
 
Nadhani anahitaji director wa movie kama Kova lazima watapata award 2015.
 
Record kubwa sana inaonyesha kuwa wanasiasa wanaokuwa na ndoto za urais kwa muda mrefu hushindwa kufanya majukumu yao vizuri wanapopata nafasi za kuwa rais na mara nyingi huvuruga sana nchi zao. Sababu mojawapo kubwa ya kushindwa huko ni kutokana na kuwa mara nyingi huwa hawana ajenda ya nchi bali ajenda yao biansfi ya kuwa rais tu. Sababu nyingine ni kuwa njia wanazotumia kupata uraisi huwafanya wakose washauri wazuri kwa vile huwa wameshavurugana na watu ambao wangewashauri vizuri.

Richard Nixon (aligombea kwa zaidi ya miaka kumi), Kikwete (alijiandaa kwa zaidi ya miaka kumi+), Bush (alijiandaa kwa miaka minane tang baba yake alivyoshindwa na alitumia pesa nyingi sana kuupata).

Mara zote marais wanaohappen kuwa na ufanisi mkubwa ni wale walioombwa na mashabiki wao kuwa wagombee, na wakapewa support kubwa sana na vyama vyao; wengine huchaguliwa kwa bahati bahati tu kwa vile walikuwa katika position fulani wakiwa hawategemei kupata nafasi hiyo ya urais; utaratibu mzima wa wao kujiandaa kugombea huwa ni muda mfupi sana. Mifano ipo ya kutosha kwa watu wa aina hiyo

Kuanzia mwaka jana (au kabla ya hapo- wakati ulipotuarifu kuwa Kikwete alipendekeza wewe ndiwe uwe rais ajaye), Mheshimiwa Zito umekuwa vocal sana katika kutangaza nia yako ya kugombea urais na mara kadhaa umekwaruzana na wenzako ndani ya chama chako kwa sababu hiyo tu. Kadri siku zinavyokwenda umekuwa unaongeza kasi hiyo ukiwa labda na lengo la ku-preempt watu wengine ndani ya chama chako wasigombee nafasi hiyo. Inawezekana mara zote hizo ni magazeti yanakunukuu vibaya ila kwa vyovyote iwapo umekuwa active kutanganza nia yako ya kugombea urais, basi utaratibu unaotumia, hauna tofauti sana na utaratibu uliotumiwa na Kikwete wakati akitaka kugombea uraisi, na leo hii sote tunajua kuwa Kashindwa kazi hiyo. Ingawa leo hii tunamwona Kikwete ni dhaifu, lakini kila mtu anajua jinsi alivyokuwa thabiti kama wewe ulivyo leo wakati yeye akiwa waziri wa fedha ambapo alibana kabisa mismaha ya kodi na kuwabana sana wafanyabishara waliokuwa wakikwepa kodi. Kwa hali hiyo, kuwa makini na hatua unazofanya sasa hivi kwani zinaweza zisiwe productive kwako binafsi, na huenda kwa chama chako pia. Usitake swala la Zito na Urais ndiyo iwe headline kila siku, kwa sababu ikitokea kuwa hutateuliwa na chama chako kwa njia halali kabisa, basi utakuwa umetia doa kwa chama chako, na kuongeza mwanya wa kushindwa na CCM tena!


Kiongozi mzuri ngazi ya Urais siyo tu yule ambaye yuko vocal bungeni kupambana na serikali, bali ni yule aliyekuwa na busara za kutosha kuangalia mambo kwa mapana kwa faida ya jamii yake. Unapokuwa unafanya mambo ambayo ni wazi yanaishiwa kuwagawa wanachama wa chama chako kwa ajili ya lengo lako la uraisi ni dalili ya kupungukiwa busara hiyo.

Nakuunga mkono.
Katika mada fulani huko nyuma iliyozungumzia vijana wanaofaa kuwa marais Zitto ndio anafaa, mimi nilijaribu kwa nguvu zote kuwa kinyume chake kabisa. Kwa mtazamo wangu zitto anafaa kwa sasa kuwa waziri lakini si kuwa Rais kwani anachofanya sasa hakiakisi uwazi na mshikamano katika chama ila ameshika njia yake binafsi kwa masilahi binafsi.

Zaidi sana haonyeshi ukomavu wa akili yake kwa sababu hutoa matamko ambayo hayaonyeshi hekima na busara itakiwayo kwa kiongozi, kwani kuna kila dalili za udhaifu kama viongozi dhaifu wengine tunaowashuhudia kwa kujionyesha kimbelembele na kukimbia matatizo au kutoyatatua.

Kikwete alifanya kila jitihada kumtolea nje Kighoma malima ili aonekane anafaa yeye, na alikuwa mchongezi sana kama alivyomchongea kiongozi wake wa jeshi kwa Nyerere kwamba ni fisadi kwa kwa kuwauzia maziwa wanajeshi wakati alikuwa ni mfano wa siasa za kujitegemea.

Ogopa ye yote anayeitafuta nafasi ya urais kwa nguvu, ni ukoma ua donda ndugu. Hatuna haja ya kwenda mbali kwani huko huko Kigoma kulitoka kauli kama hiyo ambayo ilitoka kinywani mwa Rais wa Sasa Kikwete kwamba rais ajaye awe kijana kama yeye ikiwa ni ishara ya kumpigia kampeni lakini kwa mgongo wa nyuma kuna kitu kilichofichika.

Kikwete alitafuta kwa nguvu zote, na awamu iliyopita baada ya Mkapa kumwangusha alimalizia hasira kwa hayati Laurance Gama kwamba ndiye aliyemtifulia kwa vile Gama alipokuwa Katibu Mkuu wa chama aliegemea upande wa Msuya. Alipoukwaa urais, Laurance Gama alienguliwa nafasi hata ya ukuu wa mkoa na kuishia kuishi kama mstaafu asiyelitumikia taifa lake kwa nguvu katika maisha yake hadi kifo kilipomchukua, na kumbuka baadhi ya viwanja vya mipira walivyojimilikisha CCM vilijengwa na Gama kama Majimaji Songea na Ali Hassan Mwinyi Tabora, Kikwete hakuona hilo ila Gama kuwa kinyume chake ndiyo ilikuwa deal na kumbe Gama aliona mbali.

Kikwete baada ya kuupata urais alioutafuta kwa nguvu zote yanayojilia tunayaona katika nchi yetu.

Zitto anajitokeza kifua mbele kwenye shughuli za chama pale ambapo hakuna misukosuko, lakini sehemu zote ambazo huwa na misukosuko amekwepa kabisa, huo sio ushupavu na si ukomavu, ni kasoro kubwa katika uongozi kwamba si mtu wa kujituma na kuwa tayari kwa lo lote kwa ajili ya nchi yetu na watu wake. Zitto ni mwoga. Na ujana nao ni kitu hatari kukabidhiwa ofisi kubwa nchini.

Kumchagua Zito kuwa Rais kwa tabia alizoonyesha na kutoonyesha ushirikiano na wabunge wenzake wa chama chake kama ilivyotokea sasa kuwatolea nje Halima Mdee na yule dogo wa Arusha nasema ni Zitto ni sawa na kumweka teenage kwenye nafasi hii nyeti ya kulitumikia taifa na watu wake. Zitto abaki na nafasi za utumishi wa kawaida labda baadaye ataonyesha ukomavu na kuweka kando ubinafsi ambao umejitokeza kwa kasi zaidi kuliko zamani.
 
Shida ya zitto analewa sana sifa nilwahi kuongea kwa muda mref wakati wa uchaguzi mdogo wa udiwan kirumba hapa mwanza vijana walikua wakimshabikia agombee urais atapata urais kwan anakibalika na umati ilikua mkubwa sana alionekana kuhamanika na kuvimba bichwa na saikolojia yake kwa kumtazama ilisadifu kilichomo ndani yake,zitto ajipange atapotea wakongwe wanazingatia itifaki hamuoni dr.slaa

Vijana wanamshabikia hivyo kwa vila wanajua ana njaa ya urais.
 
wakuu binafsi nimechoka kabisa kusikia au kujadili utoto wake na uroho wa madaraka! Personal sioni potential aliyonayo zito mpaka tumzungumzie na kumjadili na kupoteza wakati wetu.

Yafuatayo ni kweli kuhusu zito:

- anajiamini na kujithaminisha kuliko ukweli.
- ni mroho wa madaraka na mbinafsi.
- hana nia njema na taifa hili.
- hana lolote, like any other looser.

Kama anabisha aasi chama aone atakavyoporomoka, huyu anatengeneza kaburi lake la kisiasa.

Zittoh wewe ni mnafiki, haufai.


the good thing about freedom of speech
is that you are free to lie! Of course up to a certain extent;
...like this extent!
 
unalolidai si sahihi sana kwani kabwe ni mzuri sana wa kujenga hoja na kusimamia anachokiona kuwa kiko sahihi...Hii tabia amekua nayo toka akiwa pale UDSM na sidhani kama ni unafiki kuwa na different opinion against the majority......
 
Wakuu binafsi nimechoka kabisa kusikia Au kujadili utoto wake na uroho Wa madaraka! Personal Sioni potential aliyonayo zito mpaka tumzungumzie na kumjadili na kupoteza wakati wetu.

Yafuatayo Ni kweli kuhusu zito:

- Anajiamini na kujithaminisha kuliko ukweli.
- Ni Mroho Wa madaraka na mbinafsi.
- Hana nia Njema na taifa hili.
- Hana lolote, like any other looser.

Kama anabisha aasi Chama aone atakavyoporomoka, Huyu anatengeneza kaburi lake la kisiasa.

Zittoh Wewe Ni mnafiki, haufai.

Hahaha Silaa naona umekuja na ID nyingine kaazi kweli kweli ZZK anakunyima usingizi eeeee na yeye ana haki ya kutangaza nia?
 
Ndo maana Nkamia kawasema mnatukana watu hovyo sasa uzi kama huu si ndo unatushushia hadhi yetu wanaJF jamani
 
Status
Not open for further replies.
Back
Top Bottom