Upishi wa ovyo ovyo umefanya nimuache

Upishi wa ovyo ovyo umefanya nimuache

Toka nimuoe hajawahi kupatia kwenye mapishi, kila anachopika lazima kiwe na mapungufu; kama sio chumvi nyingi, basi chakula kitakuwa kibichi!
Lakini kweke yeye chakula kukosa chumvi ni kawaida, chumvi kuzidi kiasi ni kawaida, kuwa kibichi kawaida vilevile, chakula kukosa ladha ndo usiseme!
Kuelekezwa pia hataki, maana anakuwa anaona kama anadharauliwa!

Nimevumilia vya kutosha imefika mahali nimeona isiwe tabu.
Kwa sababu haiwezekani kusema una mke harafu kupika anazidiwa na Mama Ntilie!!!

Wanawake wana paswa kujua kuwa, hatuowi kwa sababu tu ya kurahisisha Sex-Intercourse, kuna vitu vingi sana kutia ndani mapishi mazuri nk.
Mkuu au anapika mboga mboga za majani kama anachemsha dawa za kienyeji😂😂
 
Hakuna mapenzi hapa. Nampa pole huyo dada
 
Hakuna kitu kinachouma kama mtu akosee jambo halafu ukimuelekeza anaona kama unamfokea, unamtoa kasoro au unamnyanyasa.

Mtoa mada hajamuacha mke wake kwasababu hajui kupika, kamuacha kwasababu hataki kukosolewa, akikosolewa anakua mkali, nyumba inakua chungu kwa namna hii. Nimeshawahi kuwa na mwanamke wa hivyo. Ni changamoto.

Sent from my SM-G570F using JamiiForums mobile app
 
Kuoa mwanamke asiyejua kupika ni hasara tupu.

Siwezi kufanya huo ujinga.
Serious?
Dunia hii ilivyo kasi bado kigezo cha mke ni kupika! Sasa naona umuhimu wa kipindi cha Polepole.
 
Toka nimuoe hajawahi kupatia kwenye mapishi, kila anachopika lazima kiwe na mapungufu; kama sio chumvi nyingi, basi chakula kitakuwa kibichi!
Lakini kweke yeye chakula kukosa chumvi ni kawaida, chumvi kuzidi kiasi ni kawaida, kuwa kibichi kawaida vilevile, chakula kukosa ladha ndo usiseme!
Kuelekezwa pia hataki, maana anakuwa anaona kama anadharauliwa!

Nimevumilia vya kutosha imefika mahali nimeona isiwe tabu.
Kwa sababu haiwezekani kusema una mke harafu kupika anazidiwa na Mama Ntilie!!!

Wanawake wana paswa kujua kuwa, hatuowi kwa sababu tu ya kurahisisha Sex-Intercourse, kuna vitu vingi sana kutia ndani mapishi mazuri nk.

Wengine wanalalamika sex, huyu analalamika chakula, si umvumilie tu huku ukiendelea kula nje?

Una lalama chakula huku una Acha 3000 asubuhi, chakula kitakuwaje na ladha? Wanaume wengine tuna shida sana.

Hujui thaman ya mwanamke? Ungejua usingekuja kututia aibu na vitu vya kijinga, kutokujua kupika can be fixed kirahisi tu.
 
Hakuna kitu kinachouma kama mtu akosee jambo halafu ukimuelekeza anaona kama unamfokea, unamtoa kasoro au unamnyanyasa.

Mtoa mada hajamuacha mke wake kwasababu hajui kupika, kamuacha kwasababu hataki kukosolewa, akikosolewa anakua mkali, nyumba inakua chungu kwa namna hii. Nimeshawahi kuwa na mwanamke wa hivyo. Ni changamoto.

Sent from my SM-G570F using JamiiForums mobile app
Safi sana; kwenye maelezo yangu wewe umenielewa vizuri mkuu,, [emoji122]
 
Hukumpenda , full stop.
Tofauti na upendo huo niliouonyesha tangu nimemuoa, kumvumilia wakati wote kutokana na mapungufu yake hayo, bado nimefanya jitihada za kutafuta suluhisho la mapungufu yake lakini hataki; unadhani ningeonyesha upendo gani zaidi ya huo mkuu!?
 
Wengine wanalalamika sex, huyu analalamika chakula, si umvumilie tu huku ukiendelea kula nje?

Una lalama chakula huku una Acha 3000 asubuhi, chakula kitakuwaje na ladha? Wanaume wengine tuna shida sana.

Hujui thaman ya mwanamke? Ungejua usingekuja kututia aibu na vitu vya kijinga, kutokujua kupika can be fixed kirahisi tu.
Yaelekea wewe bado kuna mambo hujayaelewa; acha nikupe mda, utaelewa baadaye mkuu
 
Tofauti na upendo huo niliouonyesha tangu nimemuoa, kumvumilia wakati wote kutokana na mapungufu yake hayo, bado nimefanya jitihada za kutafuta suluhisho la mapungufu yake lakini hataki; unadhani ningeonyesha upendo gani zaidi ya huo mkuu!?
Mletee Hg anayejua kupika.
 
Yaelekea wewe bado kuna mambo hujayaelewa; acha nikupe mda, utaelewa baadaye mkuu

Nina ndoa ya miaka 15, wakwangu alikuwa hajui kupika Kabisa, na wewe una matatizo, unaachaje kujua kuwa mwanamke hajui kupika mpaka unamwoa? Ukienda kwao mara 2 tu utajua kama ni mpishi au siyo! Au mlikutana Bar ukamwamisha kwako
 
Comon mistake; lakini tayari nilionyesha nia ya kutaka kumsaidia ajue lakini yeye hakuta! Ningefanya vipi unadhani kiongozi!?
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom