Upinzani bila kubadili siasa mtapata hasara kubwa Kwa Samia..

The Boss

JF-Expert Member
Aug 18, 2009
42,460
2,000
Hakuna kitu kinaamua siasa kama 'wakati'..
Wanasiasa wazuri ni wale wanaojua nyakati zinavyobadilika na kwenda na wakati uliopo ...

Watanzania walikuwa wamechoshwa mno na siasa za Magufuli...na uongozi wake kiujumla..
Kubanwa Uhuru wa kuongea
Kufokewa na kukaripiwa
Kutoa matamko Kwa ukali..
Kuzungumza Peke yake..
Kutokukosolewa ..
Kukosekana Kwa mijadala na majadiliano..
Na mengi yaliyoenda na hayo..

Ujio wa Samia umebadili siasa Kwa ujumla..
Samia hafoki anaongea Kwa upole na kushawishi ..
Anazungumzia mazungumzo na mijadala..
Hazuii kukosolewa badala yake anakaribisha kukosolewa Kwa serikali yake..

Kikubwa zaidi ni Mwanamke ..
Watu wanamtazama Kwa 'kumhurumia'..
Na kumpa 'all benefits of the doubts'..
Na kuelewa kuwa anapambana na mfumo dume...
Watu wengi wanaju hii nchi ngumu na wanajua Samia atahangaika kuweza kumudu ...still wanafarijika na 'kurudi Kwa Uhuru wa kuongea na kukosoa'..

Sasa kama wapinzani wanafikiri siasa za kumshambulia Rais na serikali yake zinalipa bado kama enzi za JK watakuwa wanakosea sana....
Sana Sana wataonekana 'hawana adabu'
Na wanajaribu 'kumuonea' 'Rais Mwanamke' baada ya 'kidume ' JPM
'kuwakomesha hadi wakaufyata'..

Siasa za kipindi hiki zinahitaji ubingwa wa hoja kwenye mijadala ya kistaarabu..bila
Kuwa 'boa' wananchi ambao walishachoshwa na Magufuli Sana Sana wanataka 'mzunguko' wa hela urudi kama ule wa JK....

Kuleta siasa za ulalamishi..
Siasa za uwana harakati.
Na siasa za Ku target watu na kuwashambulia bila kujua ..'role halisi' ya hao watu ni siasa ambazo zinakuwa 'outdated ' so fast...

Watu wanampenda Samia sio Kwa sababu ni kiongozi bora.. wanampenda Kwa sababu wanaona 'nafuu inakuja'
Upinzani ukicheza siasa za kuleta 'distraction'wakati watu wanasubiri nafuu ije ..hasira za wananchi zinaweza washukia wao.....

Siasa inaendana na nyakati.. wapinzani wanasoma nyakati??
 
Ahmad Abdurahman

JF-Expert Member
Mar 5, 2016
1,693
2,000
Jamaa umeandika vema. Yyte atakaeanza kumkosoa mama watu watamuona ana nongwa na ni muonevu na watahoji kwa nn aliufyata kwa mbabe jiwe? Mfano ni yule dada kule tweeter ambae watu walimbatiza jina la Ferain baada ya kumkosoa mama huku kwa jiwe akiwa ameufyata na vijitivii vyake vya mkononi kupigwa ban.

Wapinzani this time watakua ni loosers. Ishara nyingne niionayo ni bunge. Wabunge washasoma alama za nyakati na sasa wamejitwisha kazi ya upinzani kukosoa serikali na mama kaahidi hilo. So upinzani hautakua na hoja tena maana kila kitu kinafanyika. Mfano ji akina GWAJIMA, NAPE, GAMBO, MAKAMBA MUHONGO N.K
 
Vessel

JF-Expert Member
Aug 29, 2018
2,552
2,000
Je
Hakuna kitu kinaamua siasa kama 'wakati'..
Wanasiasa wazuri ni wale wanaojua nyakati zinavyobadilika na kwenda na wakati uliopo ...

Watanzania walikuwa wamechoshwa mno na siasa za Magufuli...na uongozi wake kiujumla..
Kubanwa Uhuru wa kuongea
Kufokewa na kukaripiwa
Kutoa matamko Kwa ukali..
Kuzungumza Peke yake..
Kutokukosolewa ..
Kukosekana Kwa mijadala na majadiliano..
Na mengi yaliyoenda na hayo..

Ujio wa Samia umebadili siasa Kwa ujumla..
Samia hafoki anaongea Kwa upole na kushawishi ..
Anazungumzia mazungumzo na mijadala..
Hazuii kukosolewa badala yake anakaribisha kukosolewa Kwa serikali yake..

Kikubwa zaidi ni Mwanamke ..
Watu wanamtazama Kwa 'kumhurumia'..
Na kumpa 'all benefits of the doubts'..
Na kuelewa kuwa anapambana na mfumo dume...
Watu wengi wanaju hii nchi ngumu na wanajua Samia atahangaika kuweza kumudu ...still wanafarijika na 'kurudi Kwa Uhuru wa kuongea na kukosoa'..

Sasa kama wapinzani wanafikiri siasa za kumshambulia Rais na serikali yake zinalipa bado kama enzi za JK watakuwa wanakosea sana....
Sana Sana wataonekana 'hawana adabu'
Na wanajaribu 'kumuonea' 'Rais Mwanamke' baada ya 'kidume ' JPM
'kuwakomesha hadi wakaufyata'..

Siasa za kipindi hiki zinahitaji ubingwa wa hoja kwenye mijadala ya kistaarabu..bila
Kuwa 'boa' wananchi ambao walishachoshwa na Magufuli Sana Sana wanataka 'mzunguko' wa hela urudi kama ule wa JK....

Kuleta siasa za ulalamishi..
Siasa za uwana harakati.
Na siasa za Ku target watu na kuwashambulia bila kujua ..'role halisi' ya hao watu ni siasa ambazo zinakuwa 'outdated ' so fast...

Watu wanampenda Samia sio Kwa sababu ni kiongozi bora.. wanampenda Kwa sababu wanaona 'nafuu inakuja'
Upinzani ukicheza siasa za kuleta 'distraction'wakati watu wanasubiri nafuu ije ..hasira za wananchi zinaweza washukia wao.....

Siasa inaendana na nyakati.. wapinzani wanasoma nyakati??
Je wakijani nao wameweza kusoma nyakati , mbona wengi wao bado wanalazimisha pambio zile zile, na mazoea yale yale, hata ya kushindwa kufwata sheria, kanuni na hats sheria mama. aka katiba.
 
Ahmad Abdurahman

JF-Expert Member
Mar 5, 2016
1,693
2,000
Je
Je wakijani nao wameweza kusoma nyakati , mbona wengi wao bado wanalazimisha pambio zile zile, na mazoea yale yale, hata ya kushindwa kufwata sheria, kanuni na hats sheria mama. aka katiba.
Huwaoni akina Nape, Gwajima na Gambo wameshabdili gear?
 
denooJ

JF-Expert Member
Mar 31, 2020
4,870
2,000
Chama kinachojiita "chama dola" kina hoja gani mpaka wapinzani wapate shida kushindana nacho?

"Mimi ni Rais mwenye jinsia ya kike" sounds confident, nakushangaa mleta mada unamdharau, wanawake siku zote wanapigania haki sawa, kwanini wewe unawashusha?

Samia atapingwa tu, kama alivyokuwa akipingwa Magufuli, na Kikwete, na bahati nzuri Mbowe ameshaonesha hiyo dalili, huyo mama Katiba Mpya imeshamshinda bado unataka abembelezwe!.

Huwezi kumlazimisha mtu abadili "approach" ya siasa zake kwa kisingizio chepesi "wanamuonea mama", ikulu halei watoto, anaongoza taifa linalofuata mfumo wa vyama vingi.

Akishindwa kuvumilia hayo akaanza kuwaweka ndani hatakuwa na tofauti na mtangulizi wake, kama kweli amekomaa kisiasa lazima awe na "thick skin" hizo ndio price you pay for being there at the top, not the other way round like you preach.
 
Kumbisalehe

JF-Expert Member
Nov 25, 2014
613
500
Umeandika vema ila kuna mambo ambayo huenda kama mwandishi makini ungeyaandika vinginevyo.

Ukisema watanzania walikuwa wameshoshwa na siasa za Magufuli, unamaanisha watanzania gani? Tumia neno baadhi au hata wengi wao lakini sio kweli kuwa wote walikuwa wamechoshwa na Magufuli wakati umeona kwa sehemu kubwa watu wamemlilia Magufuli sana pamoja na mapungufu yake. Ukali au kufoka ni personality yake. Hajaianza kwa sababu amekuwa Rais. Hivyo sio wote, wapo waliompenda tena sana tu.

Kitu kingine, ushauri wako kwa upinzani kuhusu nyakati pia ni mzuri. Ila kitu watu wengi wanasahau ni kuwa kuna vitu vitatu. Kuna Samia, kuna Rais Samia na kuna CCM. Kwa sehemu kubwa, Samia na Rais Samia wanamezwa na CCM ambayo ni mfumo na ni ile ile. Ukiangalia kwa makini, aliyeondoka ni Magufuli, lakini sehemu kubwa sana ya serikali ya Magufuli bado iko madarakani ni reshuffle tu imefanyika. Na approach kwa baadhi ya mambo kama kutumbua yanaendelea mpaka huko Zanzibar, kitu ambacho miaka ya nyuma hakikuwepo. Hivyo, pamoja na upole wa Mama kimtazamo wa nje, Mama yuko kwenye mfumo ule ule na anasisitiza kuwa yeye sio wa tofauti na Magufuli kama watu wanavyotaka iaminike.

Pia, umesema vizuri sana kuwa wapinzani wasome nyakati. Attacking politics zimepitwa na wakati. Huwezi lazimisha mtu mwenye madaraka makubwa kama Rais wa Tanzania kwa katiba yetu afanye unavyotaka kwa ku-tweet tweet. Watapewa nafasi ua majadiliano (kitu ukichosema vizuri pia kuwa Mama anaonyesha ushirikiano) lakini waje na hoja na wawe na staha. Nguvu au kejeli hazitawapeleka popote.

Kwa ujumla, umeandika vizuri sana na hii itawasaidia wakiifanyia kazi maana maana huo ni ukweli.
 
macho_mdiliko

JF-Expert Member
Mar 10, 2008
13,528
2,000
Hakuna kitu kinaamua siasa kama 'wakati'..
Wanasiasa wazuri ni wale wanaojua nyakati zinavyobadilika na kwenda na wakati uliopo ...

Watanzania walikuwa wamechoshwa mno na siasa za Magufuli...na uongozi wake kiujumla..
Kubanwa Uhuru wa kuongea
Kufokewa na kukaripiwa
Kutoa matamko Kwa ukali..
Kuzungumza Peke yake..
Kutokukosolewa ..
Kukosekana Kwa mijadala na majadiliano..
Na mengi yaliyoenda na hayo..

Ujio wa Samia umebadili siasa Kwa ujumla..
Samia hafoki anaongea Kwa upole na kushawishi ..
Anazungumzia mazungumzo na mijadala..
Hazuii kukosolewa badala yake anakaribisha kukosolewa Kwa serikali yake..

Kikubwa zaidi ni Mwanamke ..
Watu wanamtazama Kwa 'kumhurumia'..
Na kumpa 'all benefits of the doubts'..
Na kuelewa kuwa anapambana na mfumo dume...
Watu wengi wanaju hii nchi ngumu na wanajua Samia atahangaika kuweza kumudu ...still wanafarijika na 'kurudi Kwa Uhuru wa kuongea na kukosoa'..

Sasa kama wapinzani wanafikiri siasa za kumshambulia Rais na serikali yake zinalipa bado kama enzi za JK watakuwa wanakosea sana....
Sana Sana wataonekana 'hawana adabu'
Na wanajaribu 'kumuonea' 'Rais Mwanamke' baada ya 'kidume ' JPM
'kuwakomesha hadi wakaufyata'..

Siasa za kipindi hiki zinahitaji ubingwa wa hoja kwenye mijadala ya kistaarabu..bila
Kuwa 'boa' wananchi ambao walishachoshwa na Magufuli Sana Sana wanataka 'mzunguko' wa hela urudi kama ule wa JK....

Kuleta siasa za ulalamishi..
Siasa za uwana harakati.
Na siasa za Ku target watu na kuwashambulia bila kujua ..'role halisi' ya hao watu ni siasa ambazo zinakuwa 'outdated ' so fast...

Watu wanampenda Samia sio Kwa sababu ni kiongozi bora.. wanampenda Kwa sababu wanaona 'nafuu inakuja'
Upinzani ukicheza siasa za kuleta 'distraction'wakati watu wanasubiri nafuu ije ..hasira za wananchi zinaweza washukia wao.....

Siasa inaendana na nyakati.. wapinzani wanasoma nyakati??
Wengi sasa hivi (ukiwemo wewe na wana CCM wengi tu) wanakiri kuwa Magufuli aliharibu. Nakunukuu:
''Watanzania walikuwa wamechoshwa mno na siasa za Magufuli...na uongozi wake kiujumla..
Kubanwa Uhuru wa kuongea
Kufokewa na kukaripiwa
Kutoa matamko Kwa ukali..
Kuzungumza Peke yake..
Kutokukosolewa ..
Kukosekana Kwa mijadala na majadiliano..
Na mengi yaliyoenda na hayo..''

Mwisho wa nukuu.
Kama wakati wa Magufuli watanzania walikuwa kwenye hali mbaya namna hii (jambo ambalo ni kweli) mbona hawakufanya mabadiliko? Je, hata wakijenga hoja kipindi hiki ni nini kitawafanya watanzania wawasikilize na kuiondoa CCM?
My take: Upinzani hata uwe makini na wenye hoja namna gani, bila wananchi kujielewa na kuacha woga ni kazi bure. Kinachoendelea kuiweka CCM madarakani siyo udhaifu wa viongozi wa upinzani wala uimara wa hoja wa CCM bali wananchi wengi kutojielewa na kuwa woga.
 
macho_mdiliko

JF-Expert Member
Mar 10, 2008
13,528
2,000
Umeandika vema ila kuna mambo ambayo huenda kama mwandishi makini ungeyaandika vinginevyo.

Ukisema watanzania walikuwa wameshoshwa na siasa za Magufuli, unamaanisha watanzania gani? Tumia neno baadhi au hata wengi wao lakini sio kweli kuwa wote walikuwa wamechoshwa na Magufuli wakati umeona kwa sehemu kubwa watu wamemlilia Magufuli sana pamoja na mapungufu yake. Ukali au kufoka ni personality yake. Hajaianza kwa sababu amekuwa Rais. Hivyo sio wote, wapo waliompenda tena sana tu.

Kitu kingine, ushauri wako kwa upinzani kuhusu nyakati pia ni mzuri. Ila kitu watu wengi wanasahau ni kuwa kuna vitu vitatu. Kuna Samia, kuna Rais Samia na kuna CCM. Kwa sehemu kubwa, Samia na Rais Samia wanamezwa na CCM ambayo ni mfumo na ni ile ile. Ukiangalia kwa makini, aliyeondoka ni Magufuli, lakini sehemu kubwa sana ya serikali ya Magufuli bado iko madarakani ni reshuffle tu imefanyika. Na approach kwa baadhi ya mambo kama kutumbua yanaendelea mpaka huko Zanzibar, kitu ambacho miaka ya nyuma hakikuwepo. Hivyo, pamoja na upole wa Mama kimtazamo wa nje, Mama yuko kwenye mfumo ule ule na anasisitiza kuwa yeye sio wa tofauti na Magufuli kama watu wanavyotaka iaminike.

Pia, umesema vizuri sana kuwa wapinzani wasome nyakati. Attacking politics zimepitwa na wakati. Huwezi lazimisha mtu mwenye madaraka makubwa kama Rais wa Tanzania kwa katiba yetu afanye unavyotaka kwa ku-tweet tweet. Watapewa nafasi ua majadiliano (kitu ukichosema vizuri pia kuwa Mama anaonyesha ushirikiano) lakini waje na hoja na wawe na staha. Nguvu au kejeli hazitawapeleka popote.

Kwa ujumla, umeandika vizuri sana na hii itawasaidia wakiifanyia kazi maana maana huo ni ukweli.
Kinachoiweka CCM ni woga wa wananchi kupigania haki zao za kuchagua viongozi wanaowataka. Haya mengine mnayoandika huku ni bla bla tu.
 
Erythrocyte

JF-Expert Member
Nov 6, 2012
82,683

Magufuli alishachokwa utake usitake !
 
Kumbisalehe

JF-Expert Member
Nov 25, 2014
613
500
Magufuli alishachokwa utake usitake !

Soma vizuri, hakuna kiongozi aliyewahi kukubalika na watu wote wakati wote, lakini pia hakuna kiongozi aliyekataliwa na watu wote wakati wote.

Kama ulimchoka wewe, hilo una uhakika nalo 100% na atakayekupinga ana matatizo. Lakini kusema alishachokwa na wengine, ni jambo lenye ukweli kwa assumptions na hypothesis, lakini ukubali wapo waliompenda hasa wenye maisha duni na yeye siku zote alijitafsiri kuwa hao ndio kipaumbele chake na hasira zake ziliwashukia wakwepa kodi na wala rushwa na waonevu ikiwemo wanyonyaji mpaka kwenye madini kule.

Sasa u-balance, usilazimishe kuwa kila mtu alimchoka, ulimchoka wewe.
 
unamfahamu rafiki kipenzi wa Magufuli aliyeitwa Kakoko ? ni bwege tu atakayedhani Magufuli alikuwa rais wa wanyonge
 
Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom