Upendo huu wa mawifi zangu umenifika happaaa!

Upendo huu wa mawifi zangu umenifika happaaa!

Una mawifi wengi, it's either you'll enjoy au watakupa shida sana ndani ya ndoa.

Ila huwa sielewi kwa nini watu hupenda kuingilia mambo [ndoa/ mahusiano] ya wengine.

Huwa najisemea mwenyewe kuwa kama watu wote wangekuwa kama mimi [kutokujali ya wengine hadi ninapoombwa kuhusika] basi mitafaruku maishani ingekuwa michache sana.

Sasa mtu yuko na wake muhibu, nyie wengine inawahusu nini kuanza kufungua midomo kuhusu mavazi, urembo, na kadhalika?

Unaanzia wapi kwanza? Unaanza anzaje?

Kwa mtu ninayeongozwa na falsafa ya 'live and let live' inaniwia vigumu sana kuelewa.

Kwa sababu, kama mhusika au wahusika hawana tatizo, wewe tatizo lako nini?

Si ujali ya kwako tu....

But I know better that such isn't life.

There will always be those who like to poke their noses in other folks' businesses.
 
Ila huwa sielewi kwa nini watu hupenda kuingilia mambo [ndoa/ mahusiano] ya wengine.

Huwa najisemea mwenyewe kuwa kama watu wote wangekuwa kama mimi [kutokujali ya wengine hadi ninapoombwa kuhusika] basi mitafaruku maishani ingekuwa michache sana.

Sasa mtu yuko na wake muhibu, nyie wengine inawahusu nini kuanza kufungua midomo kuhusu mavazi, urembo, na kadhalika?

Unaanzia wapi kwanza? Unaanza anzaje?

Kwa mtu ninayeongozwa na falsafa ya 'live and let live' inaniwia vigumu sana kuelewa.

Kwa sababu, kama mhusika au wahusika hawana tatizo, wewe tatizo lako nini?

Si ujali ya kwako tu....

But I know better that such isn't life.

There will always be those who like to poke their noses in other folks' businesses
.
...and that's exactly my point. Katika ya hao sita kuna watakaojali mambo yao na watakaoingilia mambo ya kaka yao. Sio wote wanaopenda kuishi maisha yao bila kuangalia kwa jirani kuna nini.
 
Achana naye huyo kaka yao njoo kwangu Mimi napenda mwanamke kama wewe na hutasumbuliwa na mawifi zako.
 
Jamani mimi mawifi zangu (dada wa mtarajiwa wangu) wananitatiza. Mchumba wangu ni mtoto wa kiume pekee kwa wazazi wake na amebarikiwa madada sita. To be honest nawapenda mawifi zangu na wananipenda pia kwa maneno na matendo ila sasa upendo huu naona unaelekea kuwa mzito sana kwangu.

Mimi ni mwanamke simple sana. Mavazi na Hairstyle na muonekano wangu kwa ujumla ni simple. Sasa mawifi zangu tangu nimetambulishwa kwao wamekuwa ni watu wa kutaka kunibadilisha. Ninaletewa nguo, hereni, viatu na kila aina ya urembo ambao si kama ule ninaopendelea. Weekend lazima mmoja anitafute twende salon, tukifika huko nitalazimishwa mambo ya pedicure, manicure wakati sina mazoea hayo. Yani ni kama wamewekeana zamu, leo huyu kesho huyu. Mara shopping na tukifika huko sipewi uhuru wa kuchagua nivipendavyo bali naambiwa "wifi hii ndo itakupendeza bwana, tena hata kaka atapenda ukivaa hii".

Wiki iliyopita tulienda harusini mimi, mchumba wangu na dada zake wawili. Nikakutana nao mitaa ya Mwenge ili tuongozane kwenda huko. Nilikuwa nimevaa flat shoes na gauni langu la usiku. Jamani wifi zangu walilalamika kwanini nimevaa flat shoes kwa muda kama dakika 20 hadi baby ikabidi aseme mwacheni mke wangu. Leo wifi amenitag instagram kwenye picha ya viatu virefu ananiuliza kama nimevipenda. Sijajibu hadi sasa na najawa na hasira na mashaka kuwa endapo nikiolewa si watakuja kunipangia hadi nightdress za kumvalia mume wangu hawa..

Nifanye nini waniache alone bila kuwa na mtafaruku au wasijisikie vibaya kwani wananipenda na najua wanafanya kwa upendo na nafurahi kupendwa ukweni ila daaaaahhhh!
Mabadiliko ya ghafla yanaweza ikiwa faida au hasara ktkt uhusiano wenu, jaribu kutafiti labda ni maelekezo ya mmeo mtarajiwa kuwa anataka dada zake wakubadili ktk viwango anavyovitaka, ikiwa sivyo, pia jaribu kutafiti kuwa anavutiwa na mwonekano gani, ikiwa anavutiwa na usimpo wako basi mweleze awadhibiti wifi zako, endapo utaanza kupingano nao ujue hawachelewi kuleta *****.
Hapa umakini, hekima na busara vinahitajika sana kwako vinginevyo wakikugeuka imekula kwako mazima
 
Mtani, Kave uogha..?

Anyway, ku enjoy au kupata shida itategemea pia na utashi wa mumewe katika kuisimamia nyumba yake kama kiongozi wa nyumba, akilega hao madada watamkalia mkewe kichwani, but akiwa na msimamo, nataka hiki na hiki sitaki, watamuheshimu mkewe, hata wakisema watasemea huko mafichoni. I have an evidence mtani wangu.

...teh, na wewe umeolewa penye mawifi sita mtani[emoji12] .

Tatizo watu hawataki kuishi maisha yao, hasa mawifi. Wanadhani wana mandate na kaka yao. Huyo jamaa asipokuwa na principles kwenye nyumba yake, hao madada sita watamtafuna wifi yao.
 
Kwani kaka yao alipokupenda hakukuona uvaaji wako?
Lakini alikupenda ulivyo.
Pokea hizo zawadi unazoletewa na wifi zako lakini msikilize zaidi mchumba wako anapenda uvaaje.
Si kila wavaacho wifi zako eti kaka yao anapenda, mengine ya ngoswe anayakaushia tu.
 
Wanajua kaka yao anapenda wanawake wa design gani.
Either wanataka ufanane na wao au ufanane na x girl wa huyo kaka yao.
Wanakuivisha uende sawa na baby au la hasha.
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom