Queen V
JF-Expert Member
- Jan 19, 2012
- 785
- 1,368
Jamani mimi mawifi zangu (dada wa mtarajiwa wangu) wananitatiza. Mchumba wangu ni mtoto wa kiume pekee kwa wazazi wake na amebarikiwa madada sita. To be honest nawapenda mawifi zangu na wananipenda pia kwa maneno na matendo ila sasa upendo huu naona unaelekea kuwa mzito sana kwangu.
Mimi ni mwanamke simple sana. Mavazi na Hairstyle na muonekano wangu kwa ujumla ni simple. Sasa mawifi zangu tangu nimetambulishwa kwao wamekuwa ni watu wa kutaka kunibadilisha. Ninaletewa nguo, hereni, viatu na kila aina ya urembo ambao si kama ule ninaopendelea. Weekend lazima mmoja anitafute twende salon, tukifika huko nitalazimishwa mambo ya pedicure, manicure wakati sina mazoea hayo. Yani ni kama wamewekeana zamu, leo huyu kesho huyu. Mara shopping na tukifika huko sipewi uhuru wa kuchagua nivipendavyo bali naambiwa "wifi hii ndo itakupendeza bwana, tena hata kaka atapenda ukivaa hii".
Wiki iliyopita tulienda harusini mimi, mchumba wangu na dada zake wawili. Nikakutana nao mitaa ya Mwenge ili tuongozane kwenda huko. Nilikuwa nimevaa flat shoes na gauni langu la usiku. Jamani wifi zangu walilalamika kwanini nimevaa flat shoes kwa muda kama dakika 20 hadi baby ikabidi aseme mwacheni mke wangu. Leo wifi amenitag instagram kwenye picha ya viatu virefu ananiuliza kama nimevipenda. Sijajibu hadi sasa na najawa na hasira na mashaka kuwa endapo nikiolewa si watakuja kunipangia hadi nightdress za kumvalia mume wangu hawa..
Nifanye nini waniache alone bila kuwa na mtafaruku au wasijisikie vibaya kwani wananipenda na najua wanafanya kwa upendo na nafurahi kupendwa ukweni ila daaaaahhhh!