RIWAYA: Mtutu wa Bunduki (1 - 3)

Fortunatus Buyobe

JF-Expert Member
Nov 9, 2011
463
1,107
Naona alosto zimezidi. Nimeona nirushe adithi ambayo bado mtunzi anaishusha taratibu. Mara moja kwa wiki. Kumbukeni huyu ni mwandishi mahili wa vitabu kama;Tai kwenye mzoga,Mifupa 206 na Ufukwe wa Madagascar. Hivi vitabu vyote vimetoka nawaomba mjitahidi kupata nakala zenu kwa kuwasiliana na mtunzi.Tumchangie mwandishi kumpa motisha kwa kazi zake. Anaitwa KELVIN MPONDA wasiliana naye kwa namba hii 0688058669

RIWAYA: MTUTU WA BUNDUKI
SEHEMU: 1

MTUTU WA BUNDUKI

Chuo Kikuu cha Ibadan, Nigeria.
Tarehe 9 Aprili, 1980.

Ilianza miaka, ikafuata miezi na hatimaye wiki na sasa ilikuwa imesalia siku moja tu ya kuachana na chuo kikuu cha Ibadan, magharibi mwa nchini Nigeria, baada ya kuhitimu vizuri masomo yangu ya shahada ya masuala ya mahusiano ya kimataifa, kwa muda wa miaka minne.
Huzuni ya kuachana na marafiki niliozoeana nao kwa muda mrefu tangu kuanza kwa masomo yangu ilikuwa imeniganda moyoni na mandhari yale rafiki ya chuo na mazingira yake yaliendelea kunishtaki moyoni kuwa ingelinichukua muda mrefu kabla ya kumbukumbu hiyo kufutika kabisa kichwani mwangu.


Hata hivyo kwa upande mwingine nilikuwa na furaha moyoni, siyo tu furaha ya kuhitimu vizuri elimu yangu lakini pia furaha ya kurudi nyumbani jijini Dar es Salaam nchini Tanzania kuwaona ndugu zangu na marafiki niliopoteana nao kwa kitambo kirefu. Mbali na hayo idara yangu ya kijasusi jijini Dar es Salaam ilikuwa ikinihitaji kazini kama ilivyokuwa kwa wafanyakazi wengine wa serikali wanaorudi ofisini baada ya ruhusa yao ya kuwa masomoni kufika ukomo.


Wenzangu wawili walikuwa wamepelekwa kusoma kwenye vyuo vya nchi za jirani na Tanzania. Mmoja alikuwa chuo kikuu cha Makerere nchini Uganda, na mwingine alikuwa chuo kikuu cha Jomo Kenyatta, jijini Nairobi nchini Kenya. Mimi pekee ndiyo nilikuwa nimeletwa pale chuo kikuu cha Ibadan, magharibi mwa Nigeria. Sijui kigezo gani kilitumika na wakuu wetu wa kazi lakini niseme uchaguzi wao kwangu ulikuwa umenifurahisha kwa vile nilipenda kukaa mbali na nchi yangu ili nikutane na mazingira mapya na marafiki wapya wenye tamaduni tofauti.

Usiku huu, kama ilivyokuwa kwa wanafunzi wahitimu kutoka mataifa mengine ya bara la Afrika, na mimi pia nilikuwa katika harakati za kufungasha mizigo yangu katika chumba changu namba 16 kilichopo ghorofa ya pili ya jengo la hosteli ya wanafunzi wa mwaka wa mwisho liitwalo Block D ili kujiandaa na safari ya kurudi nchini kwangu Tanzania.

Zoezi hili la kufungasha mizigo yangu kwa kweli lilinipa changamoto sana kwa vile iliniwia vigumu sana kuamua niache kipi na kuchukua kipi. Mbali na hayo sikupenda kuchukua mizigo mingi kwa kukwepa usumbufu safarini. Labda ningechukua mizigo mingi kama ningekuwa na mtu wa kunisaidia mizigo hiyo. Nikawaza.

Wazo hilo ndiyo likanitumbukiza kwenye mjadala mpya ulionipelekea simanzi moyoni mwangu. Nilikuwa nimemkumbuka Mariama, msichana mzuri na mrembo au niseme kupita wasichana wote pale chuoni. Mimi na Mariama, sote tulikuwa ni wanafunzi wahitimu wa shahada ya mahusiano ya kimatifa pale chuoni.

Kwa vile tulikuwa darasa moja haikunichukua muda mrefu kuzoena na kisura huyo mapema tu tulipoanza masomo yetu pale chuoni. Urafiki wetu ukashamiri siku hadi siku, hatimaye tukajikuta tumetumbukia kwenye mapenzi mazito kiasi cha kuonewa wivu na wanafunzi wengine walioitamani sana bahati hiyo.

Kupitia urafiki wetu hatimaye nikapata kumfahamu vizuri Mariama. Jina lake kamili aliitwa Mariama Momolu, msichana kisura kutoka Liberia, zaidi ya hapo nikafahamu kuwa Mariama alikuwa mtoto wa waziri wa mambo ya ndani wa Liberia chini ya serikali ya rais wa Liberia wa wakati huo ndugu William R. Tolbert Jr.

Hata hivyo ni mimi tu ndiye niliyekuwa nikiifahamu siri hiyo kwani pamoja na uzuri wa ajabu aliokuwa nao Mariama, uwezo wake mkubwa wa akili za darasani na hali nzuri ya maisha ya nyumbani kwao lakini hakuwa mtu wa kujikweza wala majivuno. Pale chuoni aliishi maisha ya kawaida kama wanafunzi wengine, mcheshi na mwenye furaha wakati wote.

Sasa masomo yalikuwa yamefika tamati na kila mwanafunzi alitakiwa kurudi nchini kwake kujenga taifa. Loh! kwangu ilikuwa ni zaidi ya huzuni iwapatayo wapenzi wakati wa kuagana huku kila mmoja asifahamu ni lini angekutana tena na mwenza wake. Nilikuwa nimemzoea na kumpenda sana Mariama kiasi kwamba moyo wangu ulianza kusononeka sana kila nilipoufikiria wakati wa kuagana kwetu. Huku nikijiuliza maisha yatakuwaje nikiwa mbali na Mariama?

Vipi kama mara baada ya kuagana tusingeonana tena hapa duniani na hivyo mahusiano yetu kubaki historia?. Vipi kama Mariama angepata mchumba mwingine baada ya kurudi nchini kwake Liberia na hatimaye wakafunga ndoa?. Nikaendelea kujiuliza huku nikiendelea kufungasha nguo zangu. Majibu sikupata badala yake mawazo yangu yakaanza kutawaliwa na hisia za wivu mkali wa mapenzi.

Nikiwa katikati ya mawazo haya mara nikashtushwa na sauti ya mtu aliyeanza kugonga mlango wa chumba changu. Haraka nikasitisha nilichokuwa nikikifanya na kuyapeleka macho yangu hadi pale mlangoni huku akili yangu ikisumbuka kufahamu mgongaji angekuwa nani. Hata hivyo kwa kuwa nilikuwa mtu wa marafiki sikushtuka sana kwani ni mara chache sana kukuta chumba changu kikiwa pweke bila marafiki.

Nikawaza nimwambie mgongaji kuwa afungue ule mlango na kuingia ndani lakini nikawa nimekumbuka kuwa nilikuwa nimeufunga ule mlango wa chumba changu kwa funguo. Nikahisi kukereka hata hivyo kwa kuwa niliwaheshimu na kuwapenda marafiki sikuwa na namna ya kufanya ila kusimama pale kitandani nilipoketi na kuelekea mlangoni kivivuvivu.

Loh! kitendo cha kufungua mlango kikanipelekea nipigwe na butwaa kabla ya tabasamu maridhawa kuchanua usoni mwangu. Mgongaji alikuwa Mariama na kama nisingekuwa makini huwenda ningemsahau kabisa kwani uzuri wake ulikuwa umevuka mipaka.
Mariama alikuwa amevaa gauni nyepesi na nyeusi ya kata mikono iliyolichora vyema umbo lake na kuishia sentimita chache juu ya magoti yake huku mpasuo mrefu wa gauni hilo kuanzia kiunoni hadi pajani ukiliacha nusu wazi paja lake. Miguuni alikuwa amevaa skuna, viatu vyekundu vyenye visigino virefu. Macho yangu yakafanya ziara makini nikimtazama kuanzia juu na hapo nikakutana na tabasamu laini usoni mwake.

Kope zake zilikuwa zimekolea wanja kisawasawa, macho yake makubwa, meupe na legevu yakaichangamsha akili yangu. Tabasamu lake maridhawa likazisogeza kingo pana za mdomo wake juu na chini na hivyo kupelekea meno yake meupe yaliyopangika vizuri kuonekana bila kificho.

Masikioni alikuwa ametoga herini za almasi safi ya Liberia. Nywele zake nyeusi na laini alikuwa amezichoma vizuri kwa chanuo la moto na kuzibana kwa nyuma. Mkufu wake mwembamba wa dhahabu safi uliizunguka vyema shingo yake nyembamba na kisha kidani chake kupotelea katikati ya mfereji wa matiti yake mang’avu kifuani. Pochi yake ya ngozi ya mamba aliitundika begani na mkononi alivaa bangili nyingi za rangi tofauti za kuvutia. Rangi yake ya ngozi ya asili ya mwanamke wa Afrika ilikuwa imechangia ziada nyingine katika uzuri wake. Usiku huu Mariama alikuwa amependeza sana, niseme sikuwahi kumuona akiwa katika mvuto ule.

Hata hivyo niliporudia kumtazama Mariama usoni jambo moja likanitatiza. Kulikuwa na kila dalili kuwa Mariama alikuwa ametoka kulia muda mfupi uliopita kwani michirizi ya machozi yake mashavuni ilikuwa bado kufutika vizuri pamoja na jitihada za kuifuta zilizofanyika. Ingawa Mariama alijitahidi kuificha hali ile lakini hakufanikiwa.
Loh! moyo wangu ukaingiwa na ganzi huku nikijiuliza nani aliyemliza kisura wangu?. Nini kimemtokea hadi atokwe na machozi?. Majibu sikupata, hatimaye nikamshika mkono Mariama na kumkaribisha ndani. Bila upinzani wowote Mariama akaingia ndani akinifuata na nilipofunga mlango wa chumba changu nyuma yake sauti ya kilio cha kwikwi cha Mariama ikaanza kuhanikiza mle ndani.

Mariama hakuweza tena kuyazuia machozi yake. Mara hii machozi yalimbubujika upya kama chemichemi ya kijito cha kondeni. Nikawahi kumvuta karibu yangu kisha nikamshika kichwani na kumtazama kwa hamaki, kabla ya kumuuliza kwa upole.

“Nani aliyekuudhi mpenzi?”. Mariama hakunijibu badala yake akaangua kilio huku kingo za mdomo wake zikimchezacheza kama mtoto mdogo.
“Niambie Mariama wangu, nani aliyekuudhi nikamshughulikie sasa hivi?”. Swali langu likampelekea Mariama anitazame katika uso wa majuto huku macho yake yamezingirwa na machozi.
“Hakuna alieniudhi Tibba”. Sauti yake ilikuwa laini lakini yenye uchungu mwingi.

“Sasa nini kinachokuliza Mariama wangu?”. Nikamuuliza kwa udadisi.
“Wewe”. Jibu la Mariama likanistua na hapo nikamkazia macho kumtazama kama ambaye sikuwa nimemsikia vizuri.
“Mimi?”. Nikamuuliza kwa mshangao.
“Ndiyo”. Mariama akajibu huku akiendelea kuangua kilio kama mtoto anayedeka.
“Nimekufanya nini mpenzi?”
“Kutwa nzima nimejifungia hosteli chumbani kwangu nikilia. Kila nilipojitahidi kukuweka mbali na mawazo yangu nimeshindwa kabisa. Nakupenda sana Tibba, wewe ni mwanaume wa ndoto yangu na sasa naona kuwa mbali na wewe ni jambo lisilowezekana kabisa maishani mwangu”. Mariama akaweka kituo akiendelea kutiririsha machozi mashavuni mwake.

Maneno yale yakanichoma vibaya moyoni na kuongeneza maumivu makali ya hisia. Ukweli ni kwamba hata mimi nilikuwa sina furaha kuelekea kuagana na Mariama baada ya kipindi chetu cha masomo kufika ukomo na kila nilipowaza umbali uliokuwa kati yaTanzania na Liberia nikazidi kukata tamaa ya kuonana kwetu. Hivyo kama si kujikaza kisabuni huwenda hata mimi ningetokwa na machozi.

“Usihuzunike mpenzi huwenda tukaonana tena baada ya kuachana hapa”. Nikamfariji Mariama lakini moyoni nafsi yangu ikanisuta pale nilipowaza kuwa lisingekuwa jambo rahisi kama linavyoweza kusikika masikioni mwake. Mariama akaongeza kilio huku akinipigapiga ngumi hafifu kifuani.

“Unanidanganya Tibba na kujitahidi kunifariji kama mtoto. Nafsi yangu sasa inajuta kujiingiza kwenye mapenzi na wewe. Umeuteka moyo wangu na sasa siwezi tena kuwa peke yangu”
“Nakuhakikishia kuwa tutaonana tena mpenzi. Wewe ndiye mwanamke wa maisha yangu”. Nikaongea huku taratibu nikimvuta zaidi Mariama karibu yangu na hapo nikaona tabasamu hafifu likichanua usoni mwake.

“Kweli mpenzi?”
“Kweli kabisa nakuhakikishia”
“Harusi yetu itafanyika lini?”
“Nitapenda tulizungumzie hilo suala kwa pamoja”
“Tibba wewe ndiye mume wangu na baba wa watoto wangu”. Mariama akaongea huku akijifuta machozi.
“Mariama, yaani bila wewe maisha kwangu si chochote tena mpenzi”. Nikaongea kwa msisitizo na hapo nikamuona Mariama akifungua pochi yake na kutoa bahasha mbili ndogo nyeupe zenye nembo ya shirika la ndege la Nigeria.

“Nimekata tiketi mbili za ndege”. Mariama akanitahadharisha.
“Tiketi mbili zote za nini?”
“Moja ya kwangu na nyingine ya kwako. Nimekwishawajulisha nyumbani kuwa nitaenda na wewe”. Mariama akaongea huku akinitazama kwa hadhari. Taarifa zile zikawa zimenishtua.

“Loh! mpenzi mbona sasa hukuniambia mapema kuwa umepanga twende wote kwenu?”
“Kwani tatizo liko wapi?”. Mariama akaniuliza katika namna ya kukata tamaa.

“Mimi nimesomeshwa na serikali mpenzi na hivi tunavyoongea nimeshutumiwa tiketi ya ndege ya kurudi nchini kwangu Tanzania. Serikali yangu itanielewaje nisiporudi nchini kwangu wakati muda wa masomo umefika ukomo?”

“Nyumbani nimekwishawaeleza kuwa nimepata mchumba. Hivyo baba na mama wamependekeza uende kuwasalimia kabla hujarudi Tanzania”. Kama ambaye ananishawishi nikubaliane na matakwa yake Mariama akanisogelea na kukilaza kichwa chake begani kwangu huku taratibu akikipapasa kifua changu. Loh! chuchu zake zikanitekenya kidogo, joto la mwili wake likazipumbaza kidogo fikra zangu huku harufu nzuri ya manukato aliyojipaka mwilini yakinilevya.

“Tafadhali Tibba nakuomba twende wote nyumbani wazazi wangu wakuone”. Mariama akalalama kwa sauti dhaifu ya kubembeleza na kupitia maneno yake sasa nikagutuka kuwa kweli Mariama alikuwa amekufa na ameoza juu yangu. Taratibu nikamkumbatia na kumpapasa kiunoni huku nikiupisha utulivu kichwani mwangu.

Sikuwahi kufika Liberia na kwa vile ilikuwa ni ndoto yangu ya muda mrefu mara hii niliona kama bahati ya kipekee sana kuwahi kujitokeza mbele yangu. Kutembeleza nchi nzuri kama Liberia kwangu ingekuwa ziada muhimu katika historia yangu ya safari za bara la Afrika. Lakini kwa namna moja nilikuwa na wasiwasi juu ya safari ile kwa vile sikuwa na fedha za kutosha za kuniwezesha kusafiri kutoka nchini Liberia hadi Tanzania. Hivyo sikutaka kuwapa wenyeji wangu majukumu yasiyowahusu.

“Natamani sana kuwaona wazazi wako huko Liberia mpenzi lakini kuna jambo moja”. Nikaongea kwa utulivu na hapo Mariama akaondoa kichwa chake begani kwangu na kunitazama kwa hadhari.
“Jambo gani mpenzi?”
“Kwenye akiba yangu nina kiasi kidogo cha fedha”
“Kwa hiyo?”
“Hakiwezi kutosheleza kukata tiketi ya ndege ya kutoka Monrovia, Liberia hadi Dar es Salaam, Tanzania”. Mariama akanitazama kabla ya kuangua tabasamu hafifu la matumaini.
“Usijali mpenzi kwani hilo nililifahamu mapema hivyo tayari nilikuwa nimeandaa mkakati wa kulitatua”
“Mkakati upi?”. Nikauliza kwa shauku.

“Nimekwisha ongea na baba na amenihakikishia kuwa kutoka Monrovia hadi Dar es Salaam utasafiri kwenye daraja la kwanza la ndege kama mtoto wa waziri na gharama zote zitakua juu yake”. Maelezo ya Mariama yakanishangaza sana na kwa mara ya kwanza nikajikuta nikiangua kicheko hafifu cha furaha.

“Nimefurahi sana mpenzi kwa kweli sikufikiria kama ingewezekana”. Nikavunja ukimya.
“Wazazi wangu watafurahi sana kukuona Tibba”. Mariama akaongea huku akitabasamu.
“Mh! Lakini umewaambia nini wazazi wako hadi wajitoe kwangu namna hiyo?”
“Wanafanya hayo yote kwa sababu yangu. Wazazi wangu hawapendi nisononeke au nisifikie malengo ya furaha yangu. Wazazi wangu ni matajiri na mimi ni mtoto wao pekee nyumbani kwetu. Kwa vile wanavyonipenda na kunijali hawakuwa na pingamizi lolote”. Mariama akajigamba.

“Loh! kumbe wewe ni mziwanda na kitinda mimba ndiyo maana huachi kudeka”. Nikaongea huku nikitabasamu na hapo Mariama akasogea karibu na kunibusu mdomoni.
“Safari yetu itaanza kesho saa mbili asubuhi mpenzi”

“Mimi sina pingamizi tena na nimekubaliana na ombi lako mpenzi”. Wakati nikiongea maneno haya matamu nikawa nikikipapasa taratibu kiuno cha Marima.
“Ahsante sana Tibba wangu”. Mariama akaongea kwa sauti nyepesi ya kubembeleza.

“Tutaondoka kwa ndege ya shirika gani?”
“Nigeria Airways”
“Nasikia ni shirika zuri sana la ndege hilo ingawa kwangu itakuwa ni mara yangu ya kwanza kusafiri nalo”. Nikaongea huku nikiangua tabasamu.
“Tutakapofika Monrovia dereva wa baba atafika kutuchukua hadi nyumbani”. Mariama akanitoa wasiwasi. Nikataka kuongea neno hata hivyo sikufanikiwa kwani Mariama alikwisha uzamisha ulimi wake kinywani mwangu.

Ndimi zetu zikakamatana vilivyo huku pumzi nyepesi ikipita puani. Mikono yangu chakaramu ikasafiri taratibu hadi kifuani kwa Mariama na hapo nikaanza kuyatomasa matiti yake taratibu kwa ufundi wa hali ya juu. Mariama akaachia sauti hafifu ya mguno wa mahaba kama mtu aliyepagawa na wazimu wa mapenzi. Macho yake legevu yakataka kufumba lakini yaliishia katikati ya mboni zake na hivyo kumpelekea aonekane kama aliyelevywa na mvinyo mkali.

Ncha ya ulimi wangu ikasafiri haraka kufanya ziara kwenye tundu la sikio lake na hapo nikasikia tena sauti hafifu ya mguno wa mahaba kutoka kwa Mariama sambamba na mapigo ya moyo wake kuanza kwenda mbio.
Mariama hakuweza tena kuvumilia badala yake kwa papara akaanza kunivua fulana yangu na alipofanikiwa akaitoa na kuitupilia mbali na hapo akaanza tena kukipapasa kifua changu kwa fujo. Mikono yangu ikahamia kiunoni pake, nikakitekenya kidogo kitovu chake kisha nikaisogeza chini zaidi na kuanza kuyatomasa makalio yake.

Loh! Mariama akaachia tena sauti kali ya mguno wa mahaba kisha akatoa pumzi nyingi kwa mkupuo na hapo kwa wazimu wa mapenzi akauvua mkoba wake begani na kuutupa sakafuni kisha mikono yake ikasafiri haraka hadi kiunoni kwangu. Hapo akafyetua bakoni ya mkanda wangu wa suruali na kushusha chini zipu ya suruali yangu kisha haraka akachuchumaa na kuyashika mapaja yangu.

Muda mfupi uliofuata nikahisi joto zuri likipita kwenye dhakari yangu na raha ile ikanipelekea nisimame wima kama sanamu huku macho nimeyafumba, mdomo nikaachama, nywele zikanicheza na misuli ikatetema mwilini. Hatimaye nikashindwa kujizuia hivyo sauti hafifu ya mguno wa mahaba ikanitoka mdomoni na hatimaye kusukuma nje pumzi nyingi kwa mkupuo. Mariama alikuwa amenizidi utundu na mara hii nilining’inia kwa ncha za nyayo zangu kama ninayeogopa kukanyaga ardhi iliyoshika moto wa uji wa chuma.

Nilikuwa katikati ya raha isiyoelezeka.
Nikiwa bado nimefumba macho kupambana na hisia zangu mara nikashangaa nikisukumiwa kitandani kisha Mariama akafuatia juu yangu. Mara nikamuona akipandisha juu gauni lake kisha akavua nguo yake ya ndani na kuitupa kando ya kitanda. Mambo yote yakafanyika chapuchapu na wakati nikishangazwa na wazimu ule Mariama tayari alikuwa amenikalia kiunoni kisha mjongeo hafifu wa mwili wake ukaanza, akipanda juu na kushuka chini taratibu.

Sasa tulikuwa kwenye mapenzi mazito kana kwamba yangekuwa mapenzi ya mwisho kabla ya kifo chetu. Mariama alikuwa hajitambui kwa hali huku akiongea maneno mengi ya kunisifia na kuachia miguno ya hapa na pale ya mahaba na mimi sikuwa nyuma badala yake nikafanya kila liwezekanalo kuhakikisha kuwa nakata kiu yake ya mapenzi.

Usiku ule sikuhitaji marafiki kwani kila aliyegonga mlango wa chumba changu aliishia kukata tamaa ya kufunguliwa na hatimaye akaondoka zake. Lawama za marafiki nilikuwa tayari kukabiliana nazo.

MONROVIA, LIBERIA.
James Spriggs Payne Airfield. Saa 04:30 Asubuhi.

Sote tulikuwa na uchovu lakini huwenda mimi nilikuwa na uchovu mwingi zaidi. Shughuli pevu ya usiku wa jana kule chumbani kwangu kwenye hosteli ya chuo kikuu cha Ibadan nchini Nigeria ilikuwa imeniacha hoi bin taaban. Kama siyo Mariama kuwahi kushtuka alfajiri yumkini tungekuwa tumechelewa ndege ya saa mbili asubuhi.

Mkono laini wa Mariama ilinishtua taratibu kutoka usingizini kwa kunishika kichwani na hapo taratibu nikafumbua macho yangu na kuyatembeza huku na kule kabla ya kuweka kituo kishoto kwangu sehemu alipoketi Mariama. Nilichokiona usoni mwake lilikuwa ni tabasamu la kichovu lakini lenye nguvu.

“Tunakaribia kutua mpenzi”
“Loh! mara hii tum bona hata safari yenyewe sijaifaidi vizuri”. Nikaongea kichovuchovu huku nikiyapeleka macho yangu kwenye dirisha

RIWAYA: MTUTU WA BUNDUKI
SEHEMU: 2

MONROVIA, LIBERIA.
James Spriggs Payne Airfield. Saa 04:30 Asubuhi.

Sote tulikuwa na uchovu lakini huwenda mimi nilikuwa na uchovu mwingi zaidi. Shughuli pevu ya usiku wa jana kule chumbani kwangu kwenye hosteli ya chuo kikuu cha Ibadan nchini Nigeria ilikuwa imeniacha hoi bin taaban. Kama siyo Mariama kuwahi kushtuka alfajiri yumkini tungekuwa tumechelewa ndege ya saa mbili asubuhi.

Mkono laini wa Mariama ilinishtua taratibu kutoka usingizini kwa kunishika kichwani na hapo taratibu nikafumbua macho yangu na kuyatembeza huku na kule kabla ya kuweka kituo kishoto kwangu sehemu alipoketi Mariama. Nilichokiona usoni mwake lilikuwa ni tabasamu la kichovu lakini lenye nguvu.

“Tunakaribia kutua mpenzi”
“Loh! mara hii tu mbona hata safari yenyewe sijaifaidi vizuri”. Nikaongea kichovuchovu huku nikiyapeleka macho yangu kwenye dirisha la ndege kutazama chini.

“Pole sana mpenzi, kweli jana nilikuchosha sana maana safari nzima ulikuwa usingizini”. Mariama akaongea huku akiangua kicheko hafifu kilichonipelekea nitabasamu.
Tulikuwa angani kwa zaidi ya masaa mawili na ushei tukipita kwenye anga la nchi nne za Afrika, Benin, Togo, Ghana, Cote d’ivore kabla ya kutua nchini Liberia. Kupitia dirishani niliweza kuona sehemu kubwa ya bahari ya Atlantiki, barabara kuu za mijini, makazi ya watu na mto mkubwa. Nilipomuuliza Mariama juu ya mto ule akaniambia kuwa ule mto ulikuwa ukiitwa mto Mesurado, mto mkubwa kabisa nchini Liberia uliokuwa ukitapisha maji yake katika pwani ya bahari ya Atlantiki.
Ingawa ndege ilikuwa bado kutua lakini sehemu kubwa ya mandhari ya nchi ya Liberia ilikuwa imenivutia sana kwa uoto wake wa asili wa kijani kibichi na misitu mizito iliyoshona milima na mito mingi yenye maji ya kutosha. Liberia haikuelekea kuwa ni nchi iliyokuwa ikikabiliwa na majanga ya ukame na njaa hata kidogo.

Kupitia maelezo ya mwalimu wangu wa somo la jiografia wa shule ya sekondari yakanipelekea nikumbuke kuwa nchi ya Liberia ilikuwa miongoni mwa nchi za Afrika yenye utajiri mkubwa wa madini ya dhahabu, almasi na chumayanayopatikana katika eneo la Gondoja-Ndablama. Hivyo Liberia ilikuwa ni nchi miongoni mwa nchi tajiri barani Afrika.

Sauti ya msichana mhudumu wa ndege ile tuliyoiabiri ikanizindua kutoka katika fikra zangu wakati alipowatangazia abiria wote kufunga mikanda ya siti tayari kwa kujiandaa kwa tukio la kutua kwenye kiwanja cha ndege cha James Spriggs Payne Airport kilichopo umbali wa kilometa tano kutoka jiji la Monrovia.

“Bahati iliyoje kufika nchi nzuri na tajiri kama hii”. Nikanong’ona huku nikifunga mkanda wa siti yangu kisha nikageuka na kumtazama Mariama aliyekuwa ameketi kando yangu. Sote tulikuwa na furaha au niseme labda Mariama alikuwa na furaha zaidi yangu kwa vile alikuwa akirudi nyumbani kwao kuonana tena na wazazi wake, ndugu, jamaa na marafiki.

“Na mimi nimefurahi kwa kuwa utafika nyumbani kwetu na kuwaona wazazi wangu. Kesho asubuhi baada ya kupata kifungua kinywa nitamuomba dereva wetu akatutembeze sehemu mbalimbali za jiji la Monrovia. Bila shaka utapenda kutalii jiji letu”. Mariama akaongea huku akioneka mwenye furaha isiyo na kifani.
“Bila shaka Monrovia itakuwa sehemu nzuri ya kukumbuka kabla ya kurudi nyumbani Dar es Salaam nchini Tanzania”. Nikaongea kwa furaha huku nikitabasamu kisha nikasogea karibu na kumbusu Mariama shavuni bila kujali abiria wengine waliokuwa kando yetu wakitukodolea jicho la wivu.
“Ahsante Tibba wangu”. Mariama akaongea kwa furaha huku akinitazama katika uso wenye tabasamu la ukarimu kisha akauchukua mkono wangu na kuuweka pajani mwake hali iliyonipelekea nipumbazike kidogo na tukio lile.

Mtikisiko kidogo ukatokea mle ndani ya ndege baada ya magurudumu ya ndege kutua ardhini, hata hivyo baada ya kitambo kifupi hali ya utulivu ikarejea. Hatimaye ile ndege ya shirika la ndege la Nigeria ikapunguza mwendo na kwenda kusimama mbele ya jengo kubwa la kiwanja cha ndege cha James Spriggs Payne katika runway ndefu iliyotiwa lami na kuwekwa michoro elekezi kwa rubani wa ndege.

Baada ya kufungua mikanda ya siti muda mfupi uliofuata tulikuwa katika foleni ya abiria waliokuwa wakishuka kiwanjani pale. Mariama hakutaka kuwa mbali nami hivyo akapenyeza mkono wake na kunishika kiunoni pasipo kujali macho ya watu.

Tuliposhuka kwenye ndege na kuingia kwenye ofisi za uhamiaji za kiwanjani pale ndiyo nikashtukia kuwa nilikuwa nimeongozana na mtu asiye wa kawaida. Maafisa uhamiaji kiwanjani pale kila mmoja alijitahidi kumpapatikia Mariama kwa namna yake na hapo nikakumbuka kuwa Mariama alikuwa mtoto wa waziri wa ulinzi wa pale Liberia hivyo heshima ile ilitokana na baba yake ambaye sasa nilimgundua kuwa alikuwa waziri maarufu sana pale Liberia.

Kupitia Mariama, viza na pasipoti zetu zikachukuliwa haraka na dada mmoja afisa uhamiaji na kwenda kushughulikiwa pasipo sisi kupanga foleni kama abiria wengine waliotua kiwanjani pale. Badala yake tukaombwa tusubiri kwenye viti vya maafisa uhamiaji vilivyokuwa mle ndani ofisini huku tukiletewa vinywaji vya kutuburudisha ambavyo si mimi wala Mariama aliyekuwa ameagiza. Kisha wale maafisa uhamiaji wakiwa wamesimama baada ya kutupisha viti vyao wakawa kila mmoja akijitahidi kumuongelesha na kumchangamkia Mariama kadiri alivyoweza.

Tabia ile ya kuthaminiwa kutoka na kuwa na unasaba na mtu fulani sikuipenda kwani abiria wengine hawakufanyiwa kama sisi lakini kwa kuwa nilikuwa mgeni katika nchi ya watu nikabaki nikizugazuga na kutabasamu pasipo kutia neno. Akili yangu ikajikita katika kutafakari ni kwa namna gani wazazi wa Mariama watanitathmini baada ya kunikaribisha nyumbani kwao. Mgongoni nilikuwa na begi langu dogo lenye nguo chache na mahitaji yangu muhimu. Mizigo yangu mikubwa yakiwemo mabegi ya nguo na vitabu nilikuwa nimeitanguliza jijini Dar es Salaam, Tanzania ili kuepuka usumbufu.

Uwanja wa ndege wa ndege wa James Spriggs Payne haukuwa na tofauti kubwa na viwanja vya ndege vingi vya barani Afrika. Kulikuwa na pilikapilika za wasafiri waliokuwa wakiingia na kutoka jijini Monrovia hata hivyo kutokana na kiwanja kile cha ndege kuwa na runway moja hivyo ndege zilizokuwa zikitua kiwanjani pale zilikuwa ni zenye ukubwa wa wastani wa kuchukua abiria wasiozidi mia mbili hamsini. Hali ya hewa ilikuwa ya baridi ya kiasi huku sehemu kubwa ya anga la Monrovia ikiwa imefunikwa kwa wingu zito la umande wa milimani na kuashiria kuwa muda wowote mvua ingeanza kunyesha.

Wakati wale maafisa uhamiaji pale uwanjani wa ndege wakikazana kumuongelesha Mariama mimi nilikuwa nikitazamana nje ya ofisi ile kupitia kwenye vioo dirishani. Ingawa macho yangu yalikuwa yamevutiwa sana na namna ndege ziliyokuwa zikitua na kuruka kiwanjani pale lakini akili yangu ilikuwa imejikita katika kuwafikiria wazazi wa Mariama. Nafsi yangu sasa ilikuwa ikitamani kuwaona ingawa sikufahamu wangekuwa na mtazamo gani juu yangu. Kwa namna nyingine niliona kuwa Mariama alikuwa ameharakisha sana kunikutanisha na wazazi wake. Hata hivyo nilipofikiri sikuona sababu yoyote ya kucheleweshwa kwa tukio lile kwa vile alikuwa ni msichana wa ndoto yangu.

Mandhari ya jiji la Monrovia yalikuwa yamenivutia sana na kuziteka haraka fikra zangu hivyo nikatamani zile taratibu za uhamiaji ofisini pale zifanyike haraka ili tuanze safari ya kuelekea nyumbani kwa akina Mariama kwani tukiwa njiani ningeweza kupata nafasi nzuri ya kuiona mitaa na barabara za jiji la Monrovia.

Nikiwa nimazama kwenye tafakuri ile huku macho yangu yameweka kituo dirishani kutazama nje, mkono laini ukanishika begani na nilipogeuka kutazama kando yangu nikamuona Mariama katika uso wake wa tabasamu la furaha na kando yake alisimama yule dada afisa uhamiaji aliyechukua nyaraka zetu za kusafiria na mwanaume mwingine mrefu na mweusi ambaye sikumfuhamu wala kumuona hapo awali. Kwa tabasamu la kiungwana yule dada afisa uhamiaji akaturudishia hati za uthibitisho wa kinga ya homa ya manjano, viza na pasipoti zetu.

“Karibu sana Liberia ndugu Tibba Ganza. Ni matumaini yangu kuwa utafurahia safari yako”
“Ahsante sana”. Nikaitikia kwa furaha huku nikipokea nyaraka zangu mkononi mwake ingawa macho yangu yaliweka kituo kumtazama yule mwanaume kando yake ambaye umri wake usingezidi miaka thelathini na mbili, mrefu na mweusi, mwenye uso wa umbo duara na sura ya tabasamu akiwa amevaa kwa unadhifu, shati la kitenge na suruali ya dengrizi.

“Jina langu naitwa Fatiama Kamara kila mtu ananifahamu hapa. Ni matumaini yangu kuwa tutaonana tena”. Yule dada afisa uhamiaji akajigamba huku akinipa mkono wake katika tabasamu pana la kirafiki kisha akageuka na kumtazama Mariama katika tabasamu la kuagana na kupitia tabia ile nikagundua kuwa Fatiama alikuwa msichana mcheshi sana.
“Nashukuru sana kukufahamu”.
Nikaongea kwa utulivu huku tukipeana mkono wa kuagana na afisa uhamiaji yule na macho yetu yalipokutana akanikonyeza kwa siri na kuniacha na mshangao. Hata hivyo nikashukuru kuwa Mariama alikuwa hajashtukia mchezo ule vinginevyo moto ungewaka palepale.

Hatimaye yule dada afisa uhamaji akatuacha na kurudi kwenye majukumu yake na hapo nikapata wasaha mzuri wa kumsindikiza kwa macho. Loh! alikuwa msichana mrembo sana mwenye umbo la kukata na shoka.

Sasa pale tukabaki mimi, Mariama na yule mwanaume mwingine ambaye uwepo wake eneo lile ulikuwa umeanza kuziteka fikra zangu. Macho yangu tayari yakiwa yameweka kituo kumtazama yule mwanaume mara Mariama akavunja ukimya.
“Tibba, huyu ni dereva wetu anaitwa John Varma amefika hapa kuja kutupokea”. Kupitia maelezo yale yule mwanaume akasogea na kunipa mkono wa karibisho huku tabasamu pana limechanua usoni mwake.
“Poleni na safari”. Yule dereva akavunja ukimya.

“Ahsante”. Nikawahi kumuitikia huku nikiusahili wajihi wake.
“Naomba mniwie radhi sana kwa kuchelewa kufika kuwapokea. Gurudumu moja la gari lilipata pancha wakati nikija hivyo nikatumia muda kulibadili”

“Oh! pole sana hata hivyo hajachelewa sana”. Nikamtia moyo.
“Varma, huyu ni mchumba wangu kutoka Tanzania, anaitwa Tibba Ganza. Tutakuwa naye nyumbani kwa siku kadhaa kabla ya kurudi kwao Tanzania”. Mariama akanitambulisha kwa yule dereva pasipo ukakasi wowote kwenye maelezo yale huku jino la mwisho katikati ya tabasamu lake likionekana bila kificho. Utambulisho ule ukawa umemshtua kidogo yule dereva hivyo haraka akageuka tena na kunipiga ukope anisahili kwa makini kabla ya kulegeza uso wake kwa tabasamu kisha kama ambaye amebabaika akanipa tena mkono wa heshima.

“Karibu sana Monrovia ndugu Tibba Ganza. Wazazi wa Mariama bila shaka watakuwa na shauku kubwa ya kukuona”

“Nashukuru sana ndugu Varma tayari nimeshakaribia”. Nikaitikia ukaribisho ule huku nikitabasamu. Moyoni sikuwa na shaka yoyote kuwa John Varma alikuwa ni afisa usalama wa taifa pale Liberia kwani nilifahamu kuwa katika serikali nyingi za nchi za Afrika ni nadra sana kukuta dereva wa kiongozi mkubwa wa serikali kama waziri asiwe ni mtu wa usalama wa taifa. John Varma hakurusu mjadala mrefu wa maongezi kuendelea baina yetu hivyo haraka akachukua mabegi yetu na kutuomba tumfuate.

Tulipotoka nje ya ile ofisi ya uhamiaji kiwanjani pale tukashika uelekeo wa upande wa kulia tukiifuata korido ndefu iliyokuwa ikipakana na ofisi mbalimbali za utawala wa kile kiwanja cha ndege. Wakati tukitembea Mariama akapitisha mkono na kunikumbatia kiunoni huku akitabasamu na hivyo kupelekea kila mtu tuliyepishana naye ageuke na kututazama.

Sote tulikuwa tumependeza sana kwa muonekano. Mariama yeye alikuwa amevaa suruali ya Jamsuit ya rangi ya maruni, viatu vya skuna za rangi nyekundu miguuni, miwani kubwa ya jua machoni, herini za almasi na begani alikuwa amening’iniza pochi yake nzuri ya ngozi ya mbega. Mimi nilikuwa nimevaa fulana nyepesi nyeupe, juu yake nilivaa shati la jeans la rangi ya samawati la mikono mirefu, na saa ya mkononi. Kichwani nilivaa kofia nyeusi ya kapelo na miwani myeusi ya jua. Japokuwa hapakuwa na jua lakini miwani ile sasa ilitumika kunikinga na macho ya watu waliokuwa hawachoki kututazama bila haya kila tulipoelekea. Chini nilivaa suruali ya kadeti ya rangi ya kaki na buti ngumu za ngozi miguuni. Mtu yeyote ambaye angetutazama kwa makini asingesita kudhani kuwa huwenda tulikuwa wamarekani weusi tuliyofika pale jijini Monrovia kwa minajili ya kutalii.

Muda mfupi uliofuata tukawa tumetokezea kwenye korido nyingine upande wa kushoto iliyokuwa ikipakana na ofisi mbalimbali za mashirika tofauti ya ndege, mikahawa ya kisasa, maduka ya kubadilishia fedha za kigeni, ofisi za mawakala wa kampuni za utalii na clearing and forwarding pamoja na maduka ya nguo. Kulikuwa na watu wachache mle ndani ya zile ofisi. Niligundua hivyo baada ya kuchungulia mle ndani kupitia kuta safi za vioo.

Mwisho wa ile korido upande wa kulia tukawa tumetokezea eneo la nyuma la ule uwanja wa ndege sehemu kulipokuwa na maegesho ya magari. Nilimuona John Varma akielekea kwenye gari moja jeupe aina ya Land Rover 101 na hapo nikajua kuwa lile ndiyo gari alilokuja nalo kutupokea pale kiwanjani hivyo bila kuuliza tukamfuata.

John Varma akafungua sehemu ya nyuma ya gari na kuweka mabegi yetu huku kwa heshima zote na tabasamu la kirafiki akatufungulia milango ya gari na kutukaribisha tuingie.

Tulipoingia safari ya kuondoka kiwanjani pale ikaanza. Kwa dakika zisizopungua tano tulisafiri katika barabara nzuri ya lami ya kutokea kiwanjani pale iliyopakana na milingoti ya taa za barabarani muda mfupi baada ya kuvuka geti kubwa lililokuwa likitazama na mzunguko wa barabara wenye bustani nzuri ya maua.
Barabara ile ilifunikwa na kivuli cha matawi makubwa ya miti ya kando yake. Mariama hakunisemesha kitu badala yake alikuwa amezama kwenye kutazama mandhari yale baada ya kutengana nayo kwa muda mrefu. Kwangu mimi mandhari yale yalikuwa mapya kabisa hivyo kila kitu kilinivutia kushangaa. Kupitia dirishani niliweza kuona milima mirefu iliyofunikwa kwa msitu mizito ya uoto wa asili na juu ya vilele vile niliona mawingu ya umande mweupe kana kwamba ndiyo kulikuwa kunapambazuka.

Tulipofika mwisho wa barabara ile nikamuona dereva akikunja kona kuingia barabara nyingine iitwayo Airfield shortcut katika mwendo wa wastani ulioturuhusu kuona vizuri mandhari ya nje. Niliona majengo mazuri ya makazi ya watu, ofisi za serikali na mikahawa ya kisasa iliyopakana na barabara.

Baada ya safari fupi hatimaye tukaja kukutana na barabara ya Tubman Boulevard kwa upande wa kushoto. Barabara ya Tubman Boulevard ilikuwa ni barabara kubwa na maarufu sana jijini Monrovia, labda kama ingelikuwa ni jijini Dar es Salaam nchini Tanzania ningeweza kuifananisha na barabara ya Mandela au barabara ya Morogoro. Niliona majengo marefu ya ghorofa kando ya barabara ile yaliyokuwa na maduka makubwa ya mjini, hoteli za kisasa, supermarket, vituo vya kujazia mafuta, ofisi za posta na benki.

Tulipoupita mkahawa mkubwa wa Sam’s Barbeque dereva akaongeza mwendo na hapo nikagutuka kuwa tulikuwa tukisafiri kuelekea upande wa kaskazini. Pilika za wakazi wa jiji la Monrovia zilikuwa mbioni kushamiri kwani mitaa mingi ilionekana kufurika watu, pikipiki na magari.

“Monrovia ni jiji zuri sana, mgeni yeyote ambaye ni mara yake ya kwanza kufika hapa ni lazima ashangae kidogo”. Nikavunja ukimya huku nikigeuka na kumtazama Mariama kando yangu.
“Nasikia hata Dar es Salaam ni jiji zuri sana japo sijawahi kufika”. Mariama akachombeza.

“Siku ukija Dar es Salaam utajionea mwenyewe kwa macho yako. Wacha mimi nisitie neno”. Nikaongea huku nikiangua kicheko hafifu. Dereva akatuchungulia kidogo kupitia kioo cha mbele cha mle ndani na macho yetu yalipokutana hakutia neno badala yake akayahamishia macho yake kutazama mbele.

“Karibu sana nyumbani mpenzi na sitarajii kuwa utaondoka mapema”. Mariama akaongea huku amenishika mkono na kunitazama katika uso wa kusubiria jibu zuri kutoka kwangu.
“Nikilowea huku si mwishowe mtanichoka”. Nikaongea huku nikiangua kicheko dhaifu.

“Siwezi kukuchoka mpenzi kwani wewe ndiye kila kitu kwangu”. Mariama akaongea kwa sauti ya kubembeleza huku ameniegemea begani.
“Wasiwasi wangu ni juu ya wazazi wako”

“Waiwasi wa nini?”. Mariama akauliza kwa shauku huku akigeuka kunitazama.
“Huwenda wasipendezwe na mimi”. Nikachombeza utani.
“Mh! kuhusu hilo shaka ondoa kwani nimekumwagia sifa kemkem kwao”
“Sifa gani?”

“Kuwa wewe ndiye mwanaume wa ndoto yangu na furaha ya moyo wangu”. Mariama akaninong’oneza sikioni kana kwamba hakupenda yule dereva amsikie. Sote tukaangua kicheko hafifu cha furaha huku tukichagizwa kidogo na myumbo wa gari na hapo nikauweka mkono wangu begani kwa Mariama kumkumbatia.
Tabasamu lingali linaelea usoni mwangu mawazo yangu yakasafiri taratibu wakati nilipoyapeleka macho yangu kutazama nje kupitia dirishani. Hatimaye macho yangu yakaweka kituo kuitazama hoteli ya The Royal Grand iliyokuwa upande wa kulia wa barabara ile ikitazamana na barabara ya 15th Street kwa upande wa pili wa barabara.

Tulipofika barabara ya 9th Street upande wa kulia nikaona jengo la benki ya LBDI kisha mbele kidogo dereva akaongeza tena mwendo kuovateki lori la mafuta lililokuwa mbele yetu. Upande wa kushoto tukaupita mkahawa mkubwa uitwao Rangoli halafu tulipofika mbele upande wa kulia nikauona mkahawa mwingine uitwao Bella Casa mkabala na jengo kubwa la ghorofa la United Nations Mission in Liberia.

Tulipovuka eneo lile dereva akakunja kona na kushika uelekeo wa kaskazini magharibi katika barabara ya Tubman Boulevard tukipishana na magari mengi katika barabara ile.

Baada ya safari fupi katika barabara ile upande wa kulia nikayaona majengo ya chuo kikuu cha Our Lady of Lebanon St. Joseph Parish halafu baada ya mwendo mfupi tukayafikia makutano ya barabara ya Haile Selassie Avenue kwa upande wa kulia na barabara ya Camp Johson.

Tulipoyafikia makutano yale upande wa kulia nikaona majengo ya ghorofa ya Universirty of Liberia. Dereva akaingia kwenye mzunguko wa barabara ile na kushika uelekeo wa upande wa kushoto akiifuata barabara ya Camp Johnson. Ilikuwa barabara ya kisasa ya lami isiyokuwa na msongamano ikikatisha kandokando ya jiji la Monrovia.

Baada ya kitambo kifupi cha safari katika barabara ile mara nikahisi dereva alikuwa akipunguza mwendo na wakati nikiyatembeza macho yangu kutazama huku na kule mara nikaona tukichepuka na kuingia upande wa kushoto kuifuata barabara ya United Nations Drive. Barabara iliyopakana na ofisi za mashirika makubwa ya kimataifa duniani kama ofisi za UNHCR, WHO, FAO, UNICEF, Amnesty International, Human Right watch, ofisi za OAU na nyinginezo.

Kulikuwa na utulivu wa hali ya juu katika barabara ile na hata msongamano wa watu na magari haukuwepo. Nilipotazama dirishani upande wa kushoto nikaona eneo la viwanja vya wazi vya michezo liitwalo Barclay Training Center. Kisha baada ya mwendo mfupi nikauona uwanja wa mpira wa miguu maarafu jijini Monrovia uitwao Antoinette Tubman Stadium upande wa kulia.

Mbele kidogo baada ya kuupita uwanja ule dereva akapunguza mwendo na kuingia upande wa kulia akiifuata barabara ya Center Street kisha baada ya kitambo kifupi cha safari akakunja kona tena kuingia upande wa kushoto akiifuata barabara ya Sekou Toure Avenue upande wa kulia tukilipita jengo kubwa la Abi Jaoudi Supermarket katikati ya mtaa wa Gurley upande wa kulia na mtaa wa Randall upande wa kushoto. Muda mfupi uliofuata mara dereva akaanza kupunguza mwendo kama tunaokaribia kusimama.

“Tumekaribia kufika mpenzi”. Sauti ya Mariama ikanirudisha tena mle ndani na hapo nikageuka na kumtazama kwa shauku.

“Huu ni mtaa wa Sekou Toure Avenue, nyumba yetu ni ile pale mbele yenye geti jeusi”. Mariama akaongea kwa furaha huku akinivuta karibu yake na kunionesha kwa kidole geti jeusi lililokuwa upande wa kushoto na hapo tabasamu jepesi likachanua usoni.

Mtaa wa Sekou Toure Avenue ulistahili kuwa na makazi ya kiongozi yoyote wa ngazi ya juu wa serikali ya Liberia kwa vile majumba yote yaliyokuwa yakipakana na ile barabara yalikuwa ya kifahari yaliyozungukwa na kuta ndefu na mageti makubwa mbele yake. Kulikuwa na miti mizuri ya kivuli kando ya barabara ile na magari machache yalikuwa yameegeshwa. Ilikuwa barabara pana ya lami yenye usafi wa hali ya juu.

Hatimaye dereva akasimama nje ya lile geti jeusi kisha akapiga honi mara mbili. Haukupita muda mrefu mara nikaona lile geti likifunguliwa na wanajeshi wawili walioshika bunduki zao mikononi. Gari lilipoingia lile geti likafungwa nyuma yetu. Nilipogeuka kutazama nyuma nikawaona wanajeshi wengine wanne kwenye kibanda cha mlinzi mle ndani kando ya lile geti.

Baada ya kitambo kifupi cha kusafiri katika barabara ya vitofali iliyopakana na bustani nzuri ya maua, miti ya kivuli na nyasi za kijani kibichi lile gari likasimama mbele ya ngazi pana za jumba kubwa la kifahari la ghorofa mbili lenye nguzo mbili kubwa sehemu ya mbele. Sote tukiwa na furaha Mariama akageuka na kunibusu shavuni.

“Tumefika mpenzi. Hapa ndiyo nyumbani. Karibu sana Monrovia”
“Ahsante sana Mariama. Loh! hapa mahali ni pazuri sana”. Nikachombeza huku nikiyatembeza macho yangu nje kutazama mandhari ile ya kuvutia. Muda uleule mara nikaona mlango wa mbele wa lile jumba ukifunguliwa kisha akatoka mwanamke mmoja nadhifu na mrefu ngozi yake rangi ya maji ya kunde amevaa vazi la kitenge lililoshonwa na kudariziwa vizuri na kilemba kikubwa kichwani.

Nyuma yake mwanamke yule akafuatiwa na mwanaume mrefu mweusi aliyevaa joho la kitenge lililodariziwa vizuri shingoni kwa nyuzi za dhahabu, machoni amevaa miwani na bakora yake ya heshima mkononi. Mwanaume mwenye ndevu nyingi zilizompendeza kukizunguka kidevu chake. Sikuhitaji kuambiwa kuwa wale walikuwa wazazi wa Mariama kwa namna walivyofanana na binti yao. Wote walikuwa katika nyuso za furaha wakiharakisha kuja kutulaki.

Kwa furaha Mariama akafungua mlango kisha akanishika mkono kwa maringo akinitaka nishuke na kumfuata. Sikuwa na pingamizi hivyo nikashuka kwa nidhamu zote kisha tukapanda zile ngazi. Kabla hatujafika wazazi wa Mariama wakatufikia na kutulaki kwa bashasha zote ijapokuwa kwa binti yao ilikuwa ni zaidi.

Mariama hakuweza kuvumilia kwa kihoro cha furaha akawarukia baba na mama yake akiwasalimia kwa furaha baada ya kitambo kirefu kupita akiwa mbali nao. Nikasimama kando huku nikitabasamu na kupendezwa sana na upendo ule wa familia. Kabla sijatia neno Mariama akageuka kwa tabasamu pana na kuvunja ukimya.
“Tibba karibu sana nyumbani. Hawa ndiyo wazazi wangu, baba na mama yangu”. Mariama akanitambulisha huku ni mwenye furaha.
“Ahsante sana. Nashukuru sana kuwafahamu”. Nikaongea kwa utulivu na heshima kisha nilipoyatoa macho yangu kwa Mariama nikayapeleka kwa wazazi wake na kuwapa mkono.
“Shikamooni wazazi”


“Marahaba. Karibu sana kijana”. Wote wakaitikia kwa pamoja.
“Ahsanteni”


“Baba na mama, huyu ndiye mchumba wangu anaitwa Tibba Ganza kutoka Tanzania”. Loh! maneno ya Mariama yakanitia tumbo joto kwa vile sikujua ningechukulika vipi hata hivyo nilijikaza kisabuni huku nikizuga kwa tabasamu.
“Oh! karibu sana kijana na ujisikie upo nyumbani wakati wote utakapokuwa nasi hapa nyumbani Monrovia”. Baba yake Mariama akanikaribisha kwa tabasamu pana huku akinipa tena mkono.

“Nashukuru sana wazazi wangu”
Kwa kweli mapokezi ya wazazi wa Mariama pale nyumbani yalikuwa yamenifariji sana na kupitia sura zao za furaha nikamaizi mazingira mazuri ya upendo na urafiki baina yetu. Mariama alipomaliza kusalimiana na wazazi wake, baba na mama wakanikaribia pale niliposimama na pasipo kutia neno wakanipa mkono wa karibisho la heshima. Ama kweli walifanana sana na binti yao. Umri wao ungeweza kuwa kati ya miaka arobaini na tano na hamsini na tano hata hivyo sikuweza kufahamu kwanini hawakuwa na mtoto mwingine wakati wa ujana nao.


Wakati nikiendelea kusalimiana na wazazi wa Mariama mara nikawaona vijana watatu wakitoka kwenye ile nyumba na kuja kutulaki na nilipowatupia jicho kuwasahili haraka nikamaizi kuwa wangekuwa wahudumu wa pale nyumbani. Walipotufikia wakatupa mkono wa karibisho kwa heshima zote kisha wakachukua mabegi yetu na kuingia nayo ndani.

Pale nje maongezi hayakudumu sana badala yake tukakaribishwa ndani. Wanajeshi walinzi na wanausalama wa jumba lile huwenda walishikwa na butwaa wasijue lolote kuhusu mimi wakati walipositisha shughuli zao wakinishangaa hata hivyo hakuna aliyetia neno.

Ndani ya lile jumba tulipoingia nikagundua kuwa kulikuwa kumefanyika maandalizi ya hali ya juu na wazazi wa Mariama kufuatia ujio wetu. Wakati Mariama akiwa amezama kwenye maongezi na mama yake, mimi na baba tuliketi pale sebuleni kwenye kochi moja la sofa tukizidi kufahamiana zaidi. Kwa kweli hofu ya ukweni ilipungua na hapo nikajikuta nikivutiwa sana na familia ile. Baba yake Mariama alikuwa mtu mcheshi sana mwenye kuheshimu watu. Lakini vilevile niligundua kuwa alikuwa ni mtu mwenye busara ya hali ya juu na mwenye ufahamu mkubwa katika masuala ya utawala serikalini na migogoro ya nchi za Afrika.

Kupitia maongezi ya baba yake Mariama ambaye sasa nilimtambua kama waziri wa ulinzi wa Liberia niliweza kufahamu namna umoja wa Afrika OAU ulivyokuwa umepiga hatua kubwa katika kufanikisha ukombozi wa bara la Afrika kutoka katika utawala wa mabeberu. Umoja huo ukitiwa nguvu na baadhi ya viongozi wazalendo, shupavu na mashuhuri kama Mwalimu J.K Nyerere, Kwame Nkurumah, Jomo Kenyatta, Samora Machel, Robert Mugabe, Ahmed Ben Bella, Patrice Emile Lumumba, Nelson Mandela, Keneth Kaunda na wengine wengi.

Huku akinieleza baadhi ya changamoto zilizokuwa zikiukabili umoja huo kama ukosefu wa fedha, uchumi dhaifu wa nchi za Afrika, kukosekana kwa wasomi wa kutosha na viongozi imara na wimbi la vibaraka wapinga ukombozi ambao kwa ufinyu wa akili zao bado wamekuwa waumini katika dini isiyoamini ukombozi huru wa bara la Afrika kutoka kwa wakoloni wanyonyaji.

Maongezi ya baba yake Mariama yaliniingia vyema na kwa kweli nikiwa kijana mzalendo wa nchi yangu Tanzania na bara la Afrika kwa ujumla nikajikuta nikifarijika sana kukutana na mzalendo yule kindakindaki wa bara la Afrika.

Mchana ule tulizungumza mambo mengi sana juu ya bara la Afrika na harakati za ukombozi huku baba yake Mariama akinieleza namna serikali ya Liberia chini ya rais William R.Tolbert Jr ilivyokuwa mstari wa mbele katika kuwaletea maendeleo wananchi wake. Kwa kweli nilijisikia nipo nyumbani kwani wazazi wa Mariama walikuwa wakarimu sana na zaidi ya hayo walikuwa wamefarijika sana kwa kufika kwangu.

Mchana ule tukapa mlo wa pamoja katika meza kubwa iliyokuwa katika ukumbi wa chakula wa pale nyumbani huku Mariama akiitumia vyema nafasi ile kunitambulisha rasmi kwa wazazi wake. Kwa kweli ilikuwa ni siku ya furaha sana kwetu sote kwa vile wazazi wa Mariama hawakuwa na pingamizi lolote dhidi yangu badala yake wakatangaza kunipa nafasi ya mtoto wao pekee wa kiume kwa vile hawakuwa na mtoto wa kiume na mimi nikawashukuru sana. Tulipomaliza kupata mlo tukaendelea na maongezi ya hapa na pale tukizidi kufahamiana zaidi.

Jioni ile ilipofika wazazi wa Mariama wakatuaga kuwa wanaelekea ikulu kuhudhuria tafrija ya kitaifa iliyoandaliwa na rais kwa ajili ya mapokezi ya mabalozi wapya kutoka mataifa mbalimbali walioteuliwa kuziwakilisha nchi zao jijini Monrovia.
Pale nyumbani tukabaki mimi, Mariama, ndugu wawili wa familia yao, wahudumu wa mle ndani na wale wanajeshi sita waliokuwa wakilinda maskani ile. Mariama akatumia muda ule kunitembeza sehemu mbalimbali nje na ndani ya lile jumba ambalo sasa ningeweza kulifananisha na kasri ya mfalme.

Lilikuwa jumba kubwa la ghorofa na zuri lenye vyumba saba vya kulala vyenye vitanda nadhifu vya samadari, sebule mbili zenye umbo duara chini na juu, ukumbi wa chakula, sehemu ya ghorofani ya kubarizi yenye kochi za sofa, maliwato na jiko kubwa la kisasa.
Sebule ya chini mandhari yake ilipambwa kwa seti mbili za makochi ya sofa. Katikati ya sebule ile kulikuwa na meza fupi ya msonobari ya umbo mstatili juu ya kipande kidogo cha zulia la rangi ya kahawia. Kwenye kona ya sebule ile yenye madirisha mawili makubwa yaliyofunikwa pazia ndefu nyepesi za kuvutia kulikuwa na sistimu nzuri ya muziki wa Jvc. Ukutani kulitundikwa picha nzuri zilizochorwa kwa ustadi katika mazingira ya Afrika. Pia kulikuwa na picha nyingine za familia zilizopigwa katika mazingira tofauti, baadhi zilimuonesha baba yake Mariama akiwa na rais William R. Tobert Jr.

Nyingine akiwa na baadhi ya viongozi wa serikali katika hafla tofauti.
Kupitia madirisha makubwa ya sebule ile mtu yeyote ambaye angeketi pale sebuleni angeweza kuona mandhari nzuri na tulivu ya miti ya kivuli, nyasi zilizokatiwa vizuri za kijani kibichi na bustani ya maua ya kupendeza katika sehemu ya kupumzikia iliyokuwa eneo la nyuma la lile jumba kando ya bwawa kubwa la kuogolea.

Upande wa kushoto wa ukumbi wa kulia chakula kulikuwa na chumba kidogo chenye rafu za vitabu na mafaili yaliyopangwa vizuri. Kwenye kona ya chumba kile ambacho sasa ningekiita maktaba ya nyumbani kulikuwa na meza ya kusomea yenye taa nzuri ya lampshade iliyozungukwa na viti vinne vya sufi. Kwenye kona ya meza ile kulikuwa na simu ya mezani. Pembeni ya maktaba ile niliona mlango wa chumba.

Kilikuwa chumba maalum kwa wageni hivyo yale ndiyo yangekuwa makazi yangu kwa muda hadi siku nitakapoondoka kurudi kwetu jijini Dar es Salaam, Tanzania. Nilipenda kupunguza uchovu mwilini hivyo nilipoingia mle ndani nikaoga na kubadili nguo.
_____
KELELE ZA MUITO WA SIMU zilinishtua haraka kutoka usingizini pamoja na uchovu mwingi niliokuwanao. Nikatupa blanketi kando na kutega vizuri sikio. Katikati ya giza nene la mle chumbani nisingeweza kufahamu haraka kuwa muda ule ungekuwa saa ngapi. Hata hivyo nikahisi kuwa ulikuwa usiku wa manane labda saa saba au saa nane usiku kwa vile hali ilivyokuwa tulivu.


Nikakumbuka kuwa nilikuwa na Mariama mle chumbani tukiiba penzi kwa siri mara baada ya kuagana na wazazi wake na kila mmoja kuelekea chumbani kwake kulala muda mfupi baada ya kumaliza kupata mlo wa pamoja wa usiku ule mara tu baada ya wazazi wa Mariama kurudi toka kwenye tafrija ikulu.

Nikakumbuka kuwa mara baada ya penzi lile zito Mariama alikuwa ameniaga na kwenda chumbani kwake kulala na kwa kuwa nilikuwa hoi sijiwezi kwa uchovu sikuwa na namna hivyo Mariama alipotoka na kurudishia mlango wa chumba changu nikazima taa na kujitupa kitandani na baada ya kujifunikwa blanketi sikuweza kufahamu ni wakati gani usingizi ulifanikiwa kuniteka nyara pale kitandani.


Ile simu ikaendelea kuita na hapo nikaupeleka mkono wangu juu ya stuli iliyokuwa kando ya kitanda kuichukua saa yangu ya kijasusi mkononi. Nilipobofya kitufe cha mwanga kutazama majira katika saa ile nikagundua kuwa tayari ilikwishatimia saa nane na robo usiku. Kwa vile nilikuwa sijalala vizuri sambamba na uchovu mwingi niliokuwanao usingizi ulikuwa umeziteka vibaya mboni zangu hata hivyo macho yangu yalijitahidi kwa kila namna kupambana na hali ile.
Muda ulikuwa umesonga sana kwa mtu yeyote kupiga simu ya kawaida usiku wa manane kama ule. Ingawa nilikuwa bado mgeni kwenye lile jumba na taratibu zake lakini hisia zangu ziliamshwa na simu ile ya usiku wa manane, nafsi yangu nayo ikapata shauku ya kutaka kufahamu kuwa simu ile ya usiku wa manane ilikuwa imebeba ujumbe gani.


Ile simu ikaendelea kuita mara kadhaa bila kupokelewa na hatimaye ikakata. Tukio lile likanipelekea nitupe kando blanketi nililojifunika pale kitandani na kushuka chini kisha hatua zangu dhaifu zilizotawaliwa na usingizi zikanichukua hadi kwenye dirisha kubwa la kile chumba. Pale dirishani nikasogeza pazia kando na kuchungulia nje. Mwanga wa taa za nje za lile jumba ukaniwezesha kuona bwawa kubwa la kuogelea katikati ya bustani ya miti ya kivulia na maua mazuri ya kupandwa. Nyuma ya bwawa lile sikuweza kuona vizuri kufuatia giza kubwa lililotanda.
Upepo wa usiku uliokuwa ukivuma ulitengeneza sauti ya mvumo wa ajabu kwenye matawi ya miti ile kadiri yalivyocheza huku na kule kwa utulivu kama sauti ya chatu mkali aliyehisi hatari kichakani. Hisia mbaya zikapenya haraka akilini mwangu hali iliyonipelekea ghafla nianze kuyachukia mazingira yale. Upepo ule uliovuma ukalisongasonga pazia pale dirishani niliposimama na kunipelekea nihisi kuwa macho ya mchawi yalikuwa sehemu fulani juu ya miti ile ya nyuma ya lile jumba yakinitazama kwa makini. Sikuwaona wale wanajeshi walinzi wala mbwa wao hata hivyo niliamini kuwa ulinzi makini ulikuwa eneo lile.


Kitambo kifupi cha ukimya kilipopita ile simu ikaanza kuita tena na kunishtua hali iliyonipelekea nigeuke haraka na kuutazama mlango wa chumba changu. Katikati ya hali ile mara nikasikia hatua za haraka za mtu akishuka ngazi kutoka ghorofani. Nilipotega vizuri sikio langu nikagundua kuwa hatua zile zilikomea ghafla kwenye kile chumba cha jirani cha maktaba kilichokuwa kando ya sebule. Simu ile ilipopokelewa tayari sikio langu lilikuwa kwenye tundu la kitasa mlangoni na hapo nikaisikia sauti ya Mariama ikizungumza na mtu wa pili kwenye ile simu. Maongezi yale yakanishtua kidogo kwa namna yalivyokosa utulivu na hapo nikahisi jambo la hatari nisilokuwa na hakika nalo.


Ile simu ilipokatwa nikazisikia hatua za Mariama zikikaribia chumba changu na hatimaye kukomea mlangoni na kwa kuwa ule mlango haukuwa umefungwa Mariama akaufungua kwa pupa. Tayari nilikuwa kitandani nimejifunika blanketi gubigubi kama niliyemezwa na usingizi mzito wa mkesha wa siku tatu. Sikupenda Mariama anikute macho kwa kukwepa kutengeneza maswali kichwani mwake ingawa milango yangu ya fahamu ilikuwa makini kama mbwa wa polisi.
“Tibba…Tibba…”. Nikamsikia Mariama akiniita kwa sauti ya chini na namna ya uitaji wake ikanitahadharisha kuwa mambo hayakuwa shwari. Labda alikuwa akiniletea taarifa mbaya ya msiba au ajali ya kutisha.

Nikawaza hata hivyo sikuchelewa kuitika mwito ule huku nikiliondosha blanketi kichwani na kumtazama kwa shauku.
“Mariama mpenzi kuna nini?”. Nikamuuliza kwa hadhari.
“Amka Tibba tafadhali”
“Kuna nini mpenzi?”. Nikatupa kando blanketi na kusimama nikimkodolea macho Mariama.
“Taarifa mbaya”. Mariama akanisogelea huku macho yamemtoka kwa hofu.

“Taarifa gani mbaya?”. Nikamsogelea na kumshika mkono huku nikimtazama kwa makini baada ya kuwasha taa ya mle ndani.
“Kumefanyika mapinduzi ya kijeshi”. Mariama akaongea huku akiiogopa sauti yake.

“Wapi?”. Nikauliza kwa shauku.
“Mapinduzi ya kijeshi yamefanyika hapa nchini na rais William Tolbert ameuwawa ikulu kwa kupigwa risasi muda mfupi uliopita”. Mariama akaongea mikono yake kaiweka kichwani hofu na mashaka vimemtawala na macho yake yakiwa mbali na utulivu huku mdomo ukimchezacheza kwa hofu. Umbo lake matata katika vazi lake jeupe na jepesi la kulalia na chupi yake nyekundu likanipelekea niweke kituo kumtazama kwa utulivu. Taarifa zile zilikuwa zimeniacha mdomo wazi kwa sekunde kadhaa huku zikishindwa kujisajili vizuri kichwani mwangu.

“Nani aliyekupasha taarifa hizi?”. Nikauliza.
“Rafiki wa karibu wa baba ambaye ni meya wa jimbo hili”
“Loh! hizi ni taarifa za kuogopesha sana”. Nikaongea huku nikitafakari.
“Nina wasiwasi huwenda jambo baya likamtokea baba na mawaziri wenzake katika serikali iliyopinduliwa”. Mariama akaongea kwa tahadhari.

“Ni vizuri ukamuamsha na kumueleza haraka iwezekanavyo”. Nikatoa rai yangu huku mawazo yakianza kupita kichwani mwangu. Kwa upande mwingine nilianza kujiona kama mtu mwenye mkosi kwa kukaribishwa nchi ya ugenini na tukio la mapinduzi ya kijeshi. Taratibu nikaanza kubashiri hatari iliyokuwa mbele yangu na baada ya kupisha tafakuri fupi nikavunja ukimya.

“Nani aliyehusika na mapinduzi haya?”
“Samuel Gbaydee Doe, askari jeshi mwenye cheo cha Koplo akiwa na kikundi cha wanajeshi wachache amevamia ikulu na kumuua rais kwa kumpiga risasi muda mfupi uliopita usiku huu”. Maelezo ya Mariama yakasababisha ganzi isambae taratibu moyoni mwangu na hapo hofu ikaanza kunitawala…

RIWAYA: MTUTU WA BUNDUKI
SEHEMU: 3

“Mapinduzi ya kijeshi ni jambo la hatari sana Mariama. Nenda haraka chumbani kwa baba na mama uwagongee na kuwapasha habari hizi”. Bila ya kuchelewa Mariama akafungua mlango na kutoka nje. Usingizi na uchovu niliokuwa nao vikatoweka haraka. Wasiwasi ukiwa umeniingia nikaanza kubashiri hatari iliyokuwa mbele yangu. Mara nyingi mapinduzi ya kijeshi yanapofanyika na rais kuuwawa mhimili wote wa serikali iliyokuwa madarakani hupoteza muelekeo na viongozi wake hugeuka na kuwa wahanga namba moja dhidi ya serikali ya kijeshi iliyojisimika kibabe madarakani. Hivyo sikuwa na shaka yoyote kuwa muda mfupi kuanzia pale familia ile ingekuwa hatarini.

Sikutaka kupoteza muda hivyo haraka nikaanza kujiandaa nikibadili nguo na kuweka vitu vyangu muhimu kwenye begi langu la mgongoni. Nilipomaliza nikafungua mlango wa chumba na kuelekea sebuleni. Nilimkuta Mariama, baba na mama yake wakiwa wamesimama pale sebuleni wakishauriana jambo na waliponiona wakageuka na kunitazama kwa mashaka.
“Shikamooni wazazi”
“Marahaba”. Wote wakatikia wakati nikiwafikia.
“Poleni kwa kuamshwa usingizini”
“Tushapoa”. Mama akaitikia.
“Ningewaomba mjiandae haraka iwezekanavyo tunatakiwa kuondoka hapa nyumbani kabla mambo hayajakuwa mabaya zaidi”. Nikawatahadharisha. Ilikuwa kama amri lakini yenye heshima nikamuona baba yake Mariama akinikata jicho kama afikiriaye jambo.

“Hatuendi kokote kijana!”. Sauti yake ilikuwa kali na yenye mamlaka hata hivyo mzee yule hakutambua hatari iliyokuwa mbele yake. Jibu lile likanipelekea mshangao kidogo kisha kwa tahadhari nikayatembeza macho yangu kijeshi kuwatazama mmoja baada ya mwingine kabla ya kuvunja ukimya.

“Kumefanyika mapinduzi ya kijeshi muda mfupi uliopita na rais ameuwawa kwa kupigwa risasi. Hii ni ishara tosha kuwa hakuna kiongozi mwingine kwenye nchi hii anayeheshimika wala kusikilizwa kwa wakati huu. Kama wanamapinduzi wameweza kumuua rais basi mawaziri wake pia ni sehemu ya kifo hicho. Hivyo kama hatutaondoka hapa haraka ni dhahiri kuwa sote tutavamiwa na kuuwawa humu ndani”. Nikaweka kituo huku nikiyatathmini kama maelezo yangu kama yangekuwa yamewaelea vizuri.

“Mimi kama waziri wa ulinzi wa nchi hii siwezi kukimbia nchi wakati hata kiini cha mapinduzi yenyewe ya kijeshi sikifahaamu”. Baba yake Mariama akaongea kwa kujiamini.

“Utawala mpya wa kijeshi umeshaingia Ikulu na kujisimika madarakani hivyo nafasi yako haipo tena kwenye uongozi huu mpya wa kijeshi. Kuuwawa kwa rais ambaye ndiye amiri jeshi mkuu ni ishara tosha kuwa uongozi wake hautambuliwi tena. Hivyo kwa tafsiri ya haraka ni kuwa kila kiongozi aliyekuwa kwenye serikali iliyopinduliwa tayari ameshakuwa adui namba moja wa serikali ya kijeshi iliyoshika hatamu kwa mapinduzi ya umwagaji damu wakati huu. Hatua inayofuata sasa ni kukamatwa kwa viongozi wote muhimu wa serikali iliyopinduliwa, kuteswa na hatimaye kuuwawa na wewe ni miongoni mwao. Ndiyo maana nikasema tunatakiwa kuondoka hapa haraka iwezekananvyo”. Nikaweka kituo huku nikimtazama baba yake Mariama. Nikamuona akizama kwenye tafakuri na hapo nikahisi maelezo yangu yalianza kumuingia.

Ghafla wakati maongezi yale yakiendelea kelele za risasi zilizofyatuliwa jirani na jumba lile zikasikika na kusababisha mtafaruku mle ndani. Wote wakageuka kwa hofu na kunitazama kana kwamba nilikuwa nabii pekee niliyesalia hapa duniani.
“Tunaelekea wapi?”. Baba yake Mariama akaniuliza kwa mashaka.
“Jiandaeni haraka tuondoke. Hapa si mahali salama tena”.
Nikawatahadharisha huku nikipuuza swali lile. Mara hii hakuna aliyetaka mjadala badala yake kila mtu akaelekea haraka chumbani kwake kujiandaa. Wakati baba yake Mariama akiondoka pale sebuleni nikakumbuka kumuuliza.
“Una silaha yoyote ya moto humu ndani?”
“Nina bastola moja aina ya UZI silenced”
“Ina risasi?”
“Ndiyo”
“Ichukue huwenda ikatusaidia mbele ya safari”
“Sawa”
“Chukua na nyaraka zako zote muhimu za ofisini pamoja na fedha kama utakuwanazo kwani huwenda zikatusaidia huko tuendako”
“Nina fedha kidogo hapa nyumbani. Pesa zangu nyingi zipo kwenye akaunti ya benki”

“Chukua na vitabu vyako vyote vya benki”. Maelezo yangu yakampelekea baba yake Mariama atingishe kichwa kuonesha kunielewa kisha haraka akaelekea chumbani.

Nikiwa nimebaki peke yangu pale sebuleni ghafla nikashtushwa na sauti ya kishindo kikubwa mbele ya lile jumba kisha muda uleule kukafuatiwa na majibizano makali ya risasi kati ya walinzi wa mle ndani na wavamizi. Nikawahi haraka kujitupa chini kisha kwa kasi ya komando nikatambaa sakafuni hadi kwenye kona ya sebule ile ukutani sehemu kulipokuwa na mainswitch ya umeme wa lile jumba. Nikafyatua swichi na kuzima umeme. Sasa giza nene likawa limetawala mle ndani.

Tukio lile la kuzimika ghafla kwa umeme likawapelekea watu wote wa mle ndani waingiwe na hofu na hapo kila mmoja akatoka chumbani kwake na kukimbilia pale sebuleni.
“Tumevamiwa. Tafadhali misipige kelele”. Nikawaonya gizani huku nikinyata kwa tahadhari na kuchungulia nje kupitia dirishani. Mwanga wa kutoka kwenye taa zilizokuwa juu ya nguzo mbili za geti la nyumba ya jirani ukaniwezesha kuona mbele ya lile jumba. Geti la mbele la lile jumba tulilokuwa lilikuwa limefunguliwa kibabe kwa kugongwa na ngao ya gari la jeshi aina ya Jeep iliyoendeshwa kwa kasi na kuvamia mle ndani.

Niliwaona wanajeshi watatu wakiruka chini kutoka kwenye gari lile na mmoja aliyesalia juu ya gari alikuwa amekamata kitako cha machinegun yenye mkanda wa risasi iliyokuwa ikitema cheche na kutupa risasi kila eneo mle ndani kana kwamba mlengaji alikuwa amepandwa na wazimu kichwani. Walinzi wa mle ndani walijitahidi kujitetea kwa kujibu mapigo lakini hawakufua dafu kwani lilikuwa ni shambulizi baya la kushtukiza.

Sasa sikuwa na shaka yoyote kuwa tayari mambo yalikuwa yameharibika. Kwa sekunde kadhaa nikawa ni kama niliyepigwa na butwaa nikishindwa kuamini kilichokuwa kinatokea eneo lile. Yale majibizano ya risasi hatimaye yakakoma na hapo nikasikia kelele za watu wawili wakilalama kwa maumivu makali kule nje gizani. Muda uleule nikamsikia mwanajeshi mmoja miongoni mwa wale walioruka kutoka kwenye lile gari la jeshi Jeep akitoa amri kwa mwenzake.

“Wamalize wote!”
Muda uleule nikasikia milio miwili ya risasi kisha zile sauti za wale watu waliokuwa wakilalamika kwa maumivu zikakoma na eneo lile la nje likagubikwa na ukimya na hapo nikajua walinzi wa mle ndani wote walikuwa wameuwawa. Nikiwa nimeshangazwa na tukio lile nyuma yangu gizani nikamsikia mama yake Mariama na dada wa kazi wakiangua kilio cha hofu.
“Nyamazeni na mlale chini”.
Nikawatahadharisha huku nikiendelea kutazama kule nje. Mara nikawaona wanajeshi wawili kati ya wale wanajeshi wanne waliovamia mle ndani na kuvunja geti wakimburuta mwenzao mabegani hadi nyuma ya ile Jeep. Walipofika wakambeba na kumuweka kule nyuma huku akilalama sana kufuatia maumivu makali ya risasi za walinzi zilizompata.
Mwanajeshi mmoja ambaye ndiye alikuwa dereva wa lile gari akachukua kipaza sauti kisha kwa sauti ya amri akaanza kutangaza.

“Tunajua kuwa upo humo ndani na familia yako. Wote tokeni nje huku mikono mmeiweka kichwani na atakayekaidi amri hii ataona cha mtemakuni”

Haraka nikageuka na kumtazama baba yake Mariama gizani. Ingawa hatukuonana vizuri lakini niliweza kuhisi hofu aliyokuwa nayo mzee yule.
“Nitajitokeza najua wana haja na mimi. Nisingependa waidhuru familia yangu”. Baba yake Mariama akaongea kwa hofu.

“Usithubutu kufanya hivyo kwani watatuua sote humu ndani”. Nikageuka nyuma haraka na kumuonya baba yake Mariama.

“Unadhani kwa kutokutii amri yao ndiyo tutakuwa salama?”. Akaniuliza.
“Tunapaswa kufikiria namna nyingine ya kujiokoa na siyo kujisalimisha kwani huu ni mtego wa kifo ulioandaliwa”. Nikamuonya.

“Nyinyi bakini humu ndani wacha mimi nijitokeze. Hawawezi kuniua”. Nimisikia baba yake Mariama akasisitiza nyuma yangu na kabla sijatia neno akaanza kuondoka akielekea mlangoni. Tayari nilikwishaiona hatari mbele yake hivyo nikawahi kumsukuma kando na tulipoanguka chini kombora hatari la RPG likapenya mle ndani kupitia dirishani likitukosakosa kidogo pale tulipokuwa tumesimama. Muda uleule tukasikia sauti mbaya ya mlipuko nyuma ya lile jumba kwenye ile miti ya kivuli lile kombora lilipoangukia. Vumbi kali likasambaa mle ndani na hapo kila mtu akapiga mayowe na kukohoa ovyo.

“Jisalimisheni wenyewe”. Ile sauti kutoka kwenye kipaza sauti kule nje ikatuonya. Kufuatia tukio lile akili yangu ikaanza kufanya kazi haraka. Nikakumbuka kuwa upande wa kushoto wa ile sebule kulikuwa na korido fupi kuelekea jikoni. Haraka nikasimama pale chini kisha nikawataka watu wote mle ndani wanifuate. Hakuna aliyekaidi na tulipofika jikoni nikafungua makabati yaliyokuwa sehemu ya chini ya sinki la jikoni na kuwataka waingie mle ndani na kujificha. Vilikuwa vyumba vidogo sana vya kabati kwa ajili ya kuhifadhia vitu vya jikoni lakini kila mmoja alifanikiwa kuingia tena kwa haraka.
“Unafahamu kutumia bastola?”. Nikamuuliza baba yake Mariama wakati akikazana kuingia kwenye kabati dogo lisiloendana na umbo lake.
“Nafahamu”

“Sawa. Usisite kuitumia pale itakapohitajika”. Nikamtahadharisha na muda uleule nikasikia mirindimo ya risasi mle ndani. Haraka nikawahi kufunga milango ya lile kabati la jikoni kisha nikatoka na kuanza kuambaa na ile korido kurudi kule sebuleni.
Risasi ziliendelea kurindima mle ndani zikivunja vioo madirishani, kuangusha picha ukutani, kupasua milango na makabati.

Nilipofika mwisho wa ile korido nikajibanza na kuchungulia kule nje na hapo nikuona mtutu wa machinegun juu ya ile gari Jeep ukitema cheche kama ekzosi ya roketi. Mwanajeshi mmoja aliyekuwa juu ya ile Jeep alikuwa akitembeza risasi kushambulia lile jumba kama aliyepagawa. Wenzake sikuwaona na hali ile ikanigutusha.
Kwa tahadhari nikajilaza chini na kuanza kutambaa kuelekea ulipokuwa mlango wa kutokea nyuma wa lile jumba huku macho yangu yakiwa makini kutazama huku na kule.

Nilipoiacha korido ya mle ndani nikakatisha kandokando ya sebule hadi nilipoufikia ukumbi wa chakula hapo nikachepuka na kuifuata korido nyingine fupi ya kuelekea mlango wa nyuma wa lile jumba. Nilipoufikia ule mlango nikajibanza kando na kutega sikio. Sikusikia sauti ya kitu chochote na hapo nikapeleka mkono wangu kwenye kitasa nikijaribu kuufungua ule mlango. Ule mlango ulikuwa umefungwa kwa funguo na wakati nikifikiria namna ya kufanya mara nikasikia sauti ya hatua za mtu akitembea kuukaribia ule mlango. Kuona vile haraka nikachepuka kando na kujibanza. Zile hatua za mtu hatimaye zikakomea nje ya ule mlango kisha nikasikia kitasa kikizungushwa taratibu na kwa tahadhari kufunguliwa lakini kwa kuwa ule mlango ulikuwa umefungwa kwa funguo yule mtu hakuweza kuingia mle ndani.

Risasi mbili zilizofyatuliwa na yule mtu nje ya ule mlango kwa shabaha makini zikafanikiwa kuharibu kitasa cha ule mlango na kuufungua nusu wazi huku sehemu ya mlango ule mbao zake zikiwa zimepasuka na kuacha tundu ya risasi. Nikaendelea kujibanza huku macho yangu yakiwa makini kutazama pale mlangoni.

Nilimuona mwanaume mrefu aliyevaa sare za jeshi akiingia mle ndani kwa tahadhari huku ameutanguliza mbele mtutu wa bunduki yake. Sikutaka kumkawiza hivyo nikachomoka mafichoni kwa kasi ya risasi kisha kwa pigo moja makini la teke nikaipiga ile bunduki mkononi mwa yule mtu na kwa pigo lile matata ile bunduki ikamponyoka yule mtu mkononi bila kupenda. Wakati akishangazwa na tukio lile nikamuwahi haraka kwa pigo lingine hatari la ngumi ya mbavu iliyomsababishia kichomi cha ghafla chenye maumivu makali.

Yule mtu akapiga akapiga yowe kuomba msaada hata hivyo alichelewa kwani niliwahi kumshika na kumvutia mle ndani kisha nikamtuliza kwa ngumi mbaya iliyolipasua koo lake na kumpelekea akorome kama mlevi usingizini. Kwa mtindo mzuri wa judo nikamchota mtama na kuanguka naye chini katika muanguko hatari wa komando. Pigo hatari la kiwiko changu likapasua kifua chake na kumlaza chali. Kisha nikazungusha shingo yake na kumyongelea mbali. Bila kukawia nikasimama haraka na kumburuta yule mtu hadi kwenye maficho ya gizani kisha nikairudia bunduki yake pale chini ilipoangukia.

Nikiwa nimejibanza kando ya ule mlango sikusikia chochote kutoka nje na hapo nikajikuta nikiwakumbuka wale wanajeshi wavamizi wawili waliosalia kule nje ambapo yule mmoja alikuwa majeruhi hajiwezi kwa hali nyuma ya ile Jeep. Nikataka nitoke nje lakini nafsi yangu ikasita hivyo nikaendelea kujibanza mafichoni kando ya ule mlango huku nikijipa subira.

Muda ukapita na nilipoona kuwa hakuna mtu mwingine anayejitokeza nikafyatua risasi tatu hewani lengo langu likiwa kumvuta adui aje eneo lile. Adui hakutokea nje haraka kama nilivyotarajia badala yake nikamuona mtu fulani gizani akinyata kutokea kwenye ile korido ya mle ndani akija pale niliposimama. Mashaka yakaniingia nikidhani labda angekuwa baba yake Mariama na kwa kuwa sote tulikuwa gizani nikajipa utulivu.

Yule mtu akazidi kunikaribia na kiasi cha hatua kama tano kabla ya kunifikia akasimama. Sasa tukawa tukitazamana gizani kila mmoja akishindwa kumuona vizuri mwenzake.
“Blamo…Blamo..!”. Nikamsikia yule mtu akiita na sauti yake ikanipa hakika kuwa hakuwa mtu wa mle ndani.
Sikumsemesha badala yake risasi zangu mbili za kifua zikamlaza chini na kumpeleka kuzimu. Kisha mle ndani kukafuatiwa na ukimya wa kifo. Kwa kweli sikuwa nimetarajia kabisa kuwa safari yangu ya ukweni pale Monrovia, Liberia ingetumbukia nyongo namna ile. Hata hivyo kwa kuwa maji nilikwisha yavulia nguo sasa sharti ilikuwa kuyaoga.

Bila kupoteza muda nikampekuwa yule mtu pale chini na nilipomaliza nikafanikiwa kupata bastola moja aina ya CZ 52 iliyojaa risasi, kamba moja ya katani na kisu cha kuchomeka kwenye ala kiunoni. Sikuwa na shaka kuwa kamba ile ilikuwa itumike kumfunga baba yake Mariama mara baada ya kumchukua mateka na familia yake.
Nikamburuta yule mtu hadi gizani na kujibanza. Kikapita kitambo kirefu cha muda huku nimetega sikio langu kwa makini kusikiliza kama kungekuwa na mjongeo mwingine wowote. Sikusikia chochote ingawa hali ile isingenishawishi niamini kuwa mambo yalikuwa shwari.

Mawazo yangu sasa yakajikita kumuwaza yule mtu wa tatu aliyesalia ukimuondoa yule aliyejeruhiwa vibaya kwa risasi za walinzi wa mle ndani ambaye sasa alikuwa akiugulia maumivu kule nyuma ya ile Jeep. Kufuatia yule mtu wa pili kutokea mle ndani ya korido sikuwa na shaka yoyote kuwa mtu yule alikuwa ameingia mle ndani kupitia mlango wa mbele. Nikawaza kuwa hata mwenzake angeweza pia kuingia mle ndani kupitia ule mlango wa mbele ambao sasa ulikuwa wazi baada kuchakazwa vibaya na risasi.

Kufuatia wazo lile nikajikuta nikibadili nia na hivyo kuanza kunyata taratibu nikirudi kwenye ile korido. Mara hii sikufika mbali mara nikamuona mtu fulani akinyata kwa tahadhari kuelekea kwenye kile chumba cha wazazi wa Mariama. Sikuwa na shaka yoyote kuwa mtu yule angekuwa ndiye yule aliyesalia. Kwa utulivu nikachomoa kisu kutoka kiunoni nilipokichomeka kwenye mkanda wa suruali yangu kisha kwa shabaha makini nikakizungusha na ukitupa kwa yule mtu. Muda uleule nikasikia yule mtu akipiga yowe kali la maumivu baada ya kisu kile kuzama mgongoni mwake na kuacha nje sehemu ya mpini tu.

Yule mtu akapenyeza mkono wake nyuma kuchomoa kile kisu lakini ilikuwa kazi bure kwani risasi yangu moja ya shingoni ilimtupa chini na kumlaza kifudifudi. Nilipomfikia na kumchunguza nikagundua kuwa alikwisha aga dunia huku kifuani akiwa ameilalia bunduki yake Smg aliyoikamata vyema mkononi.

Bila kupoteza muda kwa tahadhari nikaondoka eneo lile na kukatisha kwenye sebule ya ile nyumba kuelekea mlango wa mbele. Ule mlango ulikuwa wazi baada ya kitasa chake kuharibiwa na kutobolewa vibaya kwa risasi. Nikatumia muda mfupi kujibanza kando ya ule mlango na nilipoona hali ni shwari nikausukuma ule mlango na kutoka nje nikikatisha chini ya miti ya kivuli kuelekea kwenye ile Jeep.

Nilipofika wenye ile Jeep na kuchungulia nyuma nikamuona yule mwanajeshi mmoja mvamizi aliyejeruhiwa vibaya kichwani na risasi za walinzi wa mle ndani akiwa anakoroma hoi hajitambui huku damu nyingi ikiendelea kuvuja kutoka kwenye majeraha yake mwilini.

Nilipomchunguza nikagundua kuwa hakuwa na muda mrefu kabla ya kuaga dunia. Roho yake ni kama ilikuwa imeshikiliwa na uzi mwembamba na dhaifu. Sikuona sababu ya kumuacha hai hivyo risasi yangu moja ya kichwa ikamzimisha kimya na kuaga dunia. Nikaendelea kuchunguza eneo lile na niliporidhika kuwa hali ilikuwa shwari haraka nikakatisha chini ya miti ya kivuli ya mle ndani kurudi kwenye lile jumba.


Nilipoingia mle ndani nikaelekea kule jikoni kwenye makabati walikojificha akina Mariama. Wote wakashtuka kiasi cha kutaka kupiga kelele za hofu wakati nilipokuwa nikiyafungua yale makabati.
“Msipige kelele tulieni na msiwe na hofu ni mimi Tibba”. Nikawatahadharisha.
“Tibba…!. Nini kimetokea?”. Mariama akaniuliza kwa udadisi.


“Tulivamiwa lakini sasa mambo ni shwari”. Kufuatia maelezo yangu wote wakashusha pumzi za hofu.
“Walinzi wetu wapo nje?”. Mama yake Mariama akaniuliza kwa shauku.
“Wote wameuwawa”
“Mungu wangu…!”. Akang’aka huku amejishika kichwani.


“Hapa siyo mahali salama tena. Tunatakiwa kuondoka sasa hivi”. Nikawatahadharisha maara baada ya wote kutoka kwenye yale makabati na wakati wakishauriana nikawaacha na kuelekea nje. Huko nikakuta magari matatu kwenye banda la maegesho ya magari. LandRover series III Station Wagon ya rangi ya kijivu, Mercedes-Benz C123 nyeupe na Volkswagen Type 2 ya rangi ya damu ya mzee. Nikafurahi kuwa gari zote zile hazikuwa mali ya serikali kwani vinginevyo zingeweza kutuletea shida barabarani.


Kutokana na ubovu wa barabara nyingi za barani Afrika nikaona kuwa ile LandRover ingeweza kufaa zaidi kukabiliana na misukosuko ya barabara mbovu za kipindi kile cha masika. Nilipochunguza vizuri kwenye stoo ndogo ya vipuli vya yale magari nikaona galeni moja ya lita ishirini ya mafuta ya petroli. Moyoni nikafarijika kuwa mafuta yale yangeweza kutufikisha mbali katika safari yetu kabla ya kupata msaada.


Niliporudi kule sebuleni nikawakuta wote mle ndani wamemaliza kujiandaa huku kila mtu na begi lake mkononi huku taa ya pale sebuleni ikiwa imewashwa. Hata hivyo nyuso zao zilikuwa katikati ya hofu na mashaka. Baba yake Mariama huwenda alikuwa kwenye hofu zaidi kwani macho yake yalikosa utulivu kabisa huku akitokwa na jasho kwenye paji lake.
“Tunaelekea wapi kijana?”. Baba yake mariama akasogea karibu na kuniuliza kwa upole.

“Sehemu yoyote mbali na jiji la Monrovia tutakapoweza kujificha hadi nchi itakaporejea kwenye utulivu”
“Tunaweza kwenda kujificha kwa shangazi”. Mariama akasogea karibu na kupendekeza huku akigeuka na kuwatazama wazazi wake usoni. Hakuna aliyepinga hoja ile hivyo ikawa imepitishwa.
“Shangazi anaishi wapi?”. Nikauliza kwa udadisi.

“Umbali wa kilometa mia tatu ishirini kaskazini mwa Monrovia”. Mariama akafafanua huku akinitazama. Kwa sekunde kadha nikimtazama Mariama huku nikifikiri jambo. Kilometa mia tatu ishirini ulikuwa ni umbali mrefu wa safari. Kwa mwendo wa barabara mbovu za kipindi cha masika kama kile safari ingetukutia njiani tayari kukiwa kumepambazuka na hiyo ingekuwa hatari zaidi. Niliwaza, hata hivyo kulikuwa na tumaini baada ya kukumbuka lile galeni la lita ishirini za mafuta ya petroli. Sikuwa na hakika sana kama mafuta yale yangetufikisha mwisho wa safari yetu lakini vilevile hatukuwa na njia mbadala. Hatimaye nikavunja ukimya nikimtazama baba yake Mariama kwa makini.
“Tutatumia LandRovel kusafari usiku huu. Nahitaji funguo zake”. Ombi langu likampelekea baba yake Mariama atumbukize mkono kwenye jaketi lake kuchukua funguo nyingi zilizokuwa mle ndani na baada ya kuzipekua vizuri akachukua ufunguo mmoja na kunipa.
“Gari lina redio?”. Nikauliza.
“Hapana”. Baba yake Mariama akavunja ukimya huku akinitazama kwa makini.


“Redio ya nini Tibba?”. Mariama akaniuliza kwa udadisi.
“Redio ni muhimu kwa ajili ya kupata taarifa juu mambo yanayoendelea hapa nchini baada ya tukio hili la mapinduzi ya kijeshi lililofanyika hivi punde”

“Ninayo redio ndogo kwenye begi langu, tunaweza kuitumia hiyo”. Baba yake Mariama akadokeza huku akitikisa kichwa kuonesha kuwa alikuwa amenielewa vizuri maelezo yangu.
Sasa tayari tulikuwa tumekamilika kwa ajili ya kuanza safari. Bila kupoteza muda nikaawacha pale sebuleni na kurudi kwenye lile banda la kegeshea magari nyuma ya lile jumba. Nilipofika nikaingia kwenye ile LandRover na kuiwasha kisha haraka nikaitoa bandani na kuelekea kwenye mlango wa mbele wa lile jumba. Huko nikawakuta Mariama, baba, mama yake, jamaa zao na wafanyakazi wa mle ndani wakinisubiri. Niliposimama haraka wakafungua milango ya gari na kuingia ndani. Ile galeni ya mafuta ya petroli, mabegi ya nguo na viloba vya chakula nikaviweka juu ya carrier ya gari na kufunika vizuri kwa turubai kwa vile kulikuwa na kila dalili kuwa mvua ingenyesha muda siyo mrefu.


Mbele ya gari tukaa mimi ambaye ndiye dereva na Mariama kando yangu kwa ajili ya kunielekeza barabara. Siti ya nyuma iliyofuata baada ya ile ya dereva wakakaa baba na mama yake Mariama na sehemu ya nyuma kabisa ya gari wakakaa wale wafanyakazi na ndugu wawili wanaume wa akina Mariama. Bila kuchelewa safari ya kuondoka pale ikaanza.

Kwa kasi ya ajabu tukaondoka mbele ya lile jumba tukipitia kwenye lile geti kubwa lililobomolewa na wavamizi na wakati tukipita eneo lile nikaiona miili ya wale wanajeshi walinzi namna ilivyozagaa chini na majeraha mabaya ya risasi. Kila mmoja akageuka na kutazama miili ile kupitia dirishani lakini hakuna aliyetia neno kwa vile hali yenyewe ilitisha sana.

Nje ya geti tulipotoka Mariama akaniambia niingie barabara ya upande wa kulia na siyo ile tuliyokuja nayo siku ya jana. Mwendo wangu ulikuwa wa kasi isiyoelezeka hata hivyo sikuacha kutazama kwenye nyumba za jirani zilizokuwa zikitazamana na ile barabara ya mtaa. Katika baadhi ya nyumba nikaona mageti yake yakiwa wazi na ndani yake nikawaona wanajeshi wakipitisha msako na kuwatoa watu waliokuwa mle ndani. Kwenye nyumba nyingine ndani ya mageti yaliyokuwa wazi niliiona miili ya watu ikiwa imetelekezwa ardhini baada ya kuuwawa kwa kupigwa risasi. Kufuatia hali ile nikamsikia mama yake Mariama akianza kuangua kilio hata hivyo mumewe alimsihi kuwa asilie huku wamekumbatiana. Mariama akaniambia kuwa mtaa ule ulikuwa na nyumba za viongozi wengi wa serikali akiwemo jaji mkuu, spika wa bunge na baadhi ya mawaziri.

Kwa kweli kufuatia tukio lile la mapinduzi ya kijeshi na kuuwawa kwa rais William R. Tolbert Jr. Hali ya machafuko na umwagaji damu wa raia wasio na hatia ilikuwa ikiongezeka kwa kasi ya kutisha kwani kila mahali sasa kulitapakaa miili ya watu. Yumkini kabisa masaa machache baada ya pale nchi nzima ingekuwa inanuka damu kufuatia mauaji yale ya kutisha.
Kulikuwa na kila hatari ya kukamatwa endapo tungezembea hivyo nilikuwa nimeazimia kuwa kabla ya kupambazuka alfajiri tayari tuwe tumeshatoka kwenye jiji la Monrovia na kufika mbali zaidi sehemu ambayo ingekuwa na unafuu wa usalama.


Kufuatia maelekezo ya Mariama niliacha barabara moja na kuingia barabara nyingine kwa kasi ya kuogopesha na tukiwa njiani tukakutana na magari mengine wa watu binafsi yaliyosheheni familia na mizigo kila mtu akiwa katika harakati za kutoroka nchi na hali ile hakika ilitia hofu. Katika baadhi ya barabara tulipishana kwa kasi na magari ya jeshi yenye wanajeshi wenye bunduki mikononi. Kwenye mitaa mingine tukapishana na vikundi vya wanajeshi watembea kwa miguu huku wakiwa na mabegi yao mgongoni na bunduki zao mikononi. Nikashukuru kuwa hatukusimamishwa.

Nilikuwa nimechukua zile bunduki za wavamizi kwa vile nilihisi kuwa huwenda zingekuwa na msaada mbele ya safari hivyo angalau nilikuwa na kiasi fulani cha kujiamini.
Kadiri tulivyokuwa tukikatisha kwenye maeneo yenye makazi ya watu wengi nikagundua kuwa miili ya watu waliouwawa barabarani ilikuwa ikiongezeka kwa kasi sana na kuna baadhi ya maeneo ilibidi tutafute njia nyingine ya kupita kufuatia vizuizi vya mawe barabarani, wingu kubwa la moshi wa magurudumu yaliyochomwa moto na kutelekezwa barabarani pamoja na kusambaa kwa miili ya watu.

Hali ya usalama wa nchi sasa ilikuwa imechukua sura mpya. Vijana waliojitokeza na mapanga na marungu barabarani walionekana kushangilia na kuunga mkono mapinduzi yale ya kijeshi na kuna baadhi ya barabara magari yalisimamishwa na vijana wale yakifanyiwa upekuzi na kila aliyeshuka aliuwawa kwa mapanga. Hata hivyo mimi sikudiriki kusimama hata niliposimamishwa.


Katika baadhi ya maduka makubwa ya mjini niliwaona baadhi ya wanajeshi na vijana wa mitaani wakivunja maduka yale na kupora bidhaa zilizokuwa mle ndani kama nguo, runinga, jokofu, redio, pombe na vyakula. Baadhi ya nyumba zilichomwa moto na watu waliotoka humo ndani na kukimbia waliuwawa kwa risasi. Kasi ya watu kuziacha nyumba zao na kuelekea maeneo mengine yenye utulivu ilikuwa ikiongezeka kwa kasi na hivyo kusababisha wimbi kubwa la wakimbizi...ITAENDELEA WIKI IJAY
 
Noo jaman malizieni ufukwe wa madasca kwanza tumeishia pati 70
 
Noo jaman malizieni ufukwe wa madasca kwanza tumeishia pati 70
Ufukwe wa madagascar mtunzi aliishia hiyo sehemu na iliyobaki kamalizia kwenye kitabu. Mtafute mtunzi kwa namba niliyotuma hapo juu upate nakala yako. Kitabu kimeshatoka
 
Ufukwe wa madagascar mtunzi aliishia hiyo sehemu na iliyobaki kamalizia kwenye kitabu. Mtafute mtunzi kwa namba niliyotuma hapo juu upate nakala yako. Kitabu kimeshatoka

Mkuu ratiba yake vipi? Usije tuacha njiani tukabaki tunateseka na arosto!!!
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom