Moyo wa upendo | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Moyo wa upendo

Discussion in 'Mahusiano, mapenzi, urafiki' started by Yona F. Maro, Sep 26, 2008.

 1. Yona F. Maro

  Yona F. Maro R I P

  #1
  Sep 26, 2008
  Joined: Nov 2, 2006
  Messages: 4,237
  Likes Received: 33
  Trophy Points: 0
  Katika maisha watu hukumbana na mambo mengi sana mengine mabaya na mazuri utafiti unaonyesha maisha ya mapenzi ndio hutokea adhari kubwa zaidi haswa za kisaikologia , mtu anaweza asile au hawezi kuwa huru kama hatoonyeshwa mapenzi ya mtu anayempenda zaidi .

  Wengine uzalendo huwashinda na kuamua kusema wanachofikiria kuhusu mapenzi namaisha ya njia za hadithi na tuongo mbali mbali ,hadithi au tungo inaweza kuwa ya kweli au ya uwongo lakini kinachotakiwa zaidi ni ujumbe unaotoka katika hadithi hiyo kama wewe hujifunzi kitu au somo Fulani basi mtumie mwenzako .

  Hadithi hii inahusu moyo wa upendo kijana mmoja amepata mpenzi lakini anaingiwa na tamaa zaidi anaamua kwenda kutafuta mwingine kwa kujua kabisa ana mpenzi .

  Sasa wengine hutoka kwa sababu hawajarithishwa na mapenzi yao waliyonayo , wengine hutoka katika mapenzi kwa sababu ya roho mbaya , chuki na kadhalika , lakini wengi wao ni tamaa za kimwili kupenda kujaribu mambo mengine ambayo kwa mpenzi wake hayuko huru kusema au kuomba .

  Katika mapenzi usipokuwa muwazi basi hauko huru na maamuzi yako au kwa mpenzi wako , ukitaka kuwa na mapenzi ya dhati lazima uwe huru kwanza yaani kusema unachotaka kwa wakati muafaka na kwa uadilifu .

  Usijaribu kufanya vitu ambavyo mwenzako haridhishwi navyo halafu ucheke au utabasamu hali hii inaweza kukufanya utengane na mpenzi wako au mwenzi wako , usionyeshe dharau au dhihaka kwa mwenzi wako siku zote sikiliza maagizo na kila kitu unachoambiwa kama unapingana nacho unamwambia tu kwamba hivi na hivi .

  Siku zote usifiche hisia zako kuhusu mapenzi na mapendo , hii itamsaidia mpenzi wako kukujua wewe zaidi na itakuwezesha wewe kumrithisha mpenzi wako kwasasababu atajua unachotaka na wewe utajua .

  Usipikuwa mwaminifu kwako na kwa mpenzi wako , usipokuwa mvumilivu , usipokuwa huru , usipokuwa mwadilifu na mpembuzi , moto utakuwakia siku moja na madhara yake makubwa , kuachwa kwa aibu yaani kwa matusi na kudhalilishana kama uswahilini walivyo , kuambukizwa ukimwi kwasababu mmoja anaweza kutoka nje ya ndoa kwa makosa yako .

  ENDELEA

  Siku moja nilienda mkoani mbeya kikazi kwa wiki moja hivi , wakati huo niliishi sehemu moja inaitwa meta lakini kazi zangu nilikuwa nafanyia kule mjini , nikazoea maisha ya mji wa mbeya kwa kipindi kifupi tu , nikajua mitaa ilivyo na watu wa kule kwahiyo sikuonekana ni mtu mgeni bali mwenyeji , mtu ambaye angajua kama mimi ni mgeni au sio mgeni ni yule anayeniongelesha au yule ambaye yuko katika ile hoteli ninayoishi kwasababu kila asubuhi nilienda kuongea na yule jamaa wa reception aniambie kuhusu mji wa mbeya watu wake na kadhalika .

  Basi huduma ya internet nilikuwa napata sehemu moja kule kule mjini mbeya , nilitumia huduma hii kwa ajili ya kutupa taarifa kuhusu kazi ninazofanya kule mbeya na mambo mengine muhimu kama picha za maeneo na mambo kama hayo , kwahiyo hali ikawa shwari kabisa , hii sehemu niliyokuwa natumia internet kuna rafiki mmoja nilimpata basi nilizoeana nae kwa muda wakati mwingine alikuwa anakuja kule ninakolala kuongea nami tunatoka usiku anaenda kunitembeza mjini na kadhalika .

  Kazi zangu ziliisha mkoani mbeya so nikaja zangu dsm kuendelea na majukumu mengine , ghafla siku moja napata email toka kwa dada mmoja anaitwa maggy , ni dada wa miaka 32 hivi , huyu akawa rafiki yangu sana lakini hana asili ya mkoa wa mbeya , yeye akawa ananiambia habari chafu kuhusu watu wa mbeya na wasichana wa mkoa ule , nahisi ilikuwa ujanja wake ili nimsikilize yeye .

  Cha muhimu zaidi nilipenda kujua kwanza amepata wapi hiyo email yangu je pale nilipokuwa natumia internet au kule nilipokuwa naenda kufanya kazi ? nikachunguza kote siku pata majibu tukaendelea hivyo hivyo tu maisha ya kawaida , so siku moja huyu dada akaanza kuniita mpenzi , ana nitaka na mambo mengine matamu tu , sikushituka sana kwasababu nilitegemea maneno kama hayo kama alishaanza kukandia msichana mwingine .

  Kwahiyo tukazoana sana , tukawa tunapigiana simu na kupeana taarifa nzuri nzuri , siku hiyo niko katika gari na wazazi wangu , huyo dada akanipigia simu , mama yangu akasikia sauti ya mwanamke , hee akaanza kushangaa yona ana mchumba , mara yule dada akanipa busu mwishoni wakati ananiaga hapo mama alianza kuniuliza kuhusu huyu msichana kulikoni mimi naye nini kinachoendelea ?

  Basi kila nikitembelea nyumbani mama akawa ananiuliza kuhusu huyu dada siku moja akaniambie nimpe namba za yule dada awe anawasiliana naye yeye , nilisita lakini mzazi ni mzazi nikampa namba za yule dada kwahiyo nikamtambukisha dada kwa mama yangu , mama yangu ni mchunguzi kidogo walipoongea kwa mara ya kwanza tu mama akaniambia ana wasi wasi na huyu dada kwanza umri wake sio miaka 25 kama anavyosema atakuwa ni zaidi .

  Maisha yaliendelea , mwaka 1 ukapita , sikupata kuonana na yule dada , mapenzi yakakolea bwana , siku hiyo akaja zake dsm kupokea majibu ya chuoni kwake , siku hiyo ndio mara yangu ya kwanza kuonana nae , alifikia sehemu moja kule sinza lile eneo alilofikia na hadithi alizokuwa ananielezea nikatiwa simanzi na mashaka kwa mara ya kwanza lakini sikujali sana .
  Jumapili ya mwisho wakati anaondoka nilienda kanisani kwao kusali nae , nikaonana na mama yake mzazi na kaka zake 2 , tukaendelea tu , jioni yake yule dada akanunua vitu ili atembelee kwa wazazi wangu , akaja mpaka nyumbani kwetu bwana halafu ilikuwa bahati ndugu zangu wengine hawakwepo lakini alionana na mama na baba na dada zangu 2 waliokuwa pale .

  Baba yangu bwana akaanza kumuuliza maswali kadha wa kadha kuhusu mimi na yeye anaonaje kuhusu kuwa pale , anafikiria nini kuhusu mimi na mambo kama hayo , anaifikiriaje siku ile , alivyokuwa anajibu basi mama akaniita nje akaniambia huyo dada hakufai mwanangu hana mapenzi ya dhati kwako kwahiyo ongea nae halafu tufahamishe .

  Tukatoka pale nyumbani nikamsindikiza nyumbani kwao alipofikia , usiku huo katika saa 2 hivi akanipigia simu kuniambia kwamba ameamua kuhamisha vitu pale sasa anaenda hotelini ili awahi kwenda katika standi ya basi asubuhi yake , kwahiyo niende katika hiyo hotel aliyohamisha vitu vyake kwenda kuongea nae mpaka usiku kisha niondoke zangu kulala , bila hiyana nilienda .

  Kuanzia usiku huu ndio nilianza majonzi zaidi , katika ile hoteli huko sinza kulikuwa na muziki unapigwa kwahiyo huyu dada alivaa jinsi anavyojua yeye , sio kiheshima tuseme mwili wake karibu wote ulikuwa mtupu , na kila niliko kanyaga nae watu walitutazama sisi , hali ikanishinda sikuweza kukaa sehemu kila mtu anawaangalia nyie tu muda wote nilimwomba atafute sehemu ingine ya kujihifadhi lakini sio pale .

  Tukakubaliana twende chumbani mwake ndio tukakae kupiga story na mambo mengine , kufika kule akasema anaenda kuoga arudi , alipofika kwenda kuoga hakutumia muda kama wasichana wengi walivyo kwa bahati mbaya akatoka huko bafuni akiwa mtupu kama hakwenda na nguo kule , alipofika pale nilimshangaa sana lakini sikumuuliza .

  Nilingoja kwanza yeye atafanya nini , kama nilivyootea akaja katika mtupu akakaa katika kochi la chumbani pale nilipokaa mimi , tukaendelea na hadithi zetu na mambo mengine yeye akiwa mtupu nilijiuliza mara nyingi kwa nini amefanya uamuzi huu sikuwa na majibu ya uhakika , nikaendelea na mambo mengine mimi na yeye .

  Ghafla akanifuata karibu yangu akanilaza katika kitanda nilichokuwa nimekaa mimi , alianza kunibusu bwana , midomoni , katika shingo , mpaka katika macho yule mwanamke alinilamba , masikioni yaani niliona karaha lakini sio raha , tukaenda akaanza nami kunivua nguo zangu alianza na shati .

  Wakati anataka kufungua vifungo vya shati langu ,nilimwambia siko tayari kuingiliana kimwili sasa hivi tafadhali

  " hauko tayari ? sasa kwanini nimevua nguo zote unaniangalia huulizi kwanini ? kama hauko tayari basi nenda zako mlango ule pale "

  Ndio hivyo nikafunga lile shati langu kujiandaa kutoka nje , ilikuwa imetimia muda wa saa 8 za usiku , kabla sijashika mlango akanifuata akanivuta na kuchana lile shati , ndani sikuwa nimevaa kitu chochote kwahiyo nikawa kifua wazi .

  Sikupenda makuu nae , nilinyamaza tu nikarudi pale kitandani kama alivyokuwa anataka basi akanivua nguo zote then akaanza kucheza na mwili wangu bila kufanya jitihada zozote za kuingiliana kimwili na mimi , kwa dakika 30 hivi mwisho akachoka kwa sababu kila alichofanya mimi sikujibu kitu nilimwachia afanye analojua yeye .

  Ndio mwishowe nikamwaga nikatoka zangu bila shati , ilipidi nichukue taxi pale nje inipeleke mpaka nyumbani nikapumzika kidogo , halafu asubuhi yake akanipigia tena muda wa saa 12 hivi akaniomba niende kumuaga pale ubungo kwasababu anaondoka nilifika pale nikamsindikiza mpaka katika basi lake la kurudi mkoani mbeya .

  Basi alipoondoka siku hiyo ya jumapili asubuhi sikua na cha maana ikabidi niende chuoni tu , nilifika kule kwanza nikaogelea kidogo kisha nikatoka kwenda darasani , huku darasani sikuwa na hamu ya kusoma basi nikaingia online bwana kuanza kuongea na wazushi mbali mbali wa mtandao .

  Nikapata dada mmoja hivi anaitwa Judy , huyu tukawa marafiki sana ila huyu umri wake ulikuwa mdogo kwangu lakini sikujali , tukaendelea kudanganyana tu , mwishowe akaniingia moyoni nikamsahau kwa muda yule maggy wa mbeya .

  Huyu judy alikuwa anafanya kazi kiwanda Fulani ya chuo hapa dare s salaam , basi akitoka kazini kwake alipitia kazini kwangu basi tunatembea kidogo kule bandarini na sehemu zingine nyakati za jioni kisha usiku ndio tunarudi nyumbani kwetu .

  Yeye alikuwa anaishi mbezi beach nami naishi zangu kimara , tukaendelea bwana na huu urafiki miezi 3 tangu kujuana nae akaamua kuhamia kimara karibu na kule ninakoishi mimi alipokuwa kule ghafla akajuaana na watu wengi kule na mimi sikupenda hiyo tabia yake ya kujuana na watu wengi .

  Hali ikaendelea , muda kidogo akajua mpaka wazazi wangu walipo wanaishije na kadhalika , alipojua vile na kujua hali ya familia yangu basi akawa karibu zaidi alipenda kunimiliki mimi , simu haziishi , kila akitoka kazini anakuja kazini kwangu , wakati mwingi wa mchana anakuja karibu na kazini kwangu kula chakula cha mchana .

  Kwahiyo kazini wakajua yule ndio mwali wangu , mitaani wakajua yule ndio mwali wangu , nyumbani napo wakasikia nina mwali , wakafikiri ni yule wa mbeya yuko dsm kumbe sio walikosea huyu ni mwingine anaitwa judy nilimtoa katika mtandao tu kama watu wengine walivyo .

  Nilimpenda naye sana lakini sikupenda tabia yake ya kunifuatilia maisha yangu kwa undani sana mpaka aamue kuhamia kimara ninapoishi kali zaidi atafute ndugu zangu awajue bila mimi kuwa na taarifa baadaye ndio aniambie kwamba anajuwana na Fulani na Fulani hali hiyo haikuniweka huru mimi kama binadamu wengine

  Siku moja nilikuwa chumbani kwa judy , nikatoka kwa muda kwenda sehemu moja hivi karibu na kwake pale , nilipotoka akachukuwa simu yangu akaiweka vocha za simu akawa anatuma sms kwa watu , moja ya sms hiyo ilimfikia maggy wa kule mbeya ujumbe ulisema hivi " MPENZI NITUMIE UJUMBE WA KULALA " basi maggy akapiga simu badala ya kutuma ujumbe .

  Hiyo ilikuwa saa 7 za usiku kwa Judy , maggy kupiga akapokea msichana ambaye ndio juddy , hapo walianza kutukanana , mimi sina taarifa , basi judy akakopy ile namba akaweka katika diary yake na simu yake .

  Asubuhi tunakuja kazini na judy katika gari , maggy ananiandikia ujumbe kuniuliza jana usiku nililala kwa nani ? nilishituka sikuamini nikamwangalia judy nikaangalia simu yangu iliongea na nani usiku ule na namba zilizopigwa , nikaona maggy alipiga muda Fulani sikwepo .

  Nilipofika kazini , maggy alinipigia simu kuniambia kwamba judy anamtukana , duh nilishutuka sana nilijihisi kwamba mimi mkosaji mkubwa nimemkosea maggy wa watu na juddy pia nilijilaumu kwanini niliacha simu yangu kwa judy nilifikiri judy ni mwaminifu asingefanya vile alichofanya .

  Nilikanuka nikamwambia maggy kwamba yule dada ni jirani yangu aliomba simu yangu ampigie mama yake alikuwa amesafiri bwana usiku ule na maelezo mengine , maggy akakubaliana na maelezo yangu hakuwa na shaka tena .

  Mwezi mmoja baada ya tukio hili , kukawa kuna kijana mmoja anawasiliana na judy basi yule judy alinipa nimwambie yule kijana kwamba mimi ndio mume wa judy , mambo yaliendelea bwana kumbe huyu kijana alilipwa na maggy achunguze kama kweli bado niko na judy na kama judy ni mpenzi wangu .

  Basi nikazoeana na huyu kijana lakini muda wote huyu kijana hakutaka kuonana na mimi , tukaendelea tu na maisha mara siku maggy alikuja tena dsm kwa mambo mengine alivyokuja cha kwanza ni kutafuta kule ninakoishi akawasiliana na yule kijana , yule kijana akamwita judy katika bar moja hivi jirani .

  Judy alipoenda pale ndio yule kijana akamwambia huyu ni maggy uliyekuwa unamtusi katika simu amekuja kukuona , walipomshika juddy nilikuwa zangu mjini , maggy akanipigia simu niende kule katika ile bar kuonana nao nilipokuwa nachelewa wakaniambia wako na judyy niende kuonana nao .

  Nilishituka sana nilivyosikia hivyo , nilijikaza kwenda kule , mara huyo judy aliwaponyoka akakimbia zake nikafika pale walikuwa wameshaondoka , na ndio nikaonana na yule kijana kumbe yule kijana ni mdogo wake maggy lakini ghafla akaondoka zake sikumwona tena .

  Moja kwa moja tulielekea sinza mimi na maggy na yule kijana alielekea zake kusiko julikana , tulipofika kule sinza katika mgahawa mmoja hivi , maggy akaanza kuniambia kuhusu kuwa mwaminifu katika mahusiano na kadhalika nilimsikiliza kwahiyo nikaachana na juddy

  Ndio hivyo tena lakini sikurudiana tena na judy kuanzia siku ile , nilimuahidi hivyo , tukapoteana tena na maggy kwa mwaka mmoja , juzi juzi hapa akaja tena dsm kuja kufanya kazi zake mwingine akanipa taarifa nami nilimpokea akaenda kuishi kule kule kwao sinza .

  Sasa alipokuja kipindi hichi alibadilika sana kwanza alikuwa mlevi , mfano nikitoka kazini kwenda kule sinza anakoishi yeye nilimkuta sehemu za kinywaji anabwia pombe au kilevi chochote kile , sasa yeye ni mtu mzima siwezi kumwambia acha hizi na zile .

  Basi ukifika wakati wa kumpa busu siwezi kwasababu ana harufu ya pombe mdomoni na mimi situmii pombe , hapo ndio mapenzi yetu yalianza kwenda kombo mimi naona kwamba yeye ni mtu mzima sio wa kuambiwa kuhusu pombe na madhara yake siku panda kumsumbua hata kidogo .

  Siku moja tena , tukapanga kwenda nyumbani ili aonane na wazazi wangu , tulikubaliana kukutana sinza kisha twende wote kimara , kufika kule sinza nilimkuta na mdogo wake mmoja hivi wameshaanza kutumia kilevi wameagiza kiti moto sehemu hiyo .

  Nilikatishwa tamaa sikuwa na hamu tena ya kwenda home kwasababu alikuwa ana kilevi kichwani na sijui akilewa au akinywa pombe ana tabia zipi anaweza kuwa ni mtusi au na tabia zingine za ujeuri , kule nyumbani walituandalia chakula kizuri cha jioni na mambo mengine mazuri tu siku ile .

  Mpaka saa 2 usiku hatukufika baba akanipigia simu kuniuliza kulikoni mbona bado hatujafika ? sikutaka kumwelezea baba kilichotokea kwasababu nilijua fika atampigia simu yule dada kumuuliza kulikoni labda yule dada anaweza kumjibu upuuzi .

  Kumbe huyu dada alikuwa pale ana mngoja jamaa mwingine ambaye mimi simjui yule jamaa alivyochelewa , maggy akampigia simu na kumtusi matusi mazito ya nguoni , kuanzia hapo nikamweka katika kundi lingine la binadamu manake mimi na matusi na lugha chafu ni vitu 2 tofauti kabisa .

  Yule jamaa kweli hakutokea , ilipibidi baadaye nimsindikize kwenda nyumbani kwao kulala , nami nililuridi zangu nyumbani kupumzika bila wasi wasi wowote ila cha muhimu nilichofikiria zaidi ni kuhusu hatima ya uhusiano wetu na maggy kwa jinsi alivyomlevi , huyu hafai kuwa mpenzi wangu hata kidogo .

  Nikaendelea kuishi maisha ya kwaida tu

  Mpaka siku ingine akaja jijini dar es salaam bila kunipa mimi taarifa , alikaa kwa siku 3 hivi , siku ya 4 nilimpigia simu kumuuliza habari za masiku ndio alinieleza kwamba yuko dsm kwa siku 3 sasa na kesho yake anaondoka sikuwa na swali la kumuuliza nilimvumilia tu .

  Lakini ndio hivyo , mpaka sasa nimeshachoka maisha na huyu dada sina la kumwambia wala kumtuhumu , najua nikiendelea nae na haya mapenzi tunaweza kufika pabaya madhara yakawa makubwa zaidi sina hakika kama niachane nae au la .

  Lakini nikiachana nae , wazazi wangu wanamtambua huyu , ikipidi niende kuonana na wazazi wangu kwanza nao waniambie inakuwaje kuhusu huyu dada najua wanaweza kutupatanisha na kumwambia huyu dada kuhusu wasichana ninaowapenda mimi na tabia zao .

  Zote hizo ni hoja lakini huyu dada ana umri wa miaka 32 , ana mtoto mmoja , wazazi wangu sikuwahi kuwaambia kama maggy ana umri huo , huwa nawaambia anamiaka 25 nampunguza pili sijawahi kuwaambia kwamba ana mtoto .

  Wewe unaonaje niachane nae niwe na mwingine au niendelee nae kwa matumaini kwamba atajirekebisha , au nikae nae karibu nimwelezee jinsi ninavyojisikia juu yake na mambo anayoyafanya ? lakini si anaweza kujitetea kwamba yeye ni mtu mzima anajua anachofanya kwahiyo nisimsumbue ?

  Bora niwe na wangu mwenyewe mwenye umri sawa na mimi mwenye moyo wa upendo kwangu au sio unaonaje ?

  HADITHI HII NI YA KUTUNGA TU
   
 2. NaimaOmari

  NaimaOmari JF-Expert Member

  #2
  Sep 26, 2008
  Joined: Sep 25, 2007
  Messages: 807
  Likes Received: 21
  Trophy Points: 35
  Pole sana Shy dunia ndivyo ilivyo .. ila nakushauri jifunze kujipenda mwenyewe kwanza mengine yatafuata .... halafu pia read signs za watu walokaribu nawewe mathalan mama yako ... hawezi kukutakia mabaya .. laiti ungemsikiliza yote yasingekukuta but now that it has happened hatuna budi kukushauri.

  Najua unampenda sana maggy sasa mpaka wewe mwenyewe uamue kwa moyo wako kwamba naweza ama siwezi kuendelea nae.. yetu yatakua kelele tu kwako
   
 3. miss chagga

  miss chagga JF-Expert Member

  #3
  Jan 30, 2015
  Joined: Jun 7, 2013
  Messages: 57,685
  Likes Received: 30,841
  Trophy Points: 280
  aisee Shy ungeandika now days too long
   
  Last edited by a moderator: Jan 4, 2016
 4. miss chagga

  miss chagga JF-Expert Member

  #4
  Jan 30, 2015
  Joined: Jun 7, 2013
  Messages: 57,685
  Likes Received: 30,841
  Trophy Points: 280
  Last edited by a moderator: Jan 4, 2016
 5. Lubebenamawe

  Lubebenamawe JF-Expert Member

  #5
  Jan 30, 2015
  Joined: Oct 27, 2014
  Messages: 1,121
  Likes Received: 561
  Trophy Points: 280
  Watu wengi ni wa ajabu sana unampa pole ya nini wakati amekwambia hii ni hadithi ya kutunga.???? Hali hakuna ushauri unaohitajika hapo.
   
 6. Freeland

  Freeland JF-Expert Member

  #6
  Jan 30, 2015
  Joined: Jan 24, 2012
  Messages: 14,468
  Likes Received: 6,761
  Trophy Points: 280
  miss chagga mtunzi wa hadithi hii anajichanganya sana

  Nimeshindwa hata ku mfuatilia mtiririko wa matukio

  Ila nilichojifunza ni mtu ambaye hana msimamo na hajitambui
   
  Last edited by a moderator: Jan 4, 2016
 7. miss chagga

  miss chagga JF-Expert Member

  #7
  Jan 30, 2015
  Joined: Jun 7, 2013
  Messages: 57,685
  Likes Received: 30,841
  Trophy Points: 280
  ndiyo ilikuwa hivyo sasa enzi hizo sasa
   
 8. miss chagga

  miss chagga JF-Expert Member

  #8
  Jan 30, 2015
  Joined: Jun 7, 2013
  Messages: 57,685
  Likes Received: 30,841
  Trophy Points: 280

  Lubebenamawe ha ha ha ha ha
   
 9. Freeland

  Freeland JF-Expert Member

  #9
  Jan 30, 2015
  Joined: Jan 24, 2012
  Messages: 14,468
  Likes Received: 6,761
  Trophy Points: 280
  Vipi unasemaje ...hii iharibike? eti hater
   
 10. miss chagga

  miss chagga JF-Expert Member

  #10
  Jan 30, 2015
  Joined: Jun 7, 2013
  Messages: 57,685
  Likes Received: 30,841
  Trophy Points: 280
  hapana hater .. tujifunze tu
   
 11. MO11

  MO11 JF-Expert Member

  #11
  Jan 30, 2015
  Joined: Mar 23, 2014
  Messages: 14,206
  Likes Received: 12,601
  Trophy Points: 280
  Last edited by a moderator: Jan 4, 2016
 12. Junior. Cux

  Junior. Cux JF-Expert Member

  #12
  Jan 30, 2015
  Joined: Feb 3, 2011
  Messages: 5,305
  Likes Received: 1,230
  Trophy Points: 280
  inahitaji moyo kuimaliza yote....
   
Loading...