*NANI KAKUZUIA KUJIPAMBA, EBU JIPAMBE DADA... JIPAMBE UWE MREMBO ZAIDI*
Leo nataka kuwatia moyo wanawake kwa habari ya kujipamba, jipambe ili mpendeze mwaya.......
Najua zipo saloon nyingi zenye hadhi mbalimbali na zina wataalamu wa viwango tofauti tofauti lakini nimegundua saloon moja haihitaji gharama kubwa sana kama unataka kupambwa. Nilikuwa napita mahali nikaiona, nikasema lazima niwashauri wanawake waende hiyo saloon wakajipambe na haipo mbali. Unakubalije kukaa bila kujipamba na wakati umeruhusiwa?
Mwanzoni nilipoiona hii saloon nilishtuka nikaambiwa, usishtuke Mhubiri, nikauliza kwanini? Nikaambiwa...... _*Maana hivyo ndivyo walivyojipamba wanawake watakatifu wa zamani, waliomtumaini Mungu na kuwatii waume zao*_1Pet 3:5 Nikauliza walitumia mapambo gani hao wanawake wa zamani? Akasema; _*Wanawake wa zamani walijipamba kwa mapambo yasiyoharibika yaani roho ya upole na ya utulivu*_ 1Pet 3:4 Nikasema.... Kumbe kuwa na roho ya upole ni pambo! Kumbe roho ya utulivu ni pambo!
Mapambo adimu sana haya kwa wanawake wengi siku za leo. Mapambo haya hayapatikani saloon za kawaida bali ndani ya Bible pekee.
Ili kujua mtu ana roho ya utulivu ni pale yanapotokea mazingira ya tafrani, misukosuko. Ukiona mwanamke unatokea msukosuko kidogo tu kwenye ndoa yake, halafu anaenda kumtangaza mumewe nje vibaya, ukiona hivi ujue huyu hajapambwa huyu. Unatembea barabarani kumbe unanuka, udhaifu wako wote umeshatolewa nje na hujui.
Na ili kujua mwanamke ana roho ya upole ni pale mazingira yanapokuwa ya fujo, kelele na vimbwanga. Ukiona mwanamke mkali kiasi kwamba mume hajisikii kuwahi nyumbani ujue huyu mwanamke kakosa pambo huyu.
Wanawake jipambeni kwa mapambo hayo jamani, ni mapambo yasiyoharibika yanadumu, hata ukinyeshewa mvua hayabanduki, sisi wanaume tunatamani kuwaona mkijipamba kwa mapambo hayo.
Lipsticks, Brazilian Hair, Expensive shoes, Expensive dresses, Manicure, Pedicure, Mascara, Eyeshadows....etc haya yanaharibika, hayafai kwa binti za Mungu. Jipambe kwa roho ya upole na utulivu ili uwe mrembo rohoni binti ya MUNGU.
*MUNGU KWANZA!!!*