Rapture Man
JF-Expert Member
- Dec 29, 2010
- 439
- 145
It hurts. Inauma sana.
kijana asante kwa taarifa.huu ni mchakato tu,uwe mpole.Wakuu saa Mtwara ni vita kamili;
-mabasi ma5 ya Champion yamebeba wanajeshi yako njiani yanakuja
-Imeripotiwa watu 7 wamefariki
-mapambano kati ya raia na polisi bado yanaendelea
-milio ya risasi na mirindimo ya mabomu bado inasikika
-nyumba za viongozi zinaendelea kuchomwa moto
-maduka yamefungwa hakuna huduma zozote zinazopatikana
-barabara zimewekwa vizuizi magogo makubwa na matairi yamechomwa moto
-jengo la mahakama ya mwanzo Mitengo limechomwa moto
Ni upepo tu unavuma na utapita lakini mwisho wa siku watakaoumia ni wale wale na wataambulia kupewa pole tu toka kwa wale wanadhani wanawaunga mkono. Inahitaji ujasiri wa ziada kwa nazi kushindana na jiwe.
Nadhani ni Wakati sasa Serikali itafakari upya mpango wake wa ujenzi wa bomba la gesi. Ni vyema iyo gesi ivunwe huko mtwara, plant ya kufua umeme ijengwe huko huko na kisha umeme usafirishwe kwa njia ya Nguzo.
Naamini gharama za kusafirisha gesi kwa bomba
Tatizo watanzania tulikubali akili ndogo kuongoza kuongoza akili kubwa haya ndiyo matokeo yake kazi tunayo watanzania.
Tunafahamu sana watu kama nyie lazima mtaanza kufaya uchocheziWakuu leo Mtwara hali nI mbaya zaidi kuliko jana kwa vitendo viovu VINAVYOFANYWA na askari wa jeshi la polisi.
Iko hivi;
-Polisi wanafyatua risai za moto kwa raia
-wanavunja mabanda ya biashara ya raia na kupora mali, fedha na chochote kilichopo KISHA KUYACHOMA MOTO
-Wanasachi na kunyang'anya fedha, simu na chochote alichonacho mfukoni kisha wanamjeruhi vibaya yeyote wanayekutana naye bila kujuwa kuwa ni nani
-wanavunja nyumba za raia na kubeba wanachoona kinawafaa
NB: Vijana wengi hasa wa mitaa ya Majengo, Mdenga na Magomeni wameyakimbia makazi yao wako mafichoni nje kdogo ya mji
Mkuu, kuna uwezekano wa kutupia picha mbili tatu?
wewe usiwe na wasiwasi,kumbuka hata kambarage nyerere ilimlazimu apeleke askarijeshi wa kizenj kule mara,hatimae walitulia.Kikwete awe mwangalifu hii nchi ni ya watanzania wote, yeye alichonacho ni dhamana ya uongozi ambayo ina hatima yake, sasa asijisahau akadhani aliinunua hii nchi kama mali yake,mamba yakizidi kuharibika huko mtwara ata ambao anadhani wako naya karibu watamruka maili mia...hapo ndio ataelewa busara inanguvu kuliko liburi na ubabe
hakuna busara mbele ya wahuni wewe,ulishaona wapi busara inatumika kumkabiri gaidi mwenye silaha na anayechoma majengo,hao ni risasi za moto tu na nguvu.Kikwete asifikiri anaongoza familia yake, jeuri yake itamtokea puani, Busara inahitajika katika kuongoza nchi, viongozi waliokosa busara na wasio na heshima kwa wananchi hawana nafasi katika Jamii yetu. Wasifikiri hii nchi ni yao, wajue kuwa nchi hii ni ya Watanzania kama wameshindwa kuongoza waondoke hatuwalazimishi na hakuna aliyelazimishwa kuongoza hii nchi.
Amani inaanza kutoweka.Mkuu, una uhakika hayo yote hapo juu yanatokea Mtwara na sio Msumbiji? Tanzania ni nchi ya amani sana, wananchi wake hata uwafanyie ubabe na uovu kiasi gani hawawezi kufanya unayosema hapo juu, wanapenda amani!