Fursa Pesa
JF-Expert Member
- May 30, 2012
- 4,633
- 3,534
kinachoonekana Mtwara hasa ni uelewa ndogo baina ya wananchi na viongozi waliopewa madaraka ya kuwaongoza wanamtwara.Miongoni mwa watu wanaosababisha vurugu hizo si wanasiasa pekee bali hata viongozi wakuu waliopewa dhamana na serikali kushindwa kutimiza wajibu wao moja kwa moja kwa wananchi kiasi cha kusababisha ugumu wa maisha uliopitiliza.Yafutayo yafanyike kwa haraka;
1.Kubadili mfumo mzima wa uongozi mkoani na wilaya zote.
2.Kufuatilia kwa karibu mienendo na mawasiliano ya viongozi wote waandamizi pasipo kuangalia sura,cheo wala itikadi zao.
3.Kuwaorodhesha vijana wote wanaotaka fursa ya gesi iwanufaishe ili wafanyiwe usaili na kubaini uwezo wao katika rasilimali watu.
4.Kufuatilia kwa karibu taarifa na mienendo ya wafanya biashara wa nishati ya gesi kwa kuwa yawezekana panaweza kukawa na mkakati maalum ili wao waendelee na biashara hiyo kwni kwa kutumia bomba kusafirisha gesi hiyo kunaweza kuathili biashara yao.
5.Kwa kuanzia wenyeviti wote wa mitaa mahala gesi inapotoka wawezeshwe vya kutosha ili waweze kubaini wakaazi wao, kwa kuwa yawezekana nguvu na ushawishi mkubwa ukatoka nje ya mpaka wa nchi au pakawepo na watu ambao si wakazi wa Mtwara na moja ya kazi iliyowapeleka huko ni kuwashikiza wananchi kugomea mikakati ya serikali.
6.Msako mkali ufanyike nyakati zote na ikiwezekana mahala popote pale ambapo wageni ufika.
7.Sensa ya watu na makazi itumike kubaini wakazi halali wa Mtwara ili fursa hii hadimu iwadondokee watanzania wazalendo na si wale ambao mguu mmoja ndani mwingine nje.
8.Wanamtwara washauliwe kuwahimiza vijana na watoto wao waende shule kuliko kukaa vijiweni au kukimbilia mijini ili siku zijazo waweze kumiliki uchumi ipasavyo na si kukaa na kusubili fursa za bure bure na huruma ya serikali.
9.Viongozi wa juu pamoja na wanasiasa wasipende kubebana-bebana katika mambo ya hatari namna hii bali kila mmoja awe ni mlinzi wa mwenzake na ikiwezekana wawasemee wale wote wanaokiuka maadili na viapo vya majukumu yao.
10.Fursa hii ya gesi isigeuzwe na wazembe wachache wenye uchu wa madaraka na sifa za kijinga kujipalilia njia zao haramu za kujinufaisha kiuchumi,kisiasa na kijamii bali iwe ni changamoto yenye kuleta mageuzi ya kweli kwa taifa zima.
Hata kama uongozi ni heshima na utukufu wa duniani,lakini uongozi wa kutafuta kwa kutumia watu wachache wasio na uelewa wa kutosha juu ya kile ulichowaaminisha ni sawa na kuwaangamiza maskini hawa wasio na kitu wala heshima yoyote mbele ya jamii na mwisho wa siku utawala wa aliyepata uongozi huo kwa kutumia kafara za watu hawa hakika hautadumu.