Mkuu kuwa na invoice mbili zenye kiasi kinachotofautiana kwa transaction moja bado nashindwa kujua ameponyokaje.Hivi kuna aliyetegemea kuwa Mahalu angeshindwa hiyo kesi?
Hatimaye Mahakama ya hakimu mkazi kisutu imemwachia huru Prof.Mahalu
Mkuu kuwa na invoice mbili zenye kiasi kinachotofautiana kwa transaction moja bado nashindwa kujua ameponyokaje.
Unataka kutuambia hawa wote rais amewaonea?
Liyumba visasi, Yona visasi, Ballali visasi, Jeetu Patel visasi, Mramba visasi, Maranda visasi, Farijala visasi, Mgonja visasi?
Kwanini mnaona kama mtu kufikishwa mahakamani ni kitu kibaya? mimi nilitegemea hao wahusika washukuru kwamba wamefikishwa mahakamani ili wapate nafasi ya kujisafisha.
Mkuu kuwa na invoice mbili zenye kiasi kinachotofautiana kwa transaction moja bado nashindwa kujua ameponyokaje.
Mahakamani watu huenda kutafuta haki. Ni haki transaction moja kuandaliwa hati za malipo mbili zenye kiasi cha malipo tofauti na hati zote zikawa valid? Hicho ndicho ninachotaka kujua bila kujali kuwa Mahalu alishirikiana na nani katika mchakato huo.Jiulize hv hizo invoice mbili hata kama aliziandaa yeye ilikuwaje waziri na Rais wazijue na wakubali hela ilipwe nyingi na ile itakayotumika italy iwe na pesa kidogo? Yet bado mahalu awe na kesi peke yake? Angekutwa amechakachua yeye kama yeye hapo sawa ila haikuwa hivyo ndugu, Mh. Rais alishasema akili za kuambiwa changanya na zako.
Kesi hii ni lazima Mahalu ashinde. Kwa mara nyingine mahakama imeingia kwenye kitendawili au kutoa haki au kusimama na aliyeianzisha mr dhaifu.
Tatizo la kikwete ni mtu wa visasi sana na amehusika sana kuitunga kesi hii na jambo hili ni dhahili wala halina kificho hata chembe.
Kweli kikwete ni dhaifu..
Chini ya Marando kesi haikatizi nendeni mahakamani tena kuhusu ile tuhuma ya CDM na usalama wa TaifaHii kitu inaweza kuwa ni stagemanaged na watu humu wanashangilia kama mazuzu.
Ndo kusema huyo jamaa alikua msafi sana au.
Eti jk amepimana ubavu na mkapa WAPI? Ingekua ndo masuala ya kupimana angesema mwacheni mkapa apumzike.suala la kiwira angechomoka vipi huyo mr clean.
Yaani humu kuna ushabiki wa ajabu sana na unakuta jitu zima na kitambi chake lenye wajukuu lakini mambo linayoshabikia ni upuuzi hasa.
Mazingira ya kuwepo kwa matumizi mabaya ya ofisi yalikuwepo, ila suala kushinda na kutoshinda na jambo lingine. Sidhani kama kulikuwa na tatizo lolote la kufunguliwa kwa kesi hiyo.
Hivi hamuoni saga yote ni mchezo wa kuigiza, changa la macho kwa Watanzania wakati WOTE lao moja?