Nasikitika ninaposikia mafanikio ya TAKUKURU kuwafikisha watuhumiwa mahakamani bila matokeo ya hukumu kwa watuhumiwa wa rushwa

Konseli Mkuu Andrew

JF-Expert Member
May 10, 2013
740
855
Kwa mujibu ya katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Ibara 107A(1) inayotamka kama ifuatavyo:

"Mamlaka ya utoaji haki katika Jamhuri ya Muungano itakuwa mikononi mwa Idara ya Mahakama na Idara ya
Mahakama ya Zanzibar, na kwa hiyo hakuna chombo cha Seriikali wala cha Bunge au Baraza la Wawakilishi la Zanzibar kitakachokuwa na kauli ya mwisho katika utoaji haki"

Hii tafsiri yake ni kuwa mamlaka ya utoaji wa haki upo juu ya Mahakama ambapo ni muhimili unaojitegemea.

Twende kwenye mada husika, juzi nimesikiliza mahojiano ya afisa wa TAKUKURU akiojiwa na kituo kimoja cha habari na kuulizwa mafanikio ya TAKUKURU akitoa orodha ya kesi zilizofika tayari Mahakamani lakini hakuorodhesha hukumu ya baadhi ya kesi hizo.

Nipende kusema jambo moja muhimu sana, kushtaki watu kuhusiana na masuala ya rushwa sio issue , issue kubwa ni mtiririko wa mwenendo wa kesi kuanzia mwanzo hadi kufikia hatua ya hukumu ndio issue.

Unakuta mtu ameshtakiwa kwa rushwa lakini anakuja kuwashinda Mahakamani kwa kitu kidogo sana unafikiri huyo mtu ataogopa kutenda tena kosa?

Wakati alishajua kuna uzembe ambao TAKUKURU wanafanya na kusaidia watuhumiwa kushinda kesi? Na mahakama huwa inahitaji ushaidi usio na doa ili kumtia mtu hatiani na si vinginevyo.
 
Hata tukilalamika hawajali, tupambane kupata Katiba mpya.

KaziKweliKweli/JobTrueTrue
 
Wao kama chombo kingine ni kukamata lakini si kuhukumu. That upto mahakama, sasa mahaka ikiwa compromised watabaki wanafanya kazi bure
 
Walaumu mahakama na DPP... Kesi nyingi za rushwa siku hizi zinawafunga wengi ila mambo ya plea bargain ndo humaliza kimyakimya. Watu wengi sana waliokwapua mabilioni wamemalizana na DPP kiaina.
 
Kesi ambazo utajua mwanzo ila mwisho wake usiujue ni pamoja na kesi za rushwa za baadhi ya wenye vyeo na pesa,maaaskari hasa wa polisi na JW wakituhumiwa kufanya makosa hata yawe ya mauaji,ulawiti hasa zinazowagusa makasisi.
Umma utajulishwa mwanzo mwa kesi,halafu KUKIPOA umma haujui mwisho.
 
Back
Top Bottom