Mabalozi waliowahi kuvuliwa hadhi ya Ubalozi

Chachu Ombara

JF-Expert Member
Dec 11, 2012
5,897
10,358
Leo Dkt . Slaa amevuliwa hadhi ya Ubalozi na Rais wa JMT, Samia Suluhu. Dkt. Slaa anaingia katika orodha ya viongozi wengine waliovuliwa hadhi ya Ubalozi.

Katika kumbukumbu zangu nakumbuka Profesa Mahalu aliyewahi kuwa Balozi wa Tanzania nchini Italy alivuliwa hadhi ya Ubalozi baada ya kuwa na kesi ya ufisadi alipokuwa akihudumu katika nafasi hiyo. Soma: (Docs): Siri ya Kesi ya Mahalu: Ununuzi wa Jengo la Ubalozi Italia

Baadaye, Hayati Rais Magufuli alimrudishia hadhi hiyo ya ubalozi baada ya kushinda kesi ya Uhujumu Uchumi. Soma: Rais Magufuli amrudishia Ubalozi Prof. Costa Mahalu baada ya kushinda kesi ya uhujumu uchumi

Mwingine ni Alfayo Kidata ambaye sasa ni Kamishna Mkuu wa TRA ambaye pia naye alivuliwa hadhi ya Ubalozi

Kama kuna wengine naomba tusaidiane kukumbushana.
 

Attachments

  • IMG-20230901-WA0032.jpg
    IMG-20230901-WA0032.jpg
    29.9 KB · Views: 6
Balozi Ngongo baada ya kuvuliwa sasa najulikana kama Dr Ngongo mtetezi mkuu wa Bandari.
 
Kasanga Tumbo kama nakumbuka vizuri alijiuzulu ubalozi mwenyewe ili arudi nyumbani, sikumbuki kama alivuliwa ubalozi.

Kuna Balozi mmoja wa kike Enzi za Nyerere jina lake nalisahau kabisa....
Kama Una acesss na wazee wa history wanaweza kumtaja...nahisi alikuwa balozi UN au nchi moja ya west ... history yake haisimuliwi sana
 
Kuna Balozi mmoja wa kike Enzi za Nyerere jina lake nalisahau kabisa....
Kama Una acesss na wazee wa history wanaweza kumtaja...nahisi alikuwa balozi UN au nchi moja ya west ... history yake haisimuliwi sana
UN hatujawahi kuwa na balozi wa kike, kwa hivyo hapo tupatoe.

Huko kwingine nakuomba uwataje vizuri zaidi, maana hapa utawanasa Mama zetu waliomo na wasiomo.

As for "the west" nikichagua UK tu herufi M napata Maajar na Migiro.

I am sure these were exemplary.

Wataje vizuri mkuu.
 
Ukijiuzulu bado unakuwa na hadhi ya ubalozi, ila unaweza ukajiuzulu na ukavuliwa pia hadhi ya ubalozi.
Naam.

Na ukivuliwa hadhi ya ubalozi unaweza kurudishiwa.

Mfano balozi Costa Mahalu alivuliwa hadhi hiyo na rais Magufuli, na baadaye akarudishiwa.
 
Back
Top Bottom