bibikuku
JF-Expert Member
- Feb 16, 2011
- 832
- 495
Wana JF
Leo mahakama ya hakimu mkazi Kisutu inatarajia kutoa hukumu katika kesi ya matumizi mabaya ya ofisi inayomkabili Prof Costa Mahalu aliyekuwa balozi wa Tz nchini Italy na mwenzake.
Mtakumbuka kesi hii ilimfikisha mahakamani Rais Mstaafu Mkapa aliyemtetea Mahalu kwa nguvu zote. Rais Kikwete alitakiwa kupanda kizimbani pia kutoa utetezi wake lakini alikwama kwa mujibu wa katiba yetu.
Hukumu ndio leo. Nikiweza nitakuwapo kutoa updates kama bepari wangu hataleta kauzibe. Vinginevyo wale watakaoweza kuwepo, ruksa kupashana kinachojiri

Leo (Agosti 09, 2012) Mahalu kaibwaga serikali katika hii kesi!
Updates zinafuatia
Mahalu kashinda kesi..
Chanzo: Radio One breaking news!
Waandishi wa habari wakimfuata Balozi Profesa Mahalu akiwa pamoja na Mdogo wake Mirasi Rama wakitoka nje ya Mahakama ya Kisutu Mchana huu mara baada ya kushinda kesi iliyokuwa ikimkabili akidaiwa kununua nyumba ya Ubalozi wa Tanzania nchini Italia, Akisoma hukumu iliyosomwa kuanzia Saa sita leo na Hakimu Mfawidhi mkazi wa mahakama ya Kisutu Mh. Ilivin Mugeta imemtoa Balozi Profesa Mahalu katika hatia na kumwachia huru (PICHA NA PHILEMON SOLOMON WA FULLSHANGWEBLOG)
Balozi Profesa Mahalu akizungumza na waandishi wa habari mara baada ya kushinda kesi yake katika mahakama ya kisutu leo.
Wakili wa Balozi Profesa Mahalu Bw. Alex Mgongolwa akizungumza na waandishi wa habari mara baada ya mteja wake kushinda kesili iliyokuwa ikimkabili kwenye mahakama ya Kisutu jijini Dar es salaam.
Balozi Profesa Mahalu katikati akitoka nje ya mahaka ya Kisutu huku akiwa ameongozana na mdogo wake Mirasi Rama kulia ni Wakili wa kujitegemea Mabere Nyaucho Marando.
Picha na Full Shangwe Blog